Shaffih Dauda #VituExtra.
MATOKEO UBAONI YANGA 4-1 SIMBA
Nilikua najaribu kuwaweka hawa ‘Mapacha wa kariakoo’ kwenye mzani ila naona mpaka naingia mitamboni mzani hauja’Balance upande wa Simba.
Tuwapime Simba na Yanga kwenye haya maeneo
Social Media Engagement & Interaction
Kuanzia Twitter, Instagram na Youtube, Simba Sc wanaupiga mwingi sana. Wamewazidi Yanga kila eneo. Data zipo wazi
Simba Twitter:1.3M, Insta: 4.7m na Youtube: 340k Subscribers
Yanga: Twitter: 247.1K, Insta: 2.4M
Youtube: 293k Subscribers
Jersey Design, Quality & Distribution
Yanga: Kwa zaidi ya misimu 4 mfululizo wametoa Jezi kali zenye concept na ambazo zina quality inayofanya wao wafanye vizuri kwenye soko la mauzo ya jezi. Yanga chini ya GSM wameset standard kwenye suala la jezi. They are simply unbeatable
Simba: Upande wa jezi, Simba design zao ni average sana, kwa ufupi ni kuwa hawana maajabu sana.
Kwa misimu kadhaa sasa wamekua hawafanyi vizuri sokoni kwenye upande wa jezi. Ucheleweshwaji wa jezi kufika kwa wakati msimu uliopita na msimu huu imekua tatizo. Ipo kazi ya kufanyika hapa
Gate Collections
Yanga: Kwa misimu miwili mfululizo zimetoka takwimu wameongoza kwa kuingiza mashabiki wengi uwanjani. Hata mapato mlangoni wameyakusanya sana zaidi ya Simba. Hii inachangiwa na perfomance nzuri ya timu.
Simba: Kwenye suala la kuingiza mashabiki wengi kwenye mechi za ligi kuu, Simba wapo ‘Hoves’ sana.
Mashabiki wa Simba wanachagua sana mechi, tuseme hawana mizuka sana na timu yao. Hii inawezekana labda ni kwa sababu kwa kiasi fulani ni kushuka kwa perfomance ya Simba kwenye mechi za ligi kuu
Fans Involvement.
Yanga: Wanaupiga mwingi kwenye ‘Uhusishwaji wa wanachama na mashabiki’ kwenye ukuaji wa timu yao. Kuanzia msimu uliopita Yanga wamesajili sana wanachama wao kwa njia ya Kidijitali. Kama club wameingiza zaidi ya 1Billion kwenye miezi 6 ya kwanza.
Simba: Kwenye suala la usajili wa wanachama Simba hawana jipya. Simba wapo nyuma hatua 10, hawaendi na kasi ya teknolojia.
Mpaka sasa Ubaoni Yanga anaongoza bao 4, Simba bao 1. Muda sasa ifanyike ‘Substitution’ ili mzani uweze ku’Balance.