Huyu ndie Cindy Le Coeur wa bendi ya Koffi Olomide !
Ukisikia sauti yake kwenye nyimbo kama Ikea ama Etoile D'Etat ama Lili Kaniki hata kama ulikuwa unakaribia kukata roho unaweza kuishi siku mbili au tatu zaidi. Huyu anaitwa Cindy. Jina lake halisi ni Candy Kunku.
Kabla ya mwaka 2007, Cindy alikuwa mwana kwaya akiimba nyimbo kanisani huko Congo kama walivyo wanamuziki wengi wa Congo. Mwaka huo au wa nyuma yake Koffi Olomide aliondokewa na wanamziki wake tegemeo hasa Fally Ipupa na Fere Gora hata hivyo huyu wa pili alikuwa hajaitumikia sana band ya Quartier Latin. Huo ndio wakati ambao mwanamzuki huyu mchanga, mwenye sauti laini na ya kuvutia masikioni aliacha kumwimbia Yesu. Akachukuliwa na Koffi. Kwa sababu ilikuwa ni nyota tayari, mawingu yalipoondoka ikaendelea kung'aa.
Koffi hakutumia nguvu sana kumfanya mwanamke huyu kung'ara.Cindy akaimbishwa, akaimba. Akachezeshwa, akacheza. Akatunga na kuimba mwenyewe. Kuanzia album ya Bord Ezanga Kombo mpaka wimbo wa hivi majuzi wa Je te Jure, Cindy anang'ara. Cindy anajua kupanda na kushuka. Unachoweza kusema ni kwamba mwanamke huyu anajua kuimba. Tena amebarikiwa sauti ya kuvutia.
Nje ya Koffi Olomide na kundi lake la Quartier Latin Cindy hajawa huru. Pengine anabanwa kama Koffi alivyofanya kwa wanamziki wake wengine kabla ya Cindy. Cindy ametoa album moja ambayo nyimbo zote pamoja na Remixes ni utunzi wa Koffi Olomide. Hata hivyo inasemwa semwa kwamba mwanamama huyu ambaye sasa ni mama wa mtoto mmoja pengine wana mahusiano mengine zaidi ya mziki na bosi wake Koffi Olomide.
Kwa sasa Cindy ndie Mkurugenzi wa bendi, yaani baada ya Koffi Olomide yeye ndie Boss. Ikea ndio wimbo wa kwanza uliomtambulisha alipojiunga na bendi ya Koffi Olomide. Ukisikiliza wimbo wa Egerie huwezi kuacha kujiuliza kwa nini Cindy bado yuko chini ya Koffi Olomide. Koffi Olomide anamwita Cindy Malkia wa Nyota. Hata hivyo wapenzi wa muziki huko Congo wanajiuliza maswali zaidi ya elfu moja, kwanini mwanamzuki huyu hana boyfriend!?
Pichani ndie Cindy akiwa na bosi wake Kofi Olomide..!
View attachment 2647312