Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230814_072606_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230814_072622_Opera%20Mini.jpg
 
Mechi ya fainali ya Ngao ya Jamii ya Simba na Yanga katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Simba SC inafanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii mbele ya Yanga kwa ushindi wa penati 3-1 baada ya dakika 90 kumalizika 0-0.

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Simba na Yanga kucheza fainali ya Ngao ya Jamii, mbili zilizopita zote alichukua Yanga SC kwa kuifunga Simba SC.
Screenshot_20230814_073252_Instagram.jpg
 
Liverpool imeachwa kwenye mataa baada ya kiungo nyota wa Southampton, Romeo Lavia, 19, kudaiwa atatimkia Chelsea mara baada ya miamba hiyo kumalizana juu ya usajili wa nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji na The Blues itaweka mezani Pauni 55 milioni.
.
Inadaiwa pia miamba hiyo ya Jiji la London, imefikia makubaliano binafsi na Lavia ambaye mkataba wake Soton ulikuwa umalizike mwaka 2027. Lavia ameondolewa kwenye mipango ya Soton msimu huu na hiyo ni ishara ya wazi ataondoka na lengo likiwa ni kupewa muda wa kujitafakari na kuchukua maamuzi kwani anasakwa na timu nyingi Ulaya.
.
Liverpool ilikuwa inamtaka Lavia ili kuziba mapengo yaliyopo eneo la kiungo baada ya kuondokewa na baadhi ya mastaa wao ikiwemo Fabinho na Jordan Henderson. Lavia ni miongoni mwa mastaa walioonyesha kiwan-mgo bora msimu uliopita na alicheza mechi 35 za michuano yote na kufunga bao moja.
Screenshot_20230814_073515_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom