Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President - Legal Affairs), Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma na uteuzi huu umeanza tarehe
20 Aprili, 2023.

Rais Samia amemteua pia Dkt. Richard Stanslaus Muyungi kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira (Advisor to the President - Climate Change and Environment), kabla ya uteuzi huu Dkt.Muyungi alikuwa Meneja wa Mazingira, katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), uteuzi huu umeanza tarehe 19 Aprili, 2023.
Screenshot_20230422_040721.jpg
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekataa kutia saini muswada mpya unaoeleza hukumu ya kifo katika baadhi ya kesi dhidi ya ushoga ambapo ameomba muswada huo ufanyiwe marekebisho kwa kuongezewa ukali zaidi kabla ya yeye kutia saini na kuifanya kuwa sheria.

Museveni pamoja na mambo mengine ametaka pia sheria irekebishwe ili kuwaruhusu Watu wanaokataa kwa hiari yao vitendo vya ushoga wapitie hatua za urekebishaji au waweze kupatiwa matibabu ya kuwabadilisha na kuwaweka sawa licha ya kwamba hatua hizo zimekataliwa na Mashirika ya matibabu kuwa hazifai na zinaweza kuleta madhara ya afya ya akili kwa wanaobadilishwa tabia.

Uamuzi huo wa Museveni umetangazwa baada ya mkutano wa Wabunge ambao takribani wote wanaunga mkono muswada ulioidhinishwa na Wabunge mwezi uliopita, Museveni amepewa siku 30 za kusaini muswada huo ili iwe sheria na kuirejesha Bungeni ili ifanyiwe marekebisho na kumjulisha Spika wa bunge kwenye maamuzi, hata hivyo, inaweza kupitishwa kuwa sheria bila kibali cha Rais iwapo muswada huo utarudishwa Bungeni mara mbili.

Muswada huo katika hali yake ya sasa umependekeza adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kufanya mapenzi ya jinsia moja hadi miaka 14 kwa kosa la ushoga na kifungo cha miaka 20 jela kwa kuajiri, kukuza na kufadhili shughuli za mapenzi ya jinsia moja.
Screenshot_20230422_040824.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewatakia Waislamu wote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr itakayoadhimishwa kesho Jumamosi Aprili 22, 2023.

Pia Rais Samia amewataka Waislamu kuendeleza misingi waliyoishi katika siku hizi 30 kwa misingi ya kutenda yaliyo mema, kuwajali wengine, sadaka, shukrani na ibada kwa Mwenyezi Mungu.

“Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr. Kuandama kwa mwezi ni hitimisho la funga yetu lakini pia ni wakati wa kuendeleza misingi tuliyoishi katika siku hizi 30; misingi ya kutenda yaliyo mema, kuwajali wengine, sadaka, shukrani na ibada kwa Mwenyezi Mungu. Eid Mubarak,” ameandika Rais Samia katika mitandao yake ya kijamii.

Screenshot_20230422_040937.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kwa kuwateua washauri wawili wa Rais katika masuala ya sheria na mabadiliko ya tabianchi na mazingira.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu leo Ijumaa, Rais Samia amemteua Jaji George Masaju kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya sheria.

Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Uteuzi huu umeanza Aprili 20, 2023.
Pia Rais Samia amemteua Dk Richard Muyungi kuwa Mshauri wa Rais katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira.

Kabla ya uteuzi huo Dk Muyungi alikuwa Meneja wa Mazingira katika Shirika la Umeme (Tanesco). Uteuzi huu umeanza Aprili 19, 2023.
Screenshot_20230422_041039.jpg
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limemtangaza waamuzi watakao chezesha Kombe la Dunia chini ya umri wa 18 yatakayofanyika nchini Argentina kuanzia Mei 20-11 Juni mwaka huu.

FIFA limewataja Issa Sy kutoka Senegal na Abongile Tom kutoka Afrika ya Kusini ni miongoni mwa waamuzi watatu kutoka Ukanda wa CAF katika mashindano hayo.

Sy atachezesha mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Wydad Casablanca na wasidizi wake Bongoura Nouha kutoka Senegal, Desire Ngoh wa Ivory Coast wamechaguliwa kuchezesha pia Kombe la Dunia.

Naye Abongile Tom kutoka Afrika ya Kusini atakayechezesha mechi ya Yanga dhidi ya Rivers United atakuwa miungoni mwa waamuzi hao waliotajwa na FIFA.

Screenshot_20230422_041134.jpg
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewaonya wakazi wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari kwani kutashuhudiwa vipindi vikubwa vya mvua kwa siku mbili kwa mikoa minne ikowepo Dar es Salaam.

Kulingana na taarifa iliyololewa leo Aprili 21, 2023 TMA mikoa hiyo mitatu ni Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar.

TMA imefafanua kuwa vipindi hivyo vya mvua vitashuhudiwa kwa siku mbili mfufulizo katika Jiji la Da es Salaam, mikoa ya pembezoni na mkoani Morogoro.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Ladislaus Chang'a amesema wanaoishi mabondeni wanapaswa kuchukua tahadhari.

Amesema mvua zinazoendelea sasa ni utabiri uliofanyika Februari 22, mwaka huu ambapo TMA ilitabiri Dar es Salaam, Pwani, Zanzibar na Mororgoro zingepata mvua za juu kuliko kawaida.

Screenshot_20230422_041228.jpg
 
Kadhi wa Wilaya ya Jinja nchini Uganda, Sheikh Ismail Adi Basoga amemtaka Rais Museveni kutoyumbishwa na maoni ya nchi nyingine na badala yake asaini muswada wa Sheria ya Kupinga mapenzi ya jinsi moja.

Sheikh Ismail Adi Basoga ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Aprili 21, 2023 wakati wa swala ya Eid el-Fitr iliyofanyika Mvule Crescent Mjini Jinja.

"Tunamtaka Rais asaini muswada huo bila kutishwa na nchi za Magharibi, hatutaki vitendo vyao viovu ambavyo haviendani na tamaduni zetu kuharibu watoto wetu na viongozi wa baadaye," amesema Sheikh Basoga.

Rais Museveni pamoja na wabunge wa National Resistance Movement (NRM), jana waliazimia kurudisha Sheria ya Kupambana na mapenzi ya jinsia moja 2023, kwa kamati ya masuala ya kisheria na Bunge ambapo uchunguzi wa kina na marekebisho yatafanywa kabla ya kuidhinishwa.
Screenshot_20230422_041332.jpg
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetangaza nafasi za kazi 42 katika taaluma mbalimbali kwa Watanzania wasiozidi umri wa miaka 45 kuanzia leo Ijumaa Aprili 21, 2023 na mwisho wa kutuma maombi ni Mei 4, 2023.

Tangazo hilo la kazi limetolewa leo Ijumaa Aprili 21, 2023 likitoa nafasi kwa madereva sita wa daraja la II, mchumi mmoja daraja la II, mhandisi umeme mmoja daraja la II, ofisa usimamizi wa fedha mmoja daraja la II, waandishi 10 wa taarifa rasmi za Bunge daraja la II.

Nafasi nyingine ni Ofisa Tehama (Network Administrator) mmoja daraja la II, Ofisa Sheria mmoja Daraja la II, Katibu wasaidizi wa Bunge (Sheria) wawili daraja la II, Katibu wasaidizi wa Bunge (Uchumi) wawili daraja la II, Katibu wasaidizi wa Bunge (Afya ya Jamii/Menejimenti ya huduma za afya) wawili daraja la II, Katibu wasaidizi wa Bunge (Usimamizi wa mazingira) mmoja daraja la II.

Katibu Msaidizi wa Bunge (sosholojia) mmoja daraja la II, Makatibu Mahsusi saba daraja la III, Mteknolojia Maabara mmoja daraja la II, Wafiziotherapia wawili daraja la II, Msaidizi wa kumbukumbu mmoja, Ofisa kumbukumbu mmoja daraja la II, Ofisa utafiti mmoja daraja la II.
Screenshot_20230422_041429.jpg
 
Kocha wa Manchester United, Erick ten Hag amesema golikipa wake David de Gea bado yupo kwenye kiwango kizuri kwakuwa anaongoza kwa 'cleansheets' Ligi Kuu England.

Takwimu zinaonyesha De Gea ndiye golikipa aliyefanya makosa mengi ya kusababisha mabao akifanya 5 tangu msimu uliopita. Jana usiku Manchester United ilichezea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Sevilla na kuondolewa Europa League huku De Gea akifanya kosa lililozaa bao la tatu.

Ten Hag amemtetea akisema kwa cleansheets alizonazo ni wazi yeye ni golikipa bora.

Screenshot_20230422_041600.jpg
 
CAF CHAMPIONS LEAGUE
.
AL AHLY RAJA CASABLANCA
Huu unatazamwa kama mchezo ambao unaweza kutoa timu itakayotinga fainali msimu huu, umebatizwa kuwa mchezo wa wababe, ambao utapigwa kesho Aprili 22, saa 4 kamili usiku kwenye uwanja wa Cairo, ukiwa unatajwa kuwa mchezo wenye msisimko mkubwa zaidi kuliko mingine ya hatua hii.
.
Al Ahly ambayo thamani yake kwa mujibu wa mtandao maarufu wa Transfer Market ni Bilioni 74.7, wanakutana na Raja ambao thamani yao ni Bilioni 38.6. Timu hizo zimekutana mara tatu kwenye michuano hii na jambo la ajabu Raja hawajashinda hata mara moja, huku Al Ahly wakishinda mara moja na sare mara mbili.
.
Ahly watatakiwa kuwa makini na mshambuliaji wa Raja, Hamza Khaba ambaye anaongoza akiwa kinara kwa sasa baada ya kufunga mabao matano msimu huu.

Lakini kwa Raja watatakiwa kuwa makini na straika wa Al Ahly, Mohammed Manem akiwa ameshafunga mabao manne. Huu unatazamwa kama mchezo ambao unaweza kutoa timu itakayotinga fainali msimu huu.

Screenshot_20230422_041751.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom