Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230626_050534_Opera%20Mini.jpg
 
UNITED YAINGILIA DILI LA CAICEDO
.
Baada ya kuachana na mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa Chelsea Mason Mount, sasa Manchester United imehamishia nguvu zao kwa viungo wengine ikiwemo kiungo wa Brighton Moises Caicedo.
.
Man United itatakiwa kushinda vita dhidi ya Chelsea ambayo kwa sasa ndio inaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuipata huduma ya fundi huyu wa kimataifa wa Ecuador
.
Chelsea imekataa ofa tatu za Man United juu ya Mount na ofa ya mwisho inadaiwa kuwa ni ile ya Pauni 55 milioni. Moja kati ya maeneo ambayo Kocha wa Man United Erik Ten Hag anataka kuyajenga upya kwenye kikosi cha Man United ni hilo la kiungo hususani cha chini.

Screenshot_20230626_071659_Instagram.jpg
 
MAN CITY KUMZUIA KIUNGO WAKE ASITIMKE
.
Manchester City imepanga kumshawishi kiungo wake, Bernardo Silva asiondoke katika dirisha hili la usajili la kiangazi kwa mujibu wa ripoti. Silva aliupiga mwingi msimu uliopita akiisaidia Man City kutwaa mataji matatu.
.
Taarifa zimeripoti Mreno huyo yupo mbioni kujiunga na PSG, lakini Man City haipo tayari kuachana na kiungo huyo na inataka kuboresha mkataba mpya kama juhudi za kumshawishi abaki Etihad msimu ujao.
.
Mbali na PSG matajiri wa Saudi Arabia, Al Hilal wameonyesha. nia ya kumsajili Silva na dili lake atakuwa akilipwa Pauni 75 milioni kila msimu. Endapo Silva ataondoka basi atakuwa mchezaji wa kwanza wa Ulaya ambaye ameenda Saudia akiwa na mafanikio mengi msimu uliopita.

Screenshot_20230626_073356_Instagram.jpg
 
SPURS WAO NA MADDISON TU
.
Tottenham itaongeza juhudi za kumsajili James Maddison kutoka Leicester City wiki hii, lakini ofa iliyotolewa na Newcastle United kwaajili ya kungo huyo huenda ikatibua mipango yao.
.
Kocha mpya wa timu hiyo Ange Postecoglou, anataka kikosi chenye wachezaji wenye ubunifu msimu ujao huku akimpendekeza Maddison. Taarifa zimeripoti wiki iliyopita kwamba Maddison yuko mbioni kutua Spurs, baada ya Newcastle kukamilisha uhamisho wa Sandro Tonali akitokea AC Milan.
.
Hata hivyo, licha ya kutumia Pauni 55 mlioni kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, mwenye umri wa miaka 21, Newcastle inaamini bado inaweza kuinasa pia saini ya Maddison. Leicester inataka Pauni 60 milioni ili kumuuza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, lakini ofa ya awali la Spurs ni nusu ya kiasi hicho.
Screenshot_20230626_083221_Instagram.jpg
 
.
MANCHESTER City inataja kutoa kiasi kikubwa cha pesa ili kuipata huduma ya beki wa kulia wa Paris St-Germain, Achraf Hakimi, 24, katika dirisha hili. Man City inataka kutoa kiasi hicho cha pesa ili kuliweka sawa eneo lao la beki wa kulia na Kayle Walker pia huenda akaondoka.
.
Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 na amekuwa pia akihusishwa na timu kubwa barani Ulaya ikiwamo Manchester United na Real Madrid.

Screenshot_20230626_083409_Instagram.jpg
 
.
KAPTENI na beki wa Chelsea, Cesar Azpilicueta yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kujiunga na Inter Milan ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuuomba uongozi wa Chelsea umuuze dirisha hili ili akatafute changamoto mpya. Azpilicueta ambaye msimu uliopita alicheza mechi 32 za michuano yote, mkataba wake wa sasa na Chelsea unamalizika mwakani.

Screenshot_20230626_083610_Instagram.jpg
 
.
BRIGHTON tayari imemjumuisha staa wa Ajax na Ghana Mohammed Kudus, 22, kwenye orodha ya wachezaji inaowatazama sana katika dirisha hili. Kudus ambaye alionyesha kiwango bora kwenye michuano ya Kombe la Dunia kule Qatar anadaiwa kukataa ofa ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Ajax na badala yake amewaambia anataka kuondoka kutafuta changamoto mpya.
Screenshot_20230626_083705_Instagram.jpg
 
Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema Viongozi na Wachezaji wa Klabu hiyo wanapenda ushirikiano na Wanachama pamoja na Mashabiki ndio maana hata kukosolewa wanapenda lakini ameomba lugha itumike ya staha kwakuwa isipokuwa hivyo huwa wanajisikia vibaya kama Binadamu.

Mangungu amesema hayo leo katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Wanachama wa Simba ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Sisi tunapenda ushirikiano na Wanachama pamoja na Mashabiki ndio maana hata kukosolewa tunapenda lakini lugha itumike ya staha kwakuwa isipokuwa hivyo huwa tunajisikia vibaya kama Binadamu”

Katika hatua nyingine Klabu imezindua Simba Chat kwa ajili ya Mashabiki na Wapenzi wa Klabu hiyo kutoa maoni na kupata taarifa za klabu yao.

Mtendaji Mkuu Imani Kajula amesema Simba Chat ni mfumo wa kuwaweka Mashabiki karibu zaidi klabu ambako baada ya Mtu kutambulika rasmi kama Shabiki wa Simba atapata fursa ya kutoa maoni, kuripoti malalamiko na kupata maswali na majibu.
Screenshot_20230627_051408_Instagram.jpg
 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azan Zungu ambaye pia ni Shabiki wa Simba amesema Wapenzi wa Klabu hiyo hawapaswi kulaumiana kwakuwa walicheza vizuri tu Morocco huku akiwataka waendelee kuiunga mkono Simba kwakuwa anaamini msimu ujao itafanya vizuri.

Zungu amesema hayo leo katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Wanachama wa Simba ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Wala hatupaswi kulaumiana, tulicheza vizuri sana kule Morocco lakini bahati haikuwa yetu, tuendelee kuiunga mkono Timu yetu naamini tutafanya vizuri msimu ujao”
Screenshot_20230627_051515_Instagram.jpg
 
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa ambaye ni Shabiki wa Simba, Job Ndugai amesema Mashabiki wa Klabu hiyo walijisikia vibaya Kocha wao Juma Mgunda alipofananishwa na andazi lakini walifurahi jinsi Mgunda alivyojibu kwa busara.

Ndugai amesema hayo leo katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Wanachama wa Simba ambao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Tulijisikia vibaya kocha wetu Juma Mgunda alivyofananishwa na andazi lakini tulifurahi alivyojibu kwa busara, hongera sana Mgunda”
Screenshot_20230627_051607_Instagram.jpg
 
Mwanaume mmoja Mkazi wa Kichangani Manispaa ya Morogoro Meshack Azikam (23) amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa misalaba 14.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema Mtuhumiwa huyo alikamatwa aking'oa msalaba katika makaburi ya Kola Manispaa ya Morogoro na baada ya kumfanyia upekuzi nyumbani kwake walikuta misalaba mingine 13 .

@ayotv_ imeongea na Msimamizi wa makaburi hayo ya Kola, Abdalah Salum ambaye amesema changamoto hiyo imekuwa kubwa katika eneo hilo na mara nyingi wizi unafanyika majira ya alfajiri na jioni ambapo licha ya kuiba misalaba pia limeibuka wimbi wa wizi wa matofali na marumaru.

"Tumeshawakamata wezi mara nne kwa nyakati tofauti na wengine tumewapeleka Polisi wengine tumewafikisha Mahakamani na misalaba mingine ipo hapa tumekuta imeng'olewa na kutelekezwa katika makaburi hayo tunaomba Ndugu waje wachukue wakarudishie kwenye makaburi ya Ndugu zao"
Screenshot_20230627_051926_Instagram.jpg
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha rasmi Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa kura 354 ambayo ni sawa 95%.

Jumla ya Wabunge waliokuwepo leo June 26, 2023 wakati wa upigaji kura ni 374 ambao hawakuwepo ni 18, kura ya hapana ni 0 na kura mabazo hazikuwa na uamuzi ni kura 20.
Screenshot_20230627_052138_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema haiutambui usajili wa Chuo cha Tanzania Aviation College kilicho na matawi katika mikoa ya Mwanza, Dares Salaam na Arusha.

Chuo hicho ambacho kimekuwa kikitumia usajili namba wa CAA/AT0/050 imebainishwa kuwa usajili wake ulifikia ukomo mwaka 2018.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari inaeleza kuwa kukoma kwa usajili huo kunafanya mafunzo ya usafiri wa anga yanayoendeshwa na chuo hicho kwa kutumia mgongo wa kutambulika na TCAA kuwa ni kinyume na sheria.

“Pia hii inafanya wahitimu wa chuo hiki kukosa sifa za kupata leseni kutoka TCAA hivyo kushindwa kupata ajira,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Screenshot_20230627_052319_Instagram.jpg
 
Wafanyakazi 15 wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwemo wahasibu, ofisa afya, mweka hazina na ofisa mtendaji wa mtaa, wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 143 yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu, matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara Halmasahuri ya Jiji la Dar es Salaam kiasi cha Sh8.9 bilioni.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo jioni, Juni 26, 2023 na Wakili wa Serikali, Faraji Ngukah akisaidiana na Pendo Temu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo.

Wakili Ngukah amedai washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kati ya Julai Mosi 2019 na Juni 6, 2021 Katika jiji la Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu na kujipatia Sh8.9 bilioni, mali ya Halmashauri ya Jiji.

Screenshot_20230627_052418_Instagram.jpg
 
Kampuni ya Taifa Gas ya Tanzania imetangaza uwekezaji mkubwa nchini Zambia wa uzalishaji umeme kwa kutumia Gesi itokanayo na mafuta (LPG).

Taifa Gas itashirikiana na Kampuni ya wazawa ya Delta Marimba Limited kuzalisha megawati 100 za umeme ambao utaingizwa kwenye gridi ya Taifa la Zambia.

Makubaliano hayo yametangazwa na pande hizo mbili leo Jumatatu, Juni 26, 2023 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Taifa Gas, Hamis Ramadhan amesema, kampuni hiyo itakua ya kwanza ya uzalishaji wa umeme kwa kutumi gesi ya LPG na mradi huyo utatekelezwa kwa Taifa hilo maarufu kwa uzalishaji wa shaba.

Vilevile Ramadhan amesema Taifa Gas itatazama fursa nyingine za biashara ya gesi ikiwemo matumizi ya kupikia biashara amabyo tayari inafanywa hapa nchini.

“Taifa Gas itaongoza uwekezaji kwenye mradi huu nchini Zambia ambao utafikia dola za Marekani milioni 100 (zaidi ya Sh240 bilioni),” amesema.

Ramadhan amesema, “uamuzi huu wa kuwekeza Zambia umechochewa na mazingira mazuri ya uwekezaji na sera madhubuti za Rais Hakainde Hichilema na chama chake cha UPND.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa Gas, Rostam Azizi amesema, Tanzania na Zambia zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu, “na uhusiano huu unapaswa kuuendeleza kwenye shughuli za kiuchumi.”

“Zambia ni nchi ambayo kwa sisi Watanzania tumekuwa na historia nao wakati wa shida na raha na mambo yanapokwenda vizuri kwenye uchumi maana yake tunapaswa kutafasiri mahusiano ya nchi mbili hizi kwa kuangalia fursa,” amesema.

Rostam amesema kampuni zake zitaendelea kutafuta fursa maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Screenshot_20230627_052517_Instagram.jpg
 
Mkongwe wa muziki, Busta Rhymes usiku wa kuamkia leo Juni 26 katika tuzo za BET alipewa tuzo ya heshima, likiwa ni tukio jingine la pekee lililowakosha wapenzi wa muziki katika hafla hiyo.

Busta Rhymes ambaye kwa miaka 37 amekuwa akihudumu kwenye tasnia cha muziki nchini Marekani alikabidhiwa tuzo huyo akishangiliwa na idadi kubwa ya mashabiki waliofurika ukumbini hapo.
Screenshot_20230627_052614_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom