Wafuasi wa Kiongozi wa upinzani nchini humo, Laila Odinga wamejikuta katika wakati mgumu baada ya maandamano yao kupigwa mabomu ya machozi huku baadhi yao wakikamatwa na Polisi katika maeneo mbalimbali nchini Kenya.
Polisi huko Nyahururu walimkamata aliyekuwa Gavana wa Laikipia, Ndiritu Muriithi na mwanasiasa wa Jubilee Carolyne Mwendia kwa madai ya kushiriki maandamano haramu.
Mapema asubuhi ya leo, baadhi ya waandamanaji waliifunga barabara kuu ya Thika na kufanya isipitike baada ya kuziba sehemu za barabara katika hoteli moja ya kitalii kwa kuwasha moto, japo baadaye waandamanaji hao walitawanywa na barabara kufunguliwa.
Mjini Mombasa, polisi walirusha mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa upinzani walioandaa maandamano katika barabara ya Moi Avenue.
Seneta wa Mombasa Mohammed Faki, Mwakilishi wa Wanawake, Zamzam Mohammed na Mbunge wa Mvita Machele Mohammed waliongoza waandamanaji kuandamana hadi katikati mwa jiji hilo.
Katika mtaa wa Kimathi jijini Nairobi, kundi la waandamanaji walilazimika kukimbia ili kujilinda baada ya maafisa wa polisi kuwarushia vitoa machozi.
Hata vivyo sehemu nyingi za Nairobi, zilibaki tulivu huku wenyeji wakiendelea na biashara zao kama kawaida.
Akiwa Kamukunji, Odinga aliwaongoza wafuasi wake katika kuwakumbuka wote waliopigania mfumo wa vyama vingi nchini humo akiwataja Kenneth Matiba, Joseph Murumbi, Jaramogi Oginga Odinga na yeye mwenyewe.
"Leo haitakuwa kama siku nyingine. Tuliwaambia wakome kuingilia vyama vyetu. Sasa, wabunge 25 wa Jubilee na saba kutoka ODM wamepelekwa UDA," alisema.
View attachment 2681587