Farhan Jr
Kila anachokifanya Tajiri MO kwenye page zake inawachanganya sana watu, MO anaweza kuja Insta na kulalamikia kitu na wote wakaamini Simba sio shwari lakini MO anatoa mzigo mfukoni analeta wachezaji ndani ya Simba, hapo ndipo anawachanganya zaidi.
Mpaka sasa kuna MO wawili, kuna MO wa Instagram na Twitter, huyo ni MO tofauti na wa taasisi, huyu wa mitandaoni ataandika anachotaka na atavuruga anavyotaka ila MO Taasisi ana watu ambao wanafanya maamuzi on behalf ambao hawana shida na MO wa Instagram na Twitter.
Huyu MO wa mitandao ya Kijamii ana msaada mkubwa sana kwa Simba, MO huyu ataileta attention kwake hata pale timu ikicheza vibaya ama kuna kitu hakipo sawa, kumjadili yeye unaipa nafasi timu kurecover na kuendelea! MO wa Insta anampa nafasi MO wa taasisi utulivu wa kufanya vitu.
MO wa Insta ananikumbusha Tajiri wa PAOK aliyetoa silaha uwanjani tena hadharani, stori haikuwa tena timu kupoteza bali tukio la Tajiri, ananikumbusha Perez alivyoona mambo hayaendi kabisa akajiuzulu 2006 akaitoa pressure kwenye timu akaondoka nayo.
Nguvu za kutomuelewa Tajiri zihamishiwe kwenye suala la kwanini mchakato haukamiliki wa mabadiliko, zihamie kwanini watu hawanunui merchandise za klabu na hawalipii card! MO anaeleweka hata pale ambapo Mashabiki hawataki kueleweka kwa kutimiza wajibu wao! Kuna ubaya anapiga na kulipa?
The game of spinning! Tajiri MO ananikumbusha Matajiri na dunia yao! Matajiri wengine hufanya wenyewe na wengine hutuma watu kufanya kwa niaba yao! Dunia ya kitaasisi inahitaji akili sana kuielewa.