Makapuku Forum

Makapuku Forum

Sky Sports wameripoti kwamba Mkali wa soka Lionel Messi anatarajiwa kujiunga na Timu ya Inter Miami ya Marekani baada ya mkataba wake na PSG kumalizika June 30 mwaka huu.

Pia Mwandishi wa Habari za Michezo Fabrizio Romano ameandika kwamba ni uhakika sasa kwamba Messi kazichinjia baharini Timu mbili zilizokua zikimtaka ambazo ni Al Hilal ya Saudi Arabia na Timu yake ya zamani ya Barcelona ambako Baba yake alionekana huko wiki hii kufanya mazungumzo lakini hayakufanikiwa na sasa Mwamba anaenda zake kwa Biden.

Mshindi huyu wa Ballon d'Or mara saba ambaye June 24 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 36, ameifungia PSG magoli 32 ndani ya mechi zote 75 alizoshiriki.
Screenshot_20230608_045037.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Neno lililopo Kijiji cha Chema, Herman Magigita (60) kwa kosa la kuwataka Waumini wake wasiende Hospitali kupata huduma ya matibabu pindi wakiugua au kuuguliwa, badala yake wapelekwe kwenye Kanisa lake liitwalo Neno kwa ajili ya kuombewa na kupata uponyaji wa magonjwa yanayowakabili.

“Tarehe 01.06.2023 muda wa 14:00 mchana huko katika Kijiji cha Chema, Tarafa ya Kahunda, Wilaya ya Sengerema, kulipatikana taarifa kuwa kuna Mtu anatoa mahubiri ya kupotosha jamii kwa kuwataka Waumini wake wasiende Hospitali kupata huduma ya matibabu pindi wakiugua au kuuguliwa, badala yake wapelekwe kwenye Kanisa lake liitwalo neno kwa ajili ya kuombewa na kupata uponyaji wa magonjwa yanayowakabili”

“Askari Polisi walifika katika Kanisa hilo lililopo Kijiji cha Chema na kufanikiwa kumkamata Herman Magigita, miaka 60, Mchungaji wa kanisa la Neno na Mkazi wa Mwangika kwa tuhuma za kosa la kufanya shughuli za Kanisa bila kuwa na kibali cha usajili kinyume cha sheria na kutoa mahubiri potofu kwa Waumini wake”

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa wito kwa Wakazi wote wa Mkoa wa Mwanza kuendelea kuliamini Jeshi la Polisi na kutoa taarifa zaidi za uhalifu na Wahalifu wote ili hatua za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi yao, kamwe tusifiche uhalifu kwa namna yoyote ile, tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinafanyiwa kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa”
Screenshot_20230608_045249.jpg
 
Mwananchi Ismail Mohamed: Bajeti hazijidhi mahitaji ya wananchi isipokuwa zile zinazotengwa kwa ajili ya kununua magari ya kifahari kwa Serikali ambayo hawanufaishi wananchi wa kawaida.

Tunajiuliza kwanini bajeti zinatengwa bungeni lakini hazitekelezwi. Serikali inapaswa kuangalia zaidi sekta za afya, kilimo na elimu kutokana na umuhimu wake.

Screenshot_20230608_045444.jpg
 
Msemaji wa sekta ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa ACT Wazalendo, Dk Nasra Nassoro: Bajeti za kisekta hazijakidhi mahitaji ya wananchi na suala hili sio la leo lipo miaka yote.

Licha ya bajeti kusomwa na kudhinishwa na Bunge hakuna hata moja ambayo inatekelezwa kwa asilimia 100. Haya yanatokea kwa sababu Serikali haina vipaumbele kwa kifupi tumekuwa tunabadilisha vipaumbele vyetu, tunashindwa kutekeleza miradi au kupeleka fedha zinakohitajika kwa sababu ya kutokuwa na mwelekeo.

Screenshot_20230608_045832.jpg
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana NCCR Mageuzi, Nicholaus Clinton: Bunge limeshindwa kuisimamia na kuiwajibisha Serikali. Ni wajibu wa Bunge kuhakikisha inaisimamia Serikali kuondoa umaskini kwa Watanzania.

Pamoja na kuwa na rasilimali za kutosha na rasilimali watu Serikali imeshindwa kuwaondoa wananchi kwenye umaskini.

Ili tutoke hapa ni lazima tuwe na Bunge linalowajibika kwa kuisimamia Serikali na sio kuipaka mafuta. Kupima utendaji wa kiongozi ni lazima Serikali ituambia ndani ya kipindi fulani imefanikisha kuwatoa Watanzania wangapi kwenye umaskini.
Screenshot_20230608_050106.jpg
 
Nicholaus Peter: Bajeti ni mipango ya Serikali ambayo inategemea kuitimiza katika mwaka unaofuata. Ni lazima tuangalia bajeti hizi kwa kiasi gani zinaweza kuondoa umaskini na ufukara kwa watanzania.

Bajeti ni lazima zijielekeze kwenye kukidhi mahitaji ya watanzania hasa katika kuondoa au kupunguza umaskini kwa watanzania.

Wabunge wanafanya kazi moja ya kuishauri Serikali na wanafanya hivyo kwa kuipaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Wabunge ndiyo wawakilishi wa wananchi, ndiyo wanaujua umaskini wa watanzania lakini wanashindwa kusimamia fedha za bajeti zitolewe kwa wakati na kwa kiasi kilichopitishwa.
Screenshot_20230608_050305.jpg
 
Kaimu Mhariri wa biashara gazeti la Mwananchi, Ephrahim Bahemu: Bajeti kuu ndiyo itakayotoa mwelekeo wa masuala ya kikodi ambayo ndiyo yatatua taswira ya gharama za bidhaa.

Wengi hawafuatilii bajeti za kisekta kwa kuwa zimetawaliwa na mipango lakini sio vitu vile vinavyoonekana kuwakwamua watu kwa sehemu kubwa mfano ni suala la kodi.
Screenshot_20230608_050444.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 7, 2023 amemteua Said Nguya kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Kabla ya uteuzi huo Nguya alikuwa mtumishi wa Chama cha Mapinduzi makao makuu.

Screenshot_20230608_050802.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Jausia Msophe kwenda jela miaka 20 au kulipa faini ya Sh500 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa mashtaka mawili likiwemo la utakatishaji wa fedha kiasi cha Sh158 milioni.

Pia mahakama hiyo imemuamuru kiasi cha fedha cha Sh158 milioni zilizokuwepo kwenye akaunti ya Ajuza Athuman ambaye ni ndugu wa Jausia, zirudishwe akaunti ya kampuni ya Glotel, huku nyumba yake iliyopo Kigamboni iuzwe na fedha itakayopatikana ipewe kampuni hiyo kwa mantinki kwamba ilitokana na utakatishaji fedha.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Yusto Ruboroga ambaye amesema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi kumi wa upande wa Jamhuri huku mshtakiwa huyo akijitetea mwenyewe, imeridhika pasipo shaka lolote.

Ruboroga alisema katika shtaka la wizi wa kujipatia kiasi cha Sh158 milioni mahakama hiyo imemtia hatiani Jausia na kumuhukumu kifungo cha miaka nane jela.

Katika shtaka la pili la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha Sh158 milioni mahakama hiyo imemuhukumu Jausia adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh 500 milioni.

"Adhabu ya kifungo itaenda Kwa pamoja hivyo mahakama hii inamfunga kifungo cha miaka 20 au kulipa faini ya Sh500 milioni," alisema Ruboroga.

Awali Wakili wa Serikali, Rhoda Mwakalemela alieleza mahakama hiyo kuwa itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.

Katika kesi ya msingi inadaiwa Juni Mosi na Septemba 26, 2019, jijini Dar es Salaam, Jausia akiwa wakala wa kampuni Glotel alijipatia Sh158 milioni baada ya kuaminiwa.

Katika shtaka la mwisho ambalo ni utakatishaji fedha, inadaiwa siku hiyo mshitakiwa baada ya kupokea fedha hizo alizitumia kwa matumizi yake, binafsi wakati akijua fedha hizo ni mazalio ya kosa la wizi.

Screenshot_20230608_050921.jpg
 
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kapteni Exacery Mloso kutoka kikosi cha 603 KJ cha Anga, Kituo cha Banana, Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kuingilia mfumo wa kompyuta na kubadilisha neno la siri.

Akisoma hati ya mashtaka leo Jumatano Juni 7, 2023 Wakili wa Serikali, Erick Davies alidai mshtakiwa huyo anakabiliwa na shtaka la kuingilia mfumo wa data za kompyuta na kuzuia matumizi ya data hizo.

Davies alidai kati Februari 11, 2023 akiwa ndani ya Jamhuri ya India, kwa makusudi kupitia mfumo wa kompyuta, aliingilia akaunti ya Instagram iitwayo mamakajatz kwa kubadili barua pepe ya mamajabackup@gmail.com kwenda zavobiashara@gmail.com huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Katika shtaka lingine inadaiwa kuwa tarehe hiyo na maeneo hayo mshtakiwa huyo aliingilia mfumo wa data wa kompyuta wenye jina la Hashim Ally Mubi, Jerson Brown na Steven Magombeka kwa kubadilisha neno la siri akaunti ya Instagram kutoka mama2022 kwenda mamakaja 1321 huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Shtaka la mwisho inadaiwa kuwa tarehe hiyo akiwa ndani ya Jamhuri ya India mshtakiwa huyo alizuia data za kompyuta kwa kuwazuia viongozi wa utawala wa akaunti ya Instagram ya mamajaztz ambao ni Hashim Ally Mubi, Jerson Brown na Steven Magombeka kwa kubadilisha neno la siri la akaunti hiyo kutoka mama2020 kwenda mamakaja 1321 huku akijua ni kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa alikana makosa yote na upelelezi bado haujakamilka.

Hakimu Mkazi Mkuu Rhoda Ngimilanga amesema mshtakiwa huyo anatakiwa awe na wadhamini wawili mmoja ambao wanatakiwa kuwa na vitambulisho vinayotambulika pamoja na barua kutoka Serikalini.

"Wadhamini hao wawe wanatoka Jiji la Dar es Salaam ambao watasaini bondi ya Sh5 milioni," amesema Ngimilanga.

Mstakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti hayo na shauri hilo limeahirishwa hadi Juni, 21 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Screenshot_20230608_051034.jpg
 
Wakati mjadala kuhusu Azimio la Serikali ya Tanzania kuingia makubaliano na Serikali ya Dubai kwa ajili ya uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam ukipamba moto, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imekanusha baadhi ya mambo na kuwataka Watanzania kutosikiliza kile inachoita upotoshaji.

Ufafanuzi wa TPA umekuja ikiwa imepita siku moja tangu Kamati ya Bunge ya Miundombinu na uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ikipokea maoni ya wadau bungeni jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na TPA jana Juni 6 kupitia mitandao ya jamii, imesema madai kuwa Serikali ina mpango wa kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya kuendesha bandari ya Dar es Salaam kwa miaka 100 siyo za kweli.

“Azimio la Bunge linalohusu mkataba ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia a Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi 12 kwa ajili ya kutoa nafasi ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika uboreshaji wa sekta ya bandari nchini Tanzania,” imesema taarifa hiyo.

TPA imefafanua kuwa ushirikiano wa nchi hizo mbili unalenga la kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya bandari ya Dar es Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda na mnyororo wa usafirishaji kwenda nchi jirani
Screenshot_20230608_051225.jpg
 
Mkuu wa kitengo cha uhalifu katika Jimbo la Free State nchini Afrika Kusini, Brigadier Jackson Mkhaulesi ambaye alikuwa akichunguza kesi ya mhalifu aliyetoroka gerezani nchini humo na kukamatwa Arusha, Thabo Bester adaiwa kujiua kwa kujipiga risasi.

Inadaiwa kuwa marehemu alikuwa akichunguza kutoroka kwa Bester na kusababisha uvumi kuhusu iwapo alikuwa na taarifa zozote ambazo zingeweza kupelekea Bester kukamatwa, hata hivyo mazingira ya kifo chake hayajawekwa na uchunguzi unaendelea.

Kamishna wa Polisi wa Kitaifa, Jenerali Fannie Masemola alimtaja afisa huyo kama mpelelezi mchapakazi, mwaminifu na aliyejitolea kwa miaka 31 akidai kuwa kuondoka kwake kunaacha pengo katika mazingira ya upelelezi.
Screenshot_20230608_051340.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 7, 2023 amemteua Cuthbert Midala kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Midala ni mtaalamu wa masuala ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia ya Kiuchumi.

Screenshot_20230608_051633.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 7, 2023 amemteua Nicodemas Tambo kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam
Kabla ya uteuzi huo Tambo alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
Screenshot_20230608_051800.jpg
 
Kombe jipya la Ligi Kuu Bara limezinduliwa leo na litakabidhiwa kwa mabingwa Yanga Ijumaa Juni 9 baada ya mechi dhidi ya Tanzania Prisons itakayochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Screenshot_20230608_052107.jpg
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba (kushoto) na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamad Hassan Chande (katikati) baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wiziara hiyo na taasisi zake jumla ya Sh16.03 trilioni jijini Dodoma leo Jumatano Juni 7, 2023.
Screenshot_20230608_052239.jpg
 
“Mtu anatoa Sh500 milioni kununua hisa lakini anaambia hana sifa ya kuwa kwenye bodi ya wakurugenzi kisa hana degree, hii si sawa.” Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ameilalamika sheria ya Benki Kuu kuzuia watu wasio na elimu ya kifedha kuwa kwenye bodi ya wakurugenzi kwenye mabenki na taasisi za kifedha.

“Mweshimiwa Naibu Spika, mimi nimekusanya Sh500 milioni alafu nazitoa kwenye benki kununua hisa naambiwa siruhusiwi kuwa kwenye bodi ya wakurugezi, kwa nini usiangalie jinsi nilivyopambana nikapata hizo fedha ukaulinganisha ni degree (shahada).”

Malalamiko hayo yameelezwa na mbunge huyo leo Jumatano Juni 7, 2023 bungeni jijini Dodoma.

Screenshot_20230608_052412.jpg
 
Watu nane wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Noah pamoja na Fuso usiku wa kuamkia leo Jumatano ya Juni 7, 2023 katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

"Hii Noah ilikuwa inatoka mwelekeo wa Mikumi inakwenda Morogoro ikagonga gari iliyokuwa inapishana nayo (lori), ikayumba ikaja kukutana na gari yangu (Fuso) uso kwa uso.

Dereva wa Noah alikuwa anasinzia akagusana na lori akanifuata mimi ila kwenye gari yangu hakuna aliyejeruhiwa zaidi ya kuanguka na kutupwa nje ya barabara," amesema Edward Chura dereva wa Fuso iliyopata ajali,

Akizungumzia majeruhi hao kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mtakatifu Kizito Mikumi, Dk Steven Mbilinyi amesema wamepokea majeruhi nane wakiwa mahututi lakini wanaendelea na matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama alipopigiwa kuhusiana na ajali hiyo, amesema anafuatilia na taarifa itatolewa.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.

Screenshot_20230608_052603.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo amemteua John Nchimbi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Uteuzi huo umeanza jana Jumanne Juni 6, 2023.

Nchimbi alishinda kura za maoni ndani ya CCM kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Songea Mjini 2017.
Screenshot_20230608_052720.jpg
 
Maelfu ya wananchi wa Ukraine wako katika hatari ya kukumbwa na mafuriko kando ya mto Dnipro baada ya bwawa la Kakhovka kuporomoka jana ambapo Moscow na Kiev zimetupiana lawama ya kuhusika na uharibifu huo.

Balozi wa Urusi, Vasily Nabezya amesema tukio hilo ni hujuma ya makusudi iliyofanywa na Ukraine na kwamba linapaswa kuainishwa kama uhalifu wa kivita au kitendo cha ugaidi huku Balozi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa, Sergiy Kylytsya akiishutumu Moscow kwa kulipua bwawa hilo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema kuwa Kakhovka ni mojawapo ya mabwawa makubwa nchini humo na kwamba miji na vijiji 80 vinaweza kufurika baada ya uharibifu wa bwawa.

Shughuli ya kuhamisha maelfu ya watu inaendelea katika eneo la Kherson ambapo badhi ya wakazi wa eneo hilo wameonekana wakijaribu kuokoa mali zao.

Screenshot_20230608_052916.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom