Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Mchezaji wa kimataifa [anaecheza kwenye klabu ambayo sio ya nchini kwake] mfano mchezaji wa nje ya Tanzania akiingia kwenye matatizo na klabu ya Tanzania, anaweza kwenda moja kwa moja FIFA.”

“Mchezaji wa Tanzania akiingia kwenye mgogoro na klabu ya Tanzania hiyo inaitwa ‘national dispute’, yeye anaweza kwenda CAS pekeyake. Kufungua tu kesi CAS ni Tsh. 56 hadi 60 milioni!

“Mimi na timu yangu ya Uingereza tunajaribu kuongea na Katibu wa FIFA na kuangalia tunasaidiaje kukifanyia kazi kipengele hicho kwa sababu fedha ni nyingi sana, kuna wachezaji wengi wa Afrika hawawezi kumudu wanashindwa kupeleka kesi zao CAS.”

“Washushe kiwango cha fedha kwa wachezaji wanaocheza Afrika ili wale wenye madai yao waweze kupeleka kesi zao CAS.”

- Jasmine Razack, Msimamizi wa Feisal Salum.
Screenshot_20230415_043940.jpg
 
“Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwasimamia wachezaji wa nje, kwa mfano Emanuel Ebue aliwahi kupitia kwenye changamoto za kimikataba. Akiwa Ulaya kuna wakati alikwaruzana na msimamizi wake wakashindwana, wakati tunahangaika na kesi yake nikamuuliza kwa nini alisaini mkataba wa aina ile?

“Akaniambia, wazazi wake walifariki na yeye alilelewa na bibi yake ambaye alikuwa anauza tumbaku sokoni kupata fedha ya kujikimu. Alipokuja mtu kuniambia ananipeleka Ulaya ninaweza kupata hadi dola 10,000 kama mchezaji unafikiri nawaza nin?

“Ebue anasema alipoletewa mkataba akasaini chapchap na kutia dole gumba! Kwa hiyo ni vigumu kuwalaumu hawa wachezaji kwa sababu wakati mwingine wanafanya hivyo kwa sababu ya hali zao na familia zao.”

“Kwa hiyo sisi ambao tunafahamu pamoja na hizi klabu zetu tunapaswa kuwasaidia wachezaji wa aina hii. Ulaya matatizo ya aina hii yalikuwa mengi hadi wakatunga sheria kwa hiyo klabu zinaogopa kuwasainisha mikataba tu kiholela.”

- Jasmine Razack, Msimamizi wa Feisal Salum.
Screenshot_20230415_044226.jpg
 
#VituExtra.

MWENYE HEKIMA NA KUHESHIMIKA ZAIDI - ACHRAF HAKIM.

Duniani kote kuna asili ya majina na maana zake. Mara nyingi kama sio mara zote kuna baadhi ya majina hubeba ‘Kusudio na suluhisho’

Jina la ACHRAF lina maana ya ‘Anaeheshimika zaidi’ na Hakim maana yake ‘Hekima’. Nmetoa hizi tafsiri kwenye lugha ya kiarabu.

Kwenye michezo story kubwa leo hii ni kuhusu nyota wa PSG, Beki wa kupanda na kushuka Achraf Hakim kwa jinsi ambavyo amecheza kama “Pele” kwa Ex-wife wake Hiba Abouk.

Achraf huu ni wakati wake wa kutumia zaidi Hekima na kutunza heshima yake. Kwanini?

Feb 24, 2023 Zilitoka taarifa kuwa mwamba akiwa kwenye hekalu lake huko Paris alishikwa na upwiru uliomkaba koo akamrukia mdada mwenye umri wake miaka 24, na inasemakana Achraf alibaka.

Lakini wakati zinatoka hizi taarifa za Achraf kubaka, mkewe alitoka hadharani na kusema wakati huo walikua tayari wameshaachana na Achraf. Mke alimkana mumewe SAA SITA KAMILI JUA KALI na aliongeza kwa kusema hawezi hata siku 1 hawezu kuwa upande wa WABAKAJI.

Mahakamani, Achraf alikana mashitaka, kesi bado ipo kwenye uchunguzi, na PSG walisema wanamuamini mchezaji wao na hawakumtema kikosini.

Fast forward, 14 April 2023 Leo zinatoka taarifa kuwa Achraf hakim ameshinda kesi dhidi ya mzazi mwenzake kwenye suala la kugawana mali.

Taarifa zinasema Achraf mali zote alizisajili kwa jina la mama yake mzazi, hvyo mke wa Achraf hana chake cha kuchukua kutoka kwa Achraf. Watu wa kubet hii mnaitaje? NO GG, au sio?

Lakini tukumbuke kesi ya Achraf ya kubaka bado inafanyiwa uchunguzi, na aliebakwa anasema ana ushahidi wote.

Hakim kama ilivyo maana ya jina lake ‘Hekima’ imemuwezesha kushinda mtego wa kwanza wa ndoa na kulinda mali zake. Je mtego wa pili wa kubaka, Ataweza kushinda kesi na kulinda Heshima ya jina lake la Achraf lenye maana ya anayeheshimika zaidi?

LETS WAIT AND SEE
Screenshot_20230415_042729.jpg
 
Aliyekuwa Mke wa Mchezaji wa Klabu ya PSG , Achraf Hakimi aitwaye Hiba Abouk baada ya kuachana na Hakimi March 27,2023 alienda Mahakamani na kuwasilisha kesi ya kudai talaka huku akitaka agawiwe nusu ya mali ya Hakimi.

Baada ya Mahakama kufanya tathimini za mali za Achraf ilibaini kuwa aliyekuwa Mume wake hamiliki chochote kwani mali yake yote imesajiliwa kwa majina ya Mama yake

Hakimi anapokea Euro Milioni Moja (zaidi ya Shilingi Bilioni 2.56 kama Mshahara ndani ya PSG kila mwezi lakini 80% (zaidi ya Shilingi Bilioni 1.64) pesa hizo huwekwa kwenye akaunti ya mama yake Bi. Fatima.

"Hana mali, magari, nyumba, vito au hata nguo kwa jina lake.Wakati wowote na akitaka chochote huwa anaulizia kwa Mama yake ambaye huwa anamnunulia"

Mahakama ilitoa taarifa hiyo.

Inakadiriwa Kuwa Hakimi Achraf ana Utajiri wa Euro Milioni 17 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 45 ila Mali zote zinamilikiwa na Mama yake, Bi Fatima.
Screenshot_20230415_042729.jpg
 
Farhan Jr

MWANAUME yoyote makini anajua tabia zote za Mke wake au Mpenzi wake, kuna muda huwa tunatulia tu kuepusha shari ila tuna mipango mingi sana tunaweka kuhakikisha ujinga wa huyo Mwanamke hautupi shida hata ukiondoka.

Okay! Pichani ni Hakim akiwa na Mama yake Mzazi, kifupi amewakumbusha Wanawake kitu muhimu sana
Screenshot_20230415_044712.jpg
 
Farhan Jr

Wakati Achraf Hakimi anapongezwa sana ila yupo Mtalaam mwingine anaitwa CRISTIANO RONALDO, yeye watoto watatu wa mwanzo aliwapata kwa mkataba maalum na Wanawake aliozaa nao, unalipwa pesa yako unasaini mkataba kuwa ukishazaa unapoteza haki zote na mtoto ni wa Ronaldo.

Kifupi ni kuwa baada tu ya kujifungua basi Mama yake Ronaldo anabeba Mjukuu wake na safari ya Ureno inaanza ya kwenda kumlea Mjukuu wake, wala hakuna mjadala mwingine

Watoto aliopata sasa kwa Georgina ni kuwa hawapo kwenye ndoa ni Wapenzi tu, hata wakiachana suala la child support sio zito kwa Ronaldo, ndio maana hata Georgina ametulizana sana anasikilizia.

Nyuma ya Hakimi kuna Mama yake Mzazi na nyuma ya Ronaldo pia kuna Mama yake Mzazi.

Wakina Mama wanawajua sana Wanawake wenzao! Watoto wa Mama
Screenshot_20230415_044817.jpg
 
Alaf Shunie naomba unisaidie jambo moja, kuna Uzi nautafuta sana. Kuna jamaa anaelezea Mzee wake alifariki, yeye akarudi home kukaa na mama yake. Baada ya muda kuna Mali akauza ili apate ada ya kuendelea na masomo. Mama yake alipojua, akamwambia aondoke home, jamaa akaenda Njombe (nahisi alikuwa mwalim pia).

Kama umeijua, naomba unitag au unitajie jina
The guy alisomea sheria and later akauza some sort of machine to pursue postgraduate Ili kua mwalimu, Ryt?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom