Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230817_063021_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230817_063037_Opera%20Mini.jpg
 
MCHANGANUO WA MSHAHARA WA NEYMAR
.
Kwa mwaka:
Pauni 137.8 milioni (Sh 437.2B)
.
Kwa mwezi:
Pauni 11.48 milioni (Sh 36.4B)
.
Kwa wiki:
Pauni 2.65 milioni (Sh 8.4B)
.
Kwa siku:
Pauni 377,534 (Sh 1.2B)
.
Kwa saa:
Pauni 15,730 (Sh 50M)
.
Kwa dakika:
Pauni 262 (Sh 831,222)
.
Kwa sekunde:
Pauni 4.3 (Sh 13,642)

…………
Screenshot_20230817_064307_Instagram.jpg
 
Klabu za Saudi Arabia zimeripotiwa kuanza mchakato wa kuvamia Arsenal kwa ajili ya kwenda kunasa huduma ya beki wa kati wa Kibrazili, Gabriel Magalhaes.

Klabu hizo zinazoshiriki Saudi Pro League zimekuwa bize kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kusajili wachezaji wenye majina makubwa kutoka Ulaya ili wakacheze kwenye ligi yao.

Klabu za soka za Ulaya zipo kwenye mashaka makubwa kutokana na dirisha la usajili la Saudi Arabia kuwa wazi hadi Septemba 20.Gabriel amekuwa mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Arsenal na mkataba wake kwenye klabu hiyo utafika tamati Juni 2.
Screenshot_20230817_064559_Instagram.jpg
 
Mbali ya Brighton, West Ham pia inatajwa ni timu nyingine kutoka England inayohitaji huduma ya kiungo wa Ajax, Mohammed Kudus katika dirisha hili.

West Ham inataka huduma ya fundi huyu kama mbadala wa staa wao kutoka Brazil, Lucas Paqueta, 25, anayehusishwa na Manchester City. Kudus anadaiwa kuomba kuondoka Ajax kwenye dirisha hili na huko nyuma aliwahi pia kuhusishwa na Manchester United akajiunge na Kocha Eric Ten Hag.
Screenshot_20230817_064645_Instagram.jpg
 
Beki wa Chelsea, Marc Cucurella, 25, ni miongoni mwa mastaa wanaodaiwa kuwa kwenye rada za Newcastle United na huenda akatua kwenye viunga hivyo kabla ya dirisha kufungwa.

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe ndiye anayedaiwa kulipendekeza jina la staa huyu na kuagizwa asajiliwe haraka iwezekanavyo ili kwenda kutengeneza ukuta imara wa kuifanya timu hiyo kutesa msimu huu.
Screenshot_20230817_064732_Instagram.jpg
 
Baada ya kuumia kwenye mechi ya juzi Jumamosi ,Arsenal imethibitisha kuwa beki wake Jurrien Timber atakuwa njee kwa miezi sita hadi saba kutokana na kupata majeraha

Pigo !View attachment 2719467

Ahsante kwa Magazine shemeji [mention]Shunie [/mention]
Sema upo busy sana au [mention]Lee [/mention] kakuficha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom