Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wanafunzi 150 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kukamilisha mwaka wao wa mwisho wa masomo.

Akiongea wakati wa kuwakaribisha wanafunzi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa hali ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini Sudani imesababisha kufungwa kwa Vyuo na baadhi ya shughuli kusimama hivyo Wataalamu hao kushindwa kuendelea na ratiba yao ya masomo ya kawaida.

ā€œWanafunzi hawa wapo mwaka wa tano wa shahada ya kwanza ya utabibu, ambapo katika mwaka huo, mafunzo hufanyika kwa vitendo zaidi, hivyo Madaktari hawa Wanafujzi watafanya mzunguko (Rotation) katika idara mbalimbali ikiwemo idara ya upasuaji chini ya usimamizi wa Madaktari bingwa ili kuhakikisha wanapata maarifa yanayotakiwaā€

Amesema kuwa MNH itatoa fursa kwa Wataalamu hao kujifunza kama ambavyo inatoa kwa Wataalamu wengine wa ndani na nje ya Nchi na hata baada ya kumaliza masomo kama watapenda kufanya mafunzo tarajali (Intenship) MNH itawapa nafasi hiyo.

Kwa upande wake Ruba Anwar Salih ambaye ni Kiongozi wa kundi la Wanafunzi hao amesema kuwa wamefurahi kupata fursa ya kuendelea na masomo katika Hospitali kubwa na yenye wataalamu wa kutosha, ni imani yao kwamba watapata fursa nzuri ya kujifunza.
Screenshot_20230619_150244_Instagram.jpg
 
Mtu mmoja amefariki na wengine wanane wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Kingolwira Manispaa ya Morogoro barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam.

RPC wa Morogoro, Alex Mkama amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo ambapo gari moja lililobeba mafuta ya petroli (Howo) lililokuwa linatokea Dar es salaam kuelekea Morogoro liligongana na basi la abiria la Kampuni ya Johanvia linalofanya safari zake Musoma - Dar es salaam na kisha basi hilo kuligonga gari la Polisi lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara.

RPC Mkama amesema aliyefariki katika ajali hiyo ni Mtuhumiwa Yohana Mwamlima (40) ambaye inadaiwa alikuwa akitokea Musoma kupelekwa Dar es salaam, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari la mafuta, Nkandi Konokwa (61) ambaye alikuwa anaendesha gari kwa mwendokasi na kwa sasa anashikiliwa na Polisi.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro amekiri kupokea mwili mmoja wa marehemu na majeruhi wanane wakiwemo Wanaume watano na Wanawake watatu.
Screenshot_20230619_150501_Instagram.jpg
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemwelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Afya kufanya uchambuzi wa kina kwenye kada za afya kuanzia ngazi ya Taifa mpaka Zahanati ikiwemo kada ya Wataalamu wa Maabara ili kuweka kipaumbele sahihi katika kuajiri Wataalamu wa kada ambazo zina upungufu mkubwa katika Sekta ya Afya kulingana na mahitaji ya Nchi.

Waziri Ummy amesema hayo akiwa anajibu hoja za Wataalamu wa Maabara waliohoji mitandaoni kuhusu changamoto ya ajira za Wataalamu wa Maabara zinazotolewa na Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

"Wataalamu wa Maabara ni kada muhimu katika utoaji huduma bora za Afya, ni kweli kuwa tiba sahihi ya ugonjwa inategemea huduma za uchunguzi wa magonjwa (Maabara na Radiolojia), kuhush idadi ndogo ya Wataalamu wa Maabara nimesikia kilio chenu na tayari nimeshamuelekeza Katibu Mkuuā€

Waziri Ummy pia amesema muundo mpya unaoelekea kuanza July 1, 2023 utakuwa na Kurugenzi kamili ya Huduma za Uchunguzi (Directorate of Diagnostic Services) ambayo kabla ya hapo ilikuwa ni eneo (Section) chini ya Idara ya Huduma za Tiba (Directorate of Curative Services).
Screenshot_20230619_150551_Instagram.jpg
 
Wanafunzi 150 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kukamilisha masomo yao kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwakaribisha wanafunzi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa, Mohamed Janabi amesema hali ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini Sudani yamesitisha baadhi ya shughuli ikiwemo kufungwa kwa vyuo.

ā€œWanafunzi hawa wapo mwaka wa tano wa shahada ya kwanza ya utabibu, ambapo katika mwaka huo, mafunzo hufanyika kwa vitendo zaidi, hivyo madaktari hawa wanafunzi watafanya mzunguko (Rotation) katika idara mbalimbali ikiwemo idara ya upasuaji chini ya usimamizi wa madaktari bingwa ili kuhakikisha wanapata maarifa yanayotakiwaā€ amesema Profesa Janabi

Profesa Janabi amesema MNH itatoa fursa kwa wataalamu hao kujifunza kama ambavyo inatoa kwa wataalamu wengine wa ndani na nje ya nchi na hata baada ya kumaliza masomo hayo iwapo watapenda kufanya mafunzo tarajali (Intenship) watapatiwa nafasi hiyo.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa chuo cha UMST, Profesa, Mamoun Homeida ameeleza kufurahishwa baada ya kuona wanafunzi kutoka chuo anachokisimamia wamepokelewa vizuri na kwamba jambo hili limetokana na mahusiano ya kindugu yaliyopo baina na Tanzania na Sudan.

Naye kiongozi wa kundi la wanafunzi hao, Ruba Anwar Salih amesema wamefurahi kupata fursa ya kuendelea na masomo katika hospitali hiyo kubwa na yenye wataalamu wa kutosha nchini huku akisema anaamini watapata fursa nzuri ya kujifunza.
Screenshot_20230619_150716_Instagram.jpg
 
Mfanyabiashara, Leonard Lubuye amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kughushi mkataba wa kukodisha eneo la UDA kwa Kampuni ya Simon Group Limited na kuisababishia hasara ya Sh 14 bilioni, shirika hilo.

Lubuye amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu Juni 19, 2023 na kusomewa kesi ya Uhujumu uchumi namba 30/2023 yenye mashtaka hayo na wakili wa Serikali, Ipyana Mwakatobe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amir Msumi.

Katika mashtaka hayo, Lubuye anadaiwa kughushi mkataba wa kukodisha eneo la UDA lenye ukubwa wa ekari 13 lililopo Kurasini kwa Kampuni ya Simon Group Limited kwa gharama ya Sh400 milioni kila mwaka ndani ya kipindi cha miaka 10, wakati akijua hati hiyo ya mkataba ni ya uongo.

Screenshot_20230619_150813_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, mratibu wa maandamano hayo, Deus Soka katika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.

Screenshot_20230619_150939_Instagram.jpg
 
Mkurugenzi mpya wa jiji la Dodoma, John Kayombo akikabidhiwa ofisi pamoja na nyaraka mbalimbali na mkurugenzi aliyehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, John Mafuru.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dodoma leo jumatatu, juni 19, 2023.

Kabla ya uteuzi huo Kayombo alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa miaka miwili, pia alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Musoma.

Kayombo pia alikuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kwa miaka mitatu.
Screenshot_20230619_151207_Instagram.jpg
 
MILIONI 600 KULIPWA PITSO NA KIKOSI KAZI
.
Kocha Pitso Mosimane akiwa na benchi lake la Ufundi; Kocha msaidizi Maahier Davids, Kocha wa makipa Hamad Alyami na Kocha wa viungo Kelly Zwane wamesaini kandarasi ya Miaka mitatu kuinoa klabu ya Al Wahda inayoshiriki Ligi Kuu ya UAE
.
Mosimane anatarajiwa kulipwa dola 130,000 zaidi ya sh 300milion huku wasaidizi wake wakilipiwa Sh 100milioni.
Screenshot_20230619_151317_Instagram.jpg
 
YANGA KUANZA NA KIZZA
.
Wakati Yanga inaonekana kuna wachezaji kadhaa wakubwa wakaondoka kwenye timu hiyo, mabosi wa timu hiyo hawajalala wameanza mazungumzo na Kizza Mustafa beki wa kushoto ambaye kwa kipindi kirefu akiwa anaitumikia timu ya KCCA ya Uganda, lakini ameshacheza nchi mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu ya Marekani (MLS).
.
Amekuwa bora kwenye michezo mingi aliyocheza, huyu ni kati ya mabeki wa pembeni wenye uwezo mzuri wa kuanzisha mashambulizi, kupanda mbele na kutoa pasi za mabao.
.
Vigogo wa Yanga wanatarajia anaweza kuziba nafasi ya Joyce Lomalisa kama akiondoka kwenye timu yao, lakini pia ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa kwenye soka la Afrika.
Screenshot_20230619_151508_Instagram.jpg
 
.
AL-HILAL imeripotiwa kufikia makubaliano binafsi na beki kisiki wa Chelsea, Kalidou Koulibaly, 31, na kwa sasa inapambana kuishawishi Chelsea ikubali kuwauzia. Koulibaly ambaye hajafanya vizuri sana kwa msimu uliopita anadaiwa kupewa ofa maradufu ya mshahara ambao anaupata kwa sasa Chelsea. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu uliopita alicheza mechi 33 za michuano yote.

Screenshot_20230619_151558_Instagram.jpg
 
.
MANCHESTER United inajiandaa kulipa Pauni 45 milioni kwenda Everton ili kuipata huduma ya kipa wa timu hiyo na timu ya taifa ya England, Jordan Pickford, 29, katika dirisha hili la usajili. Man United inataka kumsajili fundi huyu ili akawe mbadala wa David de Gea ambaye hadi sasa bado hajakubali kuongeza mkataba mpya klabuni hapo. Mkataba wa sasa wa Pickford unamalizika mwaka 2027 na United imevutiwa na kiwango chake.
Screenshot_20230619_151643_Instagram.jpg
 
KISA LUKAKU: VIGOGO CHELSEA, INTER WAKUTANA
.
Mabosi wa Chelsea wamewauliza Inter Milan ikiwa wanaweza kumjumuisha kiungo Nicolo Barella kama sehemu ya ofa ili wawauzie Romelu Lukaku katika dirisha hili. Lukaku ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Inter ameweka wazi kwamba anahitaji kuendelea kusalia Inter Milan.
.
Chelsea ipo tayari kumwachia lakini kwa sharti la pesa ama mabadilishano ya wachezaji ambapo wanamhitaji sana Barella. Lukaku anajihisi mwenye furaha kuendelea kusalia Inter na haoni ikiwa atapata nafasi ya kucheza kama anavyopata sasa ikiwa atarudi Chelsea.
.
Chelsea imevutiwa sana na kiwango cha Barella alichoonyesha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na aliisaidia Inter kufika fainali. Mkataba wa sasa wa Barella unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.Msimu uliopita alicheza mechi 52 za michuano yote, amefunga mabao tisa na kutoa asisti 10.
Screenshot_20230619_151733_Instagram.jpg
 
POGBA ALIKUWA NA MATATIZO YA SONONA
.
PAUL Pogba amelaumu changamoto alizopata tangu alipotua Juventus akidai zilisababishwa na matatizo ya kisaikolojia, vilevile alisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
.
Mfaransa huyo alirejea Juventus katika dirisha la usajili la kiangazi lililopita baada ya mkataba wake kumalizika Manchester United, Hata hivyo, mambo yalibadilika kwani Pogba alisumbuliwa na jeraha la kwanza wakati wa maandalizi ya msimu mpya na licha ya kushauriwa kufanyiwa upasuaji, aligoma lakini hakufanikiwa kupona haraka.
.
Baadaye alilazimika kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi Septemba mwaka jana, na akakosa fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar mwaka jana.
.
ā€œMajeraha yangu yalitokana na matatizo ya kiakili. Msimu uliopita ulikuwa mgumu sana kwangu, naamini nitashinda vikwazo hivi na nitarejea dimbani,ā€ alisema Pogba.

Screenshot_20230619_151820_Instagram.jpg
 
Mechi ya kwanza ya mtoano ā€˜play off’ kuwania kubaki Ligi Kuu/Kushuka daraja au Kupanda Ligi Kuu/Kubaki Ligi ya Championship itachezwa leo uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kati ya Mashujaa FC dhidi ya Mbeya City.

Mashujaa FC ilimaliza nafasi ya nne kwenye Ligi ya Championship nyuma ya Pamba FC, timu hizo zikacheza play off zenyewe kwa zenyewe kupata timu moja itakayocheza na timu iliyopoteza kwenye play off za kubaki Ligi Kuu.

Mashujaa ikashinda kwa matokeo ya jumla ā€˜aggregate’ dhidi ya Pamba na sasa itacheza dhidi ya Mbeya City kuwania kupanda Ligi Kuu.

Mbeya City yenyewe ilimaliza nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi nyuma ya KMC, timu zote zikacheza play off ya kubaki Ligi Kuu, KMC ikashinda kwa matokeo ya jumla na kusalia, Mbeya City inaenda kupambana na Mashujaa kujitetea kwa mara nyingine isishuke daraja.

Endapo Mbeya City itashinda kwa matokeo ya jumla itabaki Ligi Kuu lakini kama Mashujaa itashinda kwa matokeo ya jumla itapanda Ligi Kuu na Mbeya City itashuka daraja.

Kwa hiyo hii ni nafasi ya tatu kwa Mbeya City kujitetea isishuke daraja. Mara ya kwanza ilikuwa kwenye mechi za msimu mzima wa Ligi, nafasi ya pili ilikuwa kwenye mechi za play offs dhidi ya KMC na nafasi yao ya tatu ni play offs dhidi ya Mashujaa FC.
Screenshot_20230619_151947_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom