Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan imeuzwa kwa Sh. 10,000,000 katika mnada maalum wa kibegi pamoja na jezi zilizopelekwa kileleni mwa Mlima Kilimanjaro uliofanyika katika Ofisi za Azam TV.

Jezi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango imeuzwa kwa TSh. 3,000,000 kwa Sandland Omary 'Sandland The Only One', Jezi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi imeuzwa Tsh. 5,000,000 kwa Hasa Clearing and Forwarding.

Jezi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa imeuzwa kwa Sh. 4,000,000 kwa S & Sons LTD na Jezi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson imeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Tawi la Simba Makini .

Jezi ya Rais wa Heshima wa klabu, Mohamed Dewji 'Mo' @moodewji imeuzwa Sh. 2,000,000 na Duka la Vifaa la Michezo la Romario Sports na Kibegi kilichokuwa na jezi na kupelekwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kimeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Saleh Majapa.
View attachment 2704336
Mmmmmmmmh!
 
Baada ya JORDAN HENDERSON kutimkia Saudi Arabia sasa ni rasmi klabu hiyo imemtangaza beki wa kati VIRGIL VAN DIJK kama nahodha mpya wa kikosi hicho.

Kuna heshima kubwa sana ya kuvaa usinga wa unahodha ndani ya Liverpool kwani ni timu ambayo kuna bond kubwa na nzuri kati ya manahodha na mashabiki wa klabu hiyo ya huko kwenye viunga wa Merseyside.

Baada ya Steven Gerrard na Jordan Henderson sasa ni rasmi mlinzi huyu wa kimataifa wa Uholanzi atakuwa nahodha mpya wa klabu hiyo ya Marco Mzumbe.

Virgil Van Didjk atakuwa nahodha mkuu lakini msaidizi wake atakuwa mlinzi wa pembeni anayeweza pia kutumika kama kiungo wa kati, TRENT ALEXANDER ARNOLD.

Nahodha mpya wa majogoo wa jiji
Screenshot_20230801_052727_Instagram.jpg
 
Chelsea wamekubali makubaliano ya kimsingi na Rennes kumsajili Lesley Ugochukwu!
Ada ya karibu €27m kwa kiungo wa Ufaransa aliyezaliwa 2004 - hakuna uamuzi kama atabaki au kuondoka kwa mkopo
Screenshot_20230801_052850_Instagram.jpg
 
BREAKING: Napoli wamekataa ofa ya takriban €140M kutoka kwa Al Hilal kwa ajili ya mshambuliaji Victor Osimhen. Ofa mpya inatarajiwa hivi karibuni kulingana na L'Equipe.
Screenshot_20230801_052955_Instagram.jpg
 
Imefahamika kuwa Chelsea na Barcelona ndo vilabu vinavyofanya kazi kwa bidii zaidi kwa kuweka mchezaji pamoja na pesa kumnunua nyota wa Paris St Germain Kylian Mbappe. Vyanzo vya karibu na PSG vimedai kuwa mmiliki wa The Blues Todd Boehly anajaribu kutengeneza Ofa.

Screenshot_20230801_053044_Instagram.jpg
 
Ikiwa imesalia masaa 9 tu kipengele cha mkataba wake kuruhusu kununulia kwa €50m, Ousmane Dembélé amejitokeza kuiomba Barca 'ruhusa' rasmi ya kufanya mazungumzo na PSG Dembélé anataka kufuata hatua zote sahihi kujiunga na PSG.
Screenshot_20230801_053140_Instagram.jpg
 
Chelsea wamekamilisha usajili wa Axel Disasi - Makabidhiano ya mkatab kati ya vilabu yamekamilika

◉ Mkataba wa miaka mitano, chaguo hadi 2029.
◉ Chelsea italipa €45m kwa Monaco.
◉ Vipimo vya afya - mapema wiki ijayo.
◉ United na Newcastle walimtaka ila hawakuweka ofa.

Screenshot_20230801_053306_Instagram.jpg
 
Baada ya kutambulishwa na klabu yake mpya ya Pyramids mshambuliaji wa Zamani wa Yanga Fiston Kalala Mayele amesema kwa aina ya usajili ambao Yanga wameufanya msimu huu wanaweza kutetea ubingwa na kubeba makombe yote.

Screenshot_20230801_053440_Instagram.jpg
 
Anasema katika maisha yake amecheza dabi nyingi kabla ya kuja Yanga na timu zenye mashabiki wa kutosha, ila mechi ya watani wa jadi anaiona ni ya tofauti kwa namna inavyochukuliwa na jamii.

"Kwanza kama mchezaji ni muoga unaweza ukaogopa kucheza mechi na ukadanganya unaumwa, kwani matangazo ni mengi ambayo yanakuwa yanaleta presha kubwa sana, kwa upande mwingine ni mechi ambayo mchezaji mkubwa inakupa heshima ya kuonyesha ukubwa wako.

"Changamoto nyingine tangu nilipojiunga na Yanga tumeifunga Simba mara nyingi,viongozi walikuwa na raha kila mmoja anamsifia mchezaji, siku ambayo tumefungwa kila mmoja anaingilia mlango wake, baadhi wanakwenda mbali zaidi kuwatuhumu wachezaji kama wamechukua pesa upande wa pili jambo ambalo siyo kweli, kikubwa unapuuza."

"Mimi binafsi yalinikuta tulipopoteza dhidi ya Simba nilisikia Kuna kelele kwamba nimechukua fedha lakini kwakuwa sio kweli hazikunisumbua kichwani kwangu niliziacha na kuendelea na kazi yangu."

Anazitaja timu ambazo amecheza zina dabi na mashabiki wengi ambazo ni FC Les Stars, Motema Pembe na AS Vita za nchini kwao Congo na FAR Rabat ya Morocco.

"Pamoja na hayo mkifungwa mashabiki na viongozi walichukulia ni moja ya matokeo, ila huku ni tofauti kidogo, lazima utasikia Bangala hajakaba vizuri, kipa kafanya kile,"anasema.
Screenshot_20230801_053538_Instagram.jpg
 
Chelsea wamekamilisha usajili wa Axel Disasi - Makabidhiano ya mkatab kati ya vilabu yamekamilika

◉ Mkataba wa miaka mitano, chaguo hadi 2029.
◉ Chelsea italipa €45m kwa Monaco.
◉ Vipimo vya afya - mapema wiki ijayo.
◉ United na Newcastle walimtaka ila hawakuweka ofa.

View attachment 2704362
Safiii 👍
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom