Makapuku Forum

Makapuku Forum

Huyu ndiye mwamba aliyemtikisa Putin.. anaitwa Yevgeny Prigozhin. Historia na makuzi yake vimejaa utata mwingi.

Aliwahi kukaa gerezani karibu miaka 10 akitumikia kifungo cha miaka 13 kutokana na unyang'anyi na wizi wa kutumia silaha.

Baada ya kutoka gerezani alianzisha kampuni ya migahawa huko Urusi, mgahawa wake maarufu sana ulikuwa unaelea majini.

Putin alipenda sana mapishi yake na akawa anawapeleka wageni wake kwenye migahawa ya huyu mwamba.

Taratibu urafiki wao ukakuwa na kuimarika, akaanza kupata tenda za kulisha Ikulu. Baadae akaibukia kumiliki jeshi binafsi linaloitwa Wagner. Wanajeshi wake wengi ni mamluki na wengi wao ni wafungwa wa Kirusi.

Jeshi la Wagner linakodiwa na mtu yeyote na wanafanya kazi yoyote ile unayotaka wewe.. ukiwapa kazi ya kumtoa ex wako kucha, wao wanafanya, au ukitaka wamgonge gonge na nyundo kwenye ugoko wao hawana hiyana..ni hela yako tu.

Huko Syria wanajeshi hawa walilaumiwa kuuwa watu kwa nyundo na kuwabanika.

Huku Afrika Wagner wamehusika kulinda baadhi ya viongozi wa Afrika na kuleta vurugu katika baadhi ya nchi za Kiafrika. Idadi kubwa ya wanajeshi hawa wako Afrika ya Kati, Mali, Sudan na Msumbiji.

Wagner wameongoza uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kuuteka mji wa Bakhmut. Sasa urafiki na Putin umefika mwisho kwa madai kwamba viongozi wa Jeshi la Urusi wanamhujumu.

Juzi Mwamba akaongoza vikosi vyake kwenda Moscow, kwa madai kwamba anataka viongozi wa jeshi akiwemo waziri wa Ulinzi waondolewe. Vikosi vikafika mpaka Kilomita 200 kutoka Moscow.

Putin akawasha ndege akaikimbia Moscow. Viongozi wa Magharibi na Amerika wanasema tukio la jana limefunua udhaifu wa Putin.

Putin akamtuma msela wake Rais wa Belarus. Wakakubaliana, mwamba akasitisha uasi akageuza majeshi .

Sasa mwamba anaenda kuishi Belarus na wanajeshi wake hawatashitakiwa kwa tukio la jana.Lakini kuna tetesi kwamba mwamba hatakaa muda mrefu Belarus bali ataondoka na kuja kuishi msituni huku Afrika....!!
Screenshot_20230625_214519_Instagram.jpg
 
Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo June 25,2023 akiwa Dodoma kuongoza mbio za JKT Marathon ameonesha kutoridhishwa na Wachezaji wa kigeni pekee kutawala soka la Tanzania na kuishauri Wizara kukaa chini na TFF kujadiliana namna ya kuzalisha Wachezaji wazawa wenye ubora na umaarufu.

“Mimi bado kilio changu tukazanie kuinua vipaji vya Wachezaji wa ndani, Yanga kila siku anasifiwa Mayele, Bangala, Diarra, anasifiwa kule Baleke, Chama, Ntibanzokiza sasa katika wale wanaosifiwa Wachezaji wa Tanzania hawamo, Simba utasikia Baleke sio mchezo, kacheza mechi 6 tu, Hat-trick sijui ngapi?, Yanga kule utasikia Mayele sasa sijui akiondoka watapata nani?” ——— Dr. Kikwete.

"Hii ni seruous sio jambo dogo, nilisema siku moja nilialikwa sherehe za Yanga kwamba mbona mnachukua wengi nje jibu lao TFF wakaongeza kutoka Wachezaji wanane wakapeleka 12 wa kigeni,, siwaonei lakini kuna tatizo”

“Tatizo lenu mnasukumwa na Viongozi wa hizi Klabu kubwa ambao wao shida yao ni kushinda tu lakini katika kushinda huku Wachezaji wa Tanzania wanashinda?, hili lenu Naibu Waziri (Mwana FA) na Waziri wako mkae na TFF muangalie tunafanyaje, sisemi tusichukie wa nje tujiulize kwanini wanaong'ara ni Wachezaji wa nje, full stop” ——— amemalizia Rais Mstaafu Kikwete.
Screenshot_20230626_042931_Instagram.jpg
 
Baada ya baadhi ya Wananchi wa Kitongoji cha Chamamba maarufu kama 'Sumbawanga ndogo' Mkoani Iringa kupata taharuki baada ya kudai kumuua Mnyama wa ajabu, Mtaalamu wa Wanyama pori ameiambia @ayotv_ kuwa Mnyama huyo sio wa ajabu bali kilichotokea ni Wananchi hao kushindwa kumtambua.

Mtaalamu huyo baada ya kutazama picha zilizosambaa mtandaoni amesema Mnyama huyo ni Komba (Bush Baby) na kwamba Tanzania inao Komba wakubwa na wadogo ambapo hujulikana pia kama Watoto wa msituni (Bushbabies/Galagos) wakiwa ni Wanyama wadogo wenye asili ya nyani (primate) katika kundi la mamalia (wanaozaliana) na huonekana zaidi usiku( nocturnal) wanapokuwa wanakula na vilevile uwezo wao wa kuona mchana ni mdogo ndio maana ni nadra kuwaona mchana.

Mapema leo Wananchi wa Kijiji cha Mkombilenga walichukua maamuzi ya kumuua Mnyama huyo kwa imani kuwa anatumika kishirikina baada ya kugundua kuwa ana sauti kama ya Mtoto mchanga na sehemu zake za siri ni kama za Binadamu Mwanaume.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliiambia @ayotv_ kuwa walikiona kiumbe hicho juu ya mti na walipoulizana hata na Wazee wa Kijiji walishindwa kumfahamu kwakuwa ana mikono kama Binadamu na amechanjwa masikioni.

Mtaalamu wa Wanyamapori aliyeongea na @ayotv_ amesema "Komba wana macho makubwa na mikono yenye vidole kama Binadamu sawa na aina nyingine ya nyani, jina la Bushbaby lilitokana na Wanyama hawa kulia kama Watoto na kama unakaa maeneo yenye miti mingi usiku utawasikia na unaweza kuhisi kuna Mtoto analia msituni"
#
Screenshot_20230626_043035_Instagram.jpg
 
Ikulu ya Urusi (Kremlin) imesema Kiongozi wa Jeshi binafsi la Urusi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, amekubali kwenda uhamishoni nchini Belarus hii ni baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuafikiana na makubaliano ya msamaha kwa Kiongozi huyo ili kusitisha uasi.

@dw_kiswahili imeripoti kuwa makubaliano hayo yanaonekana kusitisha kitisho kuwa kundi hilo, linaweza kuivamia Urusi.

Mzozo wa muda mrefu kati ya Prighozin na Viongozi wa kijeshi juu ya uendeshaji wa operesheni ya Urusi huko Ukraine ulishikankasi siku ya Jumamosi, vikosi vya Wagner vilipochukua udhibiti wa kambi muhimu ya Jeshi la Urusi katika mji wa Rostov-on-Don.

Putin alishutumu hatua hiyo kama uhaini na kuapa kuwaadhibu Wahalifu, akiwatuhumu kwa kuisukuma Urusi kwenye ukingo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Screenshot_20230626_043144_Instagram.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani Jijini Arusha leo June 25,2023 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba siku hizi kuna mtindo mpya wa Watu kupasua bomba linalotoa moshi wenye sumu kwenye gari na kuchukua unga uliopo ndani yake na kuchanganywa na cocaine au heroin kisha Vijana wanavuta na kupata madhara ikiwemo kufariki.

“Tumepata taarifa kwamba kuna bidhaa zinaingizwa nchini lakini zinachanganywa na dawa za kulevya na nimeona kwenye banda la maonesho wamenionesha wanasema Mtu anaweza kuja na unga lakini ule unga usiwe wa kawaida”

“Kuna bidhaa pia zinachanganywa na cocaine na heroin ambazo zinaweza kuwa sumu, siku hizi kuna mtindo wanapasua bomba linalotoa moshi kwenye gari ndani yake kule kuna unga fulani unaosababisha control ya ule moshi sasa ule unatolewa huko kwenye magereji yetu unapelekwa kwenye maunga Vijana wetu wanayotumia lakini ule moshi una sumu kubwa sasa ukichanganya na unga wanaotumia wakijidunga ndio maana unasikia Mateja wanaanguka wanakufa, niombe Mamlaka zinazohusika tuliangalie hili”

“Wenye gereji pia walitazame hili magari wanayopelekewa Mafundi wao wanapasua wanatoa unga wanakwenda kuua Watu”
Screenshot_20230626_043237_Instagram.jpg
 
Chelsea wameweka ofa mezani kwa nyota wa Arsenal aliyeweka rekodi kuwa mchezaji mdogo zaidi kucheza Premier League, Ethan Nwaneri.

Kiungo huyo bado hajasaini mkataba akitokea Academy ya Arsenal. Japo bado hajafanya uamuzi madhubuti juu ya mustakabali wake, kwa hiyo milango yote iko wazi, lakini Chelsea wana push sana kupata saini yake.

Screenshot_20230626_043442_Instagram.jpg
 
Mbali ya ofa nono ya zaidi ya Pauni 40 milioni kwa mwaka kutoka Saudi Arabia, mshambuliaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, 30, amepokea ofa pia kutoka Lazio.

Staa huyu wa kimataifa wa Ivory Coast mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu hadi sasa bado hajafanya uamuzi wa wapi atacheza kwa msimu ujao.

Screenshot_20230626_043940_Instagram.jpg
 
Ángel Di Maria atakuwa mchezaji mpya wa Benfica wiki ijayo, kama dalili zilivyoonyeshwa siku chache zilizopita. Mkataba wa maneno umekamilika na kufungwa. #Benfica

Di Maria atasaini hadi Juni 2024, mkataba wa mwaka mmoja - pande zote mbili zilitarajia kusaini wiki ijayo, hati ziko tayari.
Screenshot_20230626_044029_Instagram.jpg
 
Borussia Dortmund imeripotiwa kuamsha upya mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Elanga baada ya kushindwa kunasa saini yake Januari. Elanga, 21, hakuwa na wakati mzuri msimu wa kwanza wa kocha Ten Hag, ambapo alishindwa kufunga bao akaishia kuasisti mara mbili.
Screenshot_20230626_044118_Instagram.jpg
 
Arsenal wanafanyia kazi dili la kumnasa beki wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Ajax Jurrien Timber

Arsenal wamewasilisha ofa ya kwanza ya Pauni Milioni 30 lakini Ajax wanahitaji Pauni Milioni 50 , licha ya kwamba Arsenal wanaamini bei itapungua. Maslahi binafsi ya mchezaji sio shida (davidornstein)

NOTE: Arsenal mbona wamekuwa serious club ghafla hivi? Usajili wa Timber ukifanikiwa wanapata mchezaji ambaye

● Anaweza kucheza nafasi ya Ben White katika jukumu lile la kubaki nyuma na kutengeneza BACK 3 ( Timber Saliba na Gabriel )

● Anaweza kucheza kama beki wa kati endapo mmojawapo Saliba au Gabriel akikosekana

● Mara kadhaa akiwa Ajax amewahi kucheza namba 6

● Silaha nzuri sana kwenye build up , kiufundi yupo vizuri akiwa na mpira maana yake inakuwa rahisi kukabiliana na pressing ya wapinzani

Screenshot_20230626_044245_Instagram.jpg
 
Brighton wamemtambua mshambuliaji wa Ajax Mohammed Kudus, 22, kama main target msimu huu baada ya Mghana huyo kukataa kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Eredivisie(Mail)

Screenshot_20230626_044334_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom