Farhan Jr
Nipe simulizi nzuri, simulizi kuhusu Kinjikitile na risasi kugeuka maji hiyo Hapana! Simulizi ya Chief Mangungo wa Msovero kuhusu mikataba na Carl Peters achana nayo, nipe simulizi nzuri.
Simulizi ambayo itaishi daima mbele ya Wajukuu zako, simulizi ambayo machozi yatakutoka na utakumbuka mchana wa jua kali Dar Es Salaam au usiku adhimu wa CAF Champions League wakati Mzambia akiwa uwanjani, tunaweza pata hizo simulizi?
Achana na simulizi za vita ya coursework za DS pale Mkwawa kwa Doctor Mlungu! Sahau kuhusu maisha ya Wema na Wanaume Mastaa! Simulizi ya Hamisa kuwa na watoto wawili wa Matajiri achana nazo, simulizi za Buga HAPANA kubaya huko.
Nipe simulizi nzuri za kueleweka, simulizi nzuri kama Mashairi ya Cheka Cheka, simulizi isiyouma kama Watoto wa Mama Ntilie, simulizi nzuri ya uhakika kama mshale wa saa na sekunde, nipe hizo simulizi nipo pae nimekaa.
Naileta hii hadithi wala sitaki mseme uongo uje na utamu ukolee! Bali mpira uje kwake na pass zitembee, hadithi nzuri na simuliI ya kuishi milele kuhusu Mwamba kutoka Kusini mwa Afrika, ardhi ya Keneth Wa Kaunda.
Ni simulizi ya kweli na uhakika! Kama ukisikia kikohozi na Konde Boy Mjeshi! Kama ukisikia Umepoa na Mwijaku, ubunifu na @cloudsfmtz ni simulizi ya kweli na uhakika katikati mwa miaka ya 2000 ni simulizi ya kweli kuhusu hiki kipaji.
Mnisamehe wajukuu zangu niwaachieni hii picha iliyopigwa na Bandeko wa Kigoma @rabbihume kumbukumbu anazo mpiga picha.
CHAMA 10:17-18 “Basi endeleeni kuzitama clip zake Azam TV, habari zake Simba App na picha zake magazetini ndio urithi wenu na faraja kwenu, alikuja kwetu kwa ajili ya soka, tukapendezwa nae mtazameni yeye” @realclatouschama
Kama umeupenda wimbo huu, bonyeza nyota utakuwa wa kwako! MMEENJOY