Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230422_041859.jpg
 
Bila Aishi tena kwa Simba kwenye hatua kubwa, wamesalia Beno David na Ally Salim, kwenye derby alianza Bwana Mdogo Ally na akatoka na cleansheet.

Kuelekea Champions League naona uwezekano ni Mkongwe Beno kurejea mbele ya Ally, mtazamo wangu.
Screenshot_20230422_042128.jpg
 
Watu kumi wa familia moja, wakiwemo wanawake saba na wanaume watatu wameuawa na watu wenye silaha siku ya Ijumaa katika mji wa Pietermaritzburg, jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.

Inaaminika kuwa watu wawili wenye silaha waliingia kwenye nyumba hiyo na kufyatua risasi kwa familia hiyo, na kwa mujibu wa polisi chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana.

Msemaji wa polisi wa kitaifa Athlenda Mathe ameiambia CNN kuwa baadhi ya watuhumiwa wa tukio hilo tayari wamekamatwa.

"Washukiwa wawili wamekamatwa, mmoja amekufa, mwingine alikimbia eneo la tukio. Polisi wanaendelea na msako,” amesema na kuongeza kuwa bunduki tatu zimepatikana kutoka kwa washukiwa hao.
Screenshot_20230422_042315.jpg
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillius Wambura amemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufuatilia tukio la mzee Abdallah Mohammed Ngombo mwenye umri wa miaka 75, mkazi wa Mkuranga aliyedaiwa kupigwa risasi mguuni na Askari Polisi nyumbani kwake wakati wakiwa katika operesheni.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime amesema Jeshi la Polisi Makao makuu limesikia taarifa hiyo na kilio cha wanandugu, hivyo linafanya uchunguzi ili haki iweze kutendeka.

“Jeshi la Polisi Makao makuu limesikia maelezo na kilio cha wanandugu pamoja na taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji. Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Camillius Wambura amemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kufuatilia tukio hilo na kufanya uchunguzi kwa kina ili haki iweze kutendeka kama wanandugu walivyoomba,” amesema.

Inadaiwa katika tukio hilo, Polisi walifika nyumbani kwa mzee huyo wakiwa na mtuhumiwa ambaye aliwapeleka nyumbani hapo kwa shutuma za wizi, na ndipo lilipotokea tukio hilo la kupigwa risasi.

Naye kijana wa mzee huyo, Mohammed Ngombo amesema kwa sasa mzee Abdallah amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu, na kwamba madaktari wameshauri akatwe mguu wake ili kuepusha madhara mengine zaidi.
Screenshot_20230422_042424.jpg
 
Simba imemkosa Sadio Kanoute katika takribani mechi tatu au nne za mwisho, kwa asilimia kubwa Erasto Nyoni amekuwa akiziba nafasi yake, licha ya Erasto kufanya kazi nzuri lakini bado Simba waliikosa roho ya paka ya Sadio katika eneo lao la kiungo.

Nafikiri Simba wanamuhitaji sana Sadio katika mechi ya kesho, kama yupo fiti ni kheri kama ataanza kwa sababu ya uwezo wake wa kukaba kwenye eneo kubwa la kiwanja, Erasto alikuwa ana hold space zaidi lakini Sadio anakaba man to man na anakimbia na mpira.

Sadio anakupa energy ileile katika dakika zote tisini kitu ambacho kwa Erasto hakikuonekana, haikushangaza kwanini alitolewa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga kwa sababu tayari pace yake ilipungua katikati ya uwanja, partnership ya Sadio na Mzamiru ni miongoni mwa partnership bora kwa sababu nchini Tanzania.

All the best kwa Simba .
Screenshot_20230422_042542.jpg
 
Happy Eid wadau wote wa jukwaa hili.

Ndugu yenu mwaliko wa jana ninautoa leo.

Shunie asante kwa magazeti na nasema tena, jukwaa hili ni sehemu nzuri kuwepo sababu ya mambo haya.
 

Nikimuusia chairman kushiriki Kili Marathon baada ya kupiga mpunga wa Eid
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom