Makapuku Forum

Makapuku Forum

LIONEL Messi amesisitiza hakutaka kuondoka Barcelona na akajiunga na Paris St-Germain kufuatia tofauti iliyotokea kati yake na klabu hivyo kutimkia Ufaransa na sasa anafurahia maisha akiwa na Inter Miami.
.
Mkali huyo mara saba wa tuzo ya Ballon d’Or alijiunga na Inter Miami sehemu ambayo amepiga hatua kwani katika mechi sita amefunga mabao tisa. Na katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari akiwa mchezaji wa Inter Miami, Messi alifichua siri alitamani kuendelea kuichezea Barcelona, lakini alilazimishwa kuondoka katika klabu yake ya utotoni 2021 kutokana na matatizo ya uchumi.
.
Alipoulizwa ana furaha kiasi gani tangu alipojiunga na Inter Miami, Messi alisema: “Nina furaha kwa sababu kuna mechi ya fainali ambayo itaendeleza furaha yangu zaidi. Nilichagua kuja hapa na ulikuwa uamuzi ambao tulifanya kwa wakati. Hatukufanya uamuzi huu kwa haraka, nilifikiria ndio maana mambo yakaenda sawa pande zote mbili.“
Screenshot_20230819_072847_Instagram.jpg
 
UWEZEKANO wa kipa wa zamani wa Manchester United, David De Gea kujiunga na Bayern Munich umekwama, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ujerumani.
.
De Gea bado hajapata timu tangu alipoondoka Old Trafford baada ya mkataba wake kumalizika Juni, mwaka huu huku taarifa zikiripoti kocha Thomas Tuchel wa Bayern Munich alikuwa akimtaka. Imeripotiwa miamba hiyo ya Ujerumani ilimhusisha De Gea kuchukua nafasi ya Manuel Neuer aliyekuwa nje ya dimba kutokana na majeraha.
.
Lakini kwa mujibu wa mwandishi mmoja wa kituo cha televisheni cha Sky Sports, Bayern haitamsajili De Gea licha ya kuonyesha nia. Wakati huohuo taarifa nyingine ziliripoti Bayern ilishindwa masharti ya De Gea kwani anataka mshahara mkubwa.
Screenshot_20230819_072941_Instagram.jpg
 
Watu zaidi ya 7 wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Kirikuu kugongana uso kwa uso na gari la polisi eneo la Dachi Kona, Kijiji Cha Wiri, Wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Timbuka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema wanafuatilia majeruhi wengine ambao wamewahishwa hospitali ili kujua hali zao.

Hata hivyo, taarifa zilizotufikia muda huu kutoka ofisi ya DC huyo, zinaonyesha kuongezeka kwa idadi ya watu waliopoteza maisha.

"Idadi ya waliopoteza maisha imeongezeka na kufukia watu 10 na amepatikana majeruhi mmoja ambaye hali yake inaendelea vizuri," amesema DC Timbuka.

DC Timbuka amesema miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni dereva aliyekuwa akiendesha gari la polisi ambaye amefariki papo hapo.

Amesema 9 waliopoteza maisha walikuwa wamepanda Kirikuu ikiwa imebeba mizigo wakiwa wanaenda mnadani eneo la Ngarenairobi ambapo tairi la mbele la gari hilo lilipasuka na kusababisha kupoteza mwelekeo na kwenda kugongana na gari la polisi lililokuwa likitokea uelekeo wa Ngarenairobi.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Siha.

Screenshot_20230819_073133_Instagram.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Spika Mstaafu, Anne Makinda, kuwa Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Agosti 18, 2023; na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu; imesema uteuzi huo unaanza mara moja.

Screenshot_20230819_073225_Instagram.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Aman Abeid Karume, Rais mstaafu Zanzibar, kuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Agosti 18, 2023; na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu; imesema uteuzi huo unaanza mara moja.

Screenshot_20230819_073314_Instagram.jpg
 
Messi alipoulizwa kuhusu Ballon d’Or nyingine msimu huu amesema !

"Siku zote nasema kuwa hii ni tuzo ambayo ina maana kubwa sana katika soka na ni moja ya tuzo bora kwa mtu binafsi, lakini sikuwahi kuipa umuhimu kiasi hicho kwani siku zote napendelea vikombe vya klabu,Kusema kweli sifikirii hilo, kama likifika ni vizuri, kama sivyo hakuna kitakachotokea tayari nimeshinda kila kitu kwenye soka na sasa naenjoy tu."
Screenshot_20230819_073534_Instagram.jpg
 
Mshambuliaji mpya wa Inter Miami Leo Messi alikuzungumza kuhusu kujiunga kwake na Inter Miami ambapo so far ameanza vizuri tofauti na ilivyokuwa alipojiunga na PSG .

" Ninafuraha sana kucheza Inter Miami kwa sababu hili ni Chaguo langu na sio kama ilivyotokea kwenda PSG halikuwa chaguo langu”.
Screenshot_20230819_073618_Instagram.jpg
 
Kundi la Taliban limewahimiza Wanawake nchini Afghanistan kufunika nyuso zao wakiwa nje ya nyumba zao huku likisema Mwanamke akiwa uso wazi thamani yake inashuka.

@DW_Kiswahili imeripoti kuwa Msemaji wa Wizara muhimu katika Serikali ya Taliban huko Afghanistan amesema Wanawake hupoteza thamani pale Wanaume wanapoziona nyuso zao zilizofunuliwa hadharani.

Amesema kidini Wasomi nchini humo wanakubaliana kwamba Mwanamke ni lazima afunike uso wake akiwa nje ya nyumba.

Molvi Mohammad Sadiq Akif, Msemaji wa Wizara ya Taliban yenye kuhusika na masuala ya jamii amesema ikiwa nyuso za Wanawake zitaonekana hadharani kuna uwezekano wa kusababisha fitina au kuanguka katika dhambi.View attachment 2721270
mambo mdogo wangu Shunie
 
Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) amemwandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Jacob Mwambegele barua ya kumuarifu kuwepo kwa nafasi moja wazi ya kiti cha Ubunge Viti Maalum Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt Tulia ameandika barua hiyo kufuatia kupokea barua kujuzulu kutoka kwa Mbunge wa Maalum Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Bahati Keneth Ndingo juzi tarehe 17 Agosti, 2023.

Mhe. Bahati amejuzulu nafasi hiyo kwa mujibu wa lbara ya 149 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya MUungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Katika banua yake kwa Mhe. Spika, ameeleza sababu za kujiuzulu ni kuangalia namna nyingine ya kuwatumikia Watanzania katika Bunge.

“...Ninakusudia kushiriki kwenye mchakato wa Uchaguzi Mdogo wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbarali unaotarajiwa kufanyika siku za hivi karibuni." imeeleza sehemu ya barua hiyo.
Screenshot_20230819_150311_Instagram.jpg
 
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amefichua kwanini walishindwa kusajili baadhi ya wachezaji akiwemo mlinzi wa Manchester United, Harry Maguire.

Akizungumza na Wanahabari Pep amesema klabu hiyo ilimtaka beki Harry Maguire kabla hajatimkia lakini walishindwa kulipa ada iliyotakiwa kwa madai kuwa alikuwa ghali sana.

“Tulimtaka Harry Maguire na hatukumsajili kwa sababu hatukutaka kulipa ada iliyotakiwa. Tulimtaka Cucurella, hatukulipa. Tulimtaka Alexis Sánchez, hatukulipa ada iliyotakiwa.

“Mwisho wa siku tutalipa kile ambacho ni sahihi kufanya hivyo." Guardiola alisema.
Screenshot_20230819_150444_Instagram.jpg
 
Ligi Kuu England inaendelea tena leo Agosti 19, 2023 huku viwanja vitano vikitarajiwa kuwaka moto.

|| saa 11:00 jioni

Liverpool v Bournemouth
Wolves v Brighton
️Fulham v Brentford

|| saa 1:30 usiku

Tottenham v Man United

|| 4:00 usiku

Man City v Newcastle United

Mabingwa watetezi Man City watakuwa nyumbani Etihad kuvaana na Newcastle United huku Manchester United wakiwa wageni wa Tottenham Hotspur katika dimba la Tottenham, London.

Liverpool watakuwa wenyeji wa Bournemouth katika dimba la Anfield.
Screenshot_20230819_150548_Instagram.jpg
 
Padri mmoja wa katoliki na wafanyakazi kadhaa wa dayosisi kuu ya Cologne nchini Ujerumani wamegundulika kutumia kompyuta za kazini kuperuzi kurasa zenye picha za ngono.

Vyombo vya habari vya nchini Ujerumani vimeeleza kuwa kompyuta hizo zimeonyesha kuwepo kwa takribani majaribio 1,000 ya kutizama kurasa hizo jambo ambalo ni kinyume na sheria za dayosisi.

Taarifa hizo zilijulikana mwezi uliopita wakati dayosisi kuu ilipokuwa ikifanya majaribio fulani kwenye mifumo ya usalama. Majaribio hayo hayakulenga kuchunguza tabia za wafanyakazi wake.

Mmoja kati ya watu 15 waliotambulika kutembelea kurasa hizo ni Padri Mkuu.

Askofu Mkuu Rainer Maria Woelki ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa hizo na ameamuru uchunguzi wa haraka ufanyike ili kuweza kuwashughulikia wahusika.

Vilevile Askofu Woelki amesema kujulikana kwa wahusika kutasaidia kuondoa wasiwasi na kuhisiwa kwa watu wengine ambao hawahusiki.

Kutizama ponografia kwenye kompyuta za Dayosisi Kuu kulishapigwa marufuku kama ilivyozuiliwa kutizama taarifa zinazohusiana na dawa za kulevya na vurugu zinginezo.

Screenshot_20230819_150837_Instagram.jpg
 
Rais Yoweri Museveni wa Uganda jana ameikosoa kwa mara nyingine tena Benki ya Dunia kwa kusitisha misaada nchini humo na kusema kuwa taasisi hiyo inakosea kama inafikiri hatua hiyo itawatisha Waganda.

Taarifa iliyotumwa kupitia mtandao wa X imemnukuu Museveni akiita Benki ya Dunia kuwa ni ”Mwigizaji wa kibeberu asiye na kina na asiyekuwa na mipaka”

”Hatua hii ya benki ya dunia ndio itaisaidia Uganda kupunguza madeni ya nje na kujitegemea zaidi”

Museveni aliongeza kwa kusema bado nchi yake inao washirika wengi wa nchi za Magharibi lakini wametishiwa kuhusu kuendelea kuisaidia Uganda.

Wiki iliyopita Benki ya Dunia ilisitisha misaada ya Uganda kutokana na sheria kali iliyowekwa na nchi hiyo dhidi ya mahusiano ya watu wenye jinsia moja.

Akiijibu Benki hiyo wiki iliyopita Museveni alisema ”benki ya dunia inajaribu kuishinikiza Uganda kubadili sheria kwa kusitisha ufadhili, Uganda itaendelea kujiendeleza bila ya sapoti ya benki ya dunia”.

Screenshot_20230819_151028_Instagram.jpg
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Mitaala mipya #ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu itaanza kutumika baada ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 kupitishwa na Mamlaka za maamuzi ambapo rasimu iliyopo inapendekeza Watoto waliopo darasa la tatu mwaka huu wasome mpaka darasa la sita kisha waende Sekondari, badala ya kuishia darasa la saba.

Prof. Mkenda amesema hayo Jijini Dodoma ambapo amesema tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa mitaala hiyo itatangazwa baada ya kupitishwa kwa Sera hiyo na kwamba itakapopitishwa utekelezaji utaanza kwa awamu.

Mkenda amesema rasimu hiyo inapendekeza Watoto waliopo darasa la tatu Mwaka huu 2023 ndio watakaosoma mpaka darasa la sita, hivyo wale waliopo darasa la nne, tano na sita wataendelea kusoma mpaka darasa la saba.

"Hatima ya yote utekelezaji huu unategemea Mamlaka ya Nchi itakaposema tuanze, matumaini yetu ni makubwa kwamba rasimu hii itapita na siku ya kutangazwa kuanza kwa utekelezaji itakuwa ni siku kubwa katika kuelekea mageuzi ya elimu nchini"
Screenshot_20230819_151133_Instagram.jpg
 
Mamlaka nchini Kenya zimeyafuta Makanisa matano likiwemo kanisa la Mshukiwa aliyewachochea zaidi ya Waumini wake 400 kufunga hadi kufa.

Msajili wa Mashirika nchini humo katika notisi iliyowekwa kwenye gazeti la Taifa amesema leseni ya Muhubiri Paul Nthenge Mackenzie wa kanisa la Good News International Ministries ilifutiliwa mbali kuanzia Mei 19 huku kutokula kukionekana ndicho chanzo kikuu cha sehemu kubwa ya hao Watu 400 waliofariki Kanisani kwake japo ripoti za upasuaji zinaonyesha wengine wakiwemo Watoto walinyongwa, kupigwa au kubanwa pumzi hadi kufa.

Mamlaka zimeyafutilia mbali Makanisa mengine 4 pia likiwemo la New Life Prayer Centre and Church lake mhubiri Ezekiel Odero ambaye amehusishwa na Mackenzie na sasa anachunguzwa kwa mashtaka kadhaa yakiwemo mauaji, itikadi kali na utakatishaji fedha.
Screenshot_20230819_151245_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom