Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wakati Reece James amesaini mkataba wa muda mrefu kuitumikia Chelsea hadi 2028 Dirisha lililopita, leo pia Dada yake Lauren James amedondosha saini hadi 2027 kuendelea kuwa mshambuliaji wa Chelsea (W)

Laurene Msimu huu
Mechi 35
Magoli 8
Assist 2

Screenshot_20230601_151900.jpg
 
“Mimi natamani jambo hili liishe hata leo lakini nafsi yangu haipotayari kurudi tena Yanga!

“Hata kama kuna gharama za kulipa nipo tayari najua ndugu zangu watanzania hawawezi kuniangusha nitaomba wanichangie na ikibidi hata kukopa ili niwe salama.”

“Lakini kama itatokea sitocheza tena mpira nipo tayari lakini sio kurudi tena Yanga kutokana na mambo niliyopitia.”

Feisal Salum on PB
Screenshot_20230601_152107.jpg
 
“Baada ya hili sakata nimeshawahi kukutana na Eng. Hersi Said mara mbili, mara ya mwisho tulikutana Mikocheni tukiwa wawili tu, tukazungumza akaniambia wanataka kunirudisha kwenye timu mimi nikamwambia siwezi kurudi.”

“Mara ya kwanza tulikutana Serena Hotel nikamwambia anipe siku tatu niende kwanza nyumbani, nikivyorudi nikampa jibu lilelile kwamba siwezi kurudi kwa sababu hata wazee wangu pia hawataki.”

Eng. Hersi akaniambia haya basi nenda CAS, kama kiongozi anakwambia hivyo maana yake hakuna suluhisho.”
Screenshot_20230601_152426.jpg
 
“Dkt. Mshindo Msolla ni mtu mkarimu sana, anajua kuishi na wachezaji, kwa mfano hata ukikosea Msolla ni mtu wa kukutia moyo lakini sio mtu wa kuongea kwenye mitandao na ukifanya vizuri anakupongeza.”

“Ndio maana kipindi cha uongozi wake mimi sikuwahi kuonekana na tatizo licha ya hali ngumu ya kiuchumi kwa wakati huo.”

“Kwa hiyo watu wajiulize kwa nini kipindi cha uongozi huu Feisai ndio kaondoka? Mimi sina akili?
Screenshot_20230601_152519.jpg
 
KUHUSU KURUDI YANGA

“Mimi sina shida na Yanga, sina ugomvi na mashabiki/wanachama wa Yanga, hata hapa nilipo ni kwa sababu ya Yanga! Bahati mbaya wanaaminishwa mimi mbaya lakini mimi nawapenda kama wanavyonipenda!

“Mimi tatizo langu kubwa ni Rais wa timu [Eng. Hersi Said] ndio maana nilipokaanae chini nilimweleza kwamba naomba tumalizane ili kila mmoja aendelee na mambo yake ili na mimi niendelee na maisha yangu.”

“Kama Eng. Hersi Said akiondoka Yanga hata leo sasa hivi mimi nipo tayari kurudi Yanga. Sina tatizo na Yanga wala mashabiki, akiondoka Rais kwenye klabu mimi sasa hivi nafunga safari ya kurudi Yanga.”

- Feisal Salum via #PowerBreakFast
Screenshot_20230601_152612.jpg
 
“Nilimpigia simu Ghalibu [GSM] akawa hapokei, nikituma sms hajibu, nikawa nahisi pengine ana kazi zake akipata muda atanitafuta. Badae nikajua simu zangu anaziona na sms anasoma lakini hazishiki.”

“Wakati huo nilikuwa namtafuta kabla ya huu mgogoro kuanza ili nimshirikishe kutafuta suluhu lakini alikuwa hanipi ushirikiano. Na sikuwahi kumpata.”

“Hili sakata lilipotokea akaanza kunipigia simu, hata ungekuwa wewe ungepokea simu yake? Wakati wewe unampigia ili kupata suluhisho yeye hapokei simu zako, sakata limekuwa bichi yeye ndo anapiga simu. Roho inaniuma hadi kesho!

“Mimi masikini sina kitu, hata kama una hela zako usinidharau. Kipaji changu ndio kinaniweka mjini. Hata kama unanidharau, kipaji alichonipa Mungu ndio kinakufanya wewe utangaze mambo yako.”

- Feisal Salum via #PowerBreakFast
Screenshot_20230601_152658.jpg
 
“Nilikutana na kipa uso kwa uso nikampa pasi Nchimbi ili kufanya urahisi kwa Nchimbi kufunga lakini hakufunga. Mechi nyingine nikafanya hivyo kwa Mayele kwakuwa ni mwanangu nataka aongoze kwa magoli na yeye hakufunga!

“Shutuma za mimi kuuza mechi zikaanzia hapo, nikatukanwa natishiwa kwa kuambiwa ‘utarudi kwenu Pemba’, mimi mtanzania usiniambie Mpemba. Hiyo ikaanza kujenga hasira kwangu na manyanyaso bado yakaendelea.”

- Feisal Salum via #PowerBreakFast
Screenshot_20230601_153433.jpg
 
KUHUSU KURUDI YANGA

“Mimi sina shida na Yanga, sina ugomvi na mashabiki/wanachama wa Yanga, hata hapa nilipo ni kwa sababu ya Yanga! Bahati mbaya wanaaminishwa mimi mbaya lakini mimi nawapenda kama wanavyonipenda!

“Mimi tatizo langu kubwa ni Rais wa timu [Eng. Hersi Said] ndio maana nilipokaanae chini nilimweleza kwamba naomba tumalizane ili kila mmoja aendelee na mambo yake ili na mimi niendelee na maisha yangu.”

“Kama Eng. Hersi Said akiondoka Yanga hata leo sasa hivi mimi nipo tayari kurudi Yanga. Sina tatizo na Yanga wala mashabiki, akiondoka Rais kwenye klabu mimi sasa hivi nafunga safari ya kurudi Yanga.”

- Feisal Salum via #PowerBreakFast View attachment 2642503
Kumbe shida yote ni hiyo?
Yanga sijui wachangie vipi karata zao kati ya mr Hers na Feisal aondoke nani?
 
Kijana Tyson Nduguru, Rafiki wa karibu wa Joel Misesemo (MC Joel) aliyejirusha ghorofa ya 7 Makumbusho Dar es salaam na kufariki dunia, ambaye aliripotiwa kutoweka ghafla siku tatu tangu kutokea kwa kifo cha Joel, amepatikana leo June 1 2023.

Mke wa Tyson, Grace Rashid ameithibitishia @ayotv_ kwa kusema yafuatayo ------> “Ni kweli Tyson amepatikana mchana wa leo, mimi nilitoka kama kawaida nilikua naendelea na mizunguko akanipigia simu yeye mwenyewe, nimefika nyumbani nimeshaonana nae ni mzima wa afya, mpaka sasa sijaongea nae lolote Watu wapo wengi tupo na familia, nitawajulisha zaidi baadae"

Ripoti za kutoweka kwa Tyson ziliibua maswali mengi kutokana na ukaribu wa wawili hao pamoja na matukio mawili tofauti yaliyowatokea kwa kupishana siku chache yakiwa na mazingira ya kutatanisha.
Screenshot_20230602_042810.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi amezindua na kukabidhi mradi wa matundu 24 ya vyoo pamoja na chumba maalum kwaajili ya Wasichana kujisitiri, uliotekelezwa na Taasisi ya Flaviana Matata katika Shule ya Sekondari Mazinge iliyopo Mkoani Shinyanga.

Mradi huu utanufaisha jumla ya Wanafunzi 1,001 katika Shule ya Mazinge, ukihusisha vyoo na sehemu ya kunawia mikono pamoja na chumba maalum cha Wasichana kujisitiri wakati wa hedhi pamoja na sehemu ya kuchomea taka hususani taulo za kike zilizo kwisha kutumika.

Miundo mbinu hii itatatua changamoto ya muda mrefu ya uhaba wa vyoo na upatikanaji wa maji Shuleni hapo ambapo hafla ya uzinduzi huu imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Flaviana Matata akiambatana na Viongozi mbalimbali wa dini na wa kimila, sambamba Mashirika Wadau ambao wanatekeleza miradi ya maji na usimamizi wa usafi ya WASH nchini Tanzania.

Licha ya idadi kubwa ya Wanafunzi, Shuleni hapo kwa miaka yote imekuwa ikitegemea matundu 6 tu ya vyoo, (kwaajili Wasichana na kwa ajili ya Wavulana, pamoja na uhaba wa maji uliochangiwa kwa kiasi kikubwa na kutokuwa na miundombinu ya kuhifadhi maji, hali ambayo imekuwa ikihatarisha afya na kutatiza masomo kwa Wanafunzi hususani Watoto wa kike, wanapokuwa katika siku zao za hedhi.
Screenshot_20230602_043009.jpg
 
Tanzania imepokea msaada wa paundi milioni tano sawa na takribani Tsh. bilioni 15 kutoka Serikali ya Uingereza kwa ajili ya awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF).

Makabidhiano ya Hati za makubaliano ya msaada huo yamefanyika Jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar.

Akiongea baada ya makabidhiano hayo, Dkt. Mwamba amesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini Tanzania unaendelea vizuri jambo linalosababisha Washirika wa maendeleo kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya mpango huo.

Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar, amesema Uingereza ni Rafiki mkubwa wa Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo, hivyo Nchi yake itaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha inatoa mchango wake katika kukabiliana na umasikini ili kuboresha hali ya maisha ya Wananchi.
Screenshot_20230602_043315.jpg
 
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni amesema kama Mataifa ya Magharibi yatawanyima misaada kutokana na kupitisha sheria ya kupinga ushoga basi watakaa chini na kupunguza matumizi ya Nchi kwa kubana matumizi huku wakipanga bajeti kwa umakini lakini kamwe hawatoifuta sheria kwa kuogopa vikwazo vya Mataifa ya magharibi.

Museveni ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na Wanachama wa Chama cha NRM katika kile kinachoonekana ni kama anamjibu Rais wa Marekani Joe Biden aliyetishia kuiwekea vikwazo Uganda baada ya kupitisha sheria hiyo.

Museveni amesema “Kuhusu biashara wakituingilia kwenye biashara zetu, tutafanya biashara na Watu wengine, hakuna Mtu atakayetubabaisha wala kututingisha, Waganda mnapaswa kuwa tayari kwa vita, vita ni ya Majasiri sio kwa Watu Wadhaifu”

Sheria hiyo mpya itawalazimu Watu wanaoshiriki kwenye vitendo vya ushoga kutumikia hadi kifungo cha maisha jela.
Screenshot_20230602_043432.jpg
 
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekaidi wito wa Mataifa ya magharibi wanaotaka sheria kali dhidi ya ushoga ifutwe ikiwa ni moja ya sheria kali zaidi duniani ambapo Mtu yeyote anayesambaza ushoga anaweza kuhukumiwa kwa kifungo cha kifo ambapo amesema sheria imeshapita na haiwezi kufutwa.

Akiongea katika mkutano wake na Wanachama wa Chama cha NRM amesema Chama hicho hakijawahi kutumia lugha mbili tofauti na kwamba wanachokisema mchana ndicho watakisema usiku “Zoezi la utiaji saini wa muswada umekamilika, hakuna Mtu atakayetubabaisha wala kututingisha, Waganda mnapaswa kuwa tayari kwa vita, vita ni ya Majasiri sio kwa Watu Wadhaifu”

Itakumbukwa baada ya muswada huo kutiwa saini, Rais wa Marekani Joe Biden ametishia kuiwekea vikwazo Uganda huku Wanaharakati wa Uganda wakitoa wito kwa Wafadhili wa Kimataifa kuweka vikwazo dhidi ya Viongozi wa Uganda, tayari Spika wa Bunge la Uganda amefutiwa visa ya kuingia Marekani baada ya kusainiwa kwa sheria hiyo.
Screenshot_20230602_043535.jpg
 
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema wamepokea malalamiko kwamba kuna Shule zinazuia Wanafunzi kwenda likizo bila kushauriana na Wazazi huku Wazazi wengine wakitakiwa kulipa ili kuwaweka Wanafunzi Shuleni ambapo amewataka Viongozi wa Shule kutambua kuwa ni haki ya Mwanafunzi kwenda likizo.

Akiongea Jijini Dodoma Mkenda amesema “Kwa Shule za Serikali kuna mwongozo umetolewa na Kamishna wa Elimu wa siku za kufunga na kufungua Shule, ni muhimu sana tukajifunza kuzingatia huo mwongozo ili Wanafunzi wapate muda pia wa kupumzika, nahimiza Wakuu wa Shule wote na Wakurugenzi wazingatie utaratibu huo"

"Kwa Shule binafsi Kamishna alisema waangalie kalenda lakini wanaweza kufanya adjustment kulingana na mahitaji yao lakini ukweli unabaki palepale kwamba Wanafunzi wetu wanahitaji kupumzika"

"Wito wetu ni kwamba tusipelekee Kamishna atoe waraka wenye masharti makali kwa Shule binafsi, Wanafunzi wana haki ya kupumzika, likizo zimewekwa ili Watoto wapate muda wa kupumzika, wakae na Wazazi wao, wapate kucheza vilevile na kubadilisha mazingira na hii huwa inawasadia"
Screenshot_20230602_043643.jpg
 
Msafara wa viongozi wa Serikali, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Yanga na mashabiki wa soka wametua salama nchini Algeria kwa ajili ya kucheza mechi ya pili fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Mechi hiyo inatajiwa kuchezwa Jumamosi Juni 3 saa 4 usiku kwa saa za Tanzania huku Yanga ikiwa na matumaini ya kupindua matokeo baada ya kupoteza mchezo wa awali nyumbani.
Screenshot_20230602_043901.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Kheri James amesema iwapo mazingira yatatumika kama njia ya kuwainua watu kiuchumi, jukumu la kuyalinda litabebwa na jamii kwa mikono miwili.

James ameyasema hayo Leo, Alhamisi ya Juni 1, 2023 katika Jukwaa la Fikra lililojadili kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ametolea mfano katika Wilaya yake, jamii ya wahadzabe wananufaika na utunzaji wa mazingira kwa kuuza miti.

"Sio kwamba wana elimu bali ni jambo linalowapa fedha kwa hiyo wenyewe wanapanda miti na kuihifadhi," amesema.

Hata hivyo, amesema vita ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ni endelevu na kila anayekabidhi silaha ahakikishe anafanya hivyo kwa wakati.

Screenshot_20230602_044007.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom