Makapuku Forum

Makapuku Forum

Nitashukuru sana mkuu. Sometime tags hazileti notifications. Ukiupata make sure na respond tag yako mkuu🙏🙏🙏
Brother, I've tried to look for it but i didn't find it
i even reviewed my chrome history but i found nothing

Buh the highlight of the story ni kua the guy alikua ni clever sana and baada ya kumaliza form four wazazi walijutahd akaenda advance baadae chuo kusoma sheria after that his pap passed away hivyo akatakiwa kurudi nyumban kumtunza mama good enough miradi mingi ya mzee alikua anaijua so after deep hustle akaamua kuuza machine moja na kusoma postgraduate ya ualimu later on time mama akajua and kukawako crisis

I don't recall everything but that it's a short highlight of the story for anyone who recall it please help us out.

I'm sorry for my bad Swahili.
 
Brother, I've tried to look for it but i didn't find it
i even reviewed my chrome history but i found nothing

Buh the highlight of the story ni kua the guy alikua ni clever sana and baada ya kumaliza form four wazazi walijutahd akaenda advance baadae chuo kusoma sheria after that his pap passed away hivyo akatakiwa kurudi nyumban kumtunza mama good enough miradi mingi ya mzee alikua anaijua so after deep hustle akaamua kuuza machine moja na kusoma postgraduate ya ualimu later on time mama akajua and kukawako crisis

I don't recall everything but that it's a short highlight of the story for anyone who recall it please help us out.

I'm sorry for my bad Swahili.
I know the story, but for now I'm more interested on the guy who posted it than then story itself. I think he's in the position of helping me with some informations.

Shukran sana kwa kujaribu kuitafuta. I hope it will pop up again, before it's too late. 🙏🙏
 
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila amewahakikishia Madereva wanaotumia Barabara ya Chalinze- Segera kuwa ukarabati wa sehemu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika eneo la Kimange utakamilika kesho na Barabara itaanza kutumika.

Mativila ambaye yupo eneo la tukio usiku huu amesema maji yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha yalikatisha juu ya Barabara na kusababisha nusu ya Barabara kukatika ambapo kazi ya kujaza mawe katika eneo hilo inaendelea usiku huu.

Kwa sasa Madereva wanapita kwenye kipande kidogo cha Barabara ambacho hakijakatika lakini Mativila amewasihi Madereva kupita eneo hilo kwa tahadhari kubwa ili kuepusha madhara kwa Binadamu.
Screenshot_20230416_033955.jpg
 
Ndege kubwa ya Airbus A380 ya Shirika la Ndege la Emirates yenye uwezo wa kubeba Abiria 550 imetua kwa dharura Jijini Dar es salaam usiku huu katika uwanja wa Julius Kambarage Nyerere ikiwa na Abiria 514.

Chanzo cha kuaminika kimeiambia @AyoTV_ Ndege hiyo ambayo imetokea Sao Paulo, Brazil kuelekea Dubai imetua kwa dharura ili kuongeza mafuta yatakayoisaidia kukamilisha safari yake ambayo sasa imerefushwa kutokana na kulazimika kuikwepa njia yake ya kawaida ambayo ilikua ni kupita kwenye anga ya Sudan ambayo kwa sasa imefungwa.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ndege hii kubwa ya Abiria duniani kutua kwa dharura nchini Tanzania kwani mwaka 2018 Airbus A380 kama hii ilishindwa kutua nchini Mauritius kutokana na hali mbaya ya hewa na badala yake ikatua Dar es salaam Abiria wakalazwa Hotelini na kuondoka kesho yake.
Screenshot_20230416_034121.jpg
 
Kenya imepeleka Satelaiti yake ya kwanza katika mzingo wa dunia, kwa kutumia roketi lililofyatuliwa kutoka California, Marekani, ripoti ya Shirika la anga za mbali la Nchini Marekani la SpaceX zimethibitisha.

@dw_kiswahili inaripoti kuwa kurushwa kwa Satelaiti hiyo kulitarajiwa majira ya usiku muda wa Marekani Jumatatu wiki hii lakini kulicheleweshwa mara kadhaa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Satelaiti hiyo ya Kenya ilisanifiwa na kikundi cha Watafiti kutoka Kenya na inanuia kutoa data za kilimo na kuchunguza mabadiliko ya kimazingira nchini Kenya, hususan wakati huu nchi hiyo inapokabiliwa na ukame wa muda mrefu.

Pattern Odhiambo, Mhandisi wa Shirika la Kenya la Anga za Mbali, KSA, amesema satelaiti hiyo iliyopewa jina la Taifa 1, itakuwa na faida za moja kwa moja katika sekta za utafiti na kuboresha mavuno ya kilimo.

Hadi mwaka 2022, Satelaiti zipatazo 50 za Mataifa ya Afrika zilikuwa zimepelekwa kwenye mzingo wa dunia, kulingana na Shirika la Nigeria linalofuatilia mipango ya Afrika ya anga za mbali.
Screenshot_20230416_034222.jpg
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetangaza ofa kuwa yoyote atakayetoa taarifa ya Mtu au Kiwanda kinachozalisha mifuko ya plastiki isiyokidhi viwango vya TBS, Baraza hilo litampa zawadi ya Tsh. Milioni moja lengo likiwa ni kuhakikisha mazingira yanatunzwa.

Akiongea wakati wa Mkutano na Wadau wa Mazingira Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka amesema NEMC itahakikisha taarifa za mtoa taarifa zinabaki kuwa ni siri baina ya NEMC na yeye.
Screenshot_20230416_034315.jpg
 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde amesema tangu kuanzishwa kwa mpango wa mwamba darasa uzalishaji wa pweza umeongezeka ambapo mwaka 2017 uzalishaji eneo la Songosongo ulikuwa tani 9.8 lakini baada ya ufungaji wa hiyari wa uvuvi wa zao hilo uzalishaji uliongezeka hadi tani 37.6 mwaka 2019 zenye thamani ya shilingi milioni 373.5.

Silinde amesema hayo wakati wa halfa ya uzinduzi wa mwongozo wa usimamizi wa ufungaji wa hiyari wa uvuvi wa Pweza (Mwamba darasa) iliyofanyika leo Aprili 15, 2023 Bagamoyo mkoani Pwani.

"Ongezeko hili la uzalishaji limesababisha kuongezeka kwa ongezeko la upatikanaji wa malighafi kwenye viwanda vyetu nchini, mfano nimearifiwa kuwa kiwanda cha kusindika samaki ikiwemo pweza cha Alfa kimeongeza uzalishaji kutoka kilo 213,945 mwaka 2020 mpaka kilo 587400 mwaka 2022"

Silinde amesema takwimu zinaonesha kuwa zao la pweza linachukua nafasi ya pili baada ya mazao ya sangara na ni la kwanza kwa upande wa mazao ya bahari ambapo mauzo yake nje ya Nchi kwa mwaka 2022 yalifikia kiasi cha tani 1056 ambao waliuzwa kwa thamani ya shilingi bilioni 19.8.

Akizungumzia mchango wa zao hilo la uvuvi kwa Mwananchi mmojammoja, Silinde amesema tofauti na mazao mengine uvuvi wa pweza unahusisha jinsia zote huku wastani wa kipato ukiwa ni shilingi 100,000 kwa mvuvi wakati wa ufunguzi wa msimu.
Screenshot_20230416_034506.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam kuelekea mechi ya Simba na Yanga kesho, limetoa tahadhari na onyo kali kwa baadhi ya tabia za Mashabiki kuwashambulia Waamuzi Wasaidizi kwa chupa za maji au chupa zenye vimiminika ambavyo vinadhaniwa kuwa na haja ndogo wakati ambao huwa hawakubaliani na baadhi ya maamuzi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema Jeshi la Polisi halitavumilia pia tabia za baadhi ya Mashabiki kuharibu miundombinu ya uwanja kama kuharibu mabomba ya vyoo na bafu pamoja na viti “Tabia hizi ni chafu na hazikubaliki na watakofanya vitendo hivyo watakamatwa wakati huohuo au baada ya mchezo kutegemea mazingira ya eneo Mtuhumiwa huyo atakapokuwa”

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linashauri pia katika mchezo wa soka au mpira wa miguu hasa kwenye Timu zenye upinzani na uwezo unaoonekana kulingana, si vema kwa Mashabiki au Wapenzi wa Timu hizi kwenda uwanjani na matokeo mfukoni kwani matokeo yoyote yatakayotokea lazima yakubaliwe na Watu waondoke bila vurugu, fujo au kufanya vitendo vya kihalifu”
Screenshot_20230416_034630.jpg
 
Hatimaye Yanga imemaliza utata wa hatma ya beki wao Dickson Job baada ya kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili.

Job ambaye mkataba wake ulikuwa unafikia tamati mwisho wa msimu huu amesaini mkataba huo akitangazwa rasmi Leo na kumfanya kuendelea kuwa klabuni hapo mpaka 2025.

Job amekiri kuwa ameamua kusalia Yanga licha ya kuwa na ofa nyingi kwa klabu zingine lakini amefanya maamuzi ya kusalia klabuni hapo alikojiunga msimu wa 2020/21 akitokea Mtibwa Sugar.

"Nikweli nilikuwa na ofa mbalimbali lakini baada ya tafakari ya kina nimeamua kubaki hapa Yanga, ni heshima kuendelea kuichezea klabu hii kubwa,"amesema Job ambaye ni nahodha msaidizi wa kikosi hicho.
Screenshot_20230416_034838.jpg
 
Kenya imepeleka Satelaiti yake ya kwanza katika mzingo wa dunia, kwa kutumia roketi lililofyatuliwa kutoka California, Marekani, ripoti ya Shirika la anga za mbali la Nchini Marekani la SpaceX zimethibitisha.

@dw_kiswahili inaripoti kuwa kurushwa kwa Satelaiti hiyo kulitarajiwa majira ya usiku muda wa Marekani Jumatatu wiki hii lakini kulicheleweshwa mara kadhaa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Satelaiti hiyo ya Kenya ilisanifiwa na kikundi cha Watafiti kutoka Kenya na inanuia kutoa data za kilimo na kuchunguza mabadiliko ya kimazingira nchini Kenya, hususan wakati huu nchi hiyo inapokabiliwa na ukame wa muda mrefu.

Pattern Odhiambo, Mhandisi wa Shirika la Kenya la Anga za Mbali, KSA, amesema satelaiti hiyo iliyopewa jina la Taifa 1, itakuwa na faida za moja kwa moja katika sekta za utafiti na kuboresha mavuno ya kilimo.

Hadi mwaka 2022, Satelaiti zipatazo 50 za Mataifa ya Afrika zilikuwa zimepelekwa kwenye mzingo wa dunia, kulingana na Shirika la Nigeria linalofuatilia mipango ya Afrika ya anga za mbali.View attachment 2589262
Sisi tupo busy tunakimbiza Mwenge wa uhuru mpaka leo..... Ila yote heri
 
Kundi la fisi limevamia kijiji cha Njoroi kata ya Ololosokwani Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha na kuua kondoo 32.

Tukio hili limetokea jana Ijumaa Aprili 14, 2023 katika kijiji hicho kinachopakana na pori la akiba la Pololeti na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Njoroi, James Memusi amesema fisi hao walivamia kijiji saa tisa usiku na kuanza kushambulia kondoo na kuwaua 20 na kisha kuvamia makazi ya Mshao Tukai na kuua kondoo 12.

"Hili ni tukio la kwanza kutokea fisi kuvamia usiku na kula mifugo wengi kiasi hiki," amesema.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Jorome Mauri amesema, "kuna wanyama wengi porini kwa nini wamekuja huku kijijini? Tunaomba uchunguzi isije kuwa kuna kichaa cha fisi."
Hata hivyo mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri), Dk Eblate Mjingo amesema hana taarifa kamili za tukio hilo.

"Kuna wataalamu wetu wapo huko tunafuatilia na tutatoa taarifa lakini yale maeneo yapo jirani ya hifadhi hivyo inawezekana fisi kuvamia hayo maboma," amesema.
Screenshot_20230416_034942.jpg
 
Mchungaji wa Kanisa la Good News International, Paul Mackenzie amejisalimisha polisi mjini Malindi, Kenya baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa anasakwa na polisi na atafikishwa mahakamani wiki ijayo.

Alhamisi Februari 13, 2023 polisi walifanya msako eneo la Shakahola ambapo wasamalia wema walitoa taarifa uwepo wa watu waliofunga mfululizo ili wakutane na Yesu ambapo 15 walikutwa wamedhoofika na wanne walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu.

Mmoja wa waliookolewa amesema alimjua mchungaji huyo kupitia kituo cha televisheni cha Times kinachoonesha mahubiri ya Mackenzie.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa Aprili 14, 2023 katika hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Malindi anakoendelea kupata matibabu, Wycliffe Timbo (43) amesema alianza kusali katika kanisa hilo baada ya kuvutiwa na mahubiri ya mchungaji huyo.
“Nilikuwa nikitazama runinga ya Border TV lakini mwaka 2017 nilipoanza kutazama runinga ya Times TV nilivutiwa sana na mafundisho ya mchungaji Mackenzie,” amesema Timbo.

Timbo amesema baada ya mchungaji huyo kufunga kanisa hilo pamoja na kituo cha runinga ya Times TV, yeye alianza kujihusisha na kilimo cha mahindi, maharage na mbogamboga.

Alhamisi iliyopita alifikishwa katika hospitali ya Malindi akiwa na hali mbaya akiwa hajala chochote kwa siku 21 baada ya kufunga ili afariki dunia na kukutana na Yesu Kristo.

Katika picha ni Wycliffe Timbo (43) akiwa katika hospitali ya Malindi akiwa na hali mbaya, hajala chochote kwa siku 21 baada ya kufunga ili afariki dunia na kukutana na Yesu Kristo.

Screenshot_20230416_035047.jpg
 
Joseph Moulton (36) amekamatwa baada ya kuvamia kituo cha polisi Naples, Kusini Magharibi mwa Florida nchini Marekani na kufanya uharibifu pamoja na kuiba mali za polisi.

Tukio hilo limetokea Alhamisi Aprili 13, 2023 ambapo aliruka uzio na kuingia polisi kisha kuketi kwa dakika kadhaa hadi alipoona watu wakitoka nje kisha kuanza kufanya uharibifu.

Moulton anadaiwa kujisaidia haja kubwa kwenye sakafu katika choo cha wanawake na wanaume na kutumbukiza redio ya polisi chooni.

Maofisa wa polisi wamesema Moulton alikamatwa muda mfupi baada ya kufanya uharibifu huo na kuiba mali za polisi zikiwemo sare na nguo maalumu za kujikinga na risasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, alifungua maji kwenye mabomba na kuyaacha yakimwagika na kusababisha yasambae katika kituo hicho.
Screenshot_20230416_035149.jpg
 
Wakati biashara ya poda za chapa ya Johnson&Johnson zikiendelea kuuzwa madukani, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka Watanzania kuacha mara moja kuzitumia wakati uchunguzi ukikamilika.

Hayo yalielezwa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Athuman Ngenya ikiwa ni siku 10 tangu shirika hilo lianze kufanya uchunguzi kuhusu poda hizo.

Aprili 4 mwaka huu, wazalishaji wa poda hizo walieleza dhamira yao ya kusitisha uzalishaji wake baada ya kushindwa kesi zilizofunguliwa na wateja wake 60,000 na kukubali kulipa fidia ya dola 8.9 bilioni baada ya kubaini kuwa kemikali ya talc inayotumika ilisababisha saratani kwa watumiaji.

Dk Ngenya aliwataka Watanzania kusitisha mara moja matumizi ya poda hizo mpaka pale TBS itakapotoa majibu kutoka maabara.

“Tumepeleka kwenye maabara ambayo haifanyi kazi kwa muda mfupi, kuna taratibu zake za kufanya uchunguzi, kwa hiyo tunategemea majibu tutapata kesho, sijajua ni muda gani lakini ndiyo yatatoka kwa namna ambavyo wanalishughulikia, Jumatatu tutawapa jibu kamili kama tuendelee nazo au tuziache kabisa,” alisema.

Screenshot_20230416_035249.jpg
 
Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida ameondolewa kwa dharura eneo la Wakayama nchini humo baada ya kurushiwa bomu la machozi leo Aprili 15, 2023.

Mtu huyo anashikiliwa na polisi katika eneo la Wakayama, ambapo Waziri Mkuu Kishida alikuwa akitoa hotuba kwa wavuvi.

Shuhuda mmoja amesema waliona mtu akirusha kitu na kufuatiwa na moshi, huku mwingine akisema walisikia kishindo kikubwa.

Picha zilionyesha maofisa wakirundikana juu ya mtu anayeaminika kuwa ndiye mtuhumiwa.

Polisi nchini humo wamethibitisha kumkamata mtu huyo anadhaniwa kufanya tukio hilo.

Shirika la Utangazaji la Japan (NHK) lilionyesha video ya umati wa watu wakikimbia kutoka eneo la tukio.

Screenshot_20230416_035413.jpg
 
Siku 10 baada ya Linda Lugala kukutwa amekufa kwenye nyumba ya kulala wageni Kibaha mkoani Pwani, Jeshi la Polisi mkoani humo limesema linaendelea na msako ili kumpata mhusika wa tukio hilo.

Linda alifika kwenye nyumba hiyo Aprili 4, 2023 saa sita usiku akiwa ameambatana na mwanaume na walichukua chumba na kulala.

Siku iliyofuata kabla ya saa 12 alfajiri mwanaume aliyekuwa naye aliondoka na kumtaka mlinzi wa nyumba hiyo ya wageni kutomuamsha Linda mapema, akisisitiza kuwa anapaswa kupumzika kwa kuwa amechoka sana.

Mlinzi huyo, Banyonga Hamisi akizungumza na Mwananchi Digital amesema hakusikia kama wawili hao waligombana wakiwa chumbani, "walikuja wakiwa na furaha na walionekana ni watu wanaopendana sana. Wakachukua chumba na kufanya malipo wakaenda kulala."

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Piusi Lutumo jana Ijumaa Aprili 14, 2023 alizungumzia tukio hilo akisema walipokea taarifa ya tukio hilo na kufika eneo la tukio mapema.

"Sisi tunaendelea na msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa au watuhumiwa wa kosa la mauaji na taarifa tulipokea Aprili 4 mwaka huu kutoka kwa mmiliki wa nyumba hiyo ya kulala wageni hivyo maofisa wa Polisi walifika na kukuta hali hiyo," amesema
Screenshot_20230416_035515.jpg
 
Siku moja kabla ya pambano la watani wa jadi Simba vs Yanga, viongozi wa timu hizo wamekutana kwenye futari Ikulu Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Rais wa Yanga Injinia Hersi Said, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Salim Abdallah (Try again) wa pili kutoka kulia pamoja na Mfadhili na Mdhamini wa Yanga, Ghalib Said Mohamed (GSM) wa pili kutoka kushoto wakiwa Ikulu Dar kwa ajili ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Samia Suluhu Hassan tarehe leo Aprili 15, 2023. Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo.

Screenshot_20230416_035726.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom