Makapuku Forum

Makapuku Forum

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ametoa Spotify playlits yake ya nyimbo 25 za Wasanii wa Afrika ambazo anazikubali ambayo ameipa jina la “Safari Zangu: Ghana, Tanzania na Zambia”, kama sehemu ya kukuza muziki na kuwapa hamasa zaidi Wasanii wa Afrika wakati huu ambapo anafanya ziara katika Nchi hizi tatu ndani ya Wiki hii.

Mtandao maarufu wa Billboard umeitaja orodha hiyo ya Wasanii wa Nchi hizi tatu na nyimbo zao ambazo Wapenzi wa Muziki Duniani wanaweza kusikiliza kupitia Spotify na platform nyingine lengo likiwa ni kukuza Wasanii na mdundo wa Kiafrika hususani kutoka kwa Wasanii wa Ghana, Tanzania na Zambia.

Wasanii wa Tanzania ambao wamo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Harmonize na wimbo wake mpya ambao video yake imeachiwa rasmi leo ya Single Again, pia Zuchu (Utaniua), Alikiba (Mahaba) Jay Melody (Sawa), Mbosso (Shetani), Jux & Marioo (Nice Kiss), Darassa (No Body) , Marioo & Abbah (Lonenly), Platform & Marioo (Fall).

Tayari Kamala ametua Ghana tangu jana ambapo pamoja na mengine anayoyapa kipaumbele kwenye ziara yake ikiwemo maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na ongezeko la idadi ya vijana pia anatarajia kukutana na Wasanii wa Kiafrika ikiwemo wale ambapo wapo kwenye playlist yake ili kuongea nao na kuona namna bora ya kuufikisha muziki wao kwenye masoko makubwa ya muziki Marekani.
#MillardAyoUPDATES
Cc: @harmonize_tz @officialalikiba @marioo_tz @officialzuchu Juma_jux @darassacmg255 @mbosso_ @realjaymelody @platform_tz
Screenshot_20230328_044444_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230328_044503_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230328_044518_OGInsta%2B.jpg
 
Mahakama ya Mwanzo iliyopo Wilaya ya Kwimba imemuhukumu Erasto Bonda (33) kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa moja lenye mashtaka mawili, kutoa lugha ya matusi pamoja na kuzusha taarifa za uongo dhidi ya Nyakia Chirukile Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba.

Kesi hiyo ya jinai namba 16, 2023 ilifunguliwa na Nyakia Chirukile ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) katika Mahakama ya Mwanzo iliyopo Wilaya ya Kwimba.

Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Michael Turuka, leo March 27, 2023 ametoa hukumu hiyo mara baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili na kumtia hatiani Mshtakiwa Erasto Bonda kwa mashtaka yote mawili na kumuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kila shtaka na adhabu zote zinataenda pamoja na kuthibitishwa na Mahakama ya Wilaya kwakuwa Mshtakiwa amefungwa zaidi ya miezi sita.

Mshtakiwa Erasto Boda inaelezwa kwa nyakati tofauti alimtusi na kumzushia uwongo Katibu Tawala Kwimba Nyakia Chirukile kwenye mitandao ya kijamii (Magroup ya WhatsApp) kuwa ameiba fedha za Serikali zaidi ya Mil. 200, pamoja na kupeleka Kwimba Waganga wa jadi kutoka Tanga na Kigoma kwenye nyumba za Serikali kumuosha dawa.
Screenshot_20230328_045606_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Nchi yake haiundi muungano wowote wa kijeshi na China na kwamba nchi hizo mbili hazifichi chochote kuhusiana na ushirikiano wao wa kijeshi.

Putin amesema pia kuwa Mataifa ya Magharibi yanajaribu kuunda miungano ya kimataifa, huku akiishutumu Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO kwa kuanza kuunda muungano mpya unaofanana na ulioijumuisha Ujerumani, Italia, na Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Putin na Rais wa China Xi Jinping Wiki iliyopita walifanya mkutano wa kilele na kusifu kile walichokitaja kuwa "enzi mpya ya uhusiano" na kuahidi kuimarisha ushirikiano wao.

Hayo yanajiri wakati Urusi inajitahidi kupiga hatua katika vita yake na Ukraine.
Screenshot_20230328_045912_OGInsta%2B.jpg
 
Kundi la watu wanaokadiriwa kufika zaidi ya 1,000 wamevamia shamba la Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta mapema leo Jumatatu Machi 27, 2023 hii, huku ikishuhudiwa mwendelezo wa maandamano ya upinzani yaliyoitishwa kila Jumatatu.

Watu hao wameonekana, wakikata miti kwa kutumia misumeno ya umeme (Chain Saw), kuiba mifugo kwa idadi isiyojulikana kisha kuchoma moto sehemu ya shamba hilo lililopo Kaunti ndogo ya Ruiru.

Tovuti ya The Standard ya nchini humo imeripoti kuwa kundi hilo linadaiwa kuwatishia kuwakata mapanga waandishi wa habari na watu watakaothubutu kuwarekodi kinachoendelea shambani hapo.
Screenshot_20230328_050519_OGInsta%2B.jpg
 
Kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh5.1 bilioni, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kile kilichoelezwa na Serikali kuwa mshtakiwa imeshindikana kufikishwa mahakamani hapo.

Gasaya anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo anazipanda ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Kesi hiyo ya jinai namba 207/2022, ilipangwa leo, Machi 27, 2023 kwa ajili ya Serikali kumsomewa mshtakiwa hoja za awali (PH), baada ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika.

Leo, Machi 27, 2023 Wakili wa Serikali Caroline Matemu, ameieleza Mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio, kuwa mshtakiwa ambaye yupo Gereza la Keko imeshindikana kuletwa Mahakama kwa ajili ya kusomewa hoja za awali, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea.

Screenshot_20230328_050821_OGInsta%2B.jpg
 
Mkazi wa Mtaa wa Ihira, Kata ya Buhongwa mkoani Mwanza, David Deogratus (32) ameuawa na wananchi wenye silaha za jadi baada ya kumshambulia akidaiwa kuiba runinga nyumbani kwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kilumba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa alisema hayo Jumamosi 25, 2023 na kufafanua kwamba hata hivyo mtuhumiwa huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

Amesema mtuhumiwa huyo inadaiwa baada ya kuiba runinga (flat screen) aliruka dirishani ndipo wananchi walipomuona na kumvamia. Pia miongoni mwa vifaa alivyokutwa navyo ilikuwa ni nyundo, bisibisi na spana ambavyo inaelezwa alivitumia kwenye shughuli zake za kihalifu.

Screenshot_20230328_051113_OGInsta%2B.jpg
 
Taifa Stars kesho itaikaribisha Uganda 'The Cranes' kwenye uwanja wa Mkapa ikiwa ni mechi ya pili kukutanisha timu hizo kundi F baada ya kwanza kumalizika ugenini kwa Stars kushinda bao 1-0.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam leo kocha wa Uganda 'The Cranes', Milutin Sredojevic 'Micho' alisema kuwa wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi ya kesho lakini hofu yao kubwa ni ubora wa Taifa Stars katika kujilinda.

"Ni vigumu kufanya transition (mabadiliko) dhidi ya timu yenye nidhamu kubwa ya kujilinda, yenye mabeki watatu wa kati, jumlisha Novatus (Dismas), jumlisha Himdi Mao na Mudathir Yahya. Ilikuwa ngumu kwetu kuvunja ukuta huo na sasa kuna Shomari (Kapombe) na Tshabalala (Mohammed Hussein)."

"Tuna wachezaji wachache waandamizi ambao wanaongoza mabadiliko ya kizazi na tunategemea zaidi kizazi kilichoshiriki Afcon U20 kule Mauritania. Hakuna mahali pazuri pa kumbadilisha mtoto kuwa mwanaume zaidi ya Benjamin Mkapa," alisema Micho

Screenshot_20230328_051353_OGInsta%2B.jpg
 
MASHABIKI wa Yanga wanatamba mtaani kutokana na timu hiyo kuongoza Ligi Kuu Bara kwa tofauti na pointi nane, lakini wakiamini watani wao wa jadi Simba watawapa taji kwa msimu wa pili mfululizo watakapovaana nao Aprili 16 timu hizo zitakapokutana kwenye Kariakoo Derby.

Hata hivyo, kocha mkuu wa Simba, Mbrazili Roberto Oliveira 'Robertinho' ameshajipanga mapema na kulikabidhi faili ya Yanga kwa mabosi wa klabu hiyo ya Msimbazi, huku akisisitiza hayupo tayari kuwa daraja la kuwapa vinara hao taji mgongoni mwake watakapovaana Kwa Mkapa.

Yanga inaongoza msimamo kwa sasa na pointi 65, huku Simba ikishika nafasi ya pili ikiwa na alama 57 na vinara wao wa Ligi Kuu na Kundi D la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika inahitaji ushindi wa mechi tatu zijazo ikiwamo dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa Aprili 11, Simba ya Aprili 16 na ile ya Singida Big Stars itakayochezwa Aprili 25 mjini Singida.

Akizungumza na Mwanaspoti, Robertinho amekiri kuna changamoto kubwa ya kuizuia Yanga kubeba ubingwa kutokana na pengo la ponti, lakini amewasilisha projekti kabambe kwa mabosi wa timu hiyo itakayokwenda kupindua ufalme wa wababe hao wenye mataji 28 ya Ligi Kuu tangu 1965.

"Nimeandaa projekti yangu ambayo ni siri yangu na viongozi wa klabu wanayo tayari, nikiri kuwa sio rahisi kuwakamata Yanga licha ya kwamba tutaendelea kukimbizana nao hadi tuone mwisho kipi kitatokea,"
Screenshot_20230328_051455_OGInsta%2B.jpg
 
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza muda wa mechi ya marudiano kati ya Tanzania 'Taifa Stars' na Uganda 'The Cranes' itapigwa saa 2:00 usiku kesho Jumanne Machi 28 badala ya saa 1:00 usiku.

Stars itaingia katika mechi hiyo ikisaka ushindi na kujihakikishia nafasi nzuri ya kufuzu Afcon 2023 baada ya kushinda mechi iliyopita ugenini kwa bao 1-0.
Screenshot_20230328_051705_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom