Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230629_064159_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230629_064216_Opera%20Mini.jpg
 
WABABE KABISA
200+ —TANGU msimu wa 2014-15 uanze wachezaji wanne ndio wamefunga mabao 200+ katika Ligi tano kubwa Ulaya:
.
261 — Robert Lewandowski
253 — Lionel Messi
234 — Cristiano Ronaldo
210 — Harry Kane

Screenshot_20230629_093349_Instagram.jpg
 
LIVERPOOL NAYO YAJITOSA KWA MBAPPE
.
Liverpool ni miongoni mwa timu zilizoingia vitani dhidi ya Real Madrid kuiwania huduma ya mshambuliaji wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe, 24, dirisha hili ama lijalo. Ili kumsajili fundi huyu dirisha hili, PSG inahitaji kupewa zaidi ya Euro 300 milioni (Sh 789bilioni) kama ada ya uhamisho jambo ambalo limesababisha timu nyingi zinazomhitaji kurudi nyuma.
.
Mbappe ambaye kwa mwaka mmoja anapata zaidi ya Pauni 170 milioni kutokana na mshahara wake na bonasi ya usajili tayari ameshawaambia mabosi wa PSG hana mpango wa kuendelea kusalia kwenye timu baada ya msimu ujao kumalizika.
.
Licha ya uwepo wa Liverpool, hadi sasa timu inayopewa nafasi kubwa zaidi ya kuipata huduma yake ni Madrid ambao hapo kabla iliwasilisha ofa ya kutaka kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana. Pia. Man United imetajwa endapo itanunuliwa na matajiri Waarabu, watahakikisha Mbappe anatua klabuni hapo kwa gharama yoyote ile ili kumchomoa PSG.
Screenshot_20230629_093458_Instagram.jpg
 
ZAHA, STORMZY WANUNUA TIMU
.
Staa wa soka, Wilfried Zaha na rapa Stormzy wametangaza mpango wao wa kuinunua timu ya Croydon Athletic. Winga, Zaha, anayemaliza mkataba wake huko Crystal Palace ameungana na rapa wa Uingereza, Stormzy kama sehemu ya watu watatu watakaoinunua klabu hiyo ya soka, Croydon Athletic.
.
Kilichoelezwa ni kwamba kwa muda mrefu wawili hao wamekuwa kwenye mchakato wa kuimiliki timu hiyo. Taarifa yao ilibainisha: “Tunafurahia kutangaza zama mpya za AFC Croydon Athletic, imebaki kwenye uthibitisho wa mwisho wa kutoka FA na ligi. Huu ni mjadala uliochukua miezi mingi ya majadiliano.”
.
Klabu hiyo ya Croydon Athletic FC iliyoanzishwa 2012 inacheza Ligi Daraja la Tisa huko England. Inamiliki uwanja wenye uwezo wa kuingiza watazamaji wanaoketi 3,000 ambao unaitwa Maryfield.
Screenshot_20230629_093612_Instagram.jpg
 
UNITED YATUA TENA KWA DE JONG
.
Manchester United imerudi tena kwenye mchakato wa kuiwania huduma ya kiungo wa Barcelona na Uholanzi, Frenkie de Jong, 26, ambaye kwa wakati huu itakuwa kuna ugumu zaidi kumpata kwani Bayern Munich nayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili.
.
Kocha wa Man United, Erik Ten Hag amewaambia mabosi wa timu hiyo moja ya maeneo anayotaka sana kuboresha ni hili kwani lina upungufu pia. Man United inadaiwa kuwa kwenye mchakato wa kutaka kumuuza Donny van de Beek na mbadala wake ndio anaonekana kuwa ni de Jong.
.
Kumekuwa na mawasiliano mazuri baina ya kocha wa Man United na De Jong hali inayozidi kuchochea asilimia za dili hili kukamilika ingawa uwepo wa Munich huenda ukabadilisha uamuzi wa staa huyu.
Screenshot_20230629_094320_Instagram.jpg
 
SIMBA YAMPIGIA HESABU PROTASIA
.
Beki mrembo na mwenye mvuto wa Timu ya Wanawake ya Fountain Gate Princess, Protasia Mbunda anatajwa kuwindwa na Simba Queens kwa ajili ya Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) na Mashindano ya Kimataifa msimu ujao. Pisi hiyo kali ambayo hucheza beki wa kushoto na namba tano pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars amekuwa na msimu bora.
.
Mrembo huyo ambaye ni nahodha wa Fountain Gate anaenda kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi na kuhakikisha ufalme wa timu hiyo unarudi msimu ujao mara baada ya msimu huu kukosa ubingwa uliochukuliwa na JKT Queens. Mbunda ameonesha uwezo mkubwa katika timu yake ya Fountain Gate kiasi cha kuwashawishi viongozi wa Simba kutaka kuinasa saini yake kwa ajili ya msimu ujao.
Screenshot_20230629_094542_Instagram.jpg
 
SINGIDA FOUNTAIN YABEBA BEKI KMC
.
Uongozi wa klabu ya Singida Fountain Gate FC umeendeleza harakati za usajili na sasa unaelezwa kukamilisha uhamisho wa beki wa kulia, Kelvin Kijiri aliyekuwa anacheza katika kikosi cha KMC.
.
Baad ya kuwa sehemu ya wachezaji walioibakisha KMC kwenye Ligi Kuu, Kijiri inaripotiww kupewa mkataba wa miaka miwili kuitumikia Singida Fountain Gate msimu ujao.

Screenshot_20230629_095452_Instagram.jpg
 
Tottenham wamefikia makubaliano ya mdomo na Leicester kumsajili James Maddison! Maslahi binafsi yamefikiwa, ada ya pauni milioni 40 baada ya mazungumzo kufikia hatua ya mwisho jana usiku. Hatua zinazofuata: vipimo vya matibabu, hati zinatayarishwa na kisha kutiwa saini.

Screenshot_20230629_095917_Instagram.jpg
 
BREAKING: Klabu ya Kaizer Chiefs yamtangaza Molefi Ntseki kama kocha mkuu kuelekea msimu ujao. Kaizer yaamua kumtosa Kocha wa zamani wa Yanga Nasriddine Nabi baada ya kushindwana maslahi binafsi. nabi alitaka kwenda na benchi lake la Ufundi kwa watu anaowataka yeye akiwemo Milton(goalkeeping coach), Helmi(fitness coach) pamoja na Khalil Ben Youssef (Video Analyst)

Screenshot_20230629_100017_Instagram.jpg
 
TETESI: Klabu ya Yanga imeripotiwa kufikia makubaliano ya masharti binafsi na mlinzi wa kushoto wa Singida Fontaine Gate FC, Nickson Kibabage kwa ajili ya kuvaa uzi wa kijani na njano msimu ujao.

Yanga SC inaendelea na majadiliano na Wakulima hao wa Alizeti juu ya dau la uhamisho. Kibabage bado ana mkataba na Singida Fontaine Gate FC.

Inaelezwa Kibabage alikuwa pendekezo la kocha Nasreddine Nabi aliyeondoka klabuni hapo hivyo Wananchi wameamua kulitekeleza baada ya kuona anafaa kuvaa uzi wa Wanajangwani.
Screenshot_20230629_100110_Instagram.jpg
 
BREAKING: Klabu ya Kaizer Chiefs yamtangaza Molefi Ntseki kama kocha mkuu kuelekea msimu ujao. Kaizer yaamua kumtosa Kocha wa zamani wa Yanga Nasriddine Nabi baada ya kushindwana maslahi binafsi. nabi alitaka kwenda na benchi lake la Ufundi kwa watu anaowataka yeye akiwemo Milton(goalkeeping coach), Helmi(fitness coach) pamoja na Khalil Ben Youssef (Video Analyst)

View attachment 2672678
Nabi atakuwa kaoewa kifuta jasho cha usumbufu
 
BREAKING: Arsenal wametuma ofa ya tatu kwa dau la hadi pauni milioni 105 kumnunua kiungo na Captain wa Westham Declan Rice.

Ofa hiyo, ambayo Arsenal wanatarajia itawashinda wapinzani wao Manchester City, inajumuisha ada ya awali ya £100m na nyongeza ya £5m

Ofa hii ni rekodi ya usajili kwa Arsenal. Kama ofa itakubaliwa basi Declan Rice ataweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kiingereza ghali zaidi kuwahi kununuliwa. [David Ornstein] #sportshqtz

Screenshot_20230629_100152_Instagram.jpg
 
AC Milan wamekamilisha makubaliano na Chelsea kumsajili Ruben Loftus Cheek

◉ Ada iliyothibitishwa kama ilivyofichuliwa jana: €16m iliyopangwa pamoja na nyongeza za €4m kwa Chelsea kwa kiungo huyo wa kati wa Uingereza.

◉ Mkataba wa muda mrefu ulikubaliwa na Ruben ambaye anakaribia kujiunga na AC Milan, akishangiliwa na sura mpya ya soka ya Italia.

◉ Vipimo vya kimatibabu vinavyoratibiwa kadri mpango unavyofanywa.
Screenshot_20230629_100627_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom