Makapuku Forum

Makapuku Forum

STAA wa Arsenal, Gabriel Jesus alifanya uamuzi wa kuachana na Manchester City baada ya kocha Pep Guardiola kumfanya amwage machozi kwa kilio.
.
“Kulikuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG nyumbani, na hapo Oleksandr Zinchenko alichezeshwa Namba 9. Vitu vya ajabu sana. Siku moja kabla, wala hakumtumia Zinchenko mazoezini, aliniweka mimi kama straika. Zinchenko alithubutu hata kunikejeli, kwamba ile siku alijisikia vibaya kwa ajili yangu.
.
“Saa mbili kabla ya mechi, kwenye mazungumzo ya timu, muda wakula. Alituambia timu itakavyokuwa, sikula,” alisema Jesus. “Nilikwenda moja kwa moja vyumbani na kuanza kulia, nilimpigia simu mama yangu na kumwambia: ‘Nataka kuondoka.’ Narudi nyumbani kwa sababu amemtumia Zinchenko si mimi, amemtumia beki wa kushoto kwenye fowadi. Nilivurugwa.
.
“Nilikuwa na mambo mengi sana na Guardiola na sio rahisi. Magumu sana. Sitaki kusema zaidi.” Jesus alielezea licha ya kutokea benchi na kuonyesha kiwango bora ikiwamo kufunga bao la ushindi, lakini bado alitupwa benchi kwenye mechi iliyofuatia dhidi ya RB Leipzig.
Screenshot_20230708_150224_Instagram.jpg
 
MANCHESTER United inakumbana na ugumu katika kumpiga bei Harry Maguire kutokana na kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wa beki huyo.
.
Man United inahitaji kuuza baadhi ya mastaa ili kuongeza bajeti ya usajili dirisha hili. Lakini, baada ya kumaliza nafasi ya tatu Ligi Kuu England msimu uliopita na kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, hapo ndipo unapoibuka ugumu wa kumuuza Maguire.
.
Kwenye mkataba wa Maguire kuna kipengele kinafichua endapo timu itapata mafanikio ya aina hiyo, basi atalazimika kuongezewa mshahara. Na hapo ugumu unakuja kwamba ili aondoke atalazimika kupunguza mshahara kitu ambacho kinawapa ugumu mabosi wa Man United kumshawishi beki huyo.
.
Maguire, 30, mkataba wake utafika tamati 2025 na kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja. Ripoti zinaeleza beki huyo yupo kwenye rada za klabu za West Ham, Tottenham na Newcastle.
Screenshot_20230708_150420_Instagram.jpg
 
Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), limemchagua Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga SC Simon Patrick kuwa Mwanasheria wa FIFA anayeshughulikia masuala ya migogoro ya Wachezaji Duniani kote kwa kipindi cha miaka mitatu.
Screenshot_20230709_052658_Instagram.jpg
 
NMB Bank imesema haijapokea maagizo au maelekezo yoyote ya kufunga akaunti za baadhi ya Wateja wake na kutaka taarifa hizo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zipuuzwe kwa kuwa hazina ukweli wowote.

Taarifa rasmi ya @nmbtanzania imesema "Uongozi wa Benki ya NMB unapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa haujapokea maelekezo kutoka kwa Mtu yeyote ya kufunga akaunti ya Mteja yeyote, tunawahakikishia Wateja wetu na Jamii kwa ujumla kwamba tutaendelea kusimamia taratibu zote za kibenki ikiwa ni pamoja na kulinda taarifa za akaunti za Wateja wetu"

Taarifa hiyo imemalizia kwa wito wa Benki hiyo kuwataka Wateja wake kuendelea kufurahia huduma zake za kibenki kupitia matawi yake yote, Mawakala pamoja na Internet Banking.
Screenshot_20230709_052812_Instagram.jpg
 
Kijana aitwaye Hassan Ally Mnali (32) Mkazi wa Mtaa wa Jamhuri, kata ya Msinjahili, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi amefariki baada ya kujinyonga usiku ikidaiwa kuwa kabla ya kujiua alikuwa akilalamika kuna Watu wanamvuruga.

Ndugu wa Marehemu wanasema hawafahamu sababu ya kujinyonga lakini mdogo wa marehemu Rashid Ally Mnali anasema kuwa kaka yake hakuwa sawa kiakili kwa madai kuna Watu wanamvuruga.

Shuhuda wa tukio hilo Salma Stambuli anasema alishtushwa usiku na kelele za Mama wa Marehemu akimtaka kufika Nyumbani kwake kumpatia msaada ambapo baada ya kufika alimkuta Hassan ameshafanya maamuzi hayo.
Screenshot_20230709_052911_Instagram.jpg
 
Mawaziri sita, watatu wa Tanzania na watatu upande wa Zambia wamefanya kikao Jijini Dar es salaam na kuingia makubaliano ya kuongeza na kuimarisha ulinzi wa bomba la mafuta la TAZAMA kutoka Dar es salaam hadi Ndola Zambia.

Baada ya makubaliano hayo, Mawaziri hao wameongea na Waandishi wa Habari na kusema wamefikia hatua hiyo baada ya bomba hilo kubadilishiwa matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi mpaka kusafirisha mafuta safi ya dizeli (diesel) lengo likiwa ni kudhibiti kujitokeza kwa matukio ya uhalifu wa wizi wa mafuta kwenye bomba hilo.

Mkutano huo uliandaliwa na Wizara ya Nishati, chini ya Waziri wa Nishati January Makamba @jmakamba na kuhudhuriwa na Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Innocent Bashungwa.

Kwa upande wa Zambia alikuwepo Waziri wa Nishati wa Zambia Mhandisi Peter Kapala, Waziri wa Ulinzi wa Zambia Ambrose Lufuma na Waziri wa Mambo ya Ndani Jacob Mwiimbu.
Screenshot_20230709_053009_Instagram.jpg
 
Aliyekuwa beki wa Bayern Munich Jerome Boateng na winga wa timu ya taifa Ufaransa na Klabu ya Bayern Munich Kingsley Coman wametembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Boateng raia wa Ujerumani na mshindi wa Kombe la Dunia 2014 wakiifunga Argentina bao 1-0 ambapo kwa sasa anacheza soka la kulipwa katika klabu ya Lyon inayoshiriki Ligue 1 ya Ufaransa na kabla ya hapo alikua akisakata kabumbu na miamba wa Ujerumani Bayern Munich.

Screenshot_20230709_053111_Instagram.jpg
 
Muda mfupi baada ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja kumtimua uanachama kada wake Balozi Ali Abeid Karume, yeye amesema bado hajapata barua ya kutimuliwa.

Amesema taarifa hizo naye amezisikia na kuziona kwenye mitandao ya kijamii, hivyo atakuwa kwenye nafasi nzuri kuzungumza jambo hilo baada ya kupokea barua ya kutimuliwa kwake uanachama katika chama hicho kikongwe nchini.

“Nasubiri barua kabla ya kujibu,” amesema Balozi Karume.

Screenshot_20230709_053209_Instagram.jpg
 
Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation (BMF), imezindua rasmi maadhimisho ya kumbukizi ya maisha na kazi za Hayati Benjamin William Mkapa.

Mkapa aliyefariki Julai 23, mwaka 2020 alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mwanzilishi wa taasisi hiyo.

Taarifa iliyotumwa na BMF, leo Jumamosi Julai 2023, imesema kumbukizi hii imeanza Julai 1 na itadumu kwa mwezi wote.

“Julai unajulikana kama mwezi wa kumbukumbu ya kazi, utumishi na yale mema aliyoyaamini na kuyaishi Hayati Mkapa na kauli mbiu ya kumbukizi kwa mwaka huu ni "Kuongeza Chachu ya Uendelevu katika Upeo Mpya",”imesema taarifa hiyo.

Screenshot_20230709_053309_Instagram.jpg
 
Serikali imesema ndege aina ya Airbus A220 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyokuwa ikishikiliwa nchini Uholanzi imeachiwa na kurejea nchini jana.

“Leo niko hapa kuwapa habari njema, siku chache zilizopita niliwajulisha kuna ndege yetu tulikuwa na kesi nchini Uholanzi ikakamatwa, ilikuwa chini ya mikono ya sheria. Bahati nzuri tumefanya mazungumzo na jambo limekwenda vizuri ndege yetu imerudi jana jioni iko Tanzania,” amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipozungumza na waandishi wa habari leo Julai 8, 2023 mjini Arusha.

Amesema ndege hiyo inaendelea kuandaliwa ili ianze shughuli zake.

“Chuma kimerejea kiko Tanzania, tunaendelea kuimarisha shirika letu, mambo yetu yatakuwa yaanaendelea kuwa mazuri,” amesema Msigwa aliyezungumzia masuala mbalimbali, ikiwamo miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo tofauti nchini.
Screenshot_20230709_053928_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi, amewataka vijana wilayani humo kujikwamua na tatizo la ajira kwa kutumia fursa nyingi za mikopo zinazotolewa na Serikali ya awamu ya sita.

Matinyi ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo mapema mwezi huu akichukua nafasi iliyoachwa na Mwanahamisi Munkunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Akitoa salamu zake katika semina ya uongozi na itifaki ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani hapo leo Julai 8, Matinyi amesema vijana wanastahili kudumisha amani na kuweka bidii katika shughuli za kiuchumi ili kuitikia mwito wa serikali wa kupunguza tatizo la ajira nchini.

Amesema fursa za mikopo zinazotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan zinawalenga zaidi vijana ambao ni nguzo muhimu ya uchumi katika taifa letu.

Ametoa mwito kwa vijana wanaotaka kuzijua fursa hizo kufika katika ofisi za wilaya ili waelimishwe.
Screenshot_20230709_054031_Instagram.jpg
 
Askari Polisi mmoja aliyetambulika kwa jina la Michael Kyalo amejiua kwa kujipiga na risasi baada ya kumjeruhi mkewe kwa risasi huko Kaunti ya Bondo nchini Kenya mapema leo, Polisi wameripoti.

Kamanda wa Polisi wa kaunti hiyo Ibrahim Kosi amesema afisa huyo aliyefariki, aliripoti kazini kama kawaida jana, Ijumaa Julai 7 ambapo baadaye aliondoka na bunduki.

Hata hivyo, badala ya kuelekea eneo alilopangiwa, Kyalo alitembea hadi nyumbani kwake ambapo kisa hicho kilitokea Jumamosi asubuhi.

Polisi wamesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea huku wakihusisha ufyatuaji huo wa risasi unatokana na msongo wa mawazo kazini.

Screenshot_20230709_054249_Instagram.jpg
 
Polisi nchini Kenya wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutawanya msafara wa Jaji mkuu wa zamani Willy Mutunga baada ya kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Nairobi, akitaka kuachiliwa huru kwa waandamanaji waliokamatwa jana.

Jaji huyo wa zamani alikuwa ameenda katika kituo hicho kufuatilia wanaharakati waliokamatwa wakati wa maandamano ya Saba Saba yaliyoitishwa na Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini humo, Raila Odinga jana Ijumaa.

Imeelezwa kuwa Jaji Mutunga ameshirikiana na wanaharakati na wanansheria akiwemo Kamishna wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya Victor Kamau na Wakili Lempaa Soyinka ambao waliweka kambi kituoni hapo kutaka kuachiliwa bila masharti kwa raia 32 ambao walikamatwa kwa kushiriki maandamano ya Saba Saba jana.

Screenshot_20230709_054359_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom