Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo May 31, 2023
Screenshot_20230531_064158_Opera%20Mini.jpg
 
WANA MWENDO BALAA!
.
Hawa hapa ndio wachezaji waliokimbia kwa spidi kali zaidi katika EPL msimu huu:
.
37.31 km/h - Kyle Walker
36.70 km/h - Brennan Johnson
36.63 km/h - Mykhailo Mudryk
36.61 km/h - Anthony Gordon
36.53 km/h - Darwin Nunez

Screenshot_20230601_151218.jpg
 
MOUNT NA WENZAKE 14 WAPO SOKONI
.
Chelsea inaripotiwa kuwa na mpango wa kupitisha panga kwenye kikosi chake na kuna orodha ya mastaa wasiopungua 15 watafunguliwa mlango wa kutokea huko
Stamford Bridge kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.
.
The Blues chini ya mmiliki wake, Todd Boehly hivi karibuni ilimteua Mauricio Pochettino kuwa kocha wao mpya, ambako ataanza kazi rasmi Julai Mosi, lakini tayari imeshafahamika majina ya wachezaji ambao safari itawahusu kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi huko Ulaya ili kupunguza idadi ya wachezaji waliopo Stamford Bridge.
.
Kilichoelezwa ni kwamba mastaa hao wanaohusishwa na mpango wa kuondoshwa Chelsea ni pamoja na mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, Mason Mount, Trevoh Chalobah, Conor Gallagher, Ruben Loftus-Cheek na Callum Hudson-Odoi. Wengine wenye uwezekano wa kuachwa waondoke ni N’Golo Kante, Hakim Ziyech, Christian Pulisic, Mateo Kovacic, Kalidou Koulibaly, Cesar Azpilicueta, Edouard Mendy na Denis Zakaria, ambaye ataruhusiwa kurudi kwenye klabu yake ya Juventus baada ya mkopo wake kufika mwisho na Chelsea haijafurahishwa kumchukua.
Screenshot_20230601_151322.jpg
 
MARTIAL NJE FAINALI KOMBE LA FA
.
Straika wa Manchester United, Anthony Martial atakosa fainali ya Kombe la FA keshokutwa baada ya kuumia katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England dhidi ya Fulham wikiendi iliyopita.
.
Kwa sasa Martial anaungana na wachezaji wengine majeruhi kama Antony na Lisandro Martinez ambao wapo nje kutokana na majeraha.
Screenshot_20230601_151427.jpg
 
BENZEMA AISHTUA MADRID
.
Imeripotiwa kwamba nyota wa Real Madrid, Karim Benzema amewekewa ofa nono mezani ya Pauni 345 milioni (Sh trillion 1) ili akajiunge na timu kutoka Saudi Arabia ambayo jina lake limewekwa siri.
.
Kwa sasa hatima ya straika huyo mwenye umri wa miaka 35 imezua utata baada ya kugoma kuongeza mkataba mpya katika kikosi hicho ambao utamalizika kipindi cha kiangazi hivi karibuni.
.
Vilevile inaelezwa kwamba usajili wake utaisaidia taifa hilo kuomba uenyeji wa kuandaa mashindano ya Kombe la Dunia 2030, huku Mfaransa huyo akiwa kama balozi.
.
Kwa mujibu wa gwiji wa habari za usajili, Fabrizio Romano, mchezaji huyo anaifikiria ofa hiyo kwa makini na wakati wowote ataweka wazi kuhusu hatima yake. Kwa upande wa Real Madrid imeingiwa na hofu kwamba huenda asiongeze mkataba mpya na atafungua mlango wa kutokea kwenda Saudi Arabia.
.
Wakati hayo yakiendelea timu hiyo inamfuatilia mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Roberto Firmino ambaye amemalizana na klabu yake. Taarifa ziliripoti fowadi huyo atakuwa chaguo sahihi kama mbadala wa Benzema endapo ataondoka katika dirisha la usajli la kiangazi.
Screenshot_20230601_151519.jpg
 
Victorien Adebayor ataondoka RS Berkane mwishoni mwa msimu. Ni suala la muda tu. . Wakala anaamini hilo litafanyika lakini anasubiri tu ofa sahihi kwa mchezaji wake. Berkane hawana mpango wa kuendelea na mfungaji bora wa muda wote wa Niger msimu ujao. Simba, Al Hilal, TP Mazembe na Al Ittihad wanafuatilia kwa makini sakata hili. [mickyjr]

Screenshot_20230601_151643.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom