Makapuku Forum

Makapuku Forum

MOSIMANE ATUA SAUDI ARABIA
.
Pitso Mosimane ametangazwa rasmi kuwa Kocha mkuu wa Klabu ya Al-Ahli Saudi inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia.
Screenshot_20220925-162312_OGInsta%2B.jpg
 
Mgunda amedai baada ya kuisoma De Agosto kwa kuchukua mikanda ya video ameamua kuipeleka Simba visiwani Zanzibar ili kusaka kuwapa vijana wake mbinu za Kiufundi kwa lengo la kuvuka kuingia hatua ya Makundi.
Screenshot_20220925-162640_OGInsta%2B.jpg
 
Hapa ndipo alipozikwa Malkia Elizabeth wa Uingereza....sehemu hiyo pia ndipo alipozikwa baba na mama yake pamoja na mume wake...magonjwa na kifo huwa havina upendeleo...tujifunze kujinyenyekeza kwa sababu sisi sote mwisho wetu ni mavumbini na tutaondoka hapa duniani kama tulivyokuja...!
Screenshot_20220925-215334_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Kocha wa kwanza kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara kufundisha Al Ahly, klabu kubwa na tajiri barani Afrika huku ikitajwa kuwa na mafanikio makubwa sana naam ni klabu ya karne inayokimbizana vikombe na Real Madrid.

Akawa Kocha wa kwanza kubeba ubingwa back to back wa Afrika kwenye klabu hiyo, alikuwa Pitso Mosimame kutoka kwenye jamii iliyochukuliwa poa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Pitso hakufika Cairo kwa bahati mbaya, bali kwa rekodi nzuri ndani ya Mamelodi Sundowns, akabeba ubingwa wa Afrika! Hata pale Ahly walipokuja kugonga mlango, Rais Pitso Mosimane hakubana akaruhusu kijana aende zake Kaskazini.

Pitso alifanya vyema Al Ahly ambao kwa kwa lugha ya Majahazi ni Nationals au kwa Kiswahili cha Kilombero nyumbani Morogoro ni WANANCHI, Yes wanatambulika hivyo kutokana na historia yao na taifa la Misri.

Hii picha nimeipenda sana, nimeipenda kwakuwa aliyewahi kuwa Kocha wa Wananchi wa Misri amepiga picha na Mwananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kizani au hadharani ni moja kati ya Pioneers wa Kizazi hiki cha dhahabu.

Nimeipenda tu hii picha, kila la kheri Kocha Pitso huko Saudi Arabia na hii picha yenu sisi tunaitunza kwenye makabati yetu, kama kuna Mwana ghetto huko anataka kukata tamaa basi aitazame hii kisha achape mwendo.

Kutokea Milima ya Uluguru na safu za Udzungwa huko nyumbani Morogoro, baada ya kuitazama picha hii tunasema “Mpaka pale zamu yetu itapofika yatupasa kuwapigia makofi wengine”

Tupo pale tunasubiri kupongeza kwakuwa rizki anatoa aliye juu, hatuna roho ya kushinda tunataka sote tushinde
Screenshot_20220927-161535_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom