Bayern wamewasilisha ombi rasmi kwa Harry Kane - lilikataliwa mara moja na Tottenham. Bayern iliweka dau karibu na €70m pamoja na nyongeza haitoshi kuwashawishi Spurs kufikia sasa.
David de Gea alitia saini mkataba wa kurefusha mkataba na Manchester United laikini klabu hiyo imeamua kukataa kuendelea na mkataba huo.
De Gea alikubali kupunguziwa kwa kiasi kikubwa kwa mshahara wake wa sasa wa pauni 375,000 kwa wiki, lakini Uongozi wa Man United umekataa kusaini mkataba huo wa kumuweka De Gea Old Trafford.
ALEXIS Mac Allister amefichua siri kwamba amegoma kuvaa jezi namba 8 Liverpool kwa sababu ina historia kubwa na iliwahi kuvaliwa na mkongwe Steven Gerrard.
.
Kiungo huyo alisajiliwa na Liverpool kwa Pauni 35 milioni akitokea Brighton mwezi uliopita baada ya kufuatiliwa msimu mzima na kocha Jurgen Klopp.
.
Baada ya kugoma Mac Allister alipewa jezi namba 10 ambayo atavaa msimu ujao, lakini akaeleza kwanini hakukubali kuvaa jezi namba 8
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane ametangaza kwamba sasa yupo tayari kurudi mzigoni. Na kwenye hilo, kocha huyo Mfaransa alisema anajiandaa kurudi kufanya kazi kwenye Ligue 1.
Kwa muda mrefu, Zidane amekuwa hana kazi tangu alipoachana na Real Madrid, ambayo aliinoa kwa awamu mbili tofauti. Ripoti zilifichua kwamba Zidane alikuwa anasubiri kazi ya kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa, lakini kibarua hicho bado kipo chini ya kocha Didier Deschamps.
Nina fani nyingi sana, kama nisingekuwa nacheza mpira hata sijui ningekuwa nafanya nini kwa sababu najua kuimba, ku-dance na kuigiza.
Nimeigiza filamu na kina Nyamayao na Kibakuli enzi za Kaole Sanaa Group, nimeimba kwaya kanisani badae nikaenda ku-dance THT enzi za Marehemu Ruge kuna siku akaniona nacheza mpira akaniambia huku [THT] hapakufai usije tena kaendelee kucheza mpira.
Wakati nacheza Morocco [Difaa El Jadida] ni wachezaji wanne tu wa kigeni walikuwa wanaruhusiwa kusajiliwa na timu moja, lakini unakuta wanaweza kuanza watatu na mmoja akasubiri wakati nacheza Wydad idadi iliongezeka na kufika hadi wachezaji watano wa kigeni.
Morocco kulinisaidia sana kunibadilisha, kwa sababu ili upate nafasi ya kucheza ni lazima uwe na kitu cha ziada kwa hiyo inibidi nijitume mara mbili zaidi.
Wachezaji wa Morocco hawapendi sana mazoezi, wanapenda kucheza mpira kwa hiyo mimi nilikuwa nakamua sana mazoezi ili kuwa fit halafu nikiwa uwanjani najitoa sana.
Timu niliyokuwa nacheza [Saudi Arabia] inashiriki Ligi ya Champioship sio Ligi Kuu, ikitoka Ligi Kuu wanayocheza kina Ronaldo Ligi inayofuata ndio nilikuwa nacheza mimi pamoja na timu ya Pitso Mosemane ambayo alifanikiwa kuipandisha Ligi Kuu.
Ligi ya juu ni ngumu lakini hata Ligi niliyokuwa nacheza [Championship] ni ngumu vilevile, wanasema Ligi ya Saudi Arabia ni ngumu ukilinganisha na Qatar. Hata mimi kabla sijaenda nilikuwa nahisi watu wanaenda kuvuna pesa lakini pesa yao unaifanyia kazi.
Niwaweke watu wazi kuhusu Ligi na soka la Saudi Arabia, kule watu hawaendi kumalizia soka kama ambavyo wengi wanafikiri, watu wanacheza kweli.
Wenzetu wanajua nini maana ya biashara kwenye wa mpira wa miguu, wamewekeza sana wakihitaji mchezaji yeyote wanamchukua.
Nimemaliza mkataba kwenye timu yangu ya Saudi Arabia [nilisaini mwaka mmoja] kwa hiyo sasa hivi naangalia sehemu nyingine lakini kama na wao watanihitaji basi tutarudi mezani kuzungumza, kwa sasa mimi ni mchezaji huru! Natamanisha.
Tayari ofa zimekuja lakini bado hakuna timu ambayo tumefikia makubaliano ila ofa nyingi zinatoka kwenye timu za bara la Asia japo hata Afrika pia zipo lakini kwa hapa nyumbani bado sijapokea ofa kutoka timu yoyote.
Kwa sasa nisiwe muongo, bado nataka kucheza nje na kuna asilimia nyingi nitaendelea kucheza nje. Nyumbani nitarejea lakini sio kwa sasa.
Mwaka 1993, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alienda Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) kushuhudia Simba ikicheza fainali ya Kombe la CAF lakini bahati mbaya kwa upande wake na Watanzania kwa ujumla taji hilo lilibebwa na Stellah Adjamen ya Ivory Coast.
.
Lakini pia Rais Mwinyi akiwa ameshastaafu mwaka 2002 alienda Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi ya Simba na Yanga iliyoisha kwa Simba kushinda mabao 4-1.
MORICE CHUKWU ATUA SINGIDA
.
Kiungo Mnigeria Morice Chukwu anatarajiwa kutua nchini ili kumalizana na Singida Fountain Gate itakayompa mkataba wa miaka mitatu tayari kujiwinda na michuano ya Caf kuanzia mwezi Agosti.
.
Fundi huyo awali alikuwa akitajwa kuwindwa na Yanga, lakini ofa ndogo alizowekewa mezani ndizo zilizomfanya aamue kuichagua Singida iliyokuwa na ofa nono zaidi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.