Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri wa TAMISEMi, Angellah Jasmine Kairuki amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 leo April 14,2023 ambapo amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, TAMISEMI imetengewa Tsh. Bilioni 16.58 kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa “Kati ya magari hayo, magari 5 ni ya Wakuu wa Mikoa, magari 2 ni ya Makatibu Tawala wa Mikoa na magari 74 ni ya Wakuu wa Wilaya”

Waziri Kairuki pia amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, Ofisi ya Rais - TAMISEMI imetengewa Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa boti 4 katika Halmashauri za Wilaya za Ludewa, Buchosa, Nyasa na Sumbawanga ili kuimarisha doria, ulinzi na ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri hizo.

“Hadi Februari, 2023, Tume imepokea Shilingi Bilioni 7.83. Majukumu yaliyotekelezwa ni pamoja na kusajili walimu 9,800, kupandishwa vyeo walimu 1,003, Walimu 3,347 wamethibitishwa kazini na Walimu 3,388 wamebadilishiwa vyeo”

“Kuhuisha TANGE za walimu kwenye Wilaya zote 139, vikao 300 vya mashauri ya nidhamu kwa walimu vya kisheria vimefanyika, Mashauri 273 ya nidhamu ya walimu yamefanyiwa uchunguzi na kuwasilishwa kwenye Kamati za Wilaya kwa ajili ya kutolewa uamuzi”
Screenshot_20230415_033042.jpg
 
Serikali imesema hakuna mikopo ambayo imeshindwa kulipa katika kipindi cha awamu zote sita za uongozi, hayo yamesemwa Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bunda, Boniphace Mwita Getere aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kupata mkopo wa fedha nyingi wa muda mrefu kwa masharti nafuu ili kulipia madeni sumbufu katika awamu zote sita.

Chande amesema katika kipindi cha awamu zote sita Serikali imeendelea kukopa na kulipa mikopo kulingana na mtiririko wa malipo kwa kila mkopo na hakuna mikopo ambayo Serikali imeshindwa kulipa “Malipo ya madeni yote ikiwemo madeni sumbufu yanaendelea kulipwa kupitia mpango na bajeti za Serikali za kila mwaka”

Amesema Serikali inaendelea kusimamia deni la Serikali kupitia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, SURA 134 inayobainisha vigezo vya kuzingatia wakati wa kutafuta fedha za mikopo kutoka ndani na nje ya Nchi ili kugharamia shughuli za Serikali, hususani miradi ya maendeleo.

Amesema Sheria hiyo pia inatumika kama nyenzo ya kudhibiti ongezeko la deni la Serikali kwa kulipa mikopo iliyoiva na kutoa kipaumbele kwa mikopo yenye masharti nafuu.
Screenshot_20230415_033543.jpg
 
Wizara ya Usawa wa Jinsia na Familia ya nchini Korea Kusini imetangaza kwamba itatoa Won 650,000 ($500) ambazo ni sawa na TZS 1,172,500 kwa mwezi kwa kila kijana anayepitia hali ya upweke kwa nia ya kuwasaidia kwenye mfumo wao wa kisaikolojia kuimarisha afya zao za akili.

Mambo mbalimbali yanayofikiriwa kwenye kuchangia hali hii ya upweke ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa fedha, magonjwa ya akili, matatizo kwenye ngazi za familia au changamoto za afya.

Hatua hizo mpya zinalenga hasa Vijana kama sehemu ya Sheria kubwa ya Usaidizi wa Ustawi wa Vijana ambayo inalenga kusaidia Watu waliojitenga sana na jamii pamoja na Vijana wasio na Mlezi au ambao hawahudhurii masomo wakiwa hatarini kujihusisha na uhalifu.

Posho ya kila mwezi itapatikana kwa waliojitenga na wanaopitia hali ya upweke wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi 24 ambao wanaishi katika Familia zenye mapato ya chini ya wastani wa mapato ya kitaifa.

Vijana wanaweza kutuma maombi kwa ajili ya programu hii katika ofisi za Ustawi wa Jamii lakini pia Walezi wao, Washauri au Waalimu wanaweza pia kutuma maombi kwa niaba yao.
Screenshot_20230415_033910.jpg
 
Leo April 14,2023 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angellah Kairuki ameliomba Bunge likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kiasi cha Shilingi Trilioni Tisa Bilioni Mia Moja Arobaini na Nne Milioni Ishirini na Moja na Mia Sita Tisini na Tisa Elfu (Tsh. 9,144,021,699,000).

Kwa upande wa Sekta ya Elimu ya Msingi na Sekondari Waziri Kairuki ametaja maendeleo yaliyopewa kipaumbele ikiwemo kugharamia elimu bila ada kwa Shule za Msingi na Sekondari ambapo Shilingi Bilioni 399.64 zimetengwa.

“Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 157.79 zimetengwa kwa ajili ya Shule za Msingi na Shilingi Bilioni 241.85 zimetengwa kwa ajili ya Shule za Sekondari”

“Bajeti hiyo ni sawa na ongezeko la Shilingi Bilioni 53.15 sawa na asilimia 15.34 ikilinganishwa na bajeti ya Shilingi Bilioni 346.49 iliyoidhinishwa katika Mwaka wa Fedha wa 2022/23, ongezeko hili linatokana na Wanafunzi wa kidato cha tano na sita kujumuishwa katika Mpango wa Elimu Bila Ada”
Screenshot_20230415_034143.jpg
 
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla amewataka Wamiliki wa Bar na kumbi za starehe na Vyombo vya muziki kufuata na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya Baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC ili kuepusha kero ya kelele za muziki kwa Wananchi.

Aidha RC Makalla amesema kumekuwa na malalamiko makubwa ya uvunjifu wa Sheria kufuatia ongezeko la Bar na kumbi Za starehe kwenye makazi ya Watu ikiwa ni pamoja na upigaji muziki usiku mzima na kuathiri Wananchi.

Katika mkutano huo uliohusisha Viongozi wa mitaa, masoko na Wadau wa mazingira, RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Serikali za Mitaa kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kudhibiti utoaji vibali vya ujenzi.

Kwa mujibu wa sheria na kanuni za NEMC makosa na adhabu kwa wanaokiuka Sheria ya kupiga mziki kwenye makazi ya Watu ni faini ya shilingi milioni 2 mpaka milioni 10, kifungo cha miaka miwili jela au vyote kwa pamoja na sheria inaruhusu upigaji muziki kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa nne usiku kwa kiwango kilichoruhusiwa na kwa bar zinazokesha nao wamepewa taratibu za kufuata Ili kupewa kibali.
Screenshot_20230415_034504.jpg
 
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Songwe, @Juliana_Shonza ametoa misaada mbalimbali zikiwemo pea 64 za traksuti na pedi 128 kwa ajili ya Wanafunzi wa Sekondari ya Vwawa waliounguliwa na bweni na kuteketeza vitu vyao vyote hadi zikiwemo nguo za kubadilisha.

Moto huo ambao chanzo chake bado hakijafahamika umeunguza bweni la Wanafunzi 64 katika Shule ya Sekondari Vwawa iliyopo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Songwe, Elautery Mremi mapema leo alisema moto huo umeanza leo Ijumaa Aprili 14, 2023 asubuhi ambapo Jeshi hilo limefanikiwa kuudhibiti usienee kwenye mabweni mengine na madarasa.

Kamanda huyo amesema hakuna majeraha wala vifo vilivyosababishwa na moto huo huku tathmini ikiendelea kubaini madhara na chanzo cha moto huo.

Kamanda Mremi amesema bweni hilo lilikuwa linatumiwa na Wanafunzi 64 ambapo vitu vilivyokuwemo ndani ya bweni hilo vimeteketea, wakati moto huo unatokea Wanafunzi walikuwa darasani wakiendelea na mitihani.
Screenshot_20230415_034807.jpg
 
Kwenye kubwa za wiki hii ni pamoja na hii, utamaduni wa namba za magari Dubai kuuzwa kwa bei kubwa pengine kuliko hata gharama za magari mengi tu ya kifahari unazidi kushika kasi ambapo kwenye habari za wiki Dubai ime-trend na 'plate number' iliyouzwa mnadani kwa kiasi cha dirham milioni 55 ( USD milioni 15) ambayo ni zaidi ya bilioni 35 kwa pesa za Tanzania.

Waandaaji wa Mnada huo “Emirates Auction” wamesema bei ya namba hiyo ambayo ni P7 imevunja rekodi ya awali iliyoshikiliwa na Saeed Abdul Ghaffar Khouri ambaye mwaka 2008 alinunua plate number ya gari kwa USD milioni 14.2 katika mnada ulioandaliwa na kampuni hiyo hiyo.

Mapato yaliyopatikana kwenye mnada huyo yamepelekwa kwenye kampeni ya “One Bilion Meals” kampeni inayoendeshwa na Mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum na Waziri Mkuu wa UAE ili kusaidia jamii zilizokumbwa na changamoto mbalimbali duniani wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Namba za magari zenye tarakamu chache ikiwemo zenye tarakimu moja Dubai zimekuwa kwenye utamaduni wa kuuzwa kwa bei ghali zaidi na huwa zina ufahari na kuwatambulisha Matajiri kwa njia ya kipekee kwani wenye pesa ndefu tu ndio wenye uwezo wa kuzinunua.
Screenshot_20230415_034932.jpg
 
Klabu ya Yanga SC imetoa salamu za pole kufuatia kifo baba mzazi wa mchezaji Mamadou Doumbia kilichotokea jana Aprili 13, 2023 nchini Mali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, beki huyo anatarajiwa kusafiri mapema leo kwenda Mali kwa ajili ya kushiriki mazishi ya baba yake.

Screenshot_20230415_035129.jpg
 
Wachungaji wawili nchini Angola wamekamatwa kwa kuvaa nguo zinazofanana na sare za jeshi na kuendesha shughuli haramu za kidini kutokana na kikundi chao kutosajiliwa.

Wachungaji hao wa kikundi kilichopewa jina la Jeshi la Imani walikamatwa baada ya kusambaa kwa video yao mtandaoni ikiwaonyesha wakiongoza hafla iliyohudhuriwa na vijana zaidi ya 80 baadhi yao wakiwa wamevaa magwanda yanayofanana na sare za jeshi.

Msemaji wa Huduma za Upelelezi (SIC), Manuel Halaiwa akizungumzia sakata hilo amesema wachungaji hao watachukuliwa hatua kisheria.
Screenshot_20230415_035223.jpg
 
Kijana Jack Teixeira (21) amekamatwa na maofisa wa Shirika la Upelelezi wa Ndani la Marekani (FBI) akishukiwa kuhusika na uvujishaji mkubwa wa nyaraka za siri ikiwemo vita vya Ukraine na Marekani.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland amesema mtuhumiwa huyo ni mfanyakazi katika jeshi la anga la walinzi wa taifa na kiongozi wa kundi la mtandaoni ambako hati hizo zilivujishwa kwa mara ya kwanza.

Ofisi ya jeshi la anga la Marekani imesema kuwa Teixeira alijiunga mwaka 2019 na alikuwa ni mtaalamu wa Tehama ambaye alikuwa amefikia kiwango cha wafanyakazi wa daraja la kwanza.

Screenshot_20230415_035329.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom