Makapuku Forum

Makapuku Forum

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kurejea upya gharama za upandikizaji wa mimba kwa Wananchi wenye matatizo ya uzazi na kutopata watoto ili kuwapunguzia mzigo wa gharama kubwa endapo watajiunga na Bima ya Afya kwa wote.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alipotembelea Taasisi ya Kairuki iliyopo Bunju A Jijini Dar es salaam ambayo inatoa huduma ya upandikizaji mimba kwa lengo la kuona huduma zinazotolewa kituoni hapo.

Waziri Ummy amesema tatizo la ugumba bado ni kubwa nchini lakini mpaka sasa hakuna takwimu rasmi za kitaifa ila ulifanyika utafiti mdogo ambao unaonesha 30% ya watu wana tatizo la ugumba huku Duniani inakadiriwa kuwa katika kila mahusiano ya wenza wanne, mmoja kati yao anakua na tatizo la kupata Watoto.

"Tatizo la kutopata Watoto lipo pande zote mbili, upande wa Wanaume na Wanawake lakini Jamii yetu inachukulia Familia isipopata Mtoto basi Mwanamke ndiyo anaonekana mwenye tatizo, naamini uwepo wa kituo hiki utasaidia kuondoa fikra potofu"

Kituo cha upandikizaji mimba cha Kairuki kinatoa huduma hiyo kwa gharama ya kuanzia Shilingi milioni 13 hadi milioni 17 kutegemea na aina ya huduma inayohitajika, hata hivyo Waziri Ummy amesema Serikali itaangalia uwezekano wa kuweka nusu ya gharama hizo katika vifurushi vya Bima ya Afya kwa Wote ili kuweza kuwapunguzia wananchi gharama za kupata huduma hiyo.
Screenshot_20230127_050159_OGInsta%2B.jpg
 
Jeshi la Polisi Tanzania limewatoa hofu Watanzania juu ya tishio la ugaidi Jijini Dar es salaam na maeneo mengin, baada ya taarifa ya tahadhari ya usalama iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Polisi imewahakikishia Wananchi kuwa hali ni shwari.

“Jeshi la Polisi limeiona taarifa jana January 25,2023 katika baadhi ya Vyombo vya Habari ikiwepo Mitandao ya Kijamii Kuhusu tahadhari kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa Wananchi wao kutembelewa na Watu wengi hapa Tanzania wakiwepo Wageni”

“Jeshi la Polisi Tanzania tulianza kulifanyia kazi taarifa hiyo kwa kina toka iliponza kusambaa, hivyo Wananchi wendelee kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida”

“Aidha pale itakapobainika jambo lenye kutia shaka au atakapo onekana mtu/watu wenye kutia mashaka kutokana na mienendo yao, basi taarifa hizo ziripotiwe kwa haraka ili ziweze
kufanyiwa kazi”

“Jeshi la Polisi Tanzania tunapenda kutoa taarifa kuwa, hali ya ulinzi na usalama wa nchi ni shwari kwani matukio makubwa yanayoweza kuleta hofu kwa wananchi yanaendelea kudhibitiwa”
Screenshot_20230127_050632_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati Papa akitarajiwa kutembelea taifa la Sudan Kusini hivi karibuni, baadhi ya wananchi nchini humo wanaamini huenda ziara hiyo ikaleta tumaini kurejea kwa amani nchini humo.

Baada ya kukaa karibu muongo mmoja katika kambi ya waliokimbia makazi yao huko Juba Sudan Kusini, Mayen Galuak anatumaini kuwa ziara ya Papa Francis katika mji mkuu wiki ijayo itawatia moyo viongozi wa kisiasa katika kurejesha amani na kumpa nafasi ya kurudi nyumbani.
Screenshot_20230127_051042_OGInsta%2B.jpg
 
Utafiti uliozinduliwa leo Januari 26, 2023 na Taasisi ya Regional Education Learning Initiative (Reli) kwa kushirikiana na taasisi ya Uwezo Tanzania umeonyesha kundi kubwa la vijana nchini halina maadili na stadi za maisha.

Ripoti hiyo ya 'Mchanganuo wa stadi za maisha na maadili katika Afrika Mashariki’ uliofanyika Julai, 2022 imehusisha vijana kuanzia umri wa miaka 13 hadi 17 katika wilaya 34, kaya 11,802 zikihusika na vijana 14,645 walihusishwa kutoka Tanzania Bara.
Utafiti huo umeonyesha kijana mmoja pekee kati ya 10 ana heshima na kujali maadili katika jamii, ambayo ni sawa na asilimia 12.5 ya vijana wote waliohusika katika utafiti huo.
Vilevile, utafiti huo umeonyesha kuwepo kwa uelewa mdogo wa vijana kujitambua na kutatua tatizo ambapo asilimia 16.8 pekee wana uwezo huo.

Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo na mdau wa Elimu, Profesa Kitila Mkumbo amesema uelewa mdogo wa kutatua matatizo na stadi za maisha unasababishwa na hali ya ubora wa elimu.

"Vijana waliohusika kwenye uchunguzi huu wengi wapo shuleni, napata mshituko kuona Wanafunzi Wana uelewa mdogo wa kutatua matatizo na nalihusisha hili na ubora wa elimu yetu," amesema.

Screenshot_20230127_051231_OGInsta%2B.jpg
 
Chama cha Wananchi (CUF) kimeeleza kusikitishwa na hatua ya Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutumia miezi 10 kukamilisha ripoti yake, ilhali kingeweza kufanya hivyo ndani ya mwezi mmoja.
Kauli hiyo imetolewa leo, Januari 26, 2023 na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipozungumza na wanahabari kuhusu kikao cha Baraza Kuu la Chama hicho kilichoketi Januari 21 na 22 mwaka huu.

Katika taarifa yake hiyo, Profesa Lipumba amesema kucheleweshwa kwa ripoti hiyo kumesababisha mambo yaliyopaswa kutekelezwa ndani ya bajeti ya 2022/23 yashindikane.

"Kama hili lingetekelezwa ndani ya mwezi mmoja bajeti ya Serikali ya wakati huo ingezingatia baadhi ya mambo, ikiwemo Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi," amesema.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo amesema katika kikao hicho baraza limempongeza Rais Samia kwa hatua yake ya kufungua mikutano ya hadhara.

Amesema zuio hilo lilikuwa kinyume na natakiwa ya Katiba na hivyo mkuu wa nchi hakuwa na mamlaka ya kuzuia.

Screenshot_20230127_051358_OGInsta%2B.jpg
 
Staa wa Bongo Flava, Marioo anatarajia kuzindua albamu yake ya The kid you know siku ya Jumamosi Januari 28 katika ukumbi wa Mlimani City.

Katika list yake ya mastaa aliowaalika wapo wasanii Diamond Platnumz, Harmonize, Alikiba ambao ni nadra kuwakuta sehemu moja kutokana na ushindani wao kimuziki.

Mara ya mwisho kufanya show ya jukwaa moja ila wakipanda kwa nyakati tofauti kwa Diamond na Alikiba ilikuwa Julai 12, 2020 jijini Dodoma kwenye sherehe za CCM.
Screenshot_20230127_051456_OGInsta%2B.jpg
 
Sakata la Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Yanga limemwibua Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya michezo nchini, Ally Mayay na amewashauri wachezaji wa Kitanzania kuwa na mameneja ambao watawasimamia mambo yao ikiwemo suala la mikataba.

Hatua hiyo imekuja baada ya Feisal na Yanga kuwa na mgogoro wa kimkataba uli0malizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kudai mchezaji huyo ni mwajiriwa wa Yanga.

Kiungo huyo alivunja mkataba wake na Wanajangwani hao ili kuwa huru kujiunga na timu nyingine huku akiweka kitita cha Sh112 milioni kwenye akaunti ya Yanga.

Akizungumzia ishu ya Fei, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema Serikali ni wazazi na wanaomba jambo hilo limalizwe ili mchezaji huyo aweze kucheza.

“Wote ni wadau wa michezo tunataka mafanikio kwa hiyo tunaomba masuala haya yamalizwe, pande zote mbili ziwe zimekubaliana kwa sababu sisi Serikali ni wazazi tunataka mafaniko ya wote.

“Kikubwa ni kuangalia kasoro kama hizi zisitokee tena ili kuhakikisha pande zote mbili zimefanikiwa, wakifanikiwa wao ndio Serikali imefanikiwa,” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.
Screenshot_20230127_051603_OGInsta%2B.jpg
 
“Badala ya kukata bima kwa Sh340,000 unasubiri maiti izuiwe hospitali ukalipe milioni sita. Wanasiasa wenzangu twendeni tukawahamasishe watanzania wajiandae kujiunga na bima ya afya.”

“Mzigo mkubwa ninaoona ni kuboresha huduma za afya katika vituo vya afya vya umma, huku juu sina wasiwasi.” Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
Screenshot_20230127_051754_OGInsta%2B.jpg
 
STRAIKA mpya wa Simba, Jean Baleke amesema anaamini anaweza kuonyesha kiwango bora zaidi ya alivyocheza mchezo wa kwanza wa kimashindano ndani ya timu hiyo na kuwataka mashabiki wampe muda.

Baleke alisema hakupata muda wa kutosha kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wote, bado hajazoea mazingira ndani ya Simba na hata nje ya timu pamoja na mambo mengine lakini atarudi kwa moto zaidi.

Alisema ameona watu haswa mashabiki wa Simba wamefurahi baada ya kufunga bao kwenye mechi ya kwanza walipowachapa Dodoma Jiji bao 1-0, ila anaamini kwenye uwezo wake anaweza kufanya zaidi ya vile alivyofanya kwa kuwa anajua ana uwezo mkubwa zaidi.

“Nashukuru Mungu amenipa uwezo wa kufunga kama nikipata muda wa kutosha kufanya mazoezi na kuzoea mazingira ya timu nitafanya vizuri zaidi ya ilivyokuwa mchezo wa kwanza mashabiki wa Simba wasiwe na hofu nami wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wananipa ushirikiano tu.

Screenshot_20230127_051934_OGInsta%2B.jpg
 
“Namfahamu Doumbia, nimecheza naye tangu tukiwa wadogo hata na Diarra (Djigui), nikiangalia ukuta wa Yanga naona nafasi yake ipo ingawa anatakiwa kujituma zaidi,”
.
“Ni beki wa kazi hasa lakini kitu kikubwa zaidi anajua sana kukabiliana na mipira ya juu, na pia ana nguvu, sio mtu rahisi kupitika.”

- Yacouba Songne
Screenshot_20230127_052211_OGInsta%2B.jpg
 
KAGOMA: KUTOKA KUWA DAKTARI HADI SOKA
.
“Ndoto yangu ilikuwa ni kuwa daktari nakumbuka tangu naanza shule nikiulizwa unasoma ili uwe nani jibu lilikuwa ni daktari ili niweze kuwatibu wagonjwa.

Lakini soka lilichukua nafasi kubwa zaidi ya masomo pamoja na kufanikiwa kumaliza kidato cha nne lakini sikuweza kutimiza ndoto yangu na kujikuta nawekeza nguvu zaidi kwenye mpira ambao pia nilikuwa naupenda.”
Screenshot_20230127_052310_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Nimeona dhihaka nyingi kuhusu usajili wa Gael Bigirimana, lakini kwa heshima ya mpira wa miguu ni kuwa Mchezaji husajiliwa kwa vitu viwili Form (Kiwango) na Class (Daraja).

Mfano Hakim Ziyech hana kiwango kizuri Chelsea lakini Milan wanamtaka sana kwakuwa wanafahamu daraja lake, mfano Erikssen alipotoka kwenye shambulio la moyo Brentford na timu nyingi zilimtaka kwakuwa wanafahamu Daraja lake.

Leo hii Ismail Sawadogo hajacheza miezi zaidi ya miwili ila Simba wamemsajili simply ni Daraja lake wote tunalifahamu au profile yake inavutia! Hata Feisal asipocheza mwaka mzima ila akirejea kila timu itamtaka simply ni Daraja lake.

Yanga walimsaini Gael Bigirimana ambaye amewahi kucheza EPL lakini hajaclick kwenye mpira wetu, sio dhambi! Kama ambavyo waliwahi kumsaini Saido aliyewahi kucheza LIGUE 1 na ikawalipa, huku Azam walimsaini Ahmada wa Ligue1 ambaye haikuwalipa.

Sio kosa Gael kusajiliwa na sioni dhambi Yanga kumwacha kwakuwa hajakidhi mahitaji na sio kosa wao kumpa sifa zake wakati wanamsaini kwakuwa profile yake ilikuwa nzuri na inavutia sana, the same case hata kwa Dejan alipokuja Simba.

Sometimes mpira wa miguu huenda beyond na mpira hiyo ni kawaida, wakati mwingine ni biashara ya kuisukuma brand yako mbali zaidi, unakumbuka usajili wa Sheva pale Chelsea na ukaribu wake na Roman? Real Madrid kuna kipindi walikuwa na mpango maalum na visiwa vya Mallorca ili kuipenyeza brand zaidi kwakuwa hawakuwa wanakubalika zaidi.

Sajili ya Gael haijawalipa uwanjani which ni kawaida lakini nje ya uwanja imewalipa na inakuwa rahisi kwa klabu kuwa na ushawishi wa kuwahi kuwa na profile kama za Saido na Gael ndani ya timu zao, ni ngumu kuona kikawaida kama tunaishi kawaida.

Perez aliwahi kusema atamsajili Luis Figo kama zawadi endapo Madridistas watamchagua ni kawaida! Hujui kwanini Boss Todd Boehly alienda fasta dili la Mudryk na wakamruhusu aingie na bendera ya Ukraine pale Stamford Bridge? One thing about football is not about football!

Sometimes it pays, sometimes it doesnt ndio football!

Screenshot_20230127_052942_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom