Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230703_055115_Opera%20Mini.jpg
 
OFFICIAL & CONFIRMED:
.
Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji hatari raia wa Cameroon Leandre Onana kwa Mkataba wa miaka miwili.
.
Onana ndiye kinara wa mabao Ligi Kuu ya Rwanda msimu uliopita akikipiga Rayon Sports.

Screenshot_20230705_161025_Instagram.jpg
 
Mabosi wa Yanga wameshtukia baada ya kutibuliwa dili la kiungo Fabrice Ngoma sasa Wamepokea simu kutoka DR Congo kuna Vigogo wazito wa Simba wameweka mzigo mezani wanataka kumaliza dili la yule winga Maxi Nzengeli ambaye anaichezea Maniema.
.
Siyo huyo tu hata yule jezi namba 6 wa Asec ambaye Yanga wanamtaka Simba wamemvutia waya. Hii si mara ya kwanza kwa klabu hizo kongwe kuingiliana kwenye ishu za usajili kwani rekodi zinaonyesha licha ya kutokiri hadharani lakini matukio kama hayo yamekuwa yakijirudia kila msimu wa usajili.
.
Simba ambayo inakusanyana Dar es Salaam tayari kwa safari ya kambini Uturuki, baada ya kupata faili la winga huyo wakatua kama mwewe na kuanza kupiga hesabu za kuwatibulia watani wao katika dili hili na wakamwekea mzigo mrefu mezani.
Screenshot_20230705_161130_Instagram.jpg
 
DODOMA Jiji imeanza usajili kwa kishindo na sasa imemsajili mshambuliaji wa Kagera Sugar na Taifa Stars, Meshack Abraham.
.
Mbali na huyo, awali timu hiyo ilisajili wachezaji kadhaa akiwemo beki wa kushoto kutoka Coastal Union, Gustavo Simon.
.
Kiongozi mmoja wa Dodoma Jiji ambaye hakutaka kutajwa jina amenidokez timu hiyo imetoa fedha za maana kupata huduma za wachezaji hao ambao walikuwa wakihitajika na timu nyingi za Ligi Kuu.
Screenshot_20230705_161257_Instagram.jpg
 
Wakati Yanga wakitamba kwamba kuna kitu jezi namba 6 kinatua kushtua nchi, imevuja hawajamalizana na mido jezi namba 6 wa Asec, Mohamed Zougrana ambaye Simba wamemwekea mkataba mezani.
.
Zougrana ambaye alionyesha uwezo wa juu kwenye michuano ya Caf msimu uliopita amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga lakini Wekundu hao wako naye mezani kuanzia wikiendi iliyopita wakipambana naye.

Zougrana ni kiungo aliyepiga kazi kubwa kwenye eneo la kati la ASEC wakiiishia nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na ubora wa kupiga pasi na hata kufunga.
Screenshot_20230705_161408_Instagram.jpg
 
01—MSIMU ujao wa 2023/24 katika Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga utaanza kwa mechi kati ya Werder Bremen na Bayern Munich. Ikiwa ni mechi 112 kuzikutanisha timu hizo hadi sasa na ndio mechi iliyochezwa zaidi katika historia ya Bundesliga tangu ianzishwe miaka 59 iliyopita.
Screenshot_20230705_161455_Instagram.jpg
 
Usiniite Mfalme, Niite Daudi: Kisa cha Daudi na mke wa Uria-1

Siku moja Mfalme Daudi alikuwa ana barizi kwenye paa la hekalu lake. Kama wanavyosema waswahili macho hayana pazia. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Mfalme Daudi. Macho yake yakatua kwa binti mmoja mrembo, aliyekuwa bafuni anaoga. Kwa sekunde kadhaa mwili wa Daudi ulikufa ganzi. Hakuamini kama aliyekuwa anamuona alikuwa ni mtu kweli au malaika.

Daudi akatuma wapambe wake. Wapambe hawakuchelewa. Wakarudisha jibu.
"Mfalme yule binti uliyemuona ni mtu kweli. Na ni mke wa mtu." Mpambe alimueleza Mfalme Daudi.
"Mke wa mtu?" Mfalme Daudi aliuliza kwa mshangao
"Ndio Bwana wangu. Ni mke wa Uria. Uria Mhiti. Yule mpiganaji wako hodari." Mpambe alimjibu Daudi.

Daudi alikuwa na kikosi cha watu 37. Hawa walikuwa wapiganaji hodari wa mfalme. Na Uria alikuwa ni mmojawapo. Wakati huu Uria alikuwa vitani.

"Hakikisha jioni unamleta kwangu " David aliongea kwa sauti nzito, kisha akageuka na kuondoka. Mpambe akainama na kuondoka pia.

Jioni ya siku hiyo yule mpambe akafanya kama alivyoagizwa na Mfalme. Daudi ni Mfalme wa pili wa Israel. Alichukuwa uongozi kutoka kwa Mfalme Sauli.

"Unaitwa nani mama", Mfamle Daudi alimuuliza yule mwanamke mrembo aliyemuona siku kadhaa zilizopita akiwa anaoga.

"Naitwa Bethsheba Bwana wangu" yule mrembo alijibu huku ameinamisha kichwa chake chini.

"Niite Daudi mrembo, usiniite Bwana wangu," Daudi alimwambia huku akimshika kichwa

"Sawa Daudi" mke wa Uria aliitikia.

Huwezi kuamini Daudi mwenye nguvu. Daudi mpakwa mafuta wa Mungu. Yule aliyemuuwa Goliath kwa kombeo. Sasa alikuwa mdogo. Mdogo zaidi ya piriton. Hapa hata angeombwa himaya yote ya Israel angeikabidhi kwa huyu kiumbe Bethsheba

Kwa kifupi Daudi alikuwa mateka. Alikuwa mateka kwa Bathsheba. Daudi alikuwa amekufa, alikuwa amekufa ameoza.

Jioni ya siku hiyo Daudi akafanikiwa kulala na mke wa Uria. Baada ya siku kadhaa mke wa Uria akarudi.

"Daudi sioni siku zangu" mke wa Uria akamwambia na kuongeza
"Nimepitiliza wiki mbili sasa"

Daudi akamuangalia kisha akasema
"Usiogope, nina jua cha kufanya"
"Si unajua mme wangu yuko vitani, sijakuatana nae zaidi ya mwezi sasa" mke wa Uria alimwambia Mfalme Daudi.

Itaendelea.....
Screenshot_20230705_201306_Instagram.jpg
 
OFFICIAL & CONFIRMED:
.
Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa Mshambuliaji hatari AUBIN KRAMO ( @kramo_aubin ) kutoka Asec Mimosas kwa Mkataba wa miaka miwili.
.
Kramo (27) raia wa Ivory Coast ana uwezo wa kucheza winga zote mbili na kucheza namba 10.
Screenshot_20230707_151909_Instagram.jpg
 
Kupitia mitandao ya kijamii ya Goree ya Senegal ilitoa barua ya kusikitishwa na kilichofanywa na Azam kwa kumtangaza mshambuliaji Allasane Diao, huku akiwa bado ana mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo.
.
“Kwa kukumbushana US Goree inapenda kudokeza mchezaji Alassane Diao, bado ana mkataba na klabu yetu na hakuna mazungumo yoyote yaliyoanzishwa na Azam FC kuhusu kumuachia,”
.
“Kwa kuheshimu maandishi yanayosimamia soka, Goree inasisitiza dhamira yake ya kufuata sheria za uhamisho zilizowekwa na FIFA na kuhakikisha maslahi ya klabu na wachezaji chini ya mkataba.”
Screenshot_20230707_152031_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom