

Farhan Jr
BAADA YA RAIS HERSI WA YANGA KUSEMA YANGA INAENDESHWA KWA HASARA, NIKAIKUMBUKA HII POST AMBAYO NILITUKANWA SANA! TUJIKUMBUSHE
・・・
Jana niliandika kitu kuhusu MO Dewji kisha nikazima data nikapumzika kwakuwa ilikuwa usiku sana, naamka napitia comments, Insta mpaka WhatsApp nahisi hatujaelewana.
Naomba siku moja nikipata wasaa nitawapa vitu kutoka kwenye kitabu kimoja nachomalizia kukisoma “FOOTBALL IS NOTHING THAN A PRESTIGIOUS GAME”
Ni kitabu kizuri sana kinachozungumzia mpira kuanzia Pre Bosman na Post Bosman era, kinazungumzia kuwa mpira sio biashara kama ambavyo wengi wanadhani bali ni Mchezo wa sifa tu.
Kitabu kinasema Matajiri wanaowekeza kwenye mpira au Matajiri wanaosimamia mpira wameingia kama sehemu ya sifa kwa timu zao na kuhakikisha timu zinapata furaha kwakuwa ni furaha yao pia.
Leo hii watu wanasema Simba ina Wadhamini ambao wanahesabika wote, lakini duniani kuna klabu kama Real Madrid na Barcelona, Manchester United na bado zina madeni, unafahamu ni kwanini? Hiyo ni homework.
Leo hii Real Madrid ili uwe mgombea wa Urais lazima uwe na sifa ya kukopesheka kwenye benki zinazotambulika na mamlaka, ambazo ni EURO MILLION 124 ambayo ni sawa na 15% ya bajeti ya Real Madrid kwa mwaka, unafikiri ni kwanini? Homework hiyo naiacha.
Juzi Rais wa Barcelona Joan Laporta na Mhazini wa klabu Ferran Olive walitoa zaidi ya Pauni Million 20 ambazo ni pesa zao binafsi, ili Jules Kounde asajiliwe kwenye mfumo wa LA LIGA, unafikiri ni kwanini? Simply ni kuwa mpira bado sio biashara mnayoisema na hauna hela hivyo.
Nachomaanisha ni kuwa sahau kuhusu hizo pesa za Wadhamini ambazo zinatoka kwa mkupuo sio zote kwa pamoja, sahau kuhusu TV rights, sio rahisi kuendesha timu za mpira na zikapata matokeo, ukihitaji timu ipate matokeo lazima uende nje ya bajeti, huo ndio ukweli.
Kwa mwaka Simba bajeti yao ni BILLION 12, hiyo ni bajeti ya kwenye makaratasi tu tena ya timu moja ya Kiume, hujataja Simba Queens na timu za vijana, can you imagine? Hizo pesa zinatoka wapi?
Ni rahisi sana kumwondoa MO kwenye equation kwasababu zenu binafsi ila mpira sio biashara duniani kote, FOOTBALL IS A PRESTIGIOUS GAME.