Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania, Abdulrahman Kinana leo Machi 28, 2023 ameongoza kikao (SUMMIT) cha wajumbe wa TCD katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na vyama vya CCM, CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na ACT Wazalendo.
View attachment 2569532
Screenshot_20230329_051124_OGInsta%2B.jpg
 
Ikiwa ni mwendelezo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Dodoma Mariam Ditopile ameandaa iftari na dua maalum ya watoto yatima na wajane kuiombea nchi na kumuombea Rais wa Tanzania, Samia Suluhu.

Hafla hiyo ya Iftari imefanyika jijini Dodoma ambapo mgeni wa heshima alikuwa ni Sheikh wa mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde na mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile.

Screenshot_20230329_051311_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewafutia kesi na kuwachia huru watu watatu wakiwemo wanandoa waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi gramu 66.70, baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa zaidi ya mara tano mfululizo bila kuendelea na usikilizwa wa upande wa mashtaka.

Sababu nyingine iliyofanya mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo ni kutokana na Serikali kushindwa kupeleka mashahidi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo.

Waliofutiwa kesi na kuachiwa huru na Mahakama hiyo ni Anjimile Chembe (40) na mume wake Shabani Abdallah (48) pamoja na Asha Mbuta (27).

Mbali na kuwafutia, Mahakama hiyo imetoa maelekezo kwa upande wa mashtaka kuwa washtakiwa hao wasikamatwe hadi Serikali ikakapokata rufaa Mahakama Kuu.
Screenshot_20230329_051636_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amekabidhi Sh21 milioni na mitungi ya gesi 700 kwa wanawake wajasiriamali 700 wa mkoa huo lengo ikiwa ni kuhamasisha kuacha matumizi ya nishati chafu (kuni na mkaa) na badala yake watumie nishati safi ili kuhifadhi mazingira.

Akizungumza baada ya kukabidhi majiko kwa niaba ya Masanja, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Reuben Jichabu amewataka wanawake hao kutumia nishati ya gesi ya oryx katika shughuli zao za ujasiriamali na kuepuka matumizi ya kuni.
Screenshot_20230329_051907_OGInsta%2B.jpg
 
Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Dk Abubakar Zubeir Bin Ally akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kulia) na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam (wa kwanza kushoto), Sheikh Wallid Alhad Omar, wakati alipowasili katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo Machi 27, 2023 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Screenshot_20230329_052515_OGInsta%2B.jpg
 
Umoja wa Afrika umetoa wito kwa raia nchini Kenya kuwa watulivu na kuanzisha mazungumzo ili kuangazia tofauti zilizopo kwa lengo la kuleta umoja na maridhiano.

Akizungumzia sala hilo, Mwenyekiti wa umoja huo, Moussa Faki Mahamat ameonyesha wasi wasi wake kutokana na ghasia zilizotokea na kusababisha kifo cha mtu mmoja huku mali zikiharibiwa kufuatia maandamano dhidi ya Serikali yaliyofanyika matika maeneo tofauti ya nchi hiyo.

Raia nchini Kenya walimiminika mitaani kwa wiki ya pili, wakipinga gharama za maisha kuwa juu.

Screenshot_20230329_052802_OGInsta%2B.jpg
 
‘Hivi ni vijimambo’ unaweza ukaita hivyo, baada ya sintofahamu kutanda katikati ya sherehe ya harusi kutokana na vurugu iliyosababishwa na taarifa iliyomfikia bibi harusi kuwa anaefunga nae ndoa ana watoto saba.

Sherehe hiyo iliyokua ikifanyika siku ya jumapili katika jimbo la Edo kusini mwa Nigeria iligeuka shubiri ambapo vilio vilitawala upande wa bibi harusi anaesemekana hakufanya uchunguzi kamili kumgundua mwenza wake huyo kabla ya kujitosa kufunga nae pingu za maisha.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha eneo la tukio kuvurugika baada ya viti, maua na mapambo yakiwa yametupwa kila mahali huku waalikwa wakiwa wamesimama kwa mshangao wakiashiria hakuna tena kinachoendelea.

Screenshot_20230329_053055_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama ya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani, Valency Panclas Mtales(43) mkazi wa kijiji cha Mamsera chini, wilayani humo, kwa kosa la kumlawiti mwanaume mwenye umri wa miaka 24.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Regina Futakamba Machi 22 mwaka huu baada ya mahakama kujiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na mashahidi wanane wa upande wa mashitaka.

Mahakama hiyo chini ya kifungu namba 154 kifungu cha kwanza A cha sheria ya kanuni ya adhabu namba 16 ambayo imefanyiwa marejeo mwaka 2022 ilimtia hatiani mshitakiwa huyo na kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani.

Screenshot_20230329_053312_OGInsta%2B.jpg
 
Takriban watu 14 wamepoteza maisha kusini mwa Somalia baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko katika miji na vijiji kadhaa.

Mvua hizo zimesababisha madaraja, barabara na nyumba kuharibika huku watu wengi wakilazimika kukimbia makazi yao kutafuta maeneo salama ya kukaa.

Mkuu wa Wilaya ya Baardhere, Mohamed Weli Yusuf akizungumza na waandishi wa habari alisema watu 14 waliuawa wakiwemo watu watatu wa familia moja.
Screenshot_20230329_053412_OGInsta%2B.jpg
 
Uongozi wa Yanga umetangaza kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Sebastian Nkoma aliyedumu kwa miezi mitatu kwenye timu hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa na uongozi huoleo Jumanne Machi 28, 2023 imesema timu hiyo kwasasa itakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna hadi msimu utakapomalizika ikiwa zimebaki mechi 6.

Yanga Princess ipo nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ikiwa na pointi 22 katika mechi 12 walizocheza ikishinda 6, droo 4 na kufungwa 2.

Nkoma ambaye aliwahi pia kuifundisha Simba Queens ikibeba ubingwa alijiunga na timu hiyo Desemba mwaka jana kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Screenshot_20230329_053512_OGInsta%2B.jpg
 
Mjadala umeibuka upya kufuatia maoni yaliyotolewa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kuhusu umri wa kuolewa ikipendekeza mtoto aliyevunja ungo aruhusiwe kuolewa hata kama hajafikisha umri wa miaka 18.

Kwa maoni hayo, ni kwamba Baraza hilo halikubali marekebisho Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 inayoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya akiwa na umri wa miaka 15 au miaka 14 kwa kibali cha mahakama, suala ambalo limepigiwa chapuo kwa muda mrefu ndani ya nje ya mahakama.

Sheria hiyo imekuwa ikipingwa na wanaharakati wa haki za watoto na wanawake wakidai inamnyima mtoto wa kike haki ya kupata elimu na kuwa utekelezaji wa sheria hiyo unakinzana na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 inayomtambua mtoto hadi umri wa 18 na tayari kuna maelekezo ya mahakama ya kutaka ibadilishwe.

Kwa habari kamili juu ya mjadala huu tembelea tovuti yetu ya www.Mwananchi.co.tz

Screenshot_20230329_053742_OGInsta%2B.jpg
 
Kenny Mchambuzii .

Sahau kuhusu Tanzania kupoteza mbele ya Uganda, NOVATUS DISMAS "MIROSHI" Kuna darasa katoa leo pale katika Uwanja wa Benjamin Mkapa,Muweke popote atakupa kazi nzuri "Uganda hawatasahau shughuli ya Kijana huyo".

Kiwango bora sana kutoka kwake, utulivu maarifa na kujiamini,kwa kiasi kikubwa alikua na mchezo bora sana.

Katika mchezo wa leo yeye ndio mchezaji aliyefanikiwa kutoa pasi sahihi na kwa wakati katika mipira ya mirefu na ya chini pia alikua bora sana katika mipira ya kuwania juu na ndie alikua tegemezi katika mipira mirefu mbele ya Uganda "Amefanikiwa kwa kiasi kikubwa".

Tanzania tumepoteza dakika za jioni kabisa mbele ya Uganda,Uganda walitengeneza nafasi na kuweza kutumia nafasi hiyo moja.

Kundi F kufuzu Afcon linazidi kuwa "Ngumu" katika timu ya kuungana na Algeria katika kufuzu makundi Afcon.

Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kusahihisha makosa ya mchezo wa leo mbele ya Uganda.

(ABDUL SULEIMAN "SOPU" ana nguvu ana kasi kubwa sana kuna muda alipeleka presha ya hali ya juu kwa Uganda lakini kuna muda akakosa mtu wa kumletea mipira na alikua chini ya ulinzi mkubwa "Kwa kiwango chake namuona akifika mbali").

NB.Tuna Timu nzuri ni muda sahihi kwa Kocha mkuu kusuka Kikosi chake,Tusife moyo bado nafasi ya kwenda makundi AFCON tunayo.
 
Farhan Jr

NOVATUS DISMAS MIROSHI, unaweza usiwe ule usiku ambao wengi waliutarajia lakini ulikuwa ni usiku ambao Mlima Kilimanjaro ulivuja theluji ya furaha kumwona mtoto kutoka ardhi yao akiibeba bendera ya Tanzania, his own mission to write his own history.

Future Stars pale Arusha waliweka alama, Academy pale Azam walisema ni Kiungo mkabaji, dimba la Karume pale Mara likampa upako wa Kikurya kuwa Muraa simamia eneo hilo na sisi tupo nyuma yako, akaondoka na baraka za ziwa Victoria na Mto Mara.

The streets of Mbagala have an affair with Winners! Walimtoa Samata kisha Azam ya Mbagala ikatupa Miroshi, imebarikiwa mikono ya Mwalimu aliyeona hiki kipaji, apewe sifa Mungu wa Isaka aliye hai na pongezi kwa @shaffihdauda_ kwa kuilinda hii dhahabu.

Ni mabadiliko kama bata kutoka Sinza mpaka Tabata, Kaka Bananga kutoka Chadema mpaka CCM ama mahaba ya Afande Sele na Wakazi wa Morogo ni kama ambavyo Miroshi na mpira, popote mtume ataitika na atakutumikia, what a talent.

Unaweza kuwa usiku wa uchambuzi mwingi sana ila kwangu ni usiku wa Mfalme anayekuja, Mlima Kilimanjaro umefurahi kwakuwa ni fahari ya Kaskazini, Arusha imebariki na tuseme Mungu Mbariki mtoto wako @novatus_40

Screenshot_20230329_054409_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

MMEAMUA KUTOMUELEWA MO DEWJI? MMEINGIA MTEGONI?

Nimesikiliza interview zote za Tajiri Kijana Afrika, MO Dewji nimetafakari kila alichosema ila headlines za wengi zimeenda tofauti na kile alichomaanisha na wengi wameelewa tofauti na alichomaanisha.

MO DEWJI amerejesha mpira kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba ambao wengi walipaswa kumuelewa ila bahati mbaya hawajaelewa, MO ameongea vitu vikubwa sana na vina maana kubwa sana.

Shabiki wa Simba sikiliza! MO DEWJI analalama kuwa kuna Watu wanakwamisha mchakato wa mabadiliko, kuna watu amesema anawafahamu! Kuna ubaya gani MO kuhitaji kila kitu kikamilike ili klabu isimame wima kwa miguu miwili?

MO anaweka pesa zake sehemu ambayo bado hatma yake haijulikani kwakuwa mchakato haujakamilika, MO ameipanua bajeti mara 10 kutoka Billion mbili mpaka BILLION 20 kwa mwaka, kwanini asiongee kama anakwamishwa?

MO ana hoja nzuri sana! Anahitaji Mashabiki na Wanachama waamke kwakuwa mabadiliko yalipitishwa na Wanachama wote hivyo anataka waielewe katiba, hapo kosa lake nini? Tajiri anapambana 51% za Wanachama ziwe na nguvu ili zisaidiane na 49% zake, hapo amekosea nini?

MO DEWJI ndani ya Simba sio suala la biashara tu bali Passion ya kweli kutoka moyoni mwake! Leo hii anawekeza kwenye timu za Vijana kuanzia U14, U16 na U20 unaweza kuelewa namna gani pesa zitamwagwa? Kuanzia watalaam na huduma zote?

Leo hii watu wanapiga kelele kuhusu MO DEWJI FOUNDATION nyuma ya jezi! Wanafahamu kuwa ndio mfuko utakaoenda kudhamini watoto wa timu za vijana kuanzia ELIMU (watasomeshwa) na pia gharama za kuishi (watatafutiwa familia Dar Es Salaam) hapo Tajiri ana kosa gani? Tumeshindwa kumuelewa?

Yes MO ana hoja! Tajiri gani angekubali kuendelea kutupa hela sehemu ambapo bado hatma ipo juu juu inaelea? Tajiri gani angeendeleza long term plans wakati hajui hatma yake? Ni suala la kimchakato.

Mashabiki na Wanachama kadhaa mmechagua kutomuelewa wakati ambao MO alipaswa kueleweka zaidi na kupewa support! Sio kwamba anasimanga ila ni ukweli kuwa mchakato umekuwa mgumu na muda unakwenda.

Mmechagua kutomuelewa Tajiri @moodewji anawakumbusha kuhusu kuheshimiwa mawazo yenu mliyopitisha kwenye mkutano mkuu??
Screenshot_20230329_054555_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom