


Farhan Jr
Acha niwape kisa kimoja kuhusu Ndugu wawili nyuma ya ADIDAS na PUMA, Yes ni Ndugu wawili kama ilivyo kwa Salaah wa Silent Ocean na Gharib wa GSM, mmoja alikuwa anaitwa Adolf na mmoja anaitwa Rudolf maarufu kama THE DASSLER BROTHERS, acha niwape kisa.
Hawa Ndugu wawili zamani kabla ya vita ya pili ya dunia walikuwa na Kampuni yao inaitwa GEDA, waliendesha kwa pamoja kabla ya kufikia 1948 ambapo walipishana kwasababu mbalimbali na kila mmoja akaanzisha Kampuni yake.
Adolf akaanzisha kampuni ya ADIDAS iliyotokana na jina lake Adolf Dassler na mdogo wake akaanzisha kampuni ya PUMA na kuiita jina la Mnyama, biashara yao ya mapambano ilianzia hapo na hawakupikika chungu kimoja inapokuja suala la maslahi.
Turejee kwenye issue ya SILENT OCEAN ambao wao wamewekeza mzigo wao pale Prisons na GSM wameweka mzigo wao pale Yanga, licha ya kuwa ni Ndugu lakini hizi ni biashara, ni zaidi ya undugu na Ushabiki wao.
Mzee wangu Jemedari ameandika kitu kuhusu INTERGRITY, lakini hakuna sehemu duniani kwenye dunia ya kitaasisi ikapimwa kisa Undugu, hakuna hata mmoja kati ya hao ndugu wawili anayetaka kufeli kwenye biashara zake, amini hilo.
Una hofu na Silent Ocean? Wangewekaje Million 20 kama Prisons watamfunga Yanga? Remember dhidi ya Simba aliahidi Million20 pia! pesa ambayo aliahidi ushindi kama Prisons atamfunga Simba leo imekaa tena palepale, una hofu mpaka hapo? Na ahadi ni mpaka mechi tofauti na Kariakoo isipokuwa dau tofauti.
TFF hawana room ya kuingilia hii kwakuwa ni battle hii, ni pesa hapo imewekwa! Licha ya kuwa wao ni Ndugu sisi watu wa mpira tunawaona ni Washindani na ndio maana Silent hayupo popote kwenye jezi ya Yanga, wao wana utawala wao na GSM wana utawala na mfumo wao.
Salaah anaweza kuwa Yanga kama ambavyo President Karia ni Coastal, Mimi ni Simba, Javier Tebas ni Madrid lakini anaongoza LA LIGA, Ushabiki wa Mtu hauwezi kuathiri kazi, mapenzi na kazi ni vitu viwili tofauti mno, ndio maana hata Rais wa nchi anaweza kupangiwa cha kufanya na Watu wake kwakuwa ni mfumo unawaongoza.
Halafu kwenye dunia ya ushindani, mara nyingi Ndugu hukamiana sana kuliko kawaida.
The corporate world, works differently from streets.