Scandal24
FOOTBALL ECONOMY || Respect

.
Mashabiki wa Yanga pamoja na viongozi wenu mjifunze kuheshimu wachezaji wakubwa, ni kweli hakuna mchezaji mkubwa kuzidi timu ila mchezaji mkubwa anaipa thamani timu.
.
Tuache zile kauli ya akitaka ende zake, tuache zile kauli za pengo lake litazibwa, ni kweli litazibwa lakini mnapaswa kumfanya mchezaji ajitoe kwa Heshima ya watu wanaomuheshimu.
.
Mashabiki wa Simba wanamuheshimu Chama, Viongozi na wanachama wanamuheshimu Chama pamoja na wachezaji wengine wakubwa. Mashabiki wa Yanga jifunzeni kuwa na Heshima.
.
Huenda mkashinda mechi, huenda mkachukua vikombe lakini kama hamuwaheshimu wanachezaji ambao ndio wanajeshi siku zote wataondoka vibaya na wala hawatajivunia kuvaa jezi yenu.
.
Sina Mengi, FEI TOTO anastahili HESHIMA.
.
NB:
Simba wametengeneza Mfalme, Yanga wanamdharau Mfalme.
.