Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mabehewa sita ya ghorofa kati ya mabehewa 30 kwa ajili ya reli ya kiwango cha SGR tayari yamewasili kwenye Bandari ya Dar es salaam yakitokea nchini Ujerumani leo June 6 2023 yakiwa aina mbili ambapo daraja la pili lina uwezo wa kubeba abiria 123 na daraja la tatu lina uwezo wa kubeba Watu 140.

Mabehewa hayo yameboreshwa na kampuni ya Luckmier Transport & Logistic ya Ujerumani ambapo mabehewa 24 yaliyosalia na vichwa viwili bado matengenezo yake yanaendelea.

Kuwasili kwa mabehewa haya ni ishara ya kujiandaa na kuanza kwa safari za treni ya kisasa ambapo itakumbukwa hivi karibuni Serikali ilisema reli ya kisasa ya SGR kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro (KM 300) itaanza majaribio mwezi wa saba na kutoa huduma mara baada ya majaribio kukamiilika mwaka huu.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete akijibu swali Bungeni aliahidi kwamba mwezi wa sita wanategemea kupokea mabehewa yenye ghorofa na mwezi wa saba mwishoni watapokea kichwa ambapo miundombinu yote ipo tayari kwa ajili ya kuanza.
Screenshot_20230607_044533.jpg
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza limerejeshewa umiliki wa kiwanja namba 111 kitalu (T) kilichopo Barabara ya Kenyatta eneo maarufu la Stendi ya Igombe, kilichokuwa chini ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

BAKWATA wamerejeshewa eneo hilo baada ya kushinda kesi dhidi ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza baada ya Halmashauri hiyo kushindwa kutimiza masharti waliyopewa na Mahakama.

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke amesema katika maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ilitoa masharti mawili kwa Halmashauri ya Jiji ikitakiwa kulipa fidia ili kumiliki eneo hilo au irudishe eneo kwa Mmiliki halali kama fidia ndani ya miezi mitatu, ambapo Halmashauri ilishindwa kutekeleza yote mawili.

Shauri hilo namba 150 la mwaka 2020 lililotokana na kesi namba 58 ya mwaka 2017 liliamuliwa June 3, 2022, ambapo kwa mujibu Mahakama ilithibitisha kwamba kiwanja hicho ni mali halali ya Baraza la Waislamu Tanzania.
Screenshot_20230607_044648.jpg
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana leo amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2023/24 Bungeni Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba Serikali inaendelea maandalizi ya ujenzi wa sanamu ya Mwl. Nyerere Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Ethiopia ambapo mradi huo utagharimu USD 205,942 (Tsh. Mil 487+).

“Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inaendelea na uratibu wa maandalizi ya ujenzi wa Sanamu ya Mwl. Nyerere inayotarajiwa kusimikwa Jijini Addis Ababa Ethiopia katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika ambapo hadi Aprili, 2023 hatua iliyofikiwa ni kuanza kwa ujenzi wa Sanamu halisi baada ya Mkandarasi, Kampuni ya EPITOME ARCHITECTS LIMITED ya Tanzania kukamilisha ujenzi wa sampuli kifani ya pili na kuridhiwa na Kamati ya Kitaifa kwa mujibu wa Sheria ya kuwaenzi Waasisi wa Taifa Na. 18 ya mwaka 2004 na Kanuni zake za mwaka 2005.

“Chimbuko la Mradi huo ni mapendekezo ya Hayati Robert Mugabe la mwaka 2015 yaliyolenga kutambua mchango uliotukuka wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika ukombozi wa Bara la Afrika hasa Mataifa yaliyo Kusini mwa Bara hilo”

“Mradi huo wenye thamani ya Dola za Marekani 205,942 unajengwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Sekretarieti ya SADC, Mameneja Mradi kwa kushirikiana na Familia ya Mwl. Nyerere na kwa mujibu wa mkataba uliopo, inatarajiwa kukamilika Desemba, 2023”
Screenshot_20230607_044748.jpg
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana leo amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2023/24 Bungeni Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba hadi kufikia Aprili, 2023 Serikali imetoa mikopo yenye thamani ya Tsh. Bil 1.077 kwa Wasanii na Wadau wengine kutoka Sekta ya Utamaduni na Sanaa.

“Katika kipindi cha July, 2022 hadi Aprili, 2023, Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ulipokea maombi ya mikopo yenye thamani ya Shilingi 9,262,096,578 kutoka kwa Waombaji 219, hadi kufikia Aprili, 2023 Mfuko umefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi 1,077,000,000 kwa miradi 45 kutoka katika maeneo mbalimbali ya Sekta ya Utamaduni na Sanaa”

“Katika miradi 45 iliyowezeshwa, maeneo ya Sekta yaliyowezeshwa na idadi yake katika mabano pamoja na thamani ya fedha iliyotolewa ni Filamu (miradi 17) iliyowezeshwa Shilingi Milioni 475 Muziki (miradi 14) iliyowezeshwa Shilingi Milioni 287 Sanaa za Ufundi (miradi 5) iliyowezeshwa Shilingi Milioni 105 Sanaa za Maonesho (miradi 3) iliyowezeshwa shilingi Milioni 30 na Sanaa ya Uandishi (mradi 1) uliowezeshwa Shilingi Milioni 10, miradi hii imetoka katika mikoa saba (7) ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Mara, Iringa, Mwanza, Mtwara na Mbeya”

“Kwa umuhimu wa mikopo hii na ili kupata njia iliyo rahisi ya kuwafikia Wajasiriamali wengi wa Sekta za Wizara hii, Wizara kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ipo katika hatua za mwisho za kuingia mkataba wa utoaji wa mikopo kupitia benki ya NBC”
Screenshot_20230607_045022.jpg
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana leo amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2023/24 Bungeni Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba BASATA kwa sasa imeendelea kutokimbilia kuwafungia Wasanii kama ilivyokuwa awali.

“Serikali kupitia BASATA imeendelea kukuza ubunifu na utengenezaji wa sanaa bora kwa lengo la kuwawezesha Wasanii kuwa Wabunifu na kubuni kazi za sanaa zilizo bora, BASATA liliendelea na mageuzi ya kiutendaji na kitaasisi ili kuwa mwezeshaji zaidi wa shughuli za sanaa badala ya kudhibiti”

“Hivyo, BASATA limeshiriki kuratibu kutatua migogoro ya wasanii kuhusu mikataba waliyoingia ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 zaidi ya migogoro mikubwa mitano imetatuliwa, BASATA pi alimekuwa likiwaita Wasanii sio tu pale kwenye upungufu bali hata pale wanapofanya vizuri na kuwapongeza”

“Sambamba na hatua hii, BASATA limeendelea kutokimbilia kuwafungia Wasanii kama ilivyokuwa awali bali kunapotokea changamoto zilizokithiri za kimaadili, kama alivyoagiza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa Tamasha la Usiku wa Msanii Joseph Mbilinyi”

“BASATA limeendelea kutoa Tuzo za Muziki wa Tanzania (TMA) kwa mara ya pili mfululizo, Tamasha la utoaji wa Tuzo hizi lilifanyika Dar es Salaam April 29, 2023, ukihusisha utoaji wa Tuzo maalumu zilizotolewa kwa Taasisi Nne ambazo ni UDSM, Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Clouds Media Group na Sauti za Busara, Zanzibar”
Screenshot_20230607_045235.jpg
 
Mtu mmoja (Dereva) amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia ajali ya gari (Scania) ambalo liliacha njia na kupinduka katika eneo la Sigino Darajani Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.

@ayotv_ imefika eneo la tukio na kuongea na Mashuhuda akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa ambaye amesema “Nilisikia kishindo kikubwa na nilifika hapa na kubahatika kumchomoa Mtu mmoja na tayari amepelekwa Hospitali, tulivyoongea nae akasema gari lilikata breki, walikuwa wanne Kwenye gari akiwemo Mwanamke mmoja, eneo hili huwa na ajali nyingi kwasababu kutoka juu kuna mteremko mkali halafu hapa kuna kona"

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema gari lililikuwa na Watu wanne na Dereva ndiye aliyefariki huku majeruhi watatu wakipelekwa katika Hospitali ya Mrara Babati.

"Gari lilikuwa likitoka Kateshi kuelekea Babati wakati wakiteremka Mlima wa Sigino gari hilo liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha Dereva huyo na majeruhi watatu huku chanzo cha ajali ikiwa ni kufeli kwa breki kwa gari hilo"
Screenshot_20230607_045330.jpg
 
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Saido Ntibazonkiza ameendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania kiatu cha ufungaji bora Ligi Kuu Bara baada ya kufunga mabao matano katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania na kumkaribia kinara Fiston Mayele.

Ntibazonkiza baada ya kufunga mabao hayo amefikisha 15 nyuma moja ya kinara amabye ni Mayele wa Yanga mwenye 16.

Simba na Yanga zote zimebakiwa na mechi moja ya Ligi Kuu ambapo Simba itaivaa Coastal Union katika Uwanja wa Chamazi na Yanga ikicheza Sumbawanga dhidi ya Tanzania Prisons.
Screenshot_20230607_045537.jpg
 
Mabao mawili ya Bernard Morrison yameitibulia Mbeya City baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Sangija na Ngodya aliyefunga mawili huku la tatu kwa Yanga likifungwa na Salum Abubakar.

Mbeya City ilienda mapumziko ikiwa na uongozi wa mabao 2-0 na muda mfupi baada ya kurudi kipindi cha pili wakaongeza bao la tatu kabla ya Yanga kuanza kuzawazisha dakika ya 65.

Screenshot_20230607_045659.jpg
 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana (aliyevaa miwani) na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamis Mwinjuma (kulia) wakipongezwa na mawaziri na wabunge baada ya Bunge kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Bunge limepitishie bajeti ya Sh35.4 bilioni kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Jumanne Juni 6, 2023 bungeni jijini Dodoma
Screenshot_20230607_050016.jpg
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Klabu ya Simba SC ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 6, Juni 2023.

Viongozi hao wameongozwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Murtaza Mangungu, Mkurugenzi Mtendaji Iman Kajula.

Pia waliambata na Mwenyekiti wa tawi la Simba mjengoni Rashid Shangazi, Makamu Mwenyekiti Hawa Mwaifunga na Katibu wa tawi hilo Waziri Kizingiti ambao hawapo pichani

Screenshot_20230607_050121.jpg
 
Mbunge wa Ngara (CCM), Ndaisaba Ruhoro anadaiwa kulazimisha picha zake zibandikwe maeneo yenye mkusanyiko wa watu ndani ya jimbo huku baadhi ya watu wakihoji kwa nini iwe lazima.

Picha hizo zinaelezwa kubandikwa maeneo ambako kuna picha za Rais na sehemu ambazo hakuna picha za kiongozi mkuu wa nchi kwa madai yeye ndiye kiongozi wa Ngara.

Mbunge huyo amekiri kuwepo na picha zake nyingi maeneo tofauti zikiwemo nyumba za watu na kutaja sababu kuwa inatokana na mapenzi waliyonayo wananchi kwake, hivyo haoni kosa kwa watu kufanya hivyo.

Ruhoro analalamikiwa kulazimisha wenye maduka, migahawa, saluni na taasisi nyingine kuwa na picha zake ilihali maeneo mengi yamebandikwa picha za Rais na viongozi wa juu.

Katika maeneo mengi ya Ngara ambayo gazeti hili lilipita, picha za mbunge huyo zinaonekana kupamba maduka na maeneo yenye mikusanyiko kwa kuwekwa kwenye vioo kama ilivyo kwa picha za Rais na kutundikwa kwenye kuta kama ishara ya kiongozi wa eneo husika.

Mmoja wa wafanyabiashara wa maduka mjini Ngara alikiri kwenye maduka yake mawili ameweka picha za mbunge huyo, lakini akaeleza kuwa si kwa utashi wake, bali anasukumwa na biashara yake.

“Sijazungumza na Ruhoro mwenyewe kuhusu hili, lakini wapambe wake wanaleta picha kwamba lazima ubandike kwenye eneo la wazi na bila kufanya hivyo usije kulaumu. Ndugu yangu utafanyaje kama ni wewe maana hawa ndiyo waamuzi wa kila kitu. Wananchi tunataka maendeleo sio kulazimishwa kubandika picha za wanasiasa kwenye biashara zetu,” alisema mfanyabiashara huyo ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini.

Akitoa ufafanuzi wa picha hizo kusambazwa jimboni, Ruhoro alisema hakuna shida wala kosa, kwani wanaozisambaza ni wananchi wenyewe kwa mapenzi yao.

Alisema hatoi hata shilingi yake mfukoni kugharamia picha hizo isipokuwa wanaompenda ndiyo huzichapisha na kuweka maeneo mengine.

Hata hivyo, alisema kuna watu wanaoogopa kivuli chake ndiyo wanalalamikia hilo akimtuhumu mmoja wa wastaafu anayedai anataka kugombea, lakini anakuwa na hofu.

Screenshot_20230607_050333.jpg
 
Kennedy Minja (47), mfanyabiashara maarufu wa Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro anayedaiwa kuua kwa kumfyatulia risasi mkazi wa Kilema, Deogratius Lyimo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi leo, Juni 6,2023.

Tukio hilo la mauaji lilitokea Mei 17, 2023 katika barabara ya Himo-Marangu kwa mujibu wa taarifa ilitolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa.

Hata hivyo, baada ya tukio hilo, inaelezwa mfanyabiashara huyo aliendesha gari lake umbali wa kilomita 27 kutoka mji wa Himo hadi Moshi mjini ambako inadaiwa alijisalimisha kituo kikuu cha polisi.
Screenshot_20230607_050515.jpg
 
OFFICIAL: KARIM Benzema, 35, amejiunga na Al-Ittihad kutoka Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka mitatu. Straika huyo alitangaza rasmi ataondoka Madrid baada ya kudumu kwa miaka 14.
.
Benzema aliwekewa mezani ofa inayogharimu Pauni 342 milioni akakipige Al-Ittihad inayoshiriki Ligi ya Saudi Arabia. Nyota huyo ameagwa rasmi leo kabla ya kutimka Saudi Arabia akakamilishe uhamisho wake kuungana na Cristiano Ronaldo kwenye ligi ya nchi hiyo.
Screenshot_20230607_050924.jpg
 
Klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya imeanza mazungumzo na beki wa Simba, Joash Onyango (29) kwa ajili ya msimu ujao.
.
Beki huyo raia wa Kenya licha ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi hicho, huenda akarejea kwao baada ya msimu huu kuisha kutokana na kile kinachoonekana kutokubalika na mashabiki wengi.
.
Chanzo changu makini kimenieleza licha ya Gor Mahia kumhitaji, Singida Big Stars nayo inahitaji saini yake.
Screenshot_20230607_051121.jpg
 
SAIDO MABAO 15 LIGI KUU
.
15’—️ Said Ntibazonkiza
20’—️ Said Ntibazonkiza
25’—️ Said Ntibazonkiza
78’—️ Said Ntibazonkiza
88’—️ Said Ntibazonkiza
.
FT: SIMBA 6-1 POLISI TZ

Screenshot_20230607_051419.jpg
 
Saido Ntibazonkiza wa Simba amefunga mabao 5 yaliyompaisha kutoka mfungaji mwenye mabao 10 hadi 15 na kumkaribia Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 16.

Simba na Yanga zote zimebakiwa na mechi moja ya Ligi Kuu ambapo Simba itaivaa Coastal Union na Yanga ikicheza Sumbawanga dhidi ya Tanzania Prisons.

Screenshot_20230607_051828.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom