Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo ambaye alifariki October 24,2022 akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group tayari umeagwa nyumbani kwa Familia Mbezi Dar es salaam baada ya kupokewa katika Uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere Dar es salaam leo January 27,2023 ambapo unatarajia kusafirishwa leo hadi Mbeya kwa maziko.

Familia imesema kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao jeneza halitofunguliwa hivyo Ndugu, Jamaa na Marafiki wameaga picha na jeneza ““Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu tutatumia mtindo wa kuaga sanduku pamoja na picha hatutaweza kulifungua sanduku kwasababu zilizo nje ya uwezo wetu”

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Tanzania iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki mapema Wiki hii, Nemes alifariki akiwa vitani nchini Ukraine baada ya kujiunga na Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group akiwa anatumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka saba alichofungwa kwa makosa ya kihalifu.

Waziri Tax alinukuliwa akisema “Tarimo akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha lakini kwa ahadi ya kuachiwa huru mara baada ya vita na umauti ulimkuta October 24,2022 na Wizara ikawasiliana na Serikali ya Urusi ili kukabidhiwa mwili”

“Nemes Tarimo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya biashara , March 2022 alihukumiwa kifungo cha miaka saba kwa vitendo vya uhalifu”
Screenshot_20230128_044200_OGInsta%2B.jpg
 
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja kwenye Record Label ya WCB, Hamisi Taletale Babutale January 27, 2023 Jijini Dar es salaam ametunukiwa shahada ya udaktari wa heshima kutokea Taasisi ya 'Academy of Universal Global Peace' (AUGP-USA) ya nchini Marekani.

Baada ya kutunukiwa Babutale amezungumza yafuatayo “Nashukuru sana kwa nafasi hii niliyopewa, hii ni kwa sababu ya yale niliyoyafanya kwenye kazi zangu za siku zote, leo hii mimi ni Artist Manager lakini vilevile ni Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, yote haya nimeyafanya kwa wakati mmoja wakaona si mbaya wanitunukie”
Screenshot_20230128_044430_OGInsta%2B.jpg
 
Katika kusheherekea siku yake kuzaliwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan (63) ametoa sadaka kwa vituo vya kulelea Watoto Yatima ikiwemo Msimbazi Center huku wito ukitolewa Jamii kupinga vitendo vya ukatili.

Akimuwakilisha Rais Dr.Samia, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema “Kwa niaba ya Rais Samia nipo hapa kukabidhi sadaka kwa ajili ya Kituo cha Watoto Yatima Msimbazi wanaoishi katika mazingira magumu kinachosimamiwa katika Kanisa Katoliki”

"Kwa niaba ya Mh Rais tunasema shukrani nyingi na tunashukuru uongozi wa Kanisa, leo ni siku maalum kwa Mheshimiwa Rais wetu ametimiza umri wa miaka 63 na katika furaha na bashasha yake ameona ashiriki katika kumtukuza na kumshuruku Mwenyezi Mungu na kutoa kwake ameamua kwa makusudi kutoa katika vituo vya watoto yatima miongoni mwa vituo ameamua kutoa katika Kituo cha Msimbazi Center na Mburahati,"

"Tunaomba Watanzania wote lakini Viongozi wa Dini tuendelee kumuombea Rais Samia aendelee kuliongoza Taifa letu kwa mafanikio makubwa ambayo kwa hakika tumeyaona ndani ya muda ambao yeye ameliongoza Taifa, tumeshuhudia mambo makubwa ikiwemo uboreshwaji wa huduma za kijamii upande wa elimu, afya na shughuli za kiuchumi tumuombee heri nyingi aendelee kulitunza na kuliongoza Taifa hili”

"Na kama unaona anafanya mambo kwa mifano, nyakati zimekuwa ngumu wapo Watu wanaofanya vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto, wakina Mama Rais ni mpenzi wa Watu wote ikiwemo Watoto na wakina mama, na ndio maana kwa kufanya hivi leo anathibitisha mapenzi yake kwa Watoto anawatakia heri nyingi sana”
Screenshot_20230128_044549_OGInsta%2B.jpg
 
Ndoa ya Dr. Juma Mwaka Juma na Mkewe Queen Oscar Masanja haijavunjika, limesema Baraza la Ulamaa lililokutana kwa dharura leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni siku chache toka Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam atangaze kuvunjika kwa Ndoa hiyo.

Taarifa ya Baraza hilo kwa Vyombo vya Habari leo imesema baada ya kuliangalia kwa kina swala la Ndoa hiyo limefikia maazimio ya mambo manne ambapo moja ni kuwa Ndoa hiyo haijavunjika hivyo kwa kuwa kuna malalamiko yaliyopelekwa katika ofisi ya Qadhi, malalamiko hayo au kesi hiyo iendelee katika ofisi ya Qadhi na Baraza la Ulamaa litafuatilia kwa karibu kinachoendelea.

Azimio la pili la Baraza hilo ni kuwafahamisha Waislamu popote pale walipo wasisite kufanya mawasiliano na Baraza la Ulamaa popote pale watakapoona kuna upindishwaji wa mambo huku azimio la tatu likiwa kuwakumbusha kuwa Muhimili wa Mahakama ya Qadhi ni Muhimili muhimu na ungojitegemea hivyo sio sahihi maamuzi yake kuingiliwa na Mamlaka za BAKWATA Wilaya au Mkoa, na pale suala litakaposhindikana katika Mahakama ya chini suala hilo litapanda katika ngazi ya juu ndani ya Muhimili huo na si vinginevyo.

Azimio la nne ni msisitizo wa Baraza la Ulamaa kwamba utaratibu uliowekwa wa mgawanyo wa madaraka kuanzia katika ngazi zote ni muhimu utaratibu huu ukafuatwa na kudumishwa kwa aili ya kuchunga dhana nzuri ya utawala bora ndani ya Baraza.
Screenshot_20230128_044722_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20230128_044736_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Marekani limefanikiwa kumuua kiongozi wa kundi la Islamic States (IS) kaskazini mwa Somalia katika oparasheni ya iliyofanywa na jeshi hilo nchini humo.

Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao maofisa wa jeshi hilo waliwaambia waandishi wa habari kuwa oparasheni hiyo ilipitishwa na Rais Joe Biden mapema wiki hii na kutekelezwa ndani ya saa 24 zilizopita.
Screenshot_20230128_044850_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali imeipa mtaji wa Sh6 bilioni Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) ili isambaze mbolea ya ruzuku nchi nzima, Ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha mbolea sahihi na bora zinawafikia wakulima wote kwa wakati na kwa bei nafuu.

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 27 Januari, 2023 Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde alipokuwa akizindua zoezi la usambazaji wa mbolea za ruzuku za TFC.

"Ni zaidi ya miaka nane sasa imepita tangu TFC mara ya mwisho wasambaze mbolea kwa wakulima. Pongezi kubwa ni kwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kwa dhati kuhakikisha kuwa TFC inasambaza mbolea kwa wakulima mpaka maeneo yote nchini hususani yale ambayo hayafikiwi na wafanyabiashara wengine.” alisema Mavunde na kuongeza,

“Serikali imeanza utekelezaji wa miradi mikubwa nchi nzima ili kuwezesha Sekta ya Kilimo kukua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030, miradi hiyo ikiwemo na ujenzi wa Mabwawa mapya 14 ya umwagiliaji ambayo yatahifadhi maji takribani lita bilioni 131 na kuhudumia zaidi ya hekta 90,000. Ni dhahiri kwamba mahitaji ya mbolea yataongezeka ili kuendelea kuzalisha kwa tija, niwaombe TFC mchangamkie fursa hii na kufanya biashara yenye tija na faida.”

Screenshot_20230128_045709_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom