Makapuku Forum

Makapuku Forum

BAADA ya kuwepo kwa sintofahamu kwa mashabiki wa Simba kuona winga wao fundi KRAMO AUBIN anasugua benchi, taarifa za ndani ya Simba zinaeleza kuwa mchezaji huyo amekuwa akiugua ghafla siku chache kabla ya mchezo.

Pamoja na changamoto hiyo, inaelezwa Kramo haimfanyi ashindwe kutimiza majukumu yake anapokuwa mazoezini na amekuwa akionyesha kiwango bora.
Screenshot_20230817_155520_Instagram.jpg
 
Uongozi wa Mtibwa Sugar kwa kushirikiana na baadhi ya wadau umekaa kikao na kutoa motisha katika timu yao ili ifanye vizuri na kuepuka kichapo leo dhidi ya Mnyama .
.
Katika kikao hicho kilichofanyia viongozi pamoja na wadau wametoa ahadi ya sh 20milioni endapo watapata Ushindi dhidi ya Simba.
Screenshot_20230817_155632_Instagram.jpg
 
Kuelekea kwenye mchezo wao wa kwanza hatua ya awali ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya ASAS ya Djibouti, Kocha wa Yanga Miguel Gamondi amewaongezea dozi ya mazoezi wachezaji wake.
.
Gamondi juzi alibadili mazoezi ya timu asubuhi kwa kuwapeleka wachezaji ‘Gym’ na baadae jioni wakafanya mazoezi ya uwanjani.
.
Akizungumza: “Tunataka ushindi, nataka kila mchezaji awe fiti kimwili, tutakuwa tukifanya mazoezi mara mbili kwa siku kadhaa tukianzia Gym, kikubwa tunataka ushindi,” alisema Gamondi.
.
“Tunaanza na Asas FC, tunahitaji matokeo mazuri kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea hatua inayofuata, Katika mchezo uliopita dhidi ya Simba tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukuzifanyia kazi, lazima niweke mambo sawa kwa sababu kuna michezo mingi mbele yetu lazima tuwe vizuri kila idara.”
Screenshot_20230817_155730_Instagram.jpg
 
“Tukutane msimu ujao. Dirisha limefunguliwa. Unatazamiwa kuwa msimu mgumu lakini bado nawapa nafasi zaidi Yanga.

Wanacheza kitimu hasa. Kikosi chao hakijabadilika sana lakini hata wageni wao wamekuja kutia nguvu zaidi kikosini. Tatizo lao linaweza kuwa ukosefu wa mabao ya Mayele.” Edo Kumwembe [via Mwanaspoti]

Screenshot_20230817_155823_Instagram.jpg
 
Serikali imesema kuendelea kuuza korosho ghafi nje ni kupeleka ajira nje Watanzania, utajiri wa Wakulima na mapato ya Tanzani, hivyo ifikapo mwaka 2026/2027 korosho zote zinazozalishwa nchini zitabanguliwa hapahapa Tanzania na kuondokana na kuuza korosho ghafi nje ya Nchi.

“Kuendelea kuuza korosho ghafi nje ni kupeleka ajira zetu, utajiri wa wakulima wetu na mapato ya nchi yetu, hili hatuwezi kulikubali na lazima lifike mwisho ifikapo mwaka 2026/2027, ni lazima tuhakikishe zaidi ya tani 300,000 zinabanguliwa nchini kwa mwaka ikiwa ni pamoja na kukamua maganda ya korosho hizo”

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde @anthonymavunde amesema hayo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho mwaka 2023 “Dhamira na shabaha ya Serikali yetu chini ya uongozi mahiri wa Mh. Dkt.Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha zao la korosho linachangia kuongeza ajira na kipato kwa wakulima kupitia uongezaji wa thamani

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mariam Ditopile @mariam_ditopile amesema juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kilimo zinaonyesha utayari wake kuiletea maendeleo Sekta ambapo ametaja moja ya maeneo ambayo Rais Samia ameweka nguvu ni kuongeza Bajeti ya kilimo kila mwaka.
Screenshot_20230819_072311_Instagram.jpg
 
Wakili Boniface Mwabukusi na Mwanaharakati Mpaluka Nyagali (Mdude) wameachiwa kwa dhamana ya Central Police, Jijini Mbeya baada ya kukaa mahabusu kwa takribani siku tano.

Philip Mwakilima ambaye ni Wakili wa Mwabukusi na Mdude, amesema Watuhumiwa hao wawili wamebadilishiwa mashtaka kutoka Uhaini kuwa Uchochezi na watatakiwa kuripoti tena Kituo cha Polisi Jumatatu August 21,2023.
Screenshot_20230819_072406_Instagram.jpg
 
Marais wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika (SADC), wameridhia kupeleka Wanajeshi wa kikosi cha kulinda amani Mashariki mwa Congo.

@DW_Kiswahili imeripoti kuwa mkutano huo wa Luanda, Angola, Marais wa Jumuiya ya SADC wamepewa taarifa kuhusu hali ya usalama Mashariki mwa Congo na kuidhinisha kutumwa kwa Wanajeshi wa Nchi za SADC huko Jimbo la Kivu.

Taarifa ya pamoja ya mkutano huo imesema Marais wa SADC wamesisitiza wito wao wa kuimarisha uratibu na uwianishaji wa mipango ya amani Mashariki mwa Congo baina ya pande nne husika ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Nchi za Afrika ya Kati na Kongomano la Nchi za Maziwa Makuu ICGLR.

Marais hao wa jumuiya ya SADC wamempongeza pia Rais wa Angola, Joao Lourencou, katika juhudi zake za upatanishi baina ya Congo na Rwanda ili kutatua mzozo wao kwa njia ya amani.
Screenshot_20230819_072508_Instagram.jpg
 
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Balozi Dkt Wilbroar Slaa ameachiwa kwa dhamana ya Polisi Oysterbay, Kinondoni, Jijini Dar es salaam leo August 18,2023 baada ya kukaa mahabusu kwa takribani siku tano kutokana na makosa mbalimbali yanayomkabili.

Tayari Dkt. Slaa ametoka Kituo cha Polisi na amefikia nyumbani kwake.
Screenshot_20230819_072556_Instagram.jpg
 
Kundi la Taliban limewahimiza Wanawake nchini Afghanistan kufunika nyuso zao wakiwa nje ya nyumba zao huku likisema Mwanamke akiwa uso wazi thamani yake inashuka.

@DW_Kiswahili imeripoti kuwa Msemaji wa Wizara muhimu katika Serikali ya Taliban huko Afghanistan amesema Wanawake hupoteza thamani pale Wanaume wanapoziona nyuso zao zilizofunuliwa hadharani.

Amesema kidini Wasomi nchini humo wanakubaliana kwamba Mwanamke ni lazima afunike uso wake akiwa nje ya nyumba.

Molvi Mohammad Sadiq Akif, Msemaji wa Wizara ya Taliban yenye kuhusika na masuala ya jamii amesema ikiwa nyuso za Wanawake zitaonekana hadharani kuna uwezekano wa kusababisha fitina au kuanguka katika dhambi.
Screenshot_20230819_072705_Instagram.jpg
 
Nyota wa zamani wa Arsenal, Theo Walcott amestaafu soka akiwa na umri wa miaka 34 na kufichua kwamba alikuwa na ofa nyingi mezani , lakini akaamua kuzipiga chini.
.
Winga huyo aliamua kutundika daruga kufuatia Southampton kushuka daraja msimu uliopita na sasa atakuwa bize na maisha mengine nje ya soka kama uchambuzi wa soka.
.
Walcott alihusishwa na uhamisho wa kujiunga na Reading inayoshiriki Ligi Daraja Kwanza, lakini alifichua kuwa alikataa ofa kutoka Saudi Arabia na timu kubwa nyingine Ulaya.
Screenshot_20230819_072800_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom