Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima ameitambulisha klabu ya Yanga SC kuwa balozi wa kampeni maalum yenye lengo la kupinga na kutokomeza mmonyoko wa maadili.

"Napenda kuchukua fursa hii kuwatambulisha rasmi Klabu ya Yanga kuwa mabalozi wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto"

Rais wa klabu hiyo, Hersi Said amesema anaungana na Waziri Gwajima katika kampeni hiyo ya kupinga mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto.
Screenshot_20230415_035448.jpg
 
Jeshi la Polisi katika Kaunti ya Malindi nchini Kenya linamtafuta Mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International kutokana na kudaiwa kuwashawishi waumini wake wafunge kisha wafe ili waweze kuingia mbinguni na kuurithi ufalme.

Taarifa za awali zinaeleza waumini wanne wamefariki wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali Kuu Kaunti Ndogo ya Malindi, huku mmoja amefariki baada ya kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Lango Baya ambako walipelekwa kwa ajili ya kutoa maelezo.

Polisi wamefanya msako baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu kuwepo kwa kanisa hilo lenye kueneza imani potofu kwa kuelekeza watu kufunga kisha wafe ili waweze kufika mbinguni.

Wakazi wa eneo la Shakahola, Kata ya Adu wamesema kwamba mhubiri huyo amekuwa akiwashawishi waumini wake wafunge bila kula, wafe ili waweze kuurithi ufalme wa mbinguni.
Screenshot_20230415_035600.jpg
 
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angella Kairuki ameliomba bunge kuidhiinisha Sh16.58 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 kwa ajili ya ofisi za wakuu wa mikoa.

Kairuki ameliomba bunge leo Ijumaa Aprili 14, 2023 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Tamisemi kwa mwaka 2023/2024.

Amesema katika mwaka huo Ofisi ya Rais -Tamisemi imetengewa Sh16.58 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 katika ofisi za wakuu wa mikoa.

Amefafanua kuwa kati ya magari hayo, magari matano ni ya wakuu wa mikoa, magari mawili ni ya makatibu tawala wa mikoa na magari 74 ni ya wakuu wa wilaya.
Screenshot_20230415_035658.jpg
 
Aliyekuwa mke wa mchezaji wa Klabu ya PSG, Achraf Hakimi aitwaye Hiba Abouk baada ya kuachana na mumewe Machi 27,2023 alienda makamani na kuwasilisha kesi ya kudai talaka huku akitaka agawiwe nusu ya mali.

Baada ya Mahakama kufanya tathimini ya mali za Hakimi ilibaini kuwa hamiliki chochote kwani vyote anavyomiliki vimesajiliwa kwa jina la mama yake mzazi.

Hakimi analipwa mshahara wa Euro 1milioni kwa mwezi ikiwa ni zaidi ya Sh2.56 bilioni ndani ya PSG lakini 80% ya mshahara huo huwekwa kwenye akaunti ya mama yake Fatima.

"Hana mali, magari, nyumba, vito au hata nguo kwa jina lake.Wakati wowote na akitaka chochote huwa anaulizia kwa mama yake ambaye huwa anamnunulia." Ilisema taarifa ya mahakama.

Abouk (36), alipompeleka mumewe mwenye umri wa miaka 24 mahakamani, alitarajia kupata mgao sawa wa Euro 70 milioni baada ya kutengana, lakini aliarifiwa kwamba nyaraka zilionyesha mali zake zote ni za mama yake.

Screenshot_20230415_040157.jpg
 
Rais, Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Aprili 14, 2023 ameongoza Kikao cha Watendaji wa Msajili wa Hazina wakiongozwa na Msajili wa Hazini, Nehemia Mchechu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Pia, kikao hicho, kimehudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka.
Screenshot_20230415_040339.jpg
 
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Dawasa) imetangaza kuwa kutakuwa na kukosekana kwa huduma ya maji kwa wateja wanaotumia mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu kwa wastani wa saa 16 siku ya Jumamosi.

Taarifa hiyo iliyotolewa leo Ijumaa, Aprili 14, 2023 na kitengo cha mawasiliano Dawasa, imeeleza kuwa katizo hilo la maji litaanza kesho saa 12 jioni hadi siku ya Jumapili saa 4 asubuhi.

“Sababu ni uruhusu matengenezo ya bomba kubwa la inchi 36 eneo la Visiga Saheni na kutoa matoleo mawili maeneo ya Kwembe na Msigani yanayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji maeneo ya Kibamba Pangaboy na Mbezi Malamba Mawili,” imeeleza taarifa hiyo.

Imetaja maeneo yatakayoathirika kuwa ni pamoja na Chalinze, Chalinze Mboga, Msoga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias na Kwa Mbonde.

Maeneo mengine ni Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mloganzila, Mbezi Magari Saba, Mbezi Kwa Yusufu, Njeteni, Msigani, Kifuru, Mbezi Inn, Mbezi Stendi ya Magufuli, Mbezi Mshikamano, Mbezi Louis, Makabe, Msakuzi, Mbezi, Kimara,Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru na Bonyokwa.

Pia wateja wa Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe watakumbwa na katizo hilo la maji
Screenshot_20230415_040547.jpg
 
Mshambuliaji hatari wa Yanga, Fiston Mayele licha ya kuifunga Simba katika mechi mbili za ngao ya hisani bado hajafanikiwa kufunga bao katika mechi tatu za Ligi Kuu walizokutana na Jumapili Aprili 16 itakuwa mechi ya nne. Je ataweza kuvunja mwiko huo katika Ligi Kuu?
Screenshot_20230415_041107.jpg
 
KIUNGO fundi wa mpira wa Simba, Saido Ntibazonkiza, amekiri wakati mwingine umaarufu huwa ni kama kero pale mashabiki wanapoingilia faragha zao, japo amesema ni changamoto ambazo kama mchezaji analazimika kuzioea kwa vile anahitaji sapoti ya watu hao katika maisha ya soka.

Kauli ya Saido imekuja baada ya juzi kuvamiwa na shabiki alipotimba kwenye Uwanja wa Uhuru kushuhudia chama lake la zamani la Geita Gold, likivaana na KMC na kutoka na ushindi wa mabao 2-0, ambapo licha ya kujichanganya na watu ili asijulikane mashabiki walibaini na kumvaa alipokuwa akitoka uwanjani hapo.

Akiwa hana hili wala lile, ghafla saido alijikuta akivamiwa na shabiki huyo aliyekuwa na nia ya kutaka kumkumbatia, huku Mwanaspoti likishuhudia, lakini staa huyo akawahi kumzuia akitaka kwanza ajitambulishe.

Shabiki huyo aliyekuwa akiongea lugha za Kiswahili na Kilingala alipiga magoti, huku akimuomba msaada wa pesa na katika kuepusha mambo mengi, Saido alitoa noti ya Sh 5,000 na kumpa licha ya kuombwa Sh 2,000.

Baada ya kupewa pesa hiyo, shabiki huyo aliyeonekana kama aliyelewa aliendelea kumng'ang'ania akitaka kumkumbatia Saido, mara apige magoti kama vile anataka kumsujudia, ghafla akaanza kumwambia amuombee, lakini staa huyo alimzuia.

Saido alipoona anaendelea kung'ang'aniwa na shabiki huyo alikubali kupiga naye picha na wakati wanapata picha ya pamoja (shabiki huyo) alipata mpenyo wa kumwambia ya moyoni kuhusu soka.

Mara baada ya kupata sekeseke hilo, Saido aliliambia Mwanaspoti,
"Naheshimu wanaotusapoti kwenye kazi zetu, ila kuna wakati zinatokea changamoto mbalimbali, ndio maana unaweza ukawakuta wachezaji wana kofia hadi usoni wanapotokea maeneo kama haya, kwani umaarufu ni gharama."

Screenshot_20230415_041219.jpg
 
SAKATA la kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum 'Fei Toto' dhidi ya Yanga limeingia sura nyingine baada ya upande wa mchezaji huyo kuwasilisha barua ya kuvunja mkataba,Fei aliamua kuandika barua kwa TFF kuomba kuvunja mkataba na Yanga kwa kufuata taratibu.
Vipengele hivyo vya barua hiyo ndivyo vilivyozaa utata na maswali matano ambayo Mwanaspoti imekuainisha hapo chini;

MASWALI MATANO

1. Ni klabu gani ambayo Fei anasema inampa ushirikiano na kujali maslahi yake tofauti na Yanga ambao ni waajiri wake?

2. Kama amekiri kimaandishi kuwa, kuna klabu inampa ushirikiano na kujali maslahi yake, kamati itambana aitaje na ikishaijua itachukua hatua gani, kwa vile kikanuni ndio iko nyuma ya uamuzi wa Fei kuikacha Yanga?

3. Fei kama alikuwa haelewani na Yanga kwa muda mrefu kama alivyoandika kuwa, amepitia manyanyaso, kwa nini alikubali kusaini mkataba mrefu wa kuitumikia timu hiyo huku akijua hana mahusiano nayo mazuri?

4. Je, kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji inayo mamlaka kuvunja mkataba halali wa mchezaji kwa sababu nyingine tofauti na zile zinazoainishwa katika muongozo wa hadhi za wachezaji wa kimataifa?

5. Iwapo Fei alikuwa ananyanyaswa kwa muda mrefu, amewahi kuwasilisha malalamiko kwa kamati hiyo au vyombo vingine vya soka vinavyowezakutumika kama uthibitisho wa ombi lake ya kuvunja mkataba na Yanga?

Bila ya shaka ni suala la kusubiri hiyo Aprili 25 kuona kama Yanga itatekelezewa vipengele na Fei atakubaliwa kuvunja mkataba huo na klabu hiyo unaotarajia kufikia tamati mwakani.

Screenshot_20230415_041359.jpg
 
MARTINEZ AIPA PIGO MAN U
.
NDIO basi tena! Ndiyo neno rahisi unaloweza kulitumia baada ya klabu ya Manchester United kutoa taarifa kuwa beki wao tegemeo, Lisandro Martinez atakaa nje ya uwanja hadi mwishoni mwa msimu.
Screenshot_20230415_042111.jpg
 
TAMBO ZA MASELA NA BUSARA ZA MZEE KUTOKA BANDA UMIZA KUELEKEA KARIAKOO DERBY.

Kwahiyo mliamua kuwapumzisha Clatous Chama na Saido Ntibazonkiza kwaajili ya game yetu sio? Ok sisi watoto wa Jangwani hatutaki sababu siku hiyo mkitaka kikosi cha Yanga mkipange nyinyi halafu refa achezeshe Murtadha Mangungu, kibendera tumuache tajiri Dewji afanye mazoezi...... hii ni sauti ya shabiki mmoja jezi nyeusi kifuani HAIER hapa Banda Umiza anapiga sana kelele anasema mechi hata ipigwe siku tano mfululizo haoni Lunyasi wakichomoka mbele ya Kuala Lumpur.

Simba hii ya Jean Baleke kuna shabiki mmoja anatuambia huu ndo wakati wa kurudisha heshima iliyopotea ruksa kwa Yanga kuingiza vikosi viwili uwanjani, katikati kuna Puttin na Mzamiru pembeni amesimama Chama na Saidoo halafu mbele kuna kiumbe kinaitwa Jean Othos Baleke, wakati huo hujamtaja kabisa Phiri Moses iyo tarehe 16 ifike tu

Mzee mmoja ananyanyuka kutoka benchi la mbele kisha anaomba apewe sikio la kila mmoja humu Banda Umiza, kuna kitu anataka kusema kuelekea kwenye mchezo huo......Nisikilizeni vijana wadogo nimeishi na kuzishuhudia Derby nyingi kuliko magoli aliyofunga Aziz Ki hapa Bongo, Nyie si mnawasifia hawa mabeki wenu!! Derby ilichezwa na Keneth Mkapa ambaye mechi nzima hajapoteza mpira, kuna mtu alikuwa anaitwa Method Mogella achana na huyu Onyango mnaesema nusu mtu nusu chuma, Mogella akija kukukaba mara moja akirudi mara ya pili unampa mpira wewe mwenyewe.

Derby ilijaa wazawa kibao achana na hii iliyojaa Wakongo na Wazambia, mnamjua Constantine Kimanda nyie? Kuna mtu alikuwa anaitwa Sanifu Lazaro "Mwiba" nyie hamjui chochote kuhusu Kariakoo Derby hapo mnapiga tu kelele, ngoja niwaambie sasa........

Screenshot_20230415_042204.jpg
 
KOCHA YANGA ATAKA SALIM ADAKE J2
.
BEKI wa zamani Coastal Union, na aliyekuwa kocha wa timu ya vijana ya Yanga Charles Makwaza amesema dakika 90 alizomwangalia kipa wa Simba, Ally Salim amegundua ana uwezo mkubwa na kama benchi la ufundi litamuamini hata Kariakoo Derby ya Jumapili anaweza kufanya vizuri.
.
“Ishu ni kumuamini kwa sababu ile mechi ndio ilionesha uwezo wake, binafsi simdai kitu na kama makocha wake wakiamua mbona anaweza kucheza hata dhidi ya Yanga?” Alihoji kocha huyo ambaye pia ni mchambuzi wa kabumbu.
.
“Lazima tuangalie mbali badala ya kukomaa na mtu mmoja lazima wapewe nafasi vijana kama hawa ambao kesho watasaidia kwenye mahitaji ya timu ya Taifa,”
Screenshot_20230415_042400.jpg
 
YANGA TUTASHINDA - DJUMA SHABANI
.
Beki Mkongoman, Djuma Shaban ametuma salam kwa Simba akisema gari lao la ushindi kwa sasa imekata breki, na malengo yao ni kushinda mechi ya Kariakoo Derby.
.
“Timu yetu kwa sasa iko na ubora mkubwa tumekuwa na muendelezo mzuri wa kushinda licha ya mabadiliko ya kikosi chetu, unapopata nafasi lazima ufanye vizuri kwa kuwa kuna wengine nao wanaweza kufanya vizuri siku wakicheza,” alisema Djuma na kuongeza;
.
“Hatujashinda ubingwa bado na ili tuchukue taji tunatakiwa kushinda mechi mbili na kuanzia hii ya Simba, hatutakiwa na mchezo hata kidogo, Yanga tutashinda mashabiki wetu waje.”

……………
Screenshot_20230415_042512.jpg
 
"Sina kitu mimi, vitu ni vya mama yangu "
Mke wa mchezaji wa timu ya PSG ya Ufaransa na raia wa Morocco, Ashraf Hakim amekutana na maajabu ya mwaka baada ya kubaini kwamba pesa zote alizokuwa anaingiza mume wake karibu zote zilikuwa zinaingia kwenye akaunti ya mama yake, bi Fatma.

Mwanamke huyo aliwasilisha madai ya talaka mahakamani na kuiomba mahakama impe nusu ya mali zote.

Hata hivyo ushahidi uliowasilishwa mahakamani unaonyesha kwamba, mchezaji huyo anapokea asilimia 20 tu ya mshahara wake na asilimia 80 inaingia kwenye akaunti ya mama yake. Pia mahakama imeelezwa kwamba Ashraf hana gari wala nyumba vyote ni vya mama yake.

Kwa mwaka mchezaji huyo analipwa karibu Shilingi bilioni 37 na mamilioni kadhaa. Ashraf Hakim ana umri wa miaka 24 na mtalaka wake bi Abouk ana umri wa miaka 36...!
Screenshot_20230415_042729.jpg
 
“Mkataba wa mchezaji na klabu unavunjika wakati wowote, mchezaji awe na sababu au asiwe na sababu...hiyo ni kwa mujibu wa sheria za FIFA. Hiyo ni haki ya mchezaji.”

“Kwa hiyo mchezaji yeyote, anaweza kuvunja mkataba wakati wowote. Sasa kunakuwa na vigezo, mfano mchezaji alikuwa na mkataba wa miaka mitatu au mitano, tunaangalia kavunja kwa sababu zipi? Labda hana sababu kinachofuata ni kulipa fidia au adhabu ya kufungiwa.”

“Lakini kumuamrisha mchezaji akatumikie mkataba wake ni kitu ambacho hakiruhusiwi. Haipo na hairuhusiwi kwenye mpira.”

“Ila tunawashauri wachezaji kwa kuangalia mikataba yao, kama vipengele ni vigumu sana tunawaambia, huu mkataba unaweza kuvunjwa lakini madhara yake ni 1, 2, 3. Unaweza kuamuriwa ulipe kiasi fulani cha pesa, unazo au utaweza kulipa? Unaweza kufungiwa, upo tayari?

“Lakini mchezaji ana haki ya kuvunja mkataba muda wowote. Anaweza kusaini leo akavunja kesho! Anaweza kusaini mkataba wa miaka mitatu akavunja mkataba baada ya mwaka mmoja.”

- Jasmine Razack, Msimamizi wa Feisal Salum.
Screenshot_20230415_043401.jpg
 
“Mimi nimekuja nimekuta Feisal ameshatuma barua Yanga, sikuwanae tangu mwanzo wa hili tatizo. Nilimkutaka akiwa hayupo sawa kiakili kwa sababu tayari watu walikuwa wamemshambulia sana kwa maneno.”

“Kwangu aliletwa na mchezaji mwenzake wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, hadi sasa Feisal hajazungumza na chombo chochote cha habari kuhusu hiki kinachoendelea.”

“Kwa hiyo haya maneno mengine yote yabatoka kwa watu wengine, kwa kuwa na mimi ni mama na nina mtoto wa kiume kama yeye niliumia! Nikachukua muda wa kuzungumza na familia yake lakini nikazungumza na watu wa karibu ya Yanga na wengine ni viongozi.”

“Kwa kuwa kuna moto katikati unawashwa na watu wengine, nikamwambia Feisal twende Umrah kwa ajili ya kufanya ibada nikiamini ataweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida na kupoa.”

“Tulivyorudi akaitwa Taifa Stars japo hakuwa katika ubora wake kutokana na kutocheza kwa muda lakini naona alikuwa tofauti ukilinganisha na nilivyomkuta mwanzo.”

- Jasmine Razack, Msimamizi wa Feisal Salum.
Screenshot_20230415_043508.jpg
 
“Msuva alipokuwa Morocco [Wydad Casablanca] alipotaka kuvunja mkataba, hakupitia chama cha soka cha Morocco. Aliandika barua moja kwa moja kwa klabu, hii ni sheria ambayo pia FIFA wanaitambua, heiwezekani ‘third part’ kuvunja mkabata.”

“Lakini Tanzania nimekutana na hiki kipengele kwenye kanuni za TFF [kanuni ya 74.14] kwamba, endapo kuna mgogoro baina ya klabu na mchezaji chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba ni Kamati ya Hadhi za Wachezaji.”

“Nilishangaa sana kwa sababu ni kitu ambacho kinakinzana na sheria za FIFA! Haiwezekani ‘third part’ ambayo si sehemu ya mkataba yenyewe ndio iwe na mamlaka ya kuvunja mkataba.”

“Nikaenda mbali zaidi kutaka kujua kwa nini hii kanuni imewekwa? Nikaambiwa imewekwa kwa ajili ya kulinda wachezaji na klabu. Zamani wachezaji walikuwa wanafukuzwa kiholela kwenye klabu zao na wachezaji walikuwa wanajiondokea.”

“Kwa hiyo vipengele hivyo viliwekwa kudhibiti kuachana kienyeji. Nikaona ni sawa. Lakini ni rahisi kwa klabu kumuacha mchezaji kwa sababu inakuwa ipo kwenye kipengele cha mkataba.”

- Jasmine Razack, Msimamizi wa Feisal Salum.
Screenshot_20230415_043814.jpg
 
“Kwa muda mfupi ambao nimesimamia kesi za wachezaji wa Tanzania nimegundua kwamba wengi hawajui haki zao, hawajui sheria zipoje unaposaini mkataba na wengi hawana wasimamizi waliobobea kwenye masuala ya soka [sio kujua kuchambua], sheria za mpira na haki za wachezaji.”

“Wachezaji hawajui wakala analipwa na nani, wachezaji wengine wanaogopa kuwa na wasimamizi kwa sababu wanajua wao [wachezaji] ndio wanapaswa kuwalipa wasimamizi! Wachezaji wengi wanawalipa wasimamizi wao, lakini mawakala wao wanapaswa kulipwa na klabu.”

“Nilipozungumza na klabu kadhaa zimesema huwa zinawalipa mawakala, kwa hiyo mawakala wanarudi tena kwa wachezaji kudai pesa na kuwatishia wasipowapa watakuwa hawachezi.”

“Wachezaji wengi wametoka kwenye familia za kawaida na hawajasoma kwa kiwango cha juu cha elimu kwa hiyo wanapokutana na pesa wanasaini mkataba kwa ajili ya kujinusuru na umasikini. Kwa hiyo unawaelewa kulingana na hali wanayokuwanayo.”

- Jasmine Razack, Msimamizi wa Feisal Salum.
Screenshot_20230415_043940.jpg
 
“Najaribu kufanya ninavyoweza lakini pia nazungumza na Katibu wa TFF Wilfred Kidao ili kujaribu kuweka utaratibu ambao utawasaidia hawa wachezaji.”

“Ikiwezekana kuwe na utaratibu klabu zinapowasainisha wachezaji mikataba kuwe na watu wanaomsimamia mchezaji. Sasa sio tu mtu yeyote bali awe na utaalam amesajiliwa na TFF inamtambua ili kuondokana na hizi kadhia za malalamiko ya kimkataba.”

- Jasmine Razack, Msimamizi wa Feisal Salum.
Screenshot_20230415_043940.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom