Makapuku Forum

Makapuku Forum

73779335-12354459-image-a-103_1690751442655.jpg

Tumeanza kukusanya kimojakimoja
 
Jezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan imeuzwa kwa Sh. 10,000,000 katika mnada maalum wa kibegi pamoja na jezi zilizopelekwa kileleni mwa Mlima Kilimanjaro uliofanyika katika Ofisi za Azam TV.

Jezi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango imeuzwa kwa TSh. 3,000,000 kwa Sandland Omary 'Sandland The Only One', Jezi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi imeuzwa Tsh. 5,000,000 kwa Hasa Clearing and Forwarding.

Jezi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa imeuzwa kwa Sh. 4,000,000 kwa S & Sons LTD na Jezi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson imeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Tawi la Simba Makini .

Jezi ya Rais wa Heshima wa klabu, Mohamed Dewji 'Mo' @moodewji imeuzwa Sh. 2,000,000 na Duka la Vifaa la Michezo la Romario Sports na Kibegi kilichokuwa na jezi na kupelekwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kimeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Saleh Majapa.
Screenshot_20230801_050836_Instagram.jpg
 
Aliyewahi kuwa DJ wa CloudsFM Steven Mdoe maarufu kama DJ Steve B amefariki dunia leo katika Hospitalini Dar es salaam huku chanzo kikitajwa kuwa ni kupanda kwa presha.

Amstrong Mdoe ambaye ni Kaka wa Marehemu ameiambia @AyoTV_ kuwa Steve B ambaye alikuwa akisumbuliwa na figo toka mwaka 2019 alipelekwa Hospitali juzi na kuwekwa ICU baada ya presha kupanda na baadaye kupanda zaidi na kumsababishia kupoteza fahamu kwa siku tatu kabla ya kufariki.

"Steve B alipoteza fahamu kwa siku 3 ambapo jioni ya leo saa 10 akafariki, alikuwa na tatizo la figo kwa miaka minne tangu 2019 lakini figo sio chanzo cha kifo chake, taratibu za mazishi bado tunazungumza tupange utaratibu lakini tunapokea rambirambi kwa namba 0678689383"

"Steve hakuwa na Mke wala hajaacha Mke na wala Mtoto, hatuna taarifa za Mtoto wake" ——— amemalizia Armstrong Mdoe. #TutaonanabaadaeSTEVEB
Screenshot_20230801_050959_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa @kissagwakisakasongwa ameagiza Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Iringa pamoja na Taasisi nyingine zinazohusika na wanyamapori wanaowatafuta Simba waliovamia katika Mji wa Makambako na kujeruhi pamoja na kuua mifugo kuhakikisha wanawatafuta na kuwapata wakiwa hai au wamekufa.

DC Kissa amesema hayo wakati akitoa salamu za Serikali kwenye kikao cha Baraza la Madiwani robo ya nne na kufunga mwaka 2022-2023 cha Halmashauri hiyo ambapo pia ametoa wito kwa Wananchi kuchukua tahadhari huku pia akiwaomba kuwasha moto karibu na mabanda ya mifugo kwa kuwa Simba wamekuwa wakiogopa moto.

"Nimepata taarifa kuwa nguvu kutoka TAWA imeongezwa na wanafanya kila jitihada kuhakikisha hao wanyama (Simba) wanakamatwa, ombi langu kwa Wananchi ni kuchukua tahadhari na niwatoe hofu kwamba Serikali jambo hili tunalishughulikia na nimeshatoa maagizo kwamba Simba wapatikane wakiwa hai au wakiwa wamekufa"

Awali Madiwani wa Halmashauri hiyo akiwemo Navy Sanga, Salum Mlumbe pamoja Hanana Mfikwa wamesema kuwa Wananchi wamekuwa na taharuki kubwa na kupelekea kushindwa kwenda kwenye shughuli zao huku pia Madiwani wengine wakiomba Wananchi jamii ya Mang'ati watumiwe kwa mkuwa wana utaalamu wa kuua Simba.
Screenshot_20230801_051114_Instagram.jpg
 
Klabu ya Simba leo Jumatatu, Julai 31, 2023 imefanya mnada wa kibegi na jezi zilizopandishwa Mlima Kilimanjaro kwa Sh29 milioni.

Jezi hizo za msimu wa mashindano 2023/24, zilizinduliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro Julai 21, 2023.

Jezi hizo za aina tatu ambazo zimepigwa mnada ni zenye majina ya viongozi, Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi.

Pia, kuna ya Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Fedha zilizopatikana katika mnada huo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Taifa ya Zanzibar (Mnazi Mmoja).
Screenshot_20230801_051244_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Kanda ya Magharibi imekamata lita 106,000 za mafuta ya dizeli yaliyokuwa kwenye magari matatu katika kituo kimoja cha mafuta Tabora Mjini yakidaiwa kufichwa na wahusika.

Meneja wa Ewura, Kanda ya Magharibi, Walter Christopher amesema mafuta hayo wameyakamata leo Jumatatu, Julai 31, 2023 yakiwa kwenye kituo hicho kwa zaidi ya saa 24 pasipo sababu za msingi na wahusika kushindwa kutoa sababu zinazoeleweka.

Walter amesema magari hayo matatu yamecheleweshwa na wahusika kufanya uwepo wa upungufu wa mafuta wakati mafuta ya kutosheleza yapo.

"Katika kufuatilia madai ya upungufu wa mafuta, tumebaini kuna ujanja unafanyika kama huu wa kuchelewesha magari yenye mafuta," amesema

Amedai hata katika kituo cha mafuta yaliyokutwa magari yenye mafuta, kulikuwa na mafuta lita 3,000 pekee na kushangaa kwanini magari hayo pia hayakushusha mafuta hapo na kusema watachukua hatua kwa wahusika.
Screenshot_20230801_051345_Instagram.jpg
 
Shughuli ya kutafuta watu 13 waliozama ndani ya Ziwa Victoria wakitumia mitumbwi imekwama kuendelea leo Jumatatu, Julai 31, 2023 kutokana na hali mbaya ya hewa ndani ya ziwa hilo. Miongoni mwa watu hao waliozama 11 ni wanafunzi wa shule ya Msingi Igundu Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Tukio la kuzama mitumbwi hiyo miwili limetokea jana Jumapili, Ziwa Victoria wakati mitumbwi hiyo iliyokuwa na watu 28 kupigwa dhrouba na kuzama ziwani.

Watu hao walikumbwa na tukio hilo walipokuwa wakitoka Kijiji cha Mchigondo kwenda Kitongoji cha Bulomba, Kijiji cha Igundu baada ya kumaliza Ibada katika Kanisa Takatifu la Mungu wa Kiroho (KTMK) lillopo Kijiji cha Mchigondo wilayani Bunda jana Jumapili saa 12.30 jioni.

Mkuu wa wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano akizungumza na Mwananchi Digital alisema, shughuli za uokoaji zilisimama kutokana na hali ya upepo,”kwahiyo tunajaribu kadri tuwezavyo kupambana na changamoto zilizopo ili tuweze kufanikisha jambo hilo la uokoaji.”

Dk Naano alisema kazi ya kutafuta watu hao wanahofiwa kufariki dunia imekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo jiografia ya eneo husika. Ndugu, jamaa na marafiki wakati wote walikuwa ufukwe wa Kijiji cha Mchigondo kusubiri hatima ya wapendwa wao.

Hadi saa 12:00 jioni ya leo, Mwananchi Digital inaondoka ufukweni hapo, shughuli za uokoaji zilikuwa zimesimama.

Screenshot_20230801_051529_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa kwa siku tatu ambapo utabiri umeonyesha kuna uwezekano wa kutokea upepo mkali na mawimbi makubwa.

Taarifa iliyotolewa na TMA inaonyesha kuwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa kutakuwa na upepo mkali unaofikia kilomita 40 na zaidi kwa saa na mawimbi yanayofikia ukubwa wa mita 2.

Hali hii inatarajiwa kutokea katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi ikihusisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mikoa mingine ambayo inaweza kukumbwa na hali hii ya hewa ni maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria ikihusisha mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mara na maeneo ya ukanda wa ziwa Tanganyika katika mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa.

Kufuatia hilo TMA imetaka tahadhari kuchukuliwa hasa kwa wanaofanya shughuli zao baharini na ziwani wakiwemo wanaotumia njia hizo kusafiri.
Screenshot_20230801_051633_Instagram.jpg
 
46— HATTRICK pekee kwenye Derby ya Kariakoo ilifungwa na Abdallah ‘King’ Kibadeni wakati Simba ikiichakaza Yanga 6-0 mwaka 1977.

Hat-trick hiyo imedumu kwa miaka 46 sasa. Wachezaji kadhaa wamewahi kufunga mabao mawili-mawili katika Derby hiyo ila matatu ni ya King tu.
Screenshot_20230801_051808_Instagram.jpg
 
Kocha Robertinho amefunguka kuwa kambi yao ya Uturuki imekuwa na manufaa makubwa kwani sasa amepata mifumo MITATU hatari ambayo Simba inaweza kutumia katika michuano yote kwa msimu unaoanza mwezi ujao.
.
Robertinho alisema mifumo hiyo imetokana na upana wa kikosi chake kufuatia ujio wa mastaa bora ambao wamekuja na nguvu kubwa kuunganisha na wale ambao wamewakuta.

Hata hivyo Kocha huyo alikataa kuanika mifumo hiyo kwa kusema ni sawa na kuuza siri za kambi ya vita, lakini akasema ataitesti kwenye mechi ya Tamasha la Simba Day dhidi ya Power Dynamos kabla ya kuhamishia kwenye Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Screenshot_20230801_051914_Instagram.jpg
 
KIPA wa Yanga, Djigui Diarra ametakiwa kupunguza kujiamini zaidi awapo langoni jambo linaloweza kumtoa mchezoni na kujikuta akiisababishia timu yake matatizo.
.
Kocha wa zamani wa makipa wa klabu hiyo, Juma Pondamali alisema, Diarra ni kipa mzuri na anayajua majukumu yake tatizo lake kubwa ni hilo asipokifanyia kazi hatoamini kitakachomkuta.
.
“Unajua Diarra kujiamini kumezidi kipa anatakiwa kujiamini kiasi, yeye kuchezea mpira kiasi kile siku akikutana na mchezaji mjanja ataharibu CV yake maana mashabiki wake hawatamuelewa na hapo imani kwake itatoweka kabisa aliangalie sana hilo,” alisema kipa huyo wa zamani.
.
WANANCHI mnakubaliana na maoni ya Kocha la makipa ..!!
Screenshot_20230801_052332_Instagram.jpg
 
SIMBA imefanya maamuzi magumu ya kumpiga chini kipa Mbrazili Jefferson Luis aliyesajiliwa hivi karibuni kwa madai ya kuwa majeruhi. Japo klabu haijatoa taarifa lakini inaelezwa Jefferson amepata majeraha makubwa, hivyo amesitishiwa mkataba kwani atakuwa nje kwa muda mrefu.
.
Kwa mujibu wa Chanzo changu cha kuaminika kinasema kwamba Jefferson alisajiliwa huku akiwa na tatizo la misuli nyuma ya paja lililogundulika juzi mazoezini, huku jina lake likiwa tayari katika usajili wa CAF. “Ni kweli amegundulika na tatizo hilo, anaweza kukaa nje kwa muda mrefu ila siwezi kusema moja kwa moja kama mkataba utavunjwa au lah! Maana maamuzi hayajafikiwa,” kilisema chanzo changu hicho cha kuaminika.
Screenshot_20230801_052441_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom