Makapuku Forum

Makapuku Forum

Ubalozi wa Tanzania nchini China umesema kumekuwa na matukio ya Watanzania wanaosafiri kwenda Hong Kong kuzuiliwa kuingia au kuhojiwa kwa muda mrefu na maafisa wa Idara ya Uhamiaji ya Hong Kong katika uwanja wa ndege wa Hong Kong ambapo hali hiyo imejitokeza zaidi hivi karibuni tangu Hong Kong ifungue mipaka yake kuruhusu Wageni baada ya miaka mitatu ya zuio la kuingia Hong Kong kwa ajili ya udhibiti wa Covid 19.

“Hatua hizo za Mamlaka za Hong Kong zimetokana na matukio ya siku za nyuma ambapo Watu wachache waliokuwa na passport ya Tanzania kufanya vitendo vya uvunjivu wa sheria, March 30 2023 Ubalozi umewasiliana na Mamlaka za Hong Kong kueleza kutoridhishwa na hatua hiyo inayochukuliwa na Maafisa wa Uhamiaji wa Hong Kong, Mamlaka za Hong Kong zilitujibu kwamba Maafisa wao watatekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa mujibu wa sheria na wametoa rai kwa Wasafiri wanaokwenda Hong Kong kuwa na nyaraka zote zinazohitajika”

“Ubalozi unatoa rai kwa Watanzania wenye safari ya kwenda Hong Kong wahakikishe wana mwaliko kutoka kwa Mwenyeji wa abiria ambaye anaweza kuwa Mtu binafsi au Kampuni, tiketi ya ndege yenye tarehe ya kuondoka Hong Kong, Booking ya Hoteli inayoonesha jina la Msafiri, kuepuka kuvunja sheria za Hong Hong kwa kubeba vitu/bidhaa ambazo ni kinyume na sheria”

“Endapo mtanzania yeyote atahitaji msaada au ufafanuzi zaidi awasiliane na Ubalozi kwa barua pepe: beijing@nje.go.tz au kwa simu kwa Afisa Ubalozi: +86 136 9336 0750 (Number hiyo haitumii whatsup- piga moja kwa moja)View attachment 2676778
Tzn hawaaminik kokote dunian
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth Gwajima amevitaka vyombo vya habari na jamii kumpa staha na utulivu mwanafunzi wa kidato cha tano Shule ya Sekondari Panda hill, Ester Noah.

Ester ambaye alitoweka shuleni hapo Mei 18 mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha na kupatikana Juni 23, 2023 mara baada ya agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutaka uongozi wa Mkoa wa Mbeya chini ya Mkuu wa Mkoa Juma Homera kumtafuta.

Dk Gwajima ameyasema hayo leo Jumapili, Julai 2, 2023 kupitia kurasa zake za kijamii za Twitter na Instagram akihamasisha jamii kuwa na mipaka na jambo hilo.
“Shukrani waliowezesha kumpata Ester. Naiomba jamii tumpe nafasi aendelee na maisha mapya badala ya kila saa yuko mitandaoni. Hata kama ni zaidi ya miaka 17, bado anahitaji staha na utulivu. Maofisa ustawi watampa ushauri nasihi. Kila la Heri Ester, mengine tuachie vyombo vya haki,” ameandika katika mtandao wake wa Twitter.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dk Gwajima ametoa shukrani na kusihi kuwa taarifa za awali kuhusu Ester zimepatikana na zimeshakusanywa, hivyo hakuna budi jamii kumuacha aendelee na maisha na si kuhojiwa maisha yake binafsi.

“Hata kama umri wake umevuka utoto, lakini ni Mtanzania anayehitaji staha, utulivu. Hivyo nimeelekeza maofisa ustawi wamefikie wampe ushauri nasihi kwani anayo nafasi ya kuanza ukurasa mpya wa historia yake na safari yake ya maisha,”amesema.

Screenshot_20230703_050522_Instagram.jpg
 
Ubalozi wa Tanzania nchini China umewataka Watanzania wanaosafiri kwenda katika Jiji la Hong Kong kukamilisha taratibu za safari zao, ikiwemo barua ya mwaliko kutoka kwa mwenyeji ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Julai 2, 2023 na ubalozi huo imetaja taratibu nyingine ni pamoja na tiketi ya abiria itakayoonyesha tarehe ya kuondoka Hong Kong na ‘booking’ ya hoteli inayoonesha jina la msafiri, tarehe ya kuingia na kutoka.

Utaratibu huo umetolewa baada ya baadhi ya Watanzania wanaosafiri kwenda Hong Kong kuzuiwa kuingia jijini humo au kuhojiwa kwa muda mrefu na maofisa wa idara ya uhamiaji katika uwanja wa ndege.

Hatua hizo za mamlaka za jiji la Hong Kong zimetokana na matukio ya siku za nyuma ambapo baadhi ya watu wachache waliokuwa na hati za kusafiria za Tanzania kufanya vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Hali hiyo imejitokeza zaidi katika kipindi cha hivi karibuni baada ya Hong Kong kufungua mipaka yake kuruhusu wageni kuingia ikiwa ni miaka mitatu ya zuio la eneo hilo ajili ya udhibiti wa maambukizi ya Uviko-19.

Katika taarifa hiyo, ubalozi wa Tanzania, umesema kutokana na kadhia hiyo Machi 30, 2023 uliwasiliana na mamlaka za Hong Kong kueleza kutoridhishwa na hatua inayochukuliwa na maofisa wa uhamiaji wa jiji hilo ya kutaka kila mwenye hati ya kusafiria ya Tanzania kuhojiwa kwa muda mrefu na wengine wachache kurejeshwa.
Screenshot_20230703_050645_Instagram.jpg
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema abiria wote wako salama na hakuna majeruhi yeyote katika ajali iliyotokea eneo la Mlima Kitonga kufuatia basi la Kampuni ya New Force kupinduka na kulalia upande mmoja.

Ajali hiyo imetokea leo saa 3:30 asubuhi Julai 2, 2023 ambapo basi hilo aina ya Zhongtong lilikuwa limebeba abiria 57 likitokea mkoani Iringa kuelekea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Kamanda Bukumbi amesema basi hilo lilipinduka na kuegama pembezoni mwa barabara wakati dereva akiyapita mabasi mengine yaliyokuwa yanateremka katika mlima huo yakiwa kwenye foleni.

“Watu wote wako salama na hakuna majeruhi yeyote na hakuna mali nyingine zilizoharibika na kinachofuata tunapima ajali na kuchukua hatua stahiki kwa dereva huyu na mmiliki kuja kuondoa gari lake eneo la tukio,”amesema.

Kamanda amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kwa kung’ang’ania kupita mazingira ambayo hakutakiwa kupita huku akijua eneo hilo kuna mteremko mkali na magari yanapita kwa foleni
Screenshot_20230703_051207_Instagram.jpg
 
Dereva wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Lusajo Makiwelu anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kummwagia kemikali mtalaka wake, Witness Nguvalwa (31) na mtoto wake mwenye umri wa miezi sita.

Tukio hilo lilitokea Juni 27, wakati mwanamke huyo na mtoto wake wakiwa wanasubiri daladala eneo la Maghorofani, jijini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo alipozungumza na Mwananchi Juni 29, 2023 na kusema wanamshikilia dereva huyo kama mshukiwa baada ya mtu asiyejulikana kufanya tukio hilo.

"Mtuhumiwa tayari ametiwa mbaroni, kwa sasa tunaendelea na mahojiano," alieleza Kamanda Otieno.

Akizungumza akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Witness ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Idedelomkazi wilayani Mufindi Mkoa wa Iringa, alisema mkasa huo ulimkuta aliposhuka kituo cha Maghorofani akitokea Mafinga mkoani Iringa alipokuwa akisubiri usafiri wa kumpeleka atakapofikia.

Alisema alikuja Dodoma kuleta wito wa Mahakama ya Mwanzo Mafinga kwa aliyekuwa mumewe ambaye walitenganishwa na mahakama hiyo.

"Nilifika kituo cha mabasi Maghorofani niliposhuka kusubiri daladala au bajaji ili niende kukabidhi wito huo,” alisema.
Screenshot_20230703_051332_Instagram.jpg
 
Vijana wengi wamejikita kufanya ujasiriamali, licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki, ikiwamo ukosefu wa maeneo rasmi ya kuendesha shughuli zao.

Kutokana na hali hiyo, baadhi yao hulazimika kufanya shughuli hizo kando mwa barabara na maeneo mengine yasiyopangwa na mamlaka husika licha ya Serikali kuweka katazo.

Maeneo mengine wanakofanyia biashara ni juu ya mitaro na mifereji, barabara za waenda kwa miguu, hifadhi ya barabara na mengine ya taasisi za Serikali na shule, hivyo kuleta usumbufu kwa wananchi na mali zao.

Septemba 2021, Rais Samia Suluhu Hassan aliwaagiza wakuu wa mikoa nchini kuwapanga wajasiriamali hao maarufu kama machinga katika maeneo stahiki bila kusababisha vurugu.

Licha ya utekelezaji wa agizo hilo, sasa wamerejea kwenye maeneo walikoondolewa, huku baadhi ya watu wakijitengenezea mazingira ya kujipatia kipato kutoka kwa wafanyabiashara hao kwa kuwapangisha katika maeneo rasmi na yasiyo rasmi.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa wiki moja kwa machinga kurudi kwenye maeneo walikohamishiwa badala ya kupanga bidhaa barabarani.

Screenshot_20230703_051448_Instagram.jpg
 
Mwaka 1972, katika sherehe za miaka 10 ya Tanganyika, Rais Julius Nyerere hakushuka chini kuzikagua Timu za Taifa za Tanzania na Sudan na kumwachia jukumu hilo Rais wa Sudan, Jaafar Nimeiry.
.
Kitendo hicho kilitokea Desemba 9, mwaka huo baada ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania kuingia uwanjani wakiwa vifua wazi. Ni kipa tu Omary Mahadhi ndiye aliyevaa jezi ya juu, lakini wachezaji wote walivaa bukta tu.
.
Jezi za Timu ya Taifa zilisahaulika, hadi wakati wa mapumziko ndipo wachezaji hao walivaa jezi zao.
Screenshot_20230703_051716_Instagram.jpg
 
KMC iko kwenye mazungumzo ya kumpata kiungo wa Namungo, Lucas Kikoti ili akaichezee timu hiyo msimu ujao.
.
Kocha wa KMC, Jamhuri Kihwelo Julio ametoa pendekezo la mchezaji huyo kwa sababu anataka kuungana naye tena kwani walishawahi kufanya kazi pamoja wakati akiifundisha Namungo.
.
Wakati KMC ikihitaji saini ya Kikoti, tayari imewasajili Juma Shemvuni aliyekuwa anaichezea Mbeya City iliyoshuka daraja, Muhsin Malima (Dodoma Jiji) na Rodgers Gabriel aliyetoka Pamba FC.
Screenshot_20230703_051853_Instagram.jpg
 
Uongozi wa GEITA GOLD umeweka wazi itaachana na Mastaa 10 ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao, huku miongoni mwa waliofyekwa ni Mjapan Shinobu Sakai Shimo.
.
Wachezaji waliopewa ‘Thank You’ ni; Fabrice Kayemba, Arakaza MacArthur, Shown Oduro, Mussa Gadi, Jeremiah Thomas, Daniel Lyanga aliyetua JKT Tanzania na Mjapani Shinobu Sakai ‘Shino’. Shinobu alijiunga na timu hiyo mwaka jana na kubeba matumaini makubwa kwenye kikosi hicho ingawa ameshindwa kupigania namba huku ikielezwa yuko mbioni kujiunga na Tokyo International ya nchini kwao
Screenshot_20230703_052406_Instagram.jpg
 
KOCHA wa zamani wa Azam FC, Abdihamid Moallin amepewa mkataba na Coastal Union kuupitia kabla ya kutoa majibu na kuusaini ili kuchukua mikoba ya Fikiri Elias aliyeachwa.
.
Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo kimeniambia kuwa Moallin aliomba kwanza kupitia mkataba huo kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho, huku akipewa kutoa majibu Jumatano ya Julai 5.
Screenshot_20230703_052530_Instagram.jpg
 
Baada ya KMC kujihakikishia kucheza Ligi Ku msimu ujao, viongozi wa timu hiyo wametenga bajeti ya Sh1 bilioni ambazo zitatumika kwa ajili ya usajili wa mastaa wengine wapya.
.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa KMC, Christina Mwagala amefunguka kuwa baada ya kusuasua msimu uliopita wameamua kuwekeza kiasi hicho cha fedha ili kutengeneza kikosi imara.
.
“Mkurugenzi wetu, Hanifa Suleiman Hamza hataki kuona timu ikipitia kile ilichopitia ndio maana bajeti imekuwa ni kubwa zaidi ya msimu uliopita ambao tulitenga Sh700 milioni,” alisema Mwagala.
Screenshot_20230703_052648_Instagram.jpg
 
Mashabiki wa Chelsea wanataka beki Reece James atangazwe kuwa nahodha mpya wa kikosi hicho. Hilo linakuja baada ya mashabiki kufurahishwa na namna beki huyo alivyojibu twitter ya shabiki wa Arsenal aliyetoa wazo kuhusu usajili wa James
.
James aliwakosha zaidi mashabiki wa Chelsea kutokana na namna alivyojibizana na shabiki wa Arsenal baada ya kuona Havertz amevua uzi wa Chelsea na kuvaa wa The Gunners aliandika kwenye twitter; "Reece James kwenda Arsenal, nani atasema hapana? Kitu kilichovutia, ni James aliyejibu na kuandika; "Nasema Hapana."
.
Ukurasa maalum wa Chelsea ulipost picha ya James akishangilia mbele ya Mashabiki wa Arsenal na kuandika; "Kijana wetu wenyewe,"Na Hapo ndipo mashabiki waliibuka wa Chelsea walimwagika na kuomba apewe unahodha.
Screenshot_20230703_052902_Instagram.jpg
 
BAADA ya kocha wa AS Roma, Jose Mourinho kuwasilisha jina lake, taarifa zinadai mchakato wa Fred kujiunga na AS Roma upo kwenye hatua nzuri na wakati wowote atasepa zake. Mourinho anadaiwa kuwa anamkubali sana Fred na yeye binafsi ndiye alifanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba kiungo huyu wa kimataifa wa Brazil anatua kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu enzi hizo akikinoa.
Screenshot_20230703_052958_Instagram.jpg
 
CHELSEA imekamilisha usajili wa straika wa Villarreal, Nicolas Jackson. Staa huyo wa kimataifa wa Senegal amesaini mkataba wa miaka minane wa kuitumikia The Blues baada ya uhamisho wake wa Pauni 30 milioni.
.
Jackson alikuwapo kwenye kikosi cha Senegal kilichokuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar.
Screenshot_20230703_053057_Instagram.jpg
 
Dili la Declan Rice la kung’oka West Ham United na kutua Arsenal linachukua muda wa kukamilika baada ya timu hizo mbili kushindwa kuafikiana kwenye mtindo wa malipo.
.
West Ham wameshakubali kumpoteza kiungo huyo matata kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Arsenal wamejiweka pazuri kwenye mchakato wa kunasa saini yake baada ya kuweka mezani ofa ya Pauni 105 milioni, wakidai watatanguliza kulipa Pauni 100 milioni na Pauni 5 milioni zilizobaki zitalipwa baadaye kulingana na maendeleo ya uwanjani ya staa huyo.
.
Lakini, West Ham wanaweka ngumu wakitaka mkwanja wote uwe umemalizwa hadi kufikia mapema 2025, wakati Arsenal wanahitaji kulipa pesa hiyo katika kipindi cha miaka mitano.
Screenshot_20230703_053242_Instagram.jpg
 
Thank You! Umtiti:

Barcelona imethibitisha kusitisha mkataba wa beki Samuel Umtiti baada ya pande mbili kuafikiana. Umtiti, 29, alijiunga na Barca akitokea Lyon kwenye majira ya kiangazi mwaka 2016 na amecheza mechi 134 na kufunga mabao mawili katika kipindi chake alichotumikia miamba hiyo ya Hispania. Akiwa na Barca, Umtiti alishinda La Liga mara mbili na Copa del Rey mara tano.
Screenshot_20230703_053341_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom