Makapuku Forum

Makapuku Forum

Che Fondoh Malone ni Mnyama

Mkataba: Miaka mitatu. Ada iliyolipwa: USD $100,000 sawa na TSH 241.5M. Atajiunga na klabu hiyo wiki ijayo wakijiandaa na msimu mpya. Che alikuwa kipaumbele kwenye list ya Simba. Simba sasa itahamia kwenye kipaumbele kingine: Golikipa.

Che Malone amesajiliwa kama mbadala wa Mohamed Ouattara na sio Onyango kama wengi wenu mlivyodhani. [MickyJr]

Screenshot_20230702_052608_Instagram.jpg
 
JUST IN: Klabu ya Yanga ilimpa Fiston Mayele ofa ya tatu Kumuongezea mshahara kutoka $ 9000 (Sh 21M) hadi $ 15,000 (Sh 36M) lakini staa huyo amechomoa ikielezwa bado amepagawa na ofa nono kutoka Esperance, Pyramids na Zamalek.

NB: Mazungumzo yanaendelea ili kupata muafaka.
Screenshot_20230702_052700_Instagram.jpg
 
Kiungo wa Singida Fountain Gate FC @bruno_barroso97 akiwa nchini kwao Brazil wakati huu wa mapumziko baada ya kumalizika kwa msimu Ligi Kuu, amefunga pingu za maisha na mpenzi wake
Screenshot_20230702_053013_Instagram.jpg
 
Juan Mata ametangaza kuachana na Galatasaray baada ya msimu mmoja nchini Uturuki.

Mata amefunga mabao matatu na kutoa asisti tatu katika mechi 18 za klabu na kuisaidia timu yake kushinda ubingwa wa Uturuki .
Screenshot_20230702_053226_Instagram.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Aliyekuwa Kiungo wa timu ya taifa ya Hispania ,klabu ya Arsenal, Barcelona, Chelsea na Monaco Cesc Fabregas ametangaza rasmi kustaafu soka lake la ushindani akiwa na miaka 36 akiwa Como
Screenshot_20230702_053314_Instagram.jpg
 
Shaffih Dauda

SEHEMU YA PILI

Watu wa Marekani wakaona thamani ya Ligi ya England duniani, wakakubaliana hii ni sehemu sahihi ya kuwekeza. Wakatengeneza mpango kazi wa namna ya kuingiza mpira wa miguu nchini kwao kwa kwao si mchezo pendwa mbele ya American Football, basketball na baseball!

Ndipo walipoamua kuanzisha Major League Soccer [MLS], na wao ili kuifanya Ligi yao iwe maarufu wakatumia mbinu kama zilizotumiwa na England [kuchukua wachezaji wenye majina makubwa] lakini wao pia wana malengo ya kutengeneza timu ya taifa imara.

Kwa hiyo wanachukua wachezaji wenye majina ili kuamsha soko lakini pia kuvutia vijana wadogo kuingia kwenye soka lakini vilevile kuvutia wawekezaji kuwekeza kwenye miundombinu.

Leo Marekani wakiia timu ya taifa karibu nusu ya wachezaji wanatoka Ulaya tena kwenye timu kubwa zinazoshiriki Ligi kubwa! Maana yake wamefanikiwa.

Kwa sasa mchezo wa soka umeshakuwa maarufu Marekani, sasa wafanya biashara wenye nguvu Marekani waliokuwa wamewekeza kwenye michezo mingine [American Football na Basketball] wameingia kwenye soccer.

Kama haitoshi wamepenya na kuingia hadi Ulaya na kuanza kuzinunua timu, leo hii mmiliki wa Man United ni raia wa Marekani, mmiliki wa Liverpool ni raia wa Marekani, Arsenal ukiangalia wamiliki wa hisa nyingi miongoni mwao ni raia wa Marekani ukienda Ufaransa!

Kwa miaka ya hivi karibuni mataifa ya kiarabu ni wapinzani wa Marekani kwenye masuala ya biashara na uchumi! Na wao wameanza kuingia kwenye soka.

Waarabu wao wameanzia juu kwa maana ya wawekezaji kuanza kununu klabu [PSG, Man City, Newcastle Unite], sasa hivi wameamua kuacha athari chanya kwenye klabu za mataifa yao.

Kwa hiyo wameanza kupeleka watu kwenye nchi zao kwa ajili ya kujenga mifumo na kutengeneza timu zao na mpira wao ili kushambulia kwenye kiwanda hiki ambacho kinaonekana kimechangamka kwenye biashara na kina zidi kukua.

Saudi Arabia ni nchi yenye utajiri mkubwa utokanao na mafuta na gesi kwa hiyo miaka kadhaa ijayo tutaona matokeo ambayo sio wao tu watanufaika bali watu wengi duniani

DIGALA .
Screenshot_20230702_053407_Instagram.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo July 02, 2023 amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Wilaya ambapo ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Rais Samia ametengua pia uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama na amemhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Hashim Shaib Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, pia amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga.
Screenshot_20230703_045008_Instagram.jpg
 
Mtibwa Sugar U-20 wamefanikiwa kutwaa Ubingwa kwa mara ya 5 mfululizo wa Ligi Kuu ya Vijana Tanzania (U-20) baada ya kuwafunga Geita Gold U-20 kwa goli 1-0.
Screenshot_20230703_045420_Instagram.jpg
 
Ubalozi wa Tanzania nchini China umesema kumekuwa na matukio ya Watanzania wanaosafiri kwenda Hong Kong kuzuiliwa kuingia au kuhojiwa kwa muda mrefu na maafisa wa Idara ya Uhamiaji ya Hong Kong katika uwanja wa ndege wa Hong Kong ambapo hali hiyo imejitokeza zaidi hivi karibuni tangu Hong Kong ifungue mipaka yake kuruhusu Wageni baada ya miaka mitatu ya zuio la kuingia Hong Kong kwa ajili ya udhibiti wa Covid 19.

“Hatua hizo za Mamlaka za Hong Kong zimetokana na matukio ya siku za nyuma ambapo Watu wachache waliokuwa na passport ya Tanzania kufanya vitendo vya uvunjivu wa sheria, March 30 2023 Ubalozi umewasiliana na Mamlaka za Hong Kong kueleza kutoridhishwa na hatua hiyo inayochukuliwa na Maafisa wa Uhamiaji wa Hong Kong, Mamlaka za Hong Kong zilitujibu kwamba Maafisa wao watatekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa mujibu wa sheria na wametoa rai kwa Wasafiri wanaokwenda Hong Kong kuwa na nyaraka zote zinazohitajika”

“Ubalozi unatoa rai kwa Watanzania wenye safari ya kwenda Hong Kong wahakikishe wana mwaliko kutoka kwa Mwenyeji wa abiria ambaye anaweza kuwa Mtu binafsi au Kampuni, tiketi ya ndege yenye tarehe ya kuondoka Hong Kong, Booking ya Hoteli inayoonesha jina la Msafiri, kuepuka kuvunja sheria za Hong Hong kwa kubeba vitu/bidhaa ambazo ni kinyume na sheria”

“Endapo mtanzania yeyote atahitaji msaada au ufafanuzi zaidi awasiliane na Ubalozi kwa barua pepe: beijing@nje.go.tz au kwa simu kwa Afisa Ubalozi: +86 136 9336 0750 (Number hiyo haitumii whatsup- piga moja kwa moja)
Screenshot_20230703_045713_Instagram.jpg
 
Mfalme wa Uholanzi Willem-Alexander ameomba msamaha wa kihistoria kwa Uholanzi kuhusika katika utumwa na ukoloni akisema ameathirika yeye binafsi tena kwa kiasi kikubwa kwakuwa Familia ya kifalme haikufanya chochoe kuzuia utumwa.

Maelfu ya vizazi vya Watumwa kutoka Taifa la Amerika Kusini la Suriname na Visiwa vya Karibea vya Aruba, Bonaire na Curacao walihudhuria sherehe hiyo Amsterdam jana Jumamosi ambapo ilifanyika kwa lengo la kuvunja minyororo katika Surinamese na kuadhimisha miaka 150 tangu desturi hiyo kusitishwa.

“Leo nimesimama hapa mbele yenu kama Mfalme wenu na kama sehemu ya Serikali, leo naomba msamaha binafsi, ninayasema haya kwa moyo na roho yangu”

Itakumbukwa Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte tayari aliomba msamaha rasmi mwezi Desemba kwa niaba ya Serikali kuhusu utumwa, tangu vuguvugu la Black Lives Matter lilipoibuka nchini Marekani, Uholanzi imeanzisha mjadala mgumu mara kwa mara kuhusu ukoloni na biashara ya Watumwa ambayo iliigeuza kuwa moja ya Nchi tajiri zaidi duniani.

Waholanzi walifadhili "Enzi ya Dhahabu" yao ya himaya na utamaduni katika karne ya 16 na 17 kwa kusafirisha karibu Waafrika 600,000 kama sehemu ya biashara ya Watumwa, wengi wao wakiwa Amerika Kusini na Karibea.
Screenshot_20230703_045954_Instagram.jpg
 
PICHA: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo J. Kidata wameshiriki Bonanza la michezo la TRA na Wafanyabiashara wa Kariakoo lengo likiwa kuboresha afya, mahusiano bora na kuhamasisha utoaji risiti za EFD.
Screenshot_20230703_050133_Instagram.jpg
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Wakuu wa Wilaya (DC) wawili wa Temeke na Kilindi na kuteua wengine kushika nyadhifa hizo.

Taarifa ya utenguzi, imetolewa usiku wa Jumapili, Julai 2, 2023 na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Screenshot_20230703_050323_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom