Makapuku Forum

Makapuku Forum

Farhan Jr

Kwanza kabisa wengi wanaamini Dejan lilikuwa chaguo la Kocha Zoran Maki, hiyo sio kweli kwakuwa Mchezaji pekee ambaye Kocha aliyepita alimpendekeza ni Momo Ouattara na aliletewa.

Taarifa za kuaminika ni kuwa Kocha Zoran alimkataa baada ya session mbili tu za mazoezi ila kuna shinikizo lilikuwepo ila nyota huyo acheze ila hakuonekana kukidhi matarajio ya Makocha.

Pili, Dejan alitakiwa kupewa mkataba wa muda mfupi ndani ya Simba ila yeye na Wakala wake waligomea na kuhitaji kandarasi ya muda mrefu klabuni hapo, ikitajwa kuwa ni zaidi ya miaka miwili.

Simba kwenye makubaliano ya kimkataba waliweka target zao pia, waliweka idadi kadhaa ya mabao ndani ya kipindi cha miezi sita iwe tayari ameyafikia nyota huyo, kitu ambacho sidhani kama angefikia.

Tatu, Dejan alihitaji kupangiwa apartment ambayo klabu ilimtafutia na kumlipia kama ilivyo utaratibu wa Simba ila inasemekana alianza kusumbua kuwa hajaipenda hata kidogo.

Bado alimwambia Meneja kuwa anataka chumba cha kulala cha peke yake, klabu ilikubali ombi lake na alikuwa analala peke yake kambini, pasipo na Mchezaji mwingine.

Nini kimetokea?? Baada ya mgogoro wa juzi kifupi Dejan anaamini hapewi ushirikiano na wenzake, anaona halishwi kama inavyotakiwa kwa Striker, hilo alisema wazi na hakuwa na furaha tena.

Ameamua kuondoka lakini vingi anavyosema walimtimizia ilisalia yeye kutimiza yale ya kimkataba ila ajabu yeye kasepa kwa kusema Simba haijatimiza yale ya kimkataba
Screenshot_20220930-041704_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Katika vitu ambavyo Simba wanapaswa kujipongeza ni kuoutsource suala la scouting za wachezaji kikosini mwao, wakafanikiwa zaidi pia kwenye kufanya performance analysis mwishoni mwa msimu (hufanyika na Watalaam kutoka Afrika Kusini).

Simba wanafanya kazi kwa ukaribu mno na AGENCIES mbalimbali za wachezaji ambazo zinawaletea quality kubwa mno ijapo baadhi wanafeli kufikia matarajio kutokana na sababu nyingi ila wengi wanafanikiwa.

Mifuko ya MO inapasuka sana, unapasuka kulipa Agencies, unapasuka kuinasa hiyo quality na unapasuka kuilea na kuilipa hiyo quality ili ikupe matokeo uwanjani, Okrah is a great player ambaye atawasaidia sana Simba.

Hata kama udalali upo upo ila kwa kiasi kikubwa umepungua kwasasa tangu waipate network nzuri ya Mawakala.

Mabadiliko yoyote yale ni process hakuna overnight process, taratibu hatua kwa hatua soka litabadilika na kufikia level kubwa.
Screenshot_20220930-041827_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

DUNIA YA MAINJINIA DHIDI YA DUNIA YENU.

Miaka 38 iliyopita miezi mitatu tu baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ndipo alizaliwa Hersi Ally Said.

Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ndipo historia yake ilipoanzia, ni moja kati ya sehemu yenye historia ndogo kwenye ile historia kubwa ya Rais wa Yanga ambaye yupo madarakani hivi sasa.

Sidhani kama Wakunga wa hospital ya Mpwapwa walifahamu wamemleta duniani kijana gani, bali walichofahamu cha kwanza ni kuhakikisha analia ili tufahamu yupo duniani.

Mkononi mwake hakushika kitu chochote lakini kichwani kwake na moyo wake ulikuja na ndoto kubwa kuhusu Dar Young Africans, sio Chuo cha DIT aliposoma wala MUST Mbeya ambapo alifundisha (Assistant Lecturer) ndoto yake ilikuwa Yanga Afrika.

Stori yetu inaenda mbele kwa haraka mpaka jioni moja kwenye mitaa yenye harakati nyingi Jijini Dar Es Salaam, wakati wengine wanagombea magari kuondoka majumbani, wakati wengine wanafunga biashara zao yeye alikuwa ofisini kwake.

Kwenye jengo refu la Mnara wa Salamander, Posta Dar Es Salaam ndani ya Ghorofa ya 10 wakati huo ni Mjumbe tu wa kamati pale Yanga, Mwalimu Mstaafu wa Chuo cha MUST (Mbeya University of Science and Technology) anapiga hesabu za kumnasa Aziz Ki wa Asec Mimosa.

Engineer Hersi project yake akiwa Rais ni kuwa Mchezaji yoyote bora ni lazima acheze Yanga, hiyo ni ndoto yake, Yanga ijae Mastaa wakubwa Afrika ili kuipa mafanikio, ndio ndoto zake kama atakuwa Rais.

Swali lake la kwanza, nampataje Stephen Aziz Ki? Sipo tayari kuwa Rais kama nitamkosa Mchezaji huyu! Kumbuka yupo ghorofani Salamander kama ambavyo Injinia mwenzake Perez alivyokuwa ghorofani pale ACS, Madrid kwenye oparesheni ya FIGO.

Hersi anainza mission ngumu sana ambayo wengi hawakuamini, Msaidizi wake Amina hajarudi kwake kwakuwa Boss hajatoka ofisini, bado anapasua kichwa anaanzaje?____

ITAENDELEA…

Screenshot_20220930-041946_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Fanya ufanyavyo ila Matajiri wengi wanapenda vitabu vibalance, wanapenda kuona CEO anaokoa hata mia mbovu ambayo ingekuwa hasara kwa Boss.

Roman Abramovich pale Chelsea alikuwa na Marina ambaye alimtoa kwenye kampuni zake za mafuta, hakuwa na interests za kimpira ila alikuwa na interests kubwa za kibiashara, yani Chelsea ikuwe na Boss asipasuke sana.

Nyote mnakumbuka namna Marina alivyosajili sana kwa bei rahisi na kuuza wachezaji kwa bei mbaya sana, nyote mnakumbuka namna Chelsea ilivyopanda thamani na NIKE walivyodouble pesa pale.

Huyu Barbra kutoka London School of Economics, anaweza asiufahamu sana mpira kama wengine ila anaifahamu biashara ndani ya mpira, anafahamu KPIs za biashara ya mpira, Boss MO amerelax tu huko Dubai.

Katika hali ya kawaida Bwana Dejan angeweza kudai mabillion ya pesa kwenye mkataba ule wa miaka mitatu lakini kwa hesabu kali za kimpira huenda akailipa Simba au waamue tu kumwachia, hesabu hizo za mpira.

Ingekuwa zamani MO angepigiwa simu na kuambiwa Boss tunapaswa kumlipa Dejan! Naam ni akili kama hizi za biashara ambazo zinachukuwa sana kwenye mpira kwakuwa wao mpira sio sifa bali BIASHARA.

Huyu akisema aseme yote yanayoendelea maishani mwake atajaza vitabu, kama ambavyo Marina alivyoingia na kugundua mengi ya Michael Emenalo na namna ambavyo sometimes alikuwa anafuja mtonyo wa Roman.

Nipo zangu kwenye Abood naelekea Nyumbani Morogoro nataka niwahi ugali na mlandu kaliandili, wapi ndipi ramani na Baunsa kutoka Mto Lumemo na Kivukoni, Ifakara
Screenshot_20220930-042052_OGInsta%2B.jpg
 
Farhan Jr

Katika vitu ambavyo Simba wanapaswa kujipongeza ni kuoutsource suala la scouting za wachezaji kikosini mwao, wakafanikiwa zaidi pia kwenye kufanya performance analysis mwishoni mwa msimu (hufanyika na Watalaam kutoka Afrika Kusini).

Simba wanafanya kazi kwa ukaribu mno na AGENCIES mbalimbali za wachezaji ambazo zinawaletea quality kubwa mno ijapo baadhi wanafeli kufikia matarajio kutokana na sababu nyingi ila wengi wanafanikiwa.

Mifuko ya MO inapasuka sana, unapasuka kulipa Agencies, unapasuka kuinasa hiyo quality na unapasuka kuilea na kuilipa hiyo quality ili ikupe matokeo uwanjani, Okrah is a great player ambaye atawasaidia sana Simba.

Hata kama udalali upo upo ila kwa kiasi kikubwa umepungua kwasasa tangu waipate network nzuri ya Mawakala.

Mabadiliko yoyote yale ni process hakuna overnight process, taratibu hatua kwa hatua soka litabadilika na kufikia level kubwa.
View attachment 2372075
hahahahaha,kwa habari hii acha nicheke kwanza
 
Farhan Jr

Fanya ufanyavyo ila Matajiri wengi wanapenda vitabu vibalance, wanapenda kuona CEO anaokoa hata mia mbovu ambayo ingekuwa hasara kwa Boss.

Roman Abramovich pale Chelsea alikuwa na Marina ambaye alimtoa kwenye kampuni zake za mafuta, hakuwa na interests za kimpira ila alikuwa na interests kubwa za kibiashara, yani Chelsea ikuwe na Boss asipasuke sana.

Nyote mnakumbuka namna Marina alivyosajili sana kwa bei rahisi na kuuza wachezaji kwa bei mbaya sana, nyote mnakumbuka namna Chelsea ilivyopanda thamani na NIKE walivyodouble pesa pale.

Huyu Barbra kutoka London School of Economics, anaweza asiufahamu sana mpira kama wengine ila anaifahamu biashara ndani ya mpira, anafahamu KPIs za biashara ya mpira, Boss MO amerelax tu huko Dubai.

Katika hali ya kawaida Bwana Dejan angeweza kudai mabillion ya pesa kwenye mkataba ule wa miaka mitatu lakini kwa hesabu kali za kimpira huenda akailipa Simba au waamue tu kumwachia, hesabu hizo za mpira.

Ingekuwa zamani MO angepigiwa simu na kuambiwa Boss tunapaswa kumlipa Dejan! Naam ni akili kama hizi za biashara ambazo zinachukuwa sana kwenye mpira kwakuwa wao mpira sio sifa bali BIASHARA.

Huyu akisema aseme yote yanayoendelea maishani mwake atajaza vitabu, kama ambavyo Marina alivyoingia na kugundua mengi ya Michael Emenalo na namna ambavyo sometimes alikuwa anafuja mtonyo wa Roman.

Nipo zangu kwenye Abood naelekea Nyumbani Morogoro nataka niwahi ugali na mlandu kaliandili, wapi ndipi ramani na Baunsa kutoka Mto Lumemo na Kivukoni, IfakaraView attachment 2372077
hahahahahaha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom