Kijana Albert Mrema ambaye alinusurika katika ajali ya gari iliyosababisha vifo vya Mama na Wanawe wawili na akawa amelazwa ICU Hospitali ya Mloganzila, nae amefariki dunia, Albert ndiye alikuwa Dereva wa gari hilo ambalo liliacha njia na kuingia Barabarani na kifo chake kinafanya Familia hiyo sasa kuwa imempoteza Mama na Wanae watatu.
Ajali hiyo imetokea Jumamosi iliyopita maeneno ya Kibamba na kusababisha vifo vya Watu watatu, Immaculata Byemerwa (49) ambaye ni Mama pamoja na Watoto wake Jolister Byemerwa (17), aliyekuwa anafanyiwa sherehe ya mahafali siku hiyo na Janeth Byemerwa (20), Mwanafunzi aliyekuwa anasoma mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Albert Mrema ambaye alizaliwa mwaka 1994 alikuwa Mtoto wa kwanza wa Immaculata kabla ya kufunga ndoa na Mhandisi Josephat Byemerwa, Baba wa Familia ambaye alifariki dunia mwezj May mwaka jana na sasa mwaka mmoja tu baada ya kifo chake Mkewe na Watoto watatu nao wamefariki.
View attachment 2436142View attachment 2436143