Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230627_060212_Opera%20Mini.jpg
 
Meli ya Titanic iligharimu $7.5 million tuu hadi kukamilika kwake mwaka 1911, hii ni pesa ndogo kuzidi hata bajeti ya filamu zilizotengenezwa baadaye kuigiza tukio la kuzama kwake mwaka 1912. Filamu ya Titanic ya mwaka 1997 ilitumia zaidi ya $200 milions hadi kukamilika

Zaidi ya wafanyakazi, wanaume 15,000 walihusika katika uundwaji wa meli hii huko Belfast, Ireland. Ilitumika miezi 26 kufanya kazi mpaka meli kukamilika, ni miaka miwili na miezi miwili.

Historia yake ni ya ajabu kuliko meli zote,sio kwasababu ya tajiri wa dunia wa kipindi hicho bwana John Jacob Astor kuwa mmoja kati ya wahanga waliopoteza uhai , lakini kwasababu ya kile ambacho hakitosahaulika

Inawezekana ni stori nyingi umezisikia, kuona kwenye filamu au hata kuzisoma kuhusiana na meli kubwa kuwahi kutengenezwa, meli ya Titanic iliyozama mwaka 1912 ikiwa baharini kutoka UK kwenda Marekani, karibu tukujuze mengi zaidi kuhusu meli hii.
 
Mwanzoni ilizua gumzo duniani kote… kwa ufahari,uzuri,ukubwa kuliko meli zote ulimwenguni pamoja na mapinduzi makubwa katika ufanisi wa wanadamu

Lakini punde ikapelekea huzuni na machungu ambayo ni kazi kuyaelezea kwa maneno ya kawaida,ajali ikaacha mafumbo yasiyo na majibu hadi hivi leo

Siku meli ya Titanic ilipozama chini ya mawimbi ya bahari ya antlantic pamoja na roho za watu zaidi ya 1500 itaendelea kubaki kumbukumbu ya majonzi katika Historia ya wanadamu


Na pamoja ya miaka 109 kupita , bado hadi hivi leo wanasayansi , wachunguzi na wasanii wanaendelea kufuatilia tukio la masaa mawili na dakika 40 lililobeba mikasa zaidi ya 2208

Nina imani ni mengi ya ajabu bado huyafahamu juu ya tukio hilo ,na leo nimekuandalia mambo 7 ya ajabu yasiyosahaulika kuhusu meli ya titanic ambayo yatakushangaza
 
KULIKUWA NA UWEZEKANO WA WATU WOTE KUOKOLEWA

Ulikuwa mwezi wa nne wa tarehe 14 mwaka 1912, saa ilisoma saa 5 na dakika 40 za usiku,Meli kubwa ya Titanic ikagonga mwamba wa barafu kwa ubavu wake wa kulia na kujisababishia matobo makubwa yaliyoanza kuingiza maji kwa nguvu ndani ya meli hiyo.

Wakati janga hilo lilipokuwa likitokea Nahodha wa meli ya Titanic alijitahidi sana kupiga simu kwenye meli ya SS carifornia waliyogundua ilikuwa jirani sana na mahali walipo lakini hakukuwa na majibu .
 
Mtu pekee aliyehusika na kupokea simu katika meli ya SS California alikuwa amelala ,yaani kama zingekuwa ni nyakati za mchana na simu hiyo ingepokelewa upesi basi hivi leo tukio hilo la kuhuzunisha lisingeongelewa kabisa

Nahodha wa Titanic akajihisi kupagawa baada ya kujaribu kila njia kuwajurisha watu waliokuwa kwenye meli ya SS California.

Inasemekana wafanyakazi wa SS california waliona mwanga wa baruti iliyopigwa kuashiria uhitaji wa msaada ,nao wakaenda upesi kumwambia Nahodha wa meli yao,lakini Nahodha huyo alichukulia poa tu,nakutaka asisumbuliwe katika nyakati hizo ,inasemekana hakujua kama meli hiyo ilikuwa ni meli ya abiria au labda zilikuwa ni akili za usingizi , na kwasababu ya baridi kali lililokuwepo labda nahodha wa meli hiyo alikuwa na mtu aliyeshindwa kumuacha ndani humo
 
Baada ya masaa machache kupita, katika mida ya wanga yaani saa 8 za usiku meli ya Titanic ikakatika Katikati na kujigawa vipande viwili na baada ya dakika chache, Meli ikazama na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 1500.

Watafiti wanadai kuwa meli ya SS California ilikuwa na uwezo wa kuokoa maisha ya watu wote waliokufa katika meli ya Titanic ,hadi hivi leo meli ya SS California inakumbukwa kwa tukio hilo la kizembe huku lawama zikimzonga Nahodha wa meli ya SS California hadi anaingia kaburini.
 
KULIKUA NA RIWAYA ZILIZOELEZEA AJALI YA TITANIC HATA KABLA MELI HIYO KUTENGENEZWA.Mwaka 1886 mwandishi kutokea british aitwae William T stead ,aliandika kitabu alichokiita “from the old world to the new world “ yaani kutokea ulimwengu wa zamani kuelekea mpya.


Kwenye kitabu hicho aliongelea meli kubwa sana iliyozama kaskazini mwa bahari ya antlantic nakusababisha vifo vya watu wengi baada ya kugonga mwamba wa barafu, na cha ajabu zaidi jina la Nahodha alilotumia katika kitabu chake lilifanana na jina la Nahodha wa Meli ya Titanic.
 
Pia mwaka 1898 yaani miaka 14 kabla ya meli ya Titanic kuzama, mwandishi mwingine aitwae Morgan Robertson aliandika riwaya aliyoiota futility. Riwaya hiyo iliongelea meli kubwa aliyoiita Titan jina lililofanana na meli halisia ya Titanic , kwenye hadithi ilielezewa meli hiyo kutokuwa na maboti ya kutosha kama ilivyokuwa kwenye meli ya Titanic ,pia meli zote mbili zilipewa jina la unsikable yaani Meli isiyozama, na kama haitoshi Meli ya Titan kwenye riwaya ya bwana Morgan ilizama mwezi wa nne kama ilivyozama meli ya Titanic,

kitabu cha Morgan Robertson kilitabiri tukio lote la kuzama kwa meli ya Titanic kiasi kwamba akakumbwa na shutuma za uchawi na wengine wakiamini yeye ndiye aliyesababisha janga hilo, hata hivyo Morgani Robertson alijibu shutuma zile kwa kudai kuwa ufanano huo ulitokana na kujua kwake mambo mengi.
 
KULIKUA NA RIWAYA ZILIZOELEZEA AJALI YA TITANIC HATA KABLA MELI HIYO KUTENGENEZWA.

Mwaka 1886 mwandishi kutokea british aitwae William T stead ,aliandika kitabu alichokiita “from the old world to the new world “ yaani kutokea ulimwengu wa zamani kuelekea mpya.


Kwenye kitabu hicho aliongelea meli kubwa sana iliyozama kaskazini mwa bahari ya antlantic nakusababisha vifo vya watu wengi baada ya kugonga mwamba wa barafu, na cha ajabu zaidi jina la Nahodha alilotumia katika kitabu chake lilifanana na jina la Nahodha wa Meli ya Titanic.

Pia mwaka 1898 yaani miaka 14 kabla ya meli ya Titanic kuzama, mwandishi mwingine aitwae Morgan Robertson aliandika riwaya aliyoiota futility. Riwaya hiyo iliongelea meli kubwa aliyoiita Titan jina lililofanana na meli halisia ya Titanic , kwenye hadithi ilielezewa meli hiyo kutokuwa na maboti ya kutosha kama ilivyokuwa kwenye meli ya Titanic ,pia meli zote mbili zilipewa jina la unsikable yaani Meli isiyozama, na kama haitoshi Meli ya Titan kwenye riwaya ya bwana Morgan ilizama mwezi wa nne kama ilivyozama meli ya Titanic,
 
kitabu cha Morgan Robertson kilitabiri tukio lote la kuzama kwa meli ya Titanic kiasi kwamba akakumbwa na shutuma za uchawi na wengine wakiamini yeye ndiye aliyesababisha janga hilo, hata hivyo Morgani Robertson alijibu shutuma zile kwa kudai kuwa ufanano huo ulitokana na kujua kwake mambo mengi.
 
WANAMZIKI WALITUMBUIZA HADI DAKIKA YA MWISHO

Kulikuwa na matukio mengi ya kishujaa yaliyofanyika usiku huo wa kihistoria,bila kusahau wahandisi waliojitoa kafara kuendelea kufanya kazi kuhakikisha meli hiyo haizami wala umeme haukatiki lakini hakukua na tukio lililogusa mioyo ya watu wengi kama tukio la bend ya muziki lililoongozwa na bwana Wallance Hartley

Inasemekana wakati meli hiyo ilipokuwa ikizidi kuzama majini kwa kila dakika,watu wengi walikuwa wakijaribu kuingia katika maboti machache yaliyokuwepo ili kuokoa maisha yao.
 
Lakini wanamuziki 8 waliokuwa wakitumbuiza waliendelea kutumbuiza kwa ajili ya kuondoa hofu na kupoza mioyo ya watu waliopaniki

Kuna baadhi ya watu waligoma kupanda maboti na kubaki wakikonga nyoyo zao wakisikiliza nyimbo zilizopigwa kwa ufanisi usiokuwa wa kawaida..

Watu waliopona walidai kusikia nyimbo iliyotumbuizwa kabla ya meli kuzama na kupotea baharini , kilikuwa kibao kilichopendwa kwenye makanisa mengi kiitwacho “Neerer,My God to thee” yaani jirani na mola wangu.

Wanamuziki hawa wote walifariki siku hiyo lakini hadi hivi leo wanakumbukwa kama mashujaa kwa jambo walilolifanya
 
Pombe yaokoa maisha ya Charles Joughin

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu, Pombe imeonekana kuwa ya muhimu kuliko vitu vyote katika ajali ya Titanic, labda hata abiria wote wangelewa usiku huo basi vifo vingekuwa vichache au visingekuwepo kabisa.


Kati ya visa zaidi ya 2208 vilivyotokea katika usiku huo wa kihistoria ,kisa kilichoduwaza watu wengi ni kisa cha mpishi wa meli ya Titanic,

Mpishi huyo Aliweza kukaa kwa takribani masaa matatu kwenye maji yenye baridi lisilo la kawaida ambalo kwa watu wengine walikufa ndani ya dakika chache

Kabla ya ajali hiyo kutokea bwana Charles Joughin alikuwa amelala,meli ilipogonga mwamba wa barafu na kupelekea mtikisiko mkubwa , Bwana Charles aliyekuwa katika mapumziko baada ya kujichokea akaamka…
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom