Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo June 3, 2023
Screenshot_20230603_062808_Opera%20Mini.jpg
 
HAALAND: TUTABEBA MAKOMBE MATATU
.
Straika wa Manchester City, Erling Haaland amesema watafanya juu chini wabebe makombe matatu msimu huu. Tayari Man City imebeba ubingwa wa Ligi Kuu England na itaongeza kombe la pili endapo itaifunga Manchester United leo kwenye fainali ya Kombe la FA.
.
Baada ya mchezo huo, Man City itajiandaa na fainali nyingine ya michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan itakayochezwa Juni 10 katika Jiji la Instabul, Uturuki.
.
Man City inataka kutengeneza historia iliyowekwa na Man United 1999 ilipobeba FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu England. Haaland alisema “Hii ndio maana (Man City) wamenisajili. Nimekuja hapa kwa ajili ya kubeba makombe. Itamaanisha kila kitu kwangu nifanye juu chini. Nitajaribu kuisaidia timu naamini ndoto zangu zitatimia. Hata hivyo haitakuwa rahisi (ni) fainali mbili dhidi ya timu mbili nzuri. tutapambana na kuzifunga,” alisema.
Haaland.

Screenshot_20230603_072649.jpg
 
VARANE AJIAPIZA KUMDHIBITI HAALAND
.
Raphael Varane ameapa kumdhibiti straika Erling Haaland ili kuitibulia Manchester City ndoto yake ya kushinda mataji matatu ndani ya msimu mmoja. Kufunga mabao 52 katika mechi 51 alizocheza Haaland zimemfanya kuwa kwenye makali kabisa huko akijiandaa kucheza fainali yake ya kwanza ya Kombe la FA. Lakini, beki wa kati wa Man United, Varane alisema kitu muhimu ni kumdhibiti Haaland na kuvunja kabisa muunganiko wake na kiungo mchezeshaji wa miamba hiyo Kevin De Bruyne.

Screenshot_20230603_072757.jpg
 
RONALDO YUPO SANA SAUDIA
.
Supastaa Cristiano Ronaldo amesisitiza kwamba atabaki Al-Nassr baada ya taarifa kudai kuwa alitarajia kurejea Madrid na kupewa kazi ya ubalozi. Hata hivyo Madrid ilimpotezea ingawa sasa amesema anataka aendelea kuichezea Al-Nassr.
.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 38 amezima uvumi kwamba anataka kurudi Ulaya kukiwa na matumaini kwamba Karim Benzema na Lionel Messi watajiunga na Ligi Kuu ya Saudi Arabia anayoichezea.
.
Ronaldo alisema: “”Kama wachezaji watakuja wakubwa na wadogo wenye majina Ligi itaimarika zaidi. Umri sio tatizo kila mchezaji kwa mchezaji aliyekamilika inategemeana na uwezo wake.”
Screenshot_20230603_072854.jpg
 
KOCHA GENK AMTULIZA SAMATTA
.
Kocha wa KRC Genk, Wouter Vrancken amewataka wachezaji wake kujitoa haswa kwenye mchezo wa mwisho wa msimu dhidi ya Royal Antwerp bila kuzingatia matokeo ya mchezo mwingine wa mchujo kati ya Royale Union Saint-Gilloise na Club Brugge kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji ‘Jupiler Pro’.
.
Raundi ya mwisho kwenye mchujo wa ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji itachezwa kesho, Jumapili, huku presha ikipanda na kushuka kwa mashabiki wa KRC Genk anayoichezea nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, Royal Antwerp na Royale Union Saint-Gilloise ambazo zipo kwenye nafasi ya kwanza hadi tatu.
.
Vrancken alisema hayo ili wachezaji wake waelekeze fikra na mawazo yao kwenye mchezo dhidi ya Royal Antwerp. ”Ni mbaya wakati unacheza kuwa na mawazo ya matokeo ya mchezo mwingine hiyo ni mbaya inaweza kupunguza ufanisi wao.”
.
“Tunatakiwa kufanya vizuri kwanza halafu hayo mambo mengine yatafuata baadae. Tunataka kuwapa kilicho bora mashabiki wetu ambao wamekuwa pamoja na sisi tangu mwanzoni mwa msimu,” alisema kocha huyo ambaye enzi zake alikuwa kiungo mkata umeme.
.
Katika mchezo huo wa mwisho wa msimu, nahodha wa Taifa Stars, Samatta ndiye atakayekuwa na jukumu la kuongoza mashambulizi ya KRC Genk ambayo ipo nafasi ya tatu.
Screenshot_20230603_073259.jpg
 
WAKALI UGENINI
.
YANGA hadi inafika fainali ndio ilikuwa timu iliyopata ushindi mara nyingi zaidi UGENINI katika mashindano ya klabu Afrika msimu huu kuliko timu nyingine yoyote.
.
Katika Mashindano ya Klabu Afrika msimu huu, Yanga imepata ushindi katika mechi tano za ugenini ambazo ni dhidi ya Club Africain, TP Mazembe, Rivers United, Marumo Gallants na USM Alger.
.
Timu inayoshika nafasi ya pili kwa kupata ushindi mara nyingi ugenini msimu huu ni Al Ahly, Raja Casablanca na Asec Mimosas ambazo kila moja imeshinda ugenini mara tatu.
Screenshot_20230604_121803.jpg
 
MOYES HATARINI KUFUTWA KAZI
.
West Ham United inaweza kumfuta kazi kocha David Moyes endapo itachapwa fainali ya Europa Conference League. West Ham itakipiga na Fiorentina, Jumatano ijayo kwenye fainali hiyo ikijaribu kusaka taji la kwanza la Ulaya baada ya miaka 47 na Moyes anahitaji kushinda ili kuwa na uhakika wa maisha yake kwenye klabu hiyo ya London.
Screenshot_20230604_122034.jpg
 
BABA AENDA KUMALIZA KAZI
.
Baba ambaye ni wakala wa kiungo wa Brighton, Alexis Mac Allister amesafiri kwenda England wikiendi hii kukamilisha dili la mwanaye anayehusishwa kuachana na timu yake.
.
Baba huyo ambaye ni beki wa zamani wa Argentina Carlos Mac Allister anaenda kushughulikia uhamisho wa mwanaye anayehusishwa na Liverpool kwenye dirisha hili.
Screenshot_20230604_122203.jpg
 
USMA MABINGWA SHIRIKISHO AFRIKA
.
FT: USM ALGER 0-1 YANGA SC
07’—️ Djuma Shaban
Agg (2-2)
.
Screenshot_20230604_122307.jpg
 
Nasreddine Nabi

“Tulipoteza fainali jijini Dar es Salaam. Tulipoteza mwelekeo kidogo kwani hii ilikuwa mara ya kwanza tulikuwa tunacheza mechi ya ukubwa huu. Hatukuwa tumezoea kuwa kwenye fainali hizo. Tulijaribu kurekebisha katika mechi ya marudiano lakini haikuwezekana.”

“Hongera USM Alger kwa ushindi wao. Nawapa pongezi na wanalostahili. Ilikuwa fainali nzuri na hali ya mashabiki ilikuwa nzuri. Kama vile kocha yeyote ningependa kushinda, lakini haikuwezekana kwetu usiku wa leo,” alisema Kocha Nabi.

Screenshot_20230604_122507.jpg
 
UBORA WA VIWANGO

◇Yanga kabla ya kushirik mashindano ya CAF msimu huu ilikuwa nafasi ya 75 katika chati ya Ubora wa klabu Afrika. Hata hivyo kwa kufika fainali, Yanga ilipanda kwa nafasi 57 hadi ile ya 18 baada ya kufikisha pointi 20 ambazo imezivuna kwa kufanya vizuri zaidi.

◇Yanga imetoka mbali hadi kufika FAINALI-CAF
"Yanga wajifunze kwa Simba"
"Nabi hawezi kimataifa"
"Eng Hersi ni mhuni tu"
"Pengo la Feitoto ni kubwa"
"Mayele ana la kujifunza kwa Baleke"
"Simba wamekusanya pesa zaidi"
"Kimataifa waachieni Simba"

Kweli mpira ni mchezo wa makosa

Screenshot_20230604_122621.jpg
 
MAVUNO YA WANANCHI

Kwa kumaliza kama washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho mwaka huu, mabingwa wa Tanzania, Yanga SC watapokea Dolla Milioni 1 sawa na Tsh.2 37 Billion kutoka CAF kama pesa za zawadi!

Screenshot_20230604_122729.jpg
 
CHUKUA MAUWA YAKO SUREBOY

○Abubakar Salum 'Sure Boy' ni kiungo mchezeshaji 'BAMIA' ambae ana uwezo mkubwa saana akiwa na mpira mguuni mwake.

○Sure Boy ameweza kumiliki vyeme dimba lake kati akiwa na uwezo mkubwa wa utulivu pale awapo ni mpira mguuni mwake.

○Amekuwa mbunifu zaidi na sii mtetemekaji amepiga side way passes nyingi na kufanya timu iweze kuwa na balance katika kucheza kwa nafasi zaid (possession playing)

○Amezitendea haki dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenye mchezo huu wa fainali ya CAFCC.

○Alafa huyu jamaa kwenye mechi na waarabu anauwashaga saana.!
Screenshot_20230604_122828.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom