Makapuku Forum

Makapuku Forum

CHELSEA, UNITED ZAPIGANA VIKUMBO KWA MARTINEZ
.
Manchester United na Chelsea zinapambana kuipata huduma ya kipa wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martinez, 30, katika dirisha hili la usajili barani Ulaya ili kwenda kuziba mapengo kwenye eneo hilo msimu ujao.
.
Chelsea inamtaka staa huyu akawe mbadala wa Eduardo Mendy aliyetimkia zake Saudi Arabia ambako anakwenda kukipiga katika timu ya Al Ahli, sawa na ilivyo kwa Man United ambayo inamtaka awe mbadala wa David de Gea ambaye dili lake na Mashetani hao wekundu wa Old Trafford linasuasua kukamilika.
.
Martinez amekuwa akihususishwa na timu nyingi kutokana na kiwango chake bora alichokionyesha kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar akiwa na timi ya taifa ya Argentina.

Screenshot_20230701_151159_Instagram.jpg
 
KOCHA WA PSG AKAMATWA NA POLISI
.
Kocha wa Paris St-Germain, Christophe Galtier amekamatwa na polisi kwa madai ya vitendo vya kibaguzi wakati akiwa anainoa Nice kwa mujibu wa ripoti. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56, ambaye yuko mbioni kuondoka PSG kipindi hiki cha kiangazi, aliinoa Nice kwa muda wa miezi 12 kabla ya kuteuliwa na miamba hiyo ya Ufaransa mwaka jana.
.
Kwa mujibu wa Kituo cha Televisheni cha Ufaransa cha RMC Sport, Galtier na mwanawe John Valovic-Galtier walikuwa chini ya ulinzi kwaajili ya uchunguzi wa madai ya ubaguzi, wawili hao ilisemekana waliitwa na wachunguzi wa tuhuma hizo za ubaguzi wa rangi waliomo ndani ya klabu ya Nice.
.
Kwa mujibu wa sheria, kocha huyo ambaye alijiunga na PSG akitokea Nice pamoja na mwanaye watasota rumande kwa saa 24 kupissha uchunguzi kabla ya kufikishwa mahakamani. Ripoti zinasema Galtier alizungumza maneno ya kibaguzi na chuki dhidi ya dini ya Kiislamu. Aidha kocha huyo alikana tuhuma hizo akidai sio za kweli.
Screenshot_20230701_151248_Instagram.jpg
 
YANNICK BANGALA :
.
“Nawahakikishia wanayanga mimi bado nina mkataba na klabu yangu mpaka mwakani, nitaendelea kuheshimu mkataba wangu,”
.
“Tulifanya vizuri Msimu uliomalizika na sasa tunajiandaa kwa ajili ya msimu ujao binafsi nitakuwa bega kwa bega na benchi jipya la ufundi,”
Screenshot_20230701_151401_Instagram.jpg
 
Kinda wa timu ya taifa ya Vijana Portugal U-21 Diego Manuel Jadon da Silva Moreira amekamilisha uhamisho wa kujiunga Chelsea akitokea Benfica kama mchezaji huru .

Usajili wa Chelsea unatoa picha gani kuelekea msimu ujao _____?
Screenshot_20230701_151629_Instagram.jpg
 
NMB yawa Benki ya Kwanza Nchini Kusajili Wanachama wa Yanga

Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya michezo nchini, leo @nmbtanzania imeingia makubaliano na timu ya @yangasc na kuwa Benki ya kwanza nchini kuwawezesha mashabiki na wanachama wa Yanga kupata kadi za uanachama kupitia matawi yote ya NMB yaliyoenea nchi nzima.

Baada ya kusaini makubaliano haya, ushirikiano wa NMB na Yanga utalenga maeneo yafuatayo:

Kutumia mtandao mpana wa NMB unaojumuisha matawi zaidi ya 228 kote nchini kufanya usajili wa wanachama na mashabiki wa Yanga, wakiwemo wenye umri chini ya miaka 18. Kadi hizi maalum zitakua na nembo za Yanga na NMB.

Mwanachama wa Yanga atalipia Shilingi 34,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Yanga (Shilingi 5,000 ni malipo ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na shilingi 24,000 ni ada ya Mwanachama kwa mwaka mzima).

Kadi za mashabiki ambao sio wanachama - Malipo yatakua shilingi 22,000 tu (shilingi 5,000 ni ya kadi, 5,000 amana ya kuanzia na shilingi 12,000 ni ada ya shabiki kwa mwaka mzima).

Kadi hizi hazitakua za uanachama/ushabiki tu, pia zina uwezo wa kufanya kazi kama kadi ya Benki! Unaweza kufanya miamala yote ya kibenki ikiwemo kuiwekea pesa, kutoa hela katika ATM na kufanya malipo mtandaoni na katika vituo vya malipo (POS).

Wanachama wanaweza kupata kadi za Malipo ya Kabla (Prepaid Card) ambayo huitaji kuwa na akaunti nasi na kufanya malipo kwa kupitia mtandao au kwenye Point of Sales (POS).

Wanachama na mashabiki watanufaika na huduma na ofa mbalimbali za NMB ikiwemo mikopo isiyokua na dhamana (Mshiko Fasta) na punguzo la bei wakifanya malipo kupitia NMB Lipa Mkononi (QR).

Benki ya NMB itawezesha matawi ya Yanga zaidi ya 900 nchi nzima kutoa huduma za uwakala wa NMB.

Mbali na huduma za uanachama, NMB itaanzisha Bima ya Mwananchi ambayo itakua na gharama nafuu.

Makubaliano haya yamesainiwa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara NMB - Filbert Mponzi na Rais wa Klabu ya Yanga – Eng. Hersi Said na kushuhudiwa na viongozi wengine wa Benki na Klabu.

Usajili huu utaanza rasmi Julai 10, 2023 kwenye matawi yote ya NMB. Tembelea tawi la NMB lililo karibu yako kupata maelezo zaidi.
Screenshot_20230701_151817_Instagram.jpg
 
Kiungo Hassan Dilunga anatajwa kumalizana na JKT Tanzania taarifa iliyowashangaza Viongozi wa Simba SC ambao walikuwa na mipango nae kuelekea msimu ujao .

Taarifa kutoka ndani ya Simba ni kuwa uongozi ulipewa jina la Dilunga na Kocha Robertinho kama sehemu ya watakaosajiliwa kwenye dirisha hili ,hii ni baada ya kumaliza matibabu na kuanza kufanya mazoezi na timu .

Simba walipendekeza Dilunga apokee Milioni 2 kila mwezi wakati anasubiri dirisha la usajili kufunguliwa lakini Mchezaji akawa anakwepa kusaini bila kutoa sababu hadi leo zilipovuja picha akisaini JKT Tanzania .
Screenshot_20230701_152051_Instagram.jpg
 
Nyota wa kimataifa wa Algeria Riyad Mahrez amepitisha suala la kujiunga Al Ahli ya Saudi Arabia baada ya kukubaliana juu ya maslahi binafsi.

Al Ahli wapo hatua ya mwisho kujadili na Manchester City kuhusu dau lake na kuna nafasi kubwa City kukubali uhamisho huu.
Screenshot_20230701_152224_Instagram.jpg
 
Marcus Thuram amekamilisha usajili wa kujiunga na Inter Milan kwa mkataba wa miaka mitano akiwa mchezaji huru akitokea Borrusia M'gladbach.

Thuram akiwa Borrusia
Amefunga Mabao 44
Asisst 29
Mechi 134.
Screenshot_20230701_152409_Instagram.jpg
 
Chelsea imekamilisha usajili wa kinda kutoka Norwich City, Alex Matos mwenye miaka 18 kama mchezaji Huru.

Huu ni usajili wa tatu kwa Chelsea hadi sasa baada ya ule wa Nkunku na Nico.
Screenshot_20230701_152502_Instagram.jpg
 
Shaffih Dauda

SEHEMU YA KWANZA

Kwenye upande wa biashara imeshathibitishwa kwamba, michezo hususan mpira wa miguu ni kiwanda ambacho kina thamani na kina mzunguko mkubwa wa fedha kutokana na biashara zinazozunguka mchezo wenyewe katika mazingira tofauti.

Marekani waliona fursa kwenye mchezo wa mpira wa miguu baada ya wataalam wa masuala ya uchumi na biashara kutoka vyuo mbalimbali mwanzoni mwa miaka ya 1990 kufanya tafiti na kugundua ukuaji wa mchezo wa mpira wa miguu duniani ulikuwa na kasi ya ajabu.

Wao wakapiga hesabu kuona ukuaji huo unaweza kuwa na tija kwa kiasi gani kwa miaka 30 baadae. Wakaona miaka 30 ijayo mpira wa miguu utakuwa maarufu na utakuwa umegusa watu wengi hasa kutokana na mabadiliko ya uendeshaji wa Ligi ya England.

1992|93 Ligi Kuu ya England ilibadilishwa uendeshaji kutoka ilivyokuwa ikiendeshwa zamani na kuiita Premier League, wakaifanya kuwa brand inayojitegemea na wakawa na mipango mahsusi ya kuitangaza duniani.

England ikafanikiwa kuifanya Ligi yake kuwa maarufu na wakaanza mipango ya kuifanya iwe bidhaa inayohitajika na kila mtu duniani!

Hapo wakaanza kuchukua wachezaji waliokuwa maarufu kwa wakati huo kutoka mataifa mbalimbali ambayo pia yalikuwa na Ligi zinazofatiliwa [Italia, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi].

Wakawachukua Gianfranco Zola, Paolo Di Canio kutoka Italy wakaenda Ujerumani wakachukua Jurgen Klinsmann, wakamshusha Eric Cantona toka Ufaransa, na wachezaji wengine wengi wenye majina makubwa hawakwenda England kwa bahati mbaya.

INAENDELEA.......
Screenshot_20230701_152548_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Coach Nabi alisaini Yanga akitoka kufutwa kazi El Merreikh ya Sudan, akaja kufanya vyema akiwa Yanga yenye kikosi bora na Uongozi imara, ndipo nae ubora wake mkubwa ukadhihirika na akafanya makubwa sana.

Coach Nabi naamini anajitahidi sana kuwa mtulivu kabla ya kuchukua project yoyote mpya, jicho lake ni ubora wa kikosi, ukubwa wa project na Uongozi uliopo kwenye klabu husika.

Ni sahihi sana kumpa credit Coach Nabi kwa alichofanya Jangwani lakini nyuma yake yatupasa tukumbuke namna Uongozi ulimpa imaan ya kuonesha alichonacho.

Nani angesubiri kumtimua punde tu baada ya kuondelewa na Al Hilal ya Sudan kwenye Champions League? Nani angesubiri kumtimua kazi punde tu baada ya sare yao dhidi ya Club Africain nyumbani? Maana yake katikati kulikuwa na MUDA plus IMAAN.

Watu wengi ikiwemo Mashabiki wa Yanga walitaka Kocha afutwe kazi, lakini utulivu wa kuamini kwenye mchakato kutoka kwa Menejimenti ukaleta matunda makubwa ya Nabi ndani ya Yanga, thats Leadership.

Nje tu na ubora wa Makocha hizi timu zimewekeza sana na zinatupa gharama kubwa sana, katazame Bonus na gharama za uendeshaji wa hizi timu kama motisha achana tu na salaries.

Viongozi kukosolewa ni kawaida sana ila kunayo room ya kuwapongeza nyuma ya mafanikio ya Yanga, they had alot of smart moves.
Screenshot_20230701_152835_Instagram.jpg
 
Mason Mount atakuwa akipokea mshahara wa Pauni 250,000 (Sh 767milioni) kwa wiki uhamisho wake utakapokamilika wiki ijayo. Kwa mujibu wa ripoti Manchester United imakubali kutoa Pauni 60 kwaajili ya kiungo huyo wa zamani wa Chelsea.
.
Mount anatajaria kusaini mkataba wa miaka mitano akipigie Man United msimu ujao. Mshahara wa Mount ni zaidi ya ule aliokuwa akipewa Chelsea Pauni 80,000.
Screenshot_20230701_153002_Instagram.jpg
 
Legend wa Arsenal, Ray Parlour ameshangaa sababu ya Arsenal kumsajili Kai Havertz kwa Pauni 65 milioni. Mjerumani huyo alikamilisha uhamisho wake wiki iliopita lakini mkongwe huyo hakupendezwa na usajili huo. Parlour anaamini Arsenal isingekubali kutoa kiwango hicho cha pesa kwaajili ya nyota huyo.
Screenshot_20230701_153052_Instagram.jpg
 
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Nishati iratibu ununuzi wa mafuta kutoka Mikoa ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa ili yachukuliwe kutokea Tanga badala ya Dar es Salaam.

Ametoa agizo hilo leo Jumamosi, Julai Mosi, 2023 mara baada ya kukagua uboreshaji wa bandari ya Tanga na hifadhi ya mafuta kwenye matenki ya GBP, eneo la Raskazoni, Jijini Tanga.

"Mikoa ya Mara, Mwanza, Manyara, Arusha, Kilimanjaro inafuata mafuta Dar es Salaam sababu ya mazoea lakini upatikanaji rahisi ni hapa Tanga, upatikanaji wa haraka sababu ya teknolojia ni hapa Tanga, Wizara ya Nishati watekeleze maelekezo haya ili wauzaji wa mafuta wayafuate Tanga”

Waziri Mkuu amesema endapo makampuni yote ya Mikoa ya Kaskazini yatachukulia mafuta Tanga, uchumi wa Mkoa huo utakua kwa haraka.

Waziri Mkuu amesema uwekezaji uliofanyika ni mkubwa kwani matenki yaliyopo yanaweza kupokea mafuta moja kwa moja kutoka bandarini na kuhifadhi lita hadi milioni 200 “Huu ni mkakati wa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuendeleza uchumi wa nchi yetu. Wakati Serikali inaongeza uwezo wa kusimamisha meli zaidi bandarini, tutahakikisha kuwa uwekezaji huu unaleta faida kwa mwekezaji na unaongeza ajira kwa Wana Tanga”
Screenshot_20230702_050732_Instagram.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amewataka wananchi kuendeleza mapambano ya kupatikana katiba mpya itakayowapa nguvu ya kuiwajibisha Serikali.

Mnyika ameyasema hayo leo Julai Mosi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Manzese jijini hapa, akisema, mbali na Katiba mpya chama chao pia kitaendelea kupigania upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi.

"Gharama za maisha zimeendelea kuwa juu, hiyo yote ni matokeo ya ubovu wa katiba mpya," amesema.

Screenshot_20230702_051340_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema ataharakisha mpango wa maduka mkoani humo kutoa huduma saa 24 unatekelezwa.

Hatua hii inakuja siku chache baada ya Serikali kuruhusu mabasi ya mikoani kusafiri saa 24.

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Julai 1, 2023 na Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila, kwenye bonanza la michezo kati ya Mamlaka ya Mapato (TRA) na wafanyabiashara wa Kariakoo.

Maamuzi ya mabasi kusafiri saa 24 yalitolewa Juni 29 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiahirisha shughuli za Bunge jijini Dodoma.

Akizungumzia namna walivyojipanga, Chalamila amesema awali walikuwa wamejipanga kufanya biashara saa 24 baada ya kumalizika kwa ujenzi wa soko la Kariakoo Oktoba mwaka huu.

Lakini kutokana na maamuzi ya kuruhusu mabasi kusafiri muda wote, wanaona kuna haja ya kuharakisha mpango huo.
Screenshot_20230702_051439_Instagram.jpg
 
Vifo katika ajali ya lori ilipoteza mwelekeo na kuparamia watu na magari kadhaa katika makutano ya barabara yenye shughuli nyingi jana jioni, imefikia 52.

Waziri wa Uchukuzi nchini Kenya, Kipchumba Murkomen amewaambia waandishi habari katika eneo ilipotokea ajali hiyo la Londiani kuwa awali idadi ya vifo ilikuwa 49.

Ajali hiyo imetokea Juni 30, 2023 usiku kwenye barabara kuu kati ya mji wa Nakuru na Kericho.

Mkuu wa Mkoa wa Bonde la Ufa, Abdi Hassan amesema zaidi ya watu 30 pia walijeruhiwa wakati lori hilo lilipoyagonga magari madogo, bodaboda na vibanda vya wafanyabiashara.

Kufuatia ajali hiyo ya kutisha Rais wa Kenya, William Ruto ametuma salamu za rambirambi kwa waathiriwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Afya wa Kaunti ya Kericho alisema jumla ya miili 49 iliepokelewa katika Hospitali ya Kaunti ya Kericho na hifadhi za maiti za Hospitali ya Londiani, mpaka leo asubuhi.
Screenshot_20230702_051615_Instagram.jpg
 
TIMU ya Tabora United (zamani Kitayosce) na Geita Gold zinawania saini ya mfungaji bora Ligi Kuu 2021/2022, George Mpole. Straika huyu yupo Bongo baada ya ligi ya DR Congo anakoitumikia FC Lupopo kusimama sababu za kiuchumi na amani.
Screenshot_20230702_051823_Instagram.jpg
 
SINGIDA Fountain Gate FC imeamua kufuata nyayo za vigogo Simba, Yanga na Azam zilizopanga kwenda kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya Wa michuano ya Ligi Kuu, Kombe la ASFC na ile ya kimataifa nje ya nchi kwa yenyewe kuichagua Tunisia
.
Timu hiyo ilipanda Ligi Kuu msimu uliopita na kumaliza nafasi ya nne kwenye msimu, imekata tiketi ya mechi za kimataifa msimu huu ikishiriki Kombe la Shirkisho Afrika sambamba na Azam FC.
.
Msemaji wa klabu hiyo, Hussein Massanza alisema kikaoo cha bodi kilichokaa kwa siku mbili jijini Dodoma tangu juzi kimekubaliana kambi ya msimu mpya itakuwa Tunisia katika klabu ya US Monastir.
Screenshot_20230702_051924_Instagram.jpg
 
Liverpool inakaribia kuinasa saini ya nyota wa RB Leipzig, Dominik Szoboszlai, kwa mujibu mkali wa masuala ya usajili Fabirizo Romano.
.
Liverpool inataka kumsajili staa huyo wa kimataifa wa Hungary haraka iwezekanavyo na hadi leo Jumamosi mazungumzo yalikuwa yakiendelea vizuri.

Uhamisho wa Szoboszlai kwenda Liverpool umeleta matunda baada ya kifungu chake chenye thamani ya Puani 60 milioni kufikia kikomo jana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikiwasha Bundesliga msimu uliopita aliwakilisha timu yake ya taifa mara 32 na kuifungia Leipzig mara 10 katika mechi 48 alizocheza.
Screenshot_20230702_052510_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom