Farhan JR
KENNEDY MUSONDA, ving’amuzi viwe tayari, mitaa iwe tayari na banda umiza mpaka Buza kwa Ujugu wawe tayari! The streets have to get used to this name, amewasili kwenye Premier League! Ni Muisrael wa mpira aliyevushwa na Musa wa soka Hersi Said kuja nchi ya ahadi, you feel me?
Mazembe walisukuma kete yao atue Lubumbashi lakini dakika kadhaa za Uwanja wa ndege wa Simon Mwansa Kapwewe alizoketi na Engineer wakati ana tiketi yake kuelekea Lubumbashi ilitosha kumwona Dar Es Salaam, nyumbani kwa visingeli na Mahindi ya kuchoma kwa chumvi.
Wakati Hersi anakata tiketi kuelekea Zambia hakuna aliyeamini pale Salamander, atawezaje kuinasa saini ya Mchezaji mwenye mkataba na Power Dynamos? Hakueleweka kirahisi mission ngumu inayohitaji wagumu! Atawezaje kumleta Mchezaji ambaye TP Mazembe walishatuma nauli wakisubiri text ya “Nishukie wapi?”
President wa Yanga na imaan yake kama Daniel dhidi ya Simba alishacheza movie kali na akaibuka starring ile The Thriller in Abdijan na Aziz Ki akatua JK Nyerere kama mateka, he knew the principles of the game, he followed the rules and won the game.
Ameenda vizuri amecheza vizuri niliwahi kumpa kisa cha dunia ya Maengineer, nikampa kisa cha Luis Campos The Wizard of the Capital Gain, usiruhusu aongee na Mchezaji wako ndio makosa ambayo Musonda aliyafanya, kumpa tu sikio
Dakika tano alizopewa ya kwanza ilikuwa kumwonesha anamhitaji sana, ya pili ilikuwa ni project kubwa ya Yanga, ya tatu ni utayari wake wa kumalizana na Power Dynamos na kuvunja mkataba, ya nne ni PESA na tano ni PESA, hakuwa na pa kurukia Musonda! Hakuwa na neno kama IFM na watoto wakali, SUA na msuli au @official_simalengatz na watu wake wa Songwe.
Nataka kupumzika ila acha niseme! Imepigwa Mazembe kwenye ofa, ukavunjwa mkataba na klabu yake ya Power Dynamos, akala Air Tanzania mpaka Tanzania na amesaini na Wananchi, karibu sana Musonda kwenye ardhi ya Mwalimu Mzanaki wa Butiama, karibu Tanzania nchi ya Wachambuzi.