Makapuku Forum

Makapuku Forum

Aisee Dunia inakwenda fasta sana.. tumemaliza ya Titanic yanakuja ya Urusi ..sasa moto unawaka huko Urusi.

Vikosi vya wanajeshi vimeasi vinaongozwa na kundi la wanajeshi mamluki la Wagner. Rais wa Urusi Vladimir Putin ameapa 'kuwanyorosha' wanajeshi hao na amewataka wajisalimishe mara moja.

Kiongozi wa kundi hilo Bwana Yevgeny Prigozhin ambaye anadaiwa kuwa rafiki wa karibu wa Putin amesema yeye hataki kufanya mapinduzi lakini anataka mabadiliko katika Uongozi wa jeshi la nchi hiyo.

Kiongozi huyo amedai uvamizi wa Putin Ukraine ulikuwa umejaa uongo mtu na hakukuwa na sababu zozote za msingi za Urusi kuivamia Ukraine isipokuwa ilichochewa sana na Waziri wa Ulinzi Bwana Sergei Shoigu ili apande cheo.

Kundi la Wagner limehusishwa na matukio ya kikatili zaidi sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Afrika ya Kati, Syria, Msumbiji na vita inayoendelea huko Ukraine. Mpaka sasa kundi hilo limetangaza kuteka miji miwili katika nchi ya Urusi..je huu ndio utakuwa mwisho wa utawala Putin..!?
Screenshot_20230624_135329_Instagram.jpg
 
Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala limepiga marufuku uingizaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa kinywaji cha kuongeza nguvu kiitwacho AKAYABAGU baada ya kufanya uchunguzi na kugundua kuwa kinywaji hicho hakijawahi kusajiliwa na Baraza hilo Nchini.

Taarifa ya Baraza hilo imesema pia limegundua kuwa kimechanganywa na dawa ya kisasa aina ya sildenafil (Viagra majina mengine Erecto ama Vega) jambo ambalo ni kinyume cha sheria hivyo Watumiaji wamedanganywa na Wahusika ambapo kwa kitendo cha kuchanganywa na Sildenafil (Viagra) kinywaji hiko sio tena cha tiba asili bali ni kinywaji chenye viagra.

“Kuanzia tarehe 23/06/2023 Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linapiga marufuku uingizaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa kinywaji hiki kote nchini, yeyote atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake na vilevile atakayepatikana akiwa na kinywaji cha AKAYABAGU atakuwa ametenda kosa na ataweza kushitakiwa kwa mujibu wa Sheria”
Screenshot_20230624_135614_Instagram.jpg
 
Ni siku zaidi ya kumi tangu simba watoroke Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kuvamia makazi ya Watu na kula mifugo huku taharuki ya Watu ikiwa iko juu, @ayotv_ imeshuhudia juhudi zinazofanywa na Jeshi la Uhifadhi zikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego kwa kutumia helikopta angani ili kuwabaini simba hao walipo na kuwadhibiti.

Hadi sasa hakuna Mtu yeyote aliyepata madhara kutokana na simba hao lakini wamejeruhi na kula mifugo kama ng’ombe, nguruwe ,mbuzi na kuku huku hofu ikitanda kwa Wananchi wa maeneo ya Tanangozi ,lyamgungwe , Kiponzelo na Maboga.

RC Dendego amewataka Wananchi wawe waangalifu kwa kuwahi kumaliza shughuli zao na kurejea majumbani katika kipindi hiki ambacho bado juhudi zinaendelea kuwatafuta simba hao.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki amesema walijaribu kuweka mitego mbalimbali kuwakamata lakini imeshindikana kwasababu simba hao wanahama kwa kasi sana.
Screenshot_20230624_135732_Instagram.jpg
 
Klabu ya Yanga imevuna kiasi cha Sh7 bilioni kwa mwaka kutokana na wadhamini mbalimbali wa timu hiyo.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa klabu hiyo, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kiasi hicho kimepatikana kwa msimu wa 2022/23 uliomalizika hivi karibuni.

"Tunawashukuru na kujivunia sana wadhamini wetu kwa sababu katika michezo mbalimbali tumetumia gharama nyingi hivyo tunajivunia uwepo wao," amesema.

Aidha Hersi aliongeza mbali na fedha hizo zinazotoka kwa wadhamini kama SportPesa, Azam TV na Kampuni ya Haier inayojihusisha na usambazaji na utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya ofisini na majumbani, Yanga pia imepata Sh3.5 bilioni kwa mwaka kutokana na ushiriki wao katika mashindano mbalimbali.

Yanga inafanya mkutano wake mkuu leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) ikiwa ni wa kwanza tangu uwaingize madarakani Rais wa klabu hiyo, Hersi Said, Makamu wa Rais, Arafat Haji na wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa Julai mwaka jana.
Screenshot_20230624_135839_Instagram.jpg
 
Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said akizungumza leo katika Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo amesema wameingia makubaliano na benki kubwa tatu NMB, CRDB na NBC ambazo sasa zitakuwa na uwezo wa kusajili wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kupitia matawi yao yaliyopo sehemu mbalimbali nchini.

Benki hizo zitakuwa na uwezo wa kusajili taarifa za wanachama, kupokea malipo ya uwanachama na kutoa kadi za wanachama papo kwa papo.

Screenshot_20230624_135928_Instagram.jpg
 
Club ya Yanga leo imemtangaza Miguel Angel Gamondi (59) Raia wa Argentina kuwa Kocha Mkuu wake mpya.

Miguel Angel Gamondi amewahi kufundisha timu mbalimbali ikiwemo Wydad Casablanca ya Morocco, Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini na CR Belouzdad ya Algeria.

Kocha Miguel Angel hadi anatangazwa Kama Kocha Mkuu wa Yanga alikuwa amefundisha jumla ya vilabu 13 katika maisha yake ya soka na Timu ya Taifa ya Burkinafaso
Screenshot_20230624_150935_Instagram.jpg
 
Kutoka katika Mkutano Mkuu wa Yanga SC wameonesha muonekano wa uwanja wataojenga Jangwani utakaokuwa na uwezo wa kuchukua Mashabiki 15,000 hadi 18,000.
Screenshot_20230624_151042_Instagram.jpg
 
Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said amesema Young Africans SC kwa msimu wa 2022-2023 imetengeneza kiasi cha Tsh. 3,550,000,000 kupitia mafanikio yatokanayo na ushiriki wa Klabu hiyo katika mashindano mbalimbali.

Akiongea kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo leo Jijini Dar es salaam, amesema “Young Africans SC kwa msimu wa 2022-2023 tumeweza kutembelea vituo 20 vya Waru wenye uhitaji na kuchangia damu chupa 637 na kuwa Klabu na Taasisi ya kwanza kutambulika rasmi na Wizara ya Afya katika uchangiaji damu kupitia Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Young Africans SC"

“Rasmi Young Africans SC imeingia makubaliano na Benki kubwa tatu nchini CRDB, NMB na katika huduma ya Usajili wa Wanachama Kidigitali kote nchini”

“Young Africans SC kwa msimu wa 2022-2023 wameweza kutengeneza kiasi cha Tsh. 7,068,127,083 kupitia wadhamini wetu ambao ni Sportpesa (Mdhamini Mkuu), Azam TV, Haier , GSM Group , Jembe Energy, CRDB Bank , Unicef , Smile, Robbialac”
Screenshot_20230624_151254_Instagram.jpg
 
YANGA YATENGE 20 BILIONI MSIMU UJAO

Yanga imetangaza bajeti ya Tsh 20.8 bilioni kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano ya ndani ya nchi [Ligi Kuu, Kombe la Azam Sports Federatio] pamoja na mashindano ya kimataifa [CAF].

Mkurugenzi wa Fedha wa Yanga, Sabri Sadick amesema kupitia bajeti hiyo anaamini italeta tija kwa klabu kwa msimu ujao na kufanya vizuri zaidi.

Kwenye vyanzo vyetu tuna Tsh. 14.8 bilioni, kwa hiyo tuna upungufu wa Tsh. 6 bilioni ambazo tunafanya jitihada za haraka kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali tuweze kufikia malengo.

Sadick amesema bajeti ya msimu ujao ni zaidi ya msimu uliopita ambapo Yanga ilitumia Tsh. 17.3 bilioni huku bajeti ikiwa ni 17.8 bilioni hivyo kubakiwa na Tsh. 581 milioni.

Kwa mijibu wa Sadick, ongezeko la bajeti kwa msimu ujao ni kwa sababu ya kuongeza ufanisi zaidi kwa klabu ya Yanga.

Sadick amesema bajeti ya msimu uliopita ilitokana na fedha za wadhamini mbalimbali wa klabu, mauzo ya jezi, mauzo ya wachezaji, viingilio vya mechi, ada za wanachama, mikopo na mapato mengine.
Screenshot_20230624_155129_Instagram.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Taarifa.
.
Young Africans SC kwa msimu wa 2022-2023 wameweza kutengeneza kiasi cha Tsh. 7,068,127,083 kupitia wadhamini wetu ambao ni:
.
1. Sportpesa (Mdhamini Mkuu)
2. Azam TV
3. Haier
4. GSM Group
5. Jembe Energy
6. CRDB Bank
7. Unicef
8. Smile
9. Robbialac
.
NB:
.
Screenshot_20230624_155244_Instagram.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Mishahara.
.
Yanga wanalipa kiasi cha Tzs 5,408,780,044 kama mishahara kwa mwaka, hili ni kadirio la Tzs 450,731,670 kwa mwezi.
.
Kwa uwezo huo wa kulipa mishahara wa Yanga kwa mwezi maana yake kama Nabi alitaka Milioni 100 na Kama Mayele atataka walau milioni 50, wanainyima Yanga uwezo.
.
Kwa Uwezo huu wa Kulipa Mishahara Ni ngumu Yanga kuwa na Kocha wa Kiwango, Wachezaji wakubwa Afrika sababu ili uwe na wachezaji wakubwa lazima uwe na uwezo wa Mishahara.
.
Hesabu Rahisi tu, Yanga haiwezi kumiliki wachezaji Watano wa mshahara wa Milioni 50 na Kocha wa Milioni 100 sababu itavuka kiwango chao cha Mishahara.
.
Yanga Bado timu ndogo Barani Afrika sababu bajeti yake sio ya kikubwa, Ukiangalia Ripoti hii unaweza kujiuliza wamefikaje Fainali ya #TotalEnergiesCafcc2023.
.
NB:
Tuna safari ya Kukua.
.
Screenshot_20230624_155403_Instagram.jpg
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Thank You.
.
Pengine Mashabiki wa Yanga hawakupaswa kumtuka Feisal Salum "Fei Toto" sababu kwa mara ya Kwanza baada ya muda mrefu klabu inasoma ripoti ya mapato yenye mjumuisho wa fedha za mauzo ya mchezaji.
.
"Thank You" Zote za Msimu huu ni Kazi Bure, biashara kichaa hakuna mauzo ni kama kupunguza wafanyakazi hewa, wanamaliza mikataba na kuondoka zao bure, pengine wangeambiwa safari njema.
.
Milioni 200 za Kitanzania, zimeongezeka kwenye ripoti ya mapato kutoka kwa Feisal Salum, Sio Morrison, sio mchezaji yoyote aliyeondoka Yanga hivi karibuni. Wengi wameondoka na bado wanadai.
.
Feisal Salum awe "Case Study" ya Mauzo ya wachezaji, awafumbue viongozi kwamba inawezekana wakapiga hela kutokana na mauzo ya wachezaji na sio mizengwe na manyanyaso. Mchezaji akiwa bora unaweza kumuuza.
.
Thank You ya Fei Toto ni Tzs Milioni 200.
.
YOWERI MUSEVENI
.
NB:
Thank you For Understanding.!
Screenshot_20230624_155550_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

MBEYA CITY NDAGHA FHIJOHatushabikii timu kwasababu ya Wachezaji au historia bali kutokana na mioyo yetu kujikuta sehemu ya timu, inakuwa maisha yetu na sehemu ya furaha yetu hii ni kaulimbiu ya Mashabiki wa soka duniani kote.

CITY leo mmeaga rasmi Premier League, a team like no other which streets will never forget! Waliifanya mitaa ya Mama John mpaka Iwambi, Nzovwe mpaka Iyunga kujiona ni sehemu ya Baba na Mama mmoja wa kuitwa Mbeya City.

Goodbye to coaster zote zilizojaza Mashabiki kutoka Ipinda huko Kyela, Makongorosi huko Chunya, Vwawa huko Mbozi, Kiwira huko Rungwe! One People One Color! One City one Team! Iliwezekana Mashabiki kushikamana na kuzisahau Kariakoo kwa miaka ile, kumbukumbu njema zitasalia daima mioyoni mwa WanaPremier League.

Nilikuwepo Mbeya kama Mwanafunzi niliyeenda kusoma, niliwaona Wanyakyusa, Wasafwa kwa Wandali wakiwa nyuma ya hii timu! Kama zao maarufu ilikuwa ni Parachichi basi timu maarufu ilikuwa City, kama damu ni nyekundu basi machozi ya City yalikuwa zambarau.

Gone are the days, the rest ni memories! Ndagha Fijho City! The streets will never forget, Go well Boys and hopeful our path will cross again! Kama kuna uonevu wowote basi SYOSA AMENYE KYALA, KYALA NNUNU

Screenshot_20230624_212656_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

MBEYA CITY hii picha ina maana kubwa sana kwenu, mliziweka hai ndoto za Vijana kutoka mitaa yote ya Jiji la Mbeya sio Ilemi wala Sinde, sio Iyunga wala Uyole kila mmoja alijiona akivaa uzi wa City na kuziishi ndoto zake, wapo mliobadili kurasa za maisha yao kutoka wimbi la ulevi maybe, kibaka likely na wakauvaa mwili mpya wa kuitwa soka, City ikawa madhahabu ya vipaji kusifu na kuimba, kesho ilipatikana kwenye dimba la Sokoine.

Wingu jeusi kwenye historia ya jiji la Mbeya, Mhuni wa Morogoro ningekuwa Ripota wa BBC ningesema Darkest day in Mbeya City history! Lakini lazima mbegu ioze, mvua inyeshe na mmea ustawi! Wao wanaiita timu ya mpira ila kwenu ni maisha, ni utamaduni wenu na ni lifestyle yenu! Mbeya city is the city you live in.

OBJECTIVE TO WIN! Ndio kunayo kesho tena ya watoto wa Mbeya kuziishi ndoto zao, mmeenda lakini sote tunaamini mtarejea kwakuwa City ni mpango wa Mungu kwa ajili ya watu wake, lakini watoto wa Mungu kuna vikombe hatupaswi kuviepuka! Kama mnaitaka Pepo ilikuwa lazima Kifo kitokee, mitaa ya Mbeya inasubiri ufufuko wenu baada ya msimu mmoja.

The Premier League will miss you! Lakini naamini Nkhamu zangu, its not a goodbye but its a see you soon! Ndoto za watoto wa Mbeya zinapaswa kuishi, go well and come back soon Boys

I LOVE YOU SO MUCH MY MBEYA BROTHERS AND SISTERS! Objective to WIN, Ndagha Fijho

Screenshot_20230624_212818_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

SIMBA IMEMPA MKONO WA KWAHERI CAPTAIN & LEGEND JONAS MKUDE

- Hii ni taarifa ya klabu kuwa imeachana na Mchezaji wake aliyeitumikia klabu kwa muda mrefu zaidi, ghafla ikaibuka agenda ya Mkude kutoagwa kwa heshima! Well ni agenda nzuri sana na wahoji wana hoja kubwa sana tena ya afya.

Lakini Uandishi wa Habari upo huru sana, linapokuja suala kama hili kuna pande mbili hapo ambao wote wanaweza kukupa ufafanuzi! Kuna JONAS MKUDE (Mchezaji) na SIMBA (Mwajiri wake wa zamani) hawa wote wanaweza kukupa majibu ya nini kifuatacho.

Nikalazimika kumpigia Afisa mmoja wa Simba jana usiku kumuuliza kuhusu suala la Jonas Mkude nae akanipa majibu yake juu ya hoja za watu wengi kama ifuatavyo.

Kaka taarifa ya Mkude kuagwa ndio mwisho pale? HAPANA, kwanza tumetoa taarifa kama inavyotakiwa hata EPL hutoa majina ya wachezaji wote wanaowaacha na wanaoendelea nao, sisi tumetoa majibu ya wachezaji tunaowaacha.

Nini kifuatacho? Ofcourse Jonas ni Mchezaji Mwandamizi na ameitumikia klabu kwa mafanikio makubwa sana, hivyo tutampa mwaliko maalum wa yeye kuja Simba Day na tutamuaga pamoja na Wanasimba.

- Mpaka sasa Simba wameaga kwenye hatua mbili! Cha kwanza taarifa rasmi ya klabu ambayo ipo Simba App, kisha video ya Mkude Jonas akiongea ambayo ipo Youtube pia akiappreciate na kuaga, hatua ya tatu ni uwanjani Simba Day kama ambavyo Afisa wa klabu alinipenyezea.

Ikumbukwe kuaga sio Kanuni bali utamaduni, Ulaya na Afrika baadhi ya klabu huishia press release pekee ila Simba wamesogeza mpaka video na Simba Day atapewa chance.

Huu ndio upande ambao haukuguswa ambao ndio upande wa Viongozi wa Simba ambapo wengi walikwepa kuwauliza na wakawapa majibu! Uandishi unaagiza sana kubalance vitu kwa pande zote.

Screenshot_20230624_213002_Instagram.jpg
 
DORTMUND WAO NA ELANGA
.
Borussia Dortmund imeripotiwa kuamsha upya mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Elanga baada ya kushindwa kunasa saini yake Januari. Elanga, 21, hakuwa na wakati mzuri msimu wa kwanza wa kocha Ten Hag, ambapo alishindwa kufunga bao akaishia kuasisti mara mbili.
Screenshot_20230625_144752_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom