Makapuku Forum

Makapuku Forum

Farhan Jr

Leo naomba niongee na CEO wangu Kajula kuhusu Simba Sports kidogo!

Kaka mkubwa Iman Kajula, tuna mambo kadhaa kwanza tuhakikishe utamaduni wa kuwa na Kocha Mzawa kwenye set up yetu, Kocha anayejua soka la Tanzania pamoja na utamaduni wake! Tunaweza kuwa na Robertinho pamoja na Msaidizi wake (Kwa mujibu wa mapendekezo yake) ila tuwe na Msaidizi wa pili ambaye ni Mtanzania hii ina maana kubwa sana.

Point yangu ni nini? Point ni kuwa Robertinho anaweza kuhitaji Msaidizi wake ila Baba Mkwe Mgunda akasalia kama Msaidizi wa pili ikimpendeza ama yoyote kwa ajili ya kuchota vitu zaidi ikitokea wameondoka, timu haiyumbi sana kimfumo, anakuwa caretaker mzuri kabla ya mipango ya klabu kuleta Kocha mpya.

Lakini faida yake nyingine inafahamika kupata mawazo tofauti tofauti! Mfano Mamelodi wana Makocha watatu wa viwango, nadhani hii ni nzuri sana! Msaidizi wa Robertinho anaweza kuja na bado Mgunda akasalia klabuni.

Kaka CEO suala lingine ni hili la Mkurugenzi wa Ufundi na Mkurugenzi wa mpira! Huyu aje kuitazama timu, atuundie falsafa yetu ili mpira wa kufanana uanze timu ya vijana mpaka senior team!

Boss MO alisema ana ndoto ya timu za Vijana bora lakini itafanikiwa kwa falsafa za kufanana, leo hii Mamelodi tunaona wanavyofaidika na watoto kutoka timu B! Leo hii tunaona Generation Foot inavyoifaidisha Senegal! Tukiwa na falsafa tutajua tunataka wachezaji gani wa kuendana nasi.

CEO la mwisho ni hili la Legends wetu wa Simba! Tuwe na utamaduni wa kuwapeleka shule wachezaji wetu wa zamani, baadhi wakasomee Ukocha waanze na timu zetu za Vijana seriously na wapelekwe course mpaka nje ya nchi wapate exposure zaidi na zaidi.

CEO hata Watendaji wa klabu tunaweza kuwapata kutoka kwa Legends wetu, uwepo mpango maalum wakale kitabu ili wakija kuwa Maafisa wa klabu watashauri kwa ufasaha.

Wasalaam!

Screenshot_20230527_132852.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemuagiza Meneja wa Tarura Mkoa wa Iringa Mhandisi Makoli Kisare kutengeneza barabarani ya KM 1 ya kuelekea Kituo cha Afya Ifingo kuanzia kesho ili kupunguza adha kwa Wananchi wanaokwenda kupata huduma.

Chongolo ametoa agizo hilo leo May 27, 2023 baada ya kukagua Kituo hicho ambapo Wananchu wamelalamika kwa Katibu Mkuu changamoto ya barabara pamoja na kutokuwepo kwa Daktari wa upasuaji.

Katika hatua nyingine Chongolo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego kuhakikisha hadi kesho Kituco hicho pia kiwe kina Daktari anayeweza kutoa matibabu ya upasuaji, ili Wananchi wawe na uhakika wa matibabu.

Chongolo yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku saba ya kukagua uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2023 ambapo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sophia Mjema na Katibu wa Nec Oganaizesheni Issa Haji Gavu.
Screenshot_20230528_050949.jpg
 
Wanawake Wilayani Mufindi wameiomba Serikali kuwapa mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri ili waweze kujiendeleza katika biashara zao na kujiinua kiuchumi na kuacha kukopa mikopo umiza maarufu kama mikopo kausha damu.

Wanawake hao wamesema hayo leo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo na kueleza kuwa wamekuwa hawapati mikopo hiyo na badala yake wanakopa mikopo ya kausha damu na kuwafanya kushindwa kurejesha mikopo hiyo na kuishia kutelekeza Familia, kuvunja ndoa zao na hata kukimbia madeni.

Akiongea mbele ya Chongolo, Mwajuma Mbata Mjumbe wa CCM shina namba 3 kata ya Boma amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa kwa masharti ya kutengeneza vikundi katika makundi maalum ya Wajasiriamali wadogo lakini wanaopata mikopo hiyo ni wale wenye uwezo wa kukopa Benki “Kukosekana kwa mikopo hiyo kunatufanya tunajiingiza katika mikopo ya moto, tukishindwa kulipa tunaachika katika ndoa zetu na kutelekeza watoto”

Akijibu hoja hiyo Chongolo amesema Serikali ilifanya maamuzi ya kusitisha mikopo ili kutengeneza utaratibu mzuri wa kuwawezesha Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi na kusema utaratibu huo utakuwa umekamilika August,2023.
Screenshot_20230528_051225.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoani Lindi limetoa taarifa ya kujinyonga hadi kufa kwa mtoto Yusra Hassan Ally (11) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili kutoka kata ya Nyengedi, Halmashauri ya Mtama, mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilieleza kuwa mtoto huyo alijinyonga kwa kutumia nguo ambapo sababu ya kufanya hivyo haijajulikana.

Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Alhaj Kabaleke Salim Hassan alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 17 majira ya saa Nane mchana.

Screenshot_20230528_051757.jpg
 
Isaack Mnyagi mkazi wa Sombetini jijini Arusha anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga mwenza wake, Jackline Mnkonyi (38) na kisha kumng’oa jino la mbele na kumtoboa jicho.

Tukio hilo limetokea juzi Alhamisi Mei 25, 2023 baada ya kutokea ugomvi ambao unadaiwa kuchangiwa na wivu wa mapenzi baina ya wenza hao.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni ,Daraja Mbili jijini Arusha, Jackline ambaye anamtoto mchanga amesema amepigwa na mumewe baada ya kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mgeni aliyefika nyumbani bila kujua Kama ni mjomba wake.

Amesema Mei 23, 2023 alitembelewa na Mjomba wake, Vicenti Matai kutoka mkoani Simiyu kwa lengo la kumsalimia baada ya kuondoka mgeni huyo mume wake saa 4.45 usiku alianza kumuhoji.

Jackline amesema alimweleza Mgeni huyo alikuwa na mjomba wake lakini mumewe alikataa na ndipo alipoanza kumshambulia kwa ngumi, mateke na mkanda na baadaye alichukua Praizi na kumng'oa jino kwa nguvu.

"Nilijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana alianza kunipiga kwa mateke na ngumi na alichukua Praizi na kuniamuru nifungue mdomo na kuning’oa jino moja ambapo damu zilianza kuchuruzika,”amesimulia kwa uchungu huku akilia.
Screenshot_20230528_052118.jpg
 
Wanawake wilayani Mufindi wameiomba serikali kuwapa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ili waweze kujiendeleza katika biashara zao na kujiinua kiuchumi na kuacha kukopa mikopo inayowaumiza

Wamesema hayo leo Jumamosi Mei 27, 2023 mbele ya
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo na kueleza kuwa wamekuwa hawapati mikopo hiyo na badala yake wanakopa mikopo yenye riba kubwa kwa muda mchache (kausha damu) na kuwafanya kushindwa kurejesha mikopo hiyo na kuishia kutelekeza familia na kukimbia madeni.

Screenshot_20230528_052223.jpg
 
Kuelekea mchezo wa kesho Mei 28, 2023 wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Alger ya Algeria itakayopigwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar saa 10:00 jioni, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema tayari limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema usalama siku ya mchezo utakuwa wa kiwango cha juu maeneo yote ya kuzunguka uwanja ndani, nje na
barabarani.

"Hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo," amesema

Amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye tabia ya kuwasha fataki au baruti uwanjani, kurusha chupa au kitu chochote.

Ameeleza kuwa hayo ni baadhi ya makosa ya mambo ya kiusalama kwenye viwanja vya soka.

"Jeshi la Polisi halitavumilia tabia hizo na zingine ambazo zimepigwa marufuku na vyama vya soka FIFA, CAF na TFF. Watakao kaidi, watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Jeshi la Polisi linawatakia mashabiki wa soka kushangilia kistaarabu,"amesema.

Screenshot_20230528_052328.jpg
 
EPL KESI IMEISHA
.
Tiketi ya kuiwakilisha Ligi Kuu England kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao imeshapata wenyewe, ambapo Manchester City itaungana na Arsenal, Manchester United na Newcastle United kwenye michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya klabu huko Ulaya.
.
Pazia la Ligi Kuu England likienda kufungwa kesho, Jumapili, Man City ndio walionyakua taji hilo, wakifanya hivyo kwa msimu wa tatu mfululizo. Arsenal ilijaribu kutunisha misuli, lakini dakika za mwisho pumzi zilikata na kujikuta wakipigwa kikumbo kwenye kilele cha msimamo wa ligi hiyo na matokeo yake, kumaliza nafasi ya pili, inayowafanya kurudi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya miaka mingi kupita. Ushindi wa Man United kwa Chelsea umewafanya kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo huo na kukata tiketi ya Ulaya, huku Newcastle wakikamilisha Top Four.
Screenshot_20230528_052925.jpg
 
Kingsley Coman ameshinda taji la ligi kwa kila msimu katika maisha yake ya soka. Huyu mwamba kapita PSG, Juventus na sasa Bayern

2012/13
2013/14
2014/15
2015/16
2015/16
2016/17
2017/18
2018/19
2019/20
2020/21
2021/22
2022/23

Jamaa bado anaendelea kucheza mpaka astaafu ni lini?
Screenshot_20230528_053238.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom