Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jemedari Said

KOCHA NASREDDINE NABI KAMA MGUNDA TU..!!!
Taarifa za uhakika zinasema Kocha NASREDDINE MOHAMED NABI naye anasubiri ruhusa (Approval) ya CAF kumuwezesha kukaa kwenye benchi hapo kesho kwenye mchezo wa Champions League.

Nabi ambaye msimu uliopita alikaa benchi kwenye mechi 2 dhidi ya Rivers United ana vyeti vya UEFA 'A' na UEFA-Pro alizosomea Belgium, lakini taarifa zake zilichelewa kupelekwa CAF.

Taarifa zinasema aliyekua Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga SC THABIT KANDORO wakati anaondolewa kwenye nafasi yake kumpisha SAAD KAWEMBA alikuwa anafanya usajili wa wachezaji na Viongozi wa benchi la ufundi.

Akiwa ameshamaliza wachezaji 7 kuwaingiza kwenye mfumo wa usajiri akakumbana na andiko la kuachishwa kazi, akamalizia wachezaji ila benchi la ufundi alikua bado hajaanza kabisa.

Kwahiyo waliochukua badala yake ni kama walipitiwa wakiamini kilakitu kiko sawa wakaja kukumbushwa na ujumbe kutoka CAF juu ya taarifa za kocha wao.

Habari zaidi zinasema taarifa zake (vyeti) zimeshawasilishwa CAF na wanasubiri Shirikisho hilo la Soka Afrika kuidhinisha tu ili akae benchini kesho.

Hali hii ni kama ambayo inamkuta Kocha Mkuu wa Simba SC JUMA MGUNDA ambaye nayeye anasubiria idhini ya CAF ili kesho akae benchini pale jijini Lilongwe kwenye mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets. Mgunda yeye amechlewa kuidhinishwa kwakuwa vyeti vyake vimechelewa kuwasilishwa kwakuwa ni kocha mpya.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)
Screenshot_20220909-203410_OGInsta%2B.jpg
 
HENRY ACHEKA KISA SPURS ITAKUWA BINGWA
.
ANACHEEEKA! Staa, Thierry Henry ameshindwa kujizuia na kuangua kicheko baada ya Clint Dempsey kusema Tottenham Hotspur itashinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
.
Henry, Dempsey na Jamie Carragher waliulizwa wachague timu zao ambazo wanadhani zitashinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
.
Carragher aliichagua Manchester City kama ambayo alivyofanya Henry, lakini Dempsey chaguo lake liliwachekesha wengi, aliposema:
.
“Nitakuwa tofauti kidogo, nitachagua timu isiyofikiriwa kabisa kama inaweza kutwaa ubingwa. Bingwa inaweza kuwa Tottenhma.” Maneno hayo yalimfanya Henry na Carragher kuangua vicheko na Henry kusema: “Acha niondoke.”
Screenshot_20220909-204407_OGInsta%2B.jpg
 
Huyu ndie Princess Diana, sasa hivi ndie angekuwa Malkia.

Sio pesa wala ukuu unaoweza kufanya ndoa yako idumu, bali heshima na upendo. Kama ungekuwa ukuu au pesa basi ndoa ya Diana na Charles isingekufa. Princess Diana alikutana kwa mara ya kwanza na Prince Charles akiwa binti mdogo kabisa mwenye umri wa miaka 16, wakati huo Prince Charles alikuwa anatoka na dada yake Diana. Diana alimpenda Charles, wakafanya mafekechee wakazama penzini japo kwa siri. Baadae wakahalalisha mahusiano yao na kufunga ndoa mwka 1981, Diana akiwa na miaka 20.

Sio kwamba Diana alitoka katika familia isiyokuwa na heshima, hapana, familia yake ni mojawapo ya familia zenye hadhi ya juu nchini Uingereza. Baada ya ndoa Diana alikuwa ni mwanamke wa Tatu mwenye heshima nchini Uingereza, baada ya Malkia na Mama yake Malkia.

Licha ya ukuu aliokuwa nao lakini Princess Diana hakuwa na furaha kwenye ndoa yake. Mume wake kuwa na mahusiano ya nje ilimtesa sana Diana. Mimba ya mtoto wake wa kwanza ikiwa na wiki 12, Diana alijirushwa kutoka kwenye ngazi na kuanguka, hata hivyo mimba haikurabika. Diana alisema alifanya hivyo kwa sababu alikuwa mpweke sana. Baada ya kujifungua mwanae wa kwanza Diana aliugua ugonjwa wa Sonona.

Baada ya miaka 5 ya ndoa kulikuwa na migogoro mikubwa sana ambayo haswa ilichangiwa na tofauti ya umri. Diana alikuwa na mchepuko wake wakati huo mumewe pia mahusiano yake na Camilla yalikuwa yamenoga. Migogoro na utofauti iliendeleq kukuwa na kupelekea ndoa yao kuvunjika miaka 15 baadae.

Akizungumza na mwandishi wa BBC, Diana alisema waliamua kutengena kwa sababu mahusiano yao yalikuwa kama ofisi ya umma, siku hizi mnasema Azam Burudani kwa Wote. Pia Diana alisema alikuwa ana mashaka sana kama Prince Charles alikuwa anafaa kuwa Mfalme wa Uingereza.

Baada ya kutengana Princess Diana alinasa kwenye penzi zito la mtoto wa Kiarabu, penzi lao halikudumu sana. Princess Diana alifariki dunia kutokana na majeraha aliyopata kutokana na ajali ya gari. Alifariki mwaka 1997, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutalakiana na Charles. Princess Diana alifariki akiwa na umri wa miaka 36, katika ndoa yao walibahatika kupata watoto wawili ambao ni Prince William na Prince Harry.View attachment 2351711
Hapa ndiyo anafanane na Mwanae Harry mno...
 
HENRY ACHEKA KISA SPURS ITAKUWA BINGWA
.
ANACHEEEKA! Staa, Thierry Henry ameshindwa kujizuia na kuangua kicheko baada ya Clint Dempsey kusema Tottenham Hotspur itashinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
.
Henry, Dempsey na Jamie Carragher waliulizwa wachague timu zao ambazo wanadhani zitashinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
.
Carragher aliichagua Manchester City kama ambayo alivyofanya Henry, lakini Dempsey chaguo lake liliwachekesha wengi, aliposema:
.
“Nitakuwa tofauti kidogo, nitachagua timu isiyofikiriwa kabisa kama inaweza kutwaa ubingwa. Bingwa inaweza kuwa Tottenhma.” Maneno hayo yalimfanya Henry na Carragher kuangua vicheko na Henry kusema: “Acha niondoke.”View attachment 2351756
Thierry Henry 14 kichogo, alinioonza kuipenda arsenal
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom