Makapuku Forum

Makapuku Forum

Je wajua inakujia na shunie shunie
Screenshot_20230128_045811_OGInsta%2B.jpg
 
Uwanja wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kushirikiana na Kampuni ya Geita Gold Mine Limited (GGML), unatarajiwa kukamilika Mei mwaka huu.

Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti anayeshughulikia Miradi Endelevu ya Ghana na Tanzania, Simon Shayo alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa uwanja huo unaojengwa katika eneo la Magogo, kata ya Bombambili, mjini Geita mkoani Geita, ipo mbioni kukamilika.

Alisema wanajenga uwanja bora na salama kwa watumiaji na kwamba kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi ikisimamiwa na mshauri ambaye ameajiriwa na halmashauri ili ashauri namna ya kumalizia awamu ya kwanza na awamu nyingine.

“Kwa kushirikiana na halmashauri na uongozi wa mkoa wa Geita, nia yetu kuhakikisha hadi kufikia Mei mwaka huu uwanja uwe umekamilika na kuanza kutumika. Kwa hiyo hii itategemea sana kasi ya wakandarasi wetu na wote tunaofanya nao kazi ambao tunaamini kwamba watahakikisha uwanja huu unakamilika kwa wakati kwani nia yetu ni kuwa na uwanja bora, hatutaki kufanya kwa kuikimbiza na kuwa na eneo ambalo watu wanaweza kupata majeraha au uwanja ambao unaweza kuwa na dosari siku zijazo. Kama mjuavyo sisi tunu yetu ya kwanza ni usalama, kwa hiyo tungependa kuona wachezaji na mashabiki wanafanya shughuli zao kwenye uwanja ambao ni salama,"

“Tumeona timu inafanya vizuri, tulishuhudia wachezaji walivyocheza mechi zilizotangulia, tumeambiwa wachezaji wanazidi kusomana na kadiri timu inavyokaa pamoja tunaamini kwamba itaendelea kuimarika zaidi. Nia yetu ni kuona kwamba Geita Gold FC inatwaa ubingwa wa Tanzania bara badala ya kuishia nne bora, licha ya kwamba mimi ni mshabiki wa Simba SC. Tunaamini siku za karibuni watu wakija Geita watakuwa wanacheza na bingwa wa ligi kuu Tanzania bara,” alisema.

Screenshot_20230128_050302_OGInsta%2B.jpg
 
UCHAWI WAMPONZA KASEKE
.
Kiungo Deus Kaseke wa Singida BS amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya laki tano kwa kosa la kufanya kítendo kinachoashiria imani za kishirikina alionekana akitupa kitu kwenye lango la Azam FC wakati timu yake ikijiandaa kupiga pigo la kona.
Screenshot_20230128_050618_OGInsta%2B.jpg
 
Mikel Arteta na Arsenal yake wanacheza kamari yao, wanaiwaza zaidi ligi kuu kuliko FA kwa aina ya kikosi chake na sub zake, wana mechi zao mbili za fainali dhidi ya City kwenye EPL.
Screenshot_20230128_051131_OGInsta%2B.jpg
 
Utani wa ngumi huu hapa! Richarlson ameenda uwanjani kutazama mechi ya Spurs U21 ambapo Luca Moura anacheza pia akiwa anatoka kwenye majeraha sasa Richarlson amebeba bango linalosema “Lucas naomba jezi yako”
Screenshot_20230128_051423_OGInsta%2B.jpg
 
Kongo wameweza kuzalisha Makocha wakubwa ambao wamezifundisha timu zao kubwa kwa mafanikio, Ibenge akiwa na Vita pamoja na timu ya taifa, bado Pamphile Kazembe akiwa na TP Mazembe wote hao wapo imara na wengine wamepata nafasi nje ya nchi.

Kwa Makocha wetu wapi tunakwama? Vyeti vyetu havisadifu yaliyomo au uoga wa kujaribu?
Screenshot_20230128_051531_OGInsta%2B.jpg
 
Nyota wa Morocco Azzedine Ounahi atajiunga na klabu ya Olympique Marseille kwa kandarasi ya muda mrefu baada ya kuonesha kiwango bora kwenye kombe la dunia nchini Qatar.
Screenshot_20230128_051620_OGInsta%2B.jpg
 
Kinda Antony Gordon amejiunga rasmi na klabu ya Newcastle kwa ada ya Pauni Million 40 akitokea Everton ambapo alilazimisha sana uhamisho huo kwa kugomea mazoezi.
Screenshot_20230128_051708_OGInsta%2B.jpg
 
Kwa mujibu wa SkySports ni kuwa muda wowote kuanzia hivi sasa Sean Dyche atangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Everton akirithi mikoba ya Frank Lampard.
Screenshot_20230128_051757_OGInsta%2B.jpg
 
Wakati Simba na Yanga zikipambana kubeba ubingwa, Azam FC na Singida Big Stars zinapigani nafasi ya tatu hai ni tofauti kule bondeni kwenye msimamo wa Ligi!

Ruvu Shooting na Polisi Tanzania zipo kwenye hatari ya kushuka daraja moja kwa moja. Ruvu ipo nafasi ya mwisho kabisa (16) kwenye Ligi ikiwa na alama 14 huku Polisi Tanzania yenyewe ikiwa nafasi ya 15 na alama zake 15. Timu zote zimecheza michezo 21 na kubakiwa na michezo tisa.

Wana-fainali wa Kombe la TFF msimu uliopita Coastal Ulion wapo nafasi ya 14, wamecheza mechi 22 wana alama 19. Dodoma Jiji ipo nafasi ya 13, imecheza michezo 21, ina alama 21.

Ukiangalia timu ambazo zipo kwenye hatari ya kushuka daraja tatu kati ya hizo zinamilikiwa na taasisi [Dodoma Jiji, Polisi Tanzania na Ruvu Shooting].

Vita ya kubaki Ligi Kuu ni kali sana kwa sababu inahusisha hadi timu ambazo hazijafikisha alama 40 ambazo kimahesabu zinaweza kufikiwa na timu ya mwisho!

Je, ni timu gani zitashuka daraja na zipi zitafanikiwa kusalia kwa ajili ya msimu ujao?
Screenshot_20230128_051852_OGInsta%2B.jpg
 
Singida Big Stars ni timu mpya kwenye Ligi ya NBC 2022|2023, inashiriki kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo.

Timu ndio mpya lakini wachezaji wake wengi ni wazoefu wa Ligi kwa miaka mingi wakiwa wametoka kwenye klabu za madaraja ya juu na kati.

Wakati Ligi ikielekea ukingoni, Singida Big Stars kwa sasa ipo nafasi ya nne (4) kwenye msimamo wa Ligi huku ikifanana kila kitu na Azam isipokuwa magoli ya kufunga na kufungwa.

Singida Big Stars na Azam zote zimecheza mechci 21, zimeshinda michezo 13, sare michezo 4, zimepoteza michezo 4, zote zina alama 43.

Kwa idadi ya mechi zilizobakiza [mechi 9] bado kuna nafasi kwa timu zote mbili [Singida Big Stars na Azam FC] kumaliza kwenye nafasi nzuri zaidi.

Singida Big Stars inaweza kumaliza hata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi ikiwa ni mara ya kwanza inashiriki Ligi Kuu.

Wakulima wa alizeti wamepita katikati ya Geita Gold na Namungo FC timu ambazo hivi karibuni zimekuwa zikipigana kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligi.

TOP FOUR NBC PL 2022|23

1. Yanga———56
2. Simba———50
3. Azam———43
4. Singida BS—43

Kwa mechi zilizobaki na mwenendo wa Ligi ulivyo ni wazi Yanga au Simba timu mmoja itakuwa bingwa na nyingine itamaliza nafasi ya pili halafu Azam na Singida Big Stars zitapigania nafasi ya tatu.
Screenshot_20230128_051941_OGInsta%2B.jpg
 
Said Ntibazonkiza yupo kila mahali, yupo kwenye orodha ya wafungaji, yupo kwenye orodha ya waliotoa pasi nyingi za magoli yupo kwenye orodha ya wachezaji waliohisika kwenye magoli mengi!

Said Ntibazonkiza magoli 9 assists 8 [17]
Fiston Mayele magoli 15 assists 2 [17]
Clatous Chama magoli 3 assists 12 [15]
Sixtus Sabilo magoli 8 assists 6 [14]
Moses Phiri magoli 10 assists 2 [12]

Screenshot_20230128_052338_OGInsta%2B.jpg
 
Said Ntibazonkiza yupo kila mahali, yupo kwenye orodha ya wafungaji, yupo kwenye orodha ya waliotoa pasi nyingi za magoli yupo kwenye orodha ya wachezaji waliohisika kwenye magoli mengi!

Said Ntibazonkiza magoli 9 assists 8 [17]
Fiston Mayele magoli 15 assists 2 [17]
Clatous Chama magoli 3 assists 12 [15]
Sixtus Sabilo magoli 8 assists 6 [14]
Moses Phiri magoli 10 assists 2 [12]

View attachment 2497798
Lala ukue
 
WAKALI WA PASI ZA MABAO NBC PL

Kwenye orodha ya wakali wa pasi za mwisho ‘assists’ Simba ina wachezaji wanne (4) kati ya wachezaji saba (7). Kwa pamoja wametengeneza magoli 30 huku timu yao ikiwa imefunga magoli 51.

Watoto wa nyumbani pia wanafanya vizuri kwenye eneo hili, kati ya wachezaji saba (7) wenye assists nyingi wachezaji watano (5) ni wazawa.

Clatous Chama [Simba] 12
Said Ntibazonkiza [Simba] 8
Ayoub Lyanga [Azam FC] 7
Sixtus Sabilo [Mbeya City] 6
Deus Kaseke [Singida BS] 5
Mohamed Hussein [Simba] 5
Mzamiru Yassin [Simba] 5
Screenshot_20230128_052724_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom