Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,906
Farhan Jr
Zipo wapi nyakati? Wakati ambao Dr Leakey Abdallah anaichukua Roma, Italia ama Venice Mji Ua mpaka sebuleni ama bandani kwako, zipo wapi nyakati wakati Fundi huyu alikuwa anaufanya mpira uvutie kuufuatilia hata kama hujawahi kufika Ulaya, zipo wapi nyakati?
Zipo wapi nyakati nauliza? Wakati mpira tunatazama kwenye nyungo kubwa za wavu? Wakati huo DTV, ITV na baadae Channel 10 tunatulia Champions League! Usiku wa maajabu ya kutisha pale Istanbul, Uturuki penye Etugru sasa hivi! Nyakati ambazo saa 3:45 Usiku wenye baiskeli, wenye tochi za Kaida na betri za National wanasaka kijiji chenye TV watazame mbungi.
Zipo wapi nyakati? Ambapo Mbalamwezi inamulika kuangaza njia za Wapenzi wa soka kufika bandani, milio ya Tembo na Simba lakini sauti za Wahafidhina wa Liverpool wakiimba Fields of Anfield Road zilivutia zaidi, wakati huo Ricardo Kaka anapiga pass kuliko Dobi, zipo wapi nyakati kipindi Andrea Pirlo anakupa Wema Sepetu mbele ya TV yako?
Gone are the days! Wakati Nemanja Vidic anacheza huku anavuja damu, aliwahi kuvunjika Mtu pale Anfield anaitwa Bill Shankly na aligoma kukaa kwenye machela, aliwaambia ni aibu uzi wa Liverpool na Mwanaume kutoka Liverpool kubebwa juu ya kitanda, zipo wapi nyakati?
Zipo wapi nyakati wakati Legend Edo Kumwembe anatawala Ukurasa namba 17 za nyuma ya pazia akimuelezea TH14 Babu Choggo kutoka visiwa vilivyosahaulika La Desarade? Kalamu ilishikwa na ikamwaga wino mzuri kama ambavyo Dada mwenye hamu atashika kalamu ili itoe wino mweupe, ziko wapi nyakati?
Zipo wapi nyakati? Baada ya kutoka bafuni na picha ya @thebestfetty unaenda darasani kutazama daftari lako ulojaza picha za Wababe kama Taribo West, Jay Jay Okocha, Dinho Gaucho, The Original Ronaldo ama Samuel Etoo, zipo wapi nyakati?
Zipo wapi nyakati wakati Cristiano Ronaldo anafunga ndoa na mabeki pale EPL mpaka Ashley Cole aliketi, zipo wapi nyakati za usiku wa baridi kali pale Stoke City, unamtazama Delap ama Shawcross wamekunja sura, wapi Blackburn ya Benjani Mwaruwari ama Wigan ya Amri Zaki? Zipo wapi nyakati? Kabla ya kizazi cha pressing, overlapping na 4-4-2 Diamond

️
"Tulimsajili Emile Heskey kwa pauni milioni 11, Arsene Wenger alimsajili Thierry Henry kwa pauni milioni 11. Tulimsajili Nick Barmby kwa pauni milioni 6, Arsenal wakamsajili Robert Pires kwa pauni milioni 6. Wenger alikuwa gwiji katika soko la usajili." alisema Jamie Carragher kuhusu tofauti kati ya Liverpool na Arsenal.
Edouard Mendy
Roberto Firmino
Riyad Mahrez