Makapuku Forum

Makapuku Forum

Huyu ni mshambuliaji wa Yanga ambaye amekuwa akifanya vizuri msimu huu akitokea DR Congo, ndiye mfungaji bora kwenye Ligi Kuu, Mayele anaongoza pia kwenye kupachika mabao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na mabao saba na pasi tatu za mabao.
.
Huyu anaishi kwenye Apartment maeneo ya Victoria, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Sehemu ambayo mchezaji huyo anakaa na familia yake na analipa dola 800 ambayo ni sawa na shilingi milioni 1.8 milioni Ana gari kali aina ya Toyota Harrier nyeusi na Toyota Premio.View attachment 2644144
umetumwa nn
 
Mshambuliaji wa Hispania Marco Asensio, 27, ameamua kujiunga na Paris St-Germain mara mkataba wake na Real Madrid utakapokamilika msimu huu wa joto. (Athletic)

Screenshot_20230603_054054.jpg
 
Napoli wako tayari kuchuana na AC Milan kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Mmarekani Folarin Balogun, 21, katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. taarifa za ndani zinasema kuwa jamaa ndiye mrithi wa Victor osimhen iwapo ataondoka viunga vya Napples (Mirror)

Screenshot_20230603_054355.jpg
 
Barcelona wanataka kumuuza mshambuliaji wa Hispania Ansu Fatu msimu huu wa joto, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa sasa hana mpango wa kuhamia Wolves, wanaotaka kutoa £26m pamoja na kiungo wao wa kati Mreno Ruben Neves, 26. (Sport).

Screenshot_20230603_054500.jpg
 
Bayern wanatazamiwa kutoa ofa kwa mawinga wa Ujerumani Serge Gnabry na Leroy Sane, wote wana miaka 27, msimu huu wa joto, pamoja na mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane - mwaka mmoja tu baada ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 31 kutoka Liverpool. (Mail via Bild)

Screenshot_20230603_054557.jpg
 
Joao Cancelo wa Manchester City kuna uwezekano mkubwa wa kufanya uhamisho wake wa mkopo kwenda Bayern Munich kuwa wa kudumu msimu huu wa joto. Beki huyo wa pembeni wa Ureno, 29, hataki kurejea England - kuichezea Arsenal wanaomtaka na ambao wamemaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi. (Abendzeitung)

Screenshot_20230603_054823.jpg
 
Mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 35, atajiunga na klabu ya Saudi Arabia Al-Ittihad mara mkataba wake wa Real Madrid utakapokamilika mwezi huu. (ESPN)
Screenshot_20230603_054922.jpg
 
Newcastle wanajiandaa kupambana na Manchester United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24, kutoka Napoli. (Gazzetta dello Sport via Mirror)
Screenshot_20230603_055043.jpg
 
Inter Miami wamempa Lionel Messi ofa ya euro 50m kwa mwaka (£42.9m) ili kuitumikia klabu hiyo ya MLS kwa miaka minne baada ya mshambuliaji huyo wa Argentina, 35, kuondoka Paris St-Germain msimu huu. (Sport)

Screenshot_20230603_055143.jpg
 
MAREFA

1st Leg CAFCL FINAL

Mwamuzi wa kati kutoka nchini Libya Mutaz Ibrahim (33) ataamua dakika 90' za kwanza pale Misri Fainali ya CAFCL Alahly VS Wydad Jumapili , June 4, 2023

2nd Leg CAFCL FINAL

Mwamuzi kutoka Ethiopia Bamlak Tessema Weyesa (42) atachezesha Fainali ya mkondo wa pili June 11 katika Dimba la Mohameed V Morocco

Screenshot_20230603_060030.jpg
 
Shaffih Dauda

Tulipofika sasa hivi ni lazima tujue kutofautisha urafiki na kazi, lazima kuwe na weledi ili kuzuia mikingamo na ugomvi.

Ukifatilia sakata la Feitoto utagundua hakukuwa na weledi kuanzia awali kabisa badala yake ilikuwa ni jambo la mahusiano.

Ndio maana leo hii Feisal analalamika kunyanyaswa na mtu lakini sio taasisi. Hili inaonekana ni jambo la watu wawili ambao wameshindwa kuelewana.

Kama wote wawili walipaswa kutofautisha kazi na mambo/mahusiano binafsi, kiongozi wa taasisi angemhudumia mchezaji kama mfanyakazi wa taasisi sio kama washkaji.

Kuna wakati kiongozi na mfanyakazi wanaishi kama marafiki lakini wakati wa kazi lazima kila mmoja abaki katika nafasi yake. Kwa hiyo kiongozi alipaswa kujua wakati gani anaiwakilisha taasisi kwenye kazi na wakati gani wa ushkaji.

Ukifatilia sakata zima unaona kuna mapungufu mengi yamejitokeza, sisi kama wadau ambao jambo hili linatuhusu huu ndio wakati wa kufanya mageuzi ya namna gani tunavyofanya vitu vyetu.
Screenshot_20230603_060218.jpg
 
Shaffih Dauda

Baada ya Feisal kuzungumza kupitia #PowerBreakFast @cloudsfmtz imetupa fursa ya kufanya mjadala ambao ni balanced, tumezisikia pande zote mbili.

Tangu mwanzo kabisa mimi nilikuwa naliangalia hili jambo kama sehemu ya kujifunza kwa manufaa ya tasnia nzima.

Ukiliangalia hili jambo kama la Feisal pekeyake unaweza ukapotea lakini ukilibeba kwa picha kubwa kwamba kuna matukio mengi ya aina hii na mengine yanaweza kutoke huko mbele.

Kupitia hili la Feisal kuna vitu vingi sana vya kujifunza;

Makubaliano ya mchezaji na klabu kuanzia hatua za mwanzo kabisa na kujua kila upande unapaswa kutekeleza majukumu gani kwa wakati gani.

Kuacha kufanya vitu kienyeji kama ambavyo tumezoea, sio kwakuwa klabu inamtaka mchezaji inamfata na kumsaini.

Kwenye masuala ya kazi mchezaji anapaswa kuishi kama taasisi sio mtu mmoja. Wanapokuwa wanaenda kwenye masuala ya usajili waende kama taasisi yenye watu wengi nyuma kwa ajili ya maslahi mapana kwa ajili ya leo na kesho yao.

Klabu nazo zisikubali kufanya mazungumzo na mchezaji pekeake bila wasimamizi, lazima awe na watu wa kumsaidia kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ya kimikataba. Wasitumie kama fursa pindi mchezaji anapokuwa pekeake.

Hiki kilichotokea kati ya Yanga na Feisal iwe fundisho na sehemu ya mabadiliko kwenye tasnia nzima na masuala ya mikataba na usajili kati ya mchezaji na klabu.

Mfano mchezaji akiishi kama taasisi hizi habari za simu kutokupokelewa hazitakuwepo kwa sababu kutakuwa na mawasiliano rasmi kati ya taasisi moja na nyingine.

Inatoka barua kutoka upande wa mchezaji inaenda kwa klabu, tarehe fulani wawakilishi wa mchezaji wanaomba kikao na upande wa klabu na kusubiri majibu.

Kama hawajajibu kwenye tarehe ambayo waliomba kikao inatumwa barua nyingine ya kuwakumbusha kwamba tarehe fulani ilikuja ikiomba kikao.

Leo hii kungekuwa na ushahidi wa kimaandishi ambao hata wanasheria wa mchezaji wanaweza kumtetea mchezaji wao.
Screenshot_20230603_060526.jpg
 
Nyota wa Arsenal Bukayo Ayoyinka Saka yupo nchini Nigeria na inaelezwa atatumia siku kadhaa nchini humo na maeneo mengine ya Afrika Magharibi kama sehemu ya mapumziko yake ya mwisho wa msimu.

Licha ya kukipiga timu ya taifa ya Uingereza lakini asili yake ni taifa la Nigeria nyumbani kwa Rema, Joe Boy, Ruger, Asake, Burna Boy na kina Dada Tiwa Savage na Ayra Star wengine utaongezea
Screenshot_20230603_060653.jpg
 
Mshambuliaji kinara wa upachikaji mabao wa Manchester City na EPL 2022/23 Earling Haaland , amezungumza kuelekea fainali ya UCL akisema lengo la Klabu kumsajili ni kushinda ubingwa wa Ulaya.

Erling Haaland - " Ubingwa wa Ulaya ndio sababu ya mimi kuwa hapa , Man City wamenisajili kwa lengo moja tu tupate ubingwa wala hakuna sababu ya kuficha hili "

Screenshot_20230603_060811.jpg
 
Ripoti ya Daily Mail na vyombo vya habari vya kimataifa zinasema Man United imepanga kumtoa Beki wake Harry Magire na kiasi cha pesa Euro Milioni 30 kwenda Chelsea ili kumpata Mason Mount .

Maguire - € 30 M to Chelsea
Mount to United
Screenshot_20230603_060918.jpg
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kuongezeka kwa mapato yatokanayo na Watalii kutoka Dola za Marekani milioni 1,310 mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani Milioni 2,527.72 kwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la 93%.

“Wizara imeendelea kutangaza Utalii kwa kutumia mikakati mbalimbali ikiwemo kuisambaza filamu ya Tanzania - The Royal Tour ambayo imesikika, imetazamwa na kufuatiliwa na Watu takriban bilioni 1.2 duniani ikijumuisha masoko ya kimkakati ya Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia na China.

“Kauli mbiu ya Tanzania Unforgettable itaendelea kutangazwa katika ligi kubwa za michezo Marekani, Uingereza na Hispania, uendelezaji wa Programu hii, umewezesha kuleta matokeo chanya kwa kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini, Mathalan, idadi ya Watalii imeongezeka kutoka 922,692 mwaka 2021 hadi kufikia 1,454,920 mwaka 2022 sawa na ongezeko la 57.7% na mapato yatokanayo na watalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 1,310 mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani Milioni 2,527.72 kwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la 93%”

“Vilevile, idadi ya Watalii wa ndani katika robo ya kwanza ya mwaka 2023 imeongezeka hadi kufikia Watalii 409,092 sawa na ongezeko la 41.4% ikilinganishwa na Watalii 289,372 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2022”
Screenshot_20230603_061457.jpg
 
Askari wa Wanyamapori kwa kushirikiana na Wananchi wa Mtaa wa Itezi Magharibi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kumuua Simba dume baada ya kuua ng'ombe wawili na punda mmoja katika Kijiji cha llowelo Kata ya Lwanjilo Wilaya ya Mbeya.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilowelo, Yona Mbalila amesema Simba huyo aliibuka siku sita zilizopita ambapo walitoa taarifa Maliasili na walifika na kuanza msako.

Baada ya kugundua anasakwa Simba huyo aliondoka na kuvamia Mtaa wa Itezi Magharibi ambapo aliua punda watatu na ng'ombe mmoja ambapo Mwenyekiti wa Mtaa wa Itezi Magharibi Mario Paul amesema Simba huyo alikuwa tishio ambapo walifanikiwa kumuua korongoni wakati akila mzoga wa punda.

Afisa Wanyampori Wilaya ya Chunya Jacob Mpinga amesema baada ya Askari kufanikiwa kukabiliana na Simba huyo walimuua na mwili wake kuchukuliwa na kuhifadhi nyara hiyo ofisi za Maliasili “Ni kawaida kwa Wanyama kutoka hifadhini wakifuata ushoroba kwenda maeneo mengine”
Screenshot_20230603_061607.jpg
 
Wanahisa wa Benki ya NMB wameidhinisha gawio la Shilingi Bilioni 143.1 kwa mwaka 2022 sawa na shilingi 286 kwa kila hisa moja katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 23 wa Wanahisa uliofanyika kwa njia ya mtandao leo, hili ni ongezeko la 48% ukilinganisha na gawio la jumla la Shilingi Bilioni 96.7 lililolipwa mwaka 2021.

Benki hiyo ikiwa inaandika historia ya kutimiza miaka 25 ya kuwahudumia Watanzania, hili ni gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na Taasisi ya fedha nchini kwa Wanahisa wake, gawio hilo litalipwa kufikia tarehe 14 Juni 2023.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna “Miaka minne iliyopita, tulilipa gawio la shilingi bilioni 33 kwa Wanahisa wetu lakini kwa mwaka 2022 gawio limeongezeka na kufikia Shilingi Bilioni 143.1, ongezeko hili la gawio linaendana na ongezeko la mchango wetu katika uchumi wa Taifa letu na maendeleo ya Wananchi kupitia programu yetu ya uwajibikaji kwa Jamii, ambapo kwa mwaka huu tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 6.2 zinazoelekezwa kwenye sekta ya afya, elimu, mazingira, elimu ya fedha na usaidizi wa majanga”

“Mafanikio ya Benki yetu ni matokeo ya mazingira mazuri ya kibiashara yaliowekwa na Serikali yetu, imani ya Wanahisa na Wateja wetu, juhudi za Wafanyakazi wetu, usimamizi mzuri wa Benki Kuu ya Tanzania na ushirikiano mzuri uliopo na Wadau wetu wote, tunawashukuru na tuendelee kuwa pamoja katika safari yetu ya mafanikio”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NMB, Dkt. Edwin P. Mhede amesema “Bodi yetu itaendelea kuwa ya kibunifu na kusimamia ukuaji wa Benki ili kuhakikisha wanahisa wetu wanaendelea kunufaika na uwekezaji wao, Bodi ina imani kubwa na mikakati iliyopo na imedhamiria kuhakikisha NMB inaendelea kuwa Benki kiongozi nchini na inakuwa na mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii”
Screenshot_20230603_061717.jpg
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu @ummymwalimu leo tarehe 02 Juni 2023 akiwa Bukoba Mkoani Kagera ametangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.

“Kwa mujibu wa miongozo ya Shirika la Afya la Duniani (WHO), tangu tulipomruhusu mgonjwa wa mwisho, tulipaswa kuendelea kuchukua hatua za udhibiti ikiwemo ufuatiliaji wa tetesi katika jamii na kuchunguza Wahisiwa wote kwa siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho alipopona Virusi vya Marburg, kwa hesabu hizo, ilipofika juzi tarehe 31 Mei 2023, tulifikisha siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho kupona Virusi vya Marburg, na hivyo kukidhi vigezo vya WHO vya kutangaza mwisho wa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg”

“Nawakumbusha Wananchi wote kuwa, kumalizika kwa mlipuko huu isiwe mwisho wa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza kama inavyoelekezwa na Wataalamu wa Afya na kwa Wataalamu wa Afya tuendelee kuchukua tahadhari wakati wote kama miongozo yetu inavyotutaka”
Screenshot_20230603_061906.jpg
 
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ambayo ipo chini ya Wizara ya Katiba imetangaza matokeo ya uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi wa UDOM, Nusura Abdallah yanayoonesha kuwa kifo hicho hakikuwa na uhusiano wowote na ajali ya gari aina ya Toyota Land Cruiser GXR V8 iliyomhusisha Naibu Waziri Dkt. Festo John Dugange usiku wa April 26, 2023 Iyumbu, Dodoma.

Tume hiyo imesema kifo cha Nusura kilitokea baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwa Mchumba wake Juma Mohamed Kundya, Mjini Moshi alikokwenda kwa ajili ya kupanga siku ya Mchumba wake kwenda kujitambulisha nyumbani kwao Singida.

Taarifa imeendelea kueleza kuwa Nusura alipelekwa Hospitali ya Faraja na baadae kufariki ambapo vipimo vilivyofanywa na Hospitali vilionesha kuwa kifo chake kilitokana na shambulio kali la kupanda kwa sukari na upungufu wa damu.

“THBUB haikuweza kuthibitisha Mtu yeyote kuhusika na kifo cha Nusura kutokana na vielelezo vya Hospitali ya Faraja, Mkemia Mkuu wa Serikali, maelezo ya mengine ya Mashahidi, Daktari aliyempatia huduma na Ndugu wa Marehemu walioutayarisha mwili kwa ajili ya mazishi na kuuona mwili huo kabla ya mazishi walithibitisha kuwa haukuwa na dalili za kupigwa, kujeruhiwa wala majeraha”

“Gari iliyopata ajali ilikuwa ni gari binafsi aina ya Toyota Land Cruiser GXR V8 yenye namba za Usajili T454 DWV iliyokuwa ikiendeshwa na Dugange na alikuwa peke yake katika gari hilo” ——— imeeleza taarifa ya THBUB
Screenshot_20230603_062006.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom